Haki Jinai na Jinai Yetu Sote Katika Utoaji wa Haki

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
Na Johnson Gerald

Nimefuatilia ripoti ya Jaji Othman Chande kuhusu changamoto mbalimbali katika utoaji wa haki katika mawanda za jinai nchini. Nataka kuamini Jaji Chande amewasemea wananchi wengi katika ripoti yake lakini pia ametusema sote tuliochangia jinai hiyo.

Ungana nami katika kuangalia masuala haya 10 aliyoibua Jaji Chande na wito kwetu sisi sote kujikosoa ili kujisahihisha ndio maana anuani ya Makala yangu leo inasema: “Haki Jinai na Jinai Yetu Sote Katika Utoaji wa Haki.”

1. Jaji Anasema: Ukamataji Umejaa Jinai

Hili lazima wahusika wajitazame. Sheria inasema kila mtuhumiwa si mkosaji mpaka ithibitike hivyo Mahakamani. Kwamba Jaji Chande amebaini mabavu, visa na uonevu katika kukamata raia, wengine wema na wengine wakosaji, inaumiza na ni suala la kila mmoja wetu polisi, majeshi, magereza na hata raia tunapochoma wenzetu moto kisa tuhuma tu, tujitazame. Tuikatae jinai hii.

2. Kwamba Kesi Za Kubumba!

Inaumiza, kwamba mwanadamu aliyekuwa katika mihangaiko yake ya kila siku anabambikiwa kesi, anafungwa na kunyang’anywa uhuru wake na familia yake. Hili ni suala ningedhani wanaharakati kuanzia TLS hadi akina Anna Henga wa Legal and Human Rights Center jana ile ile wangetambua kazi kubwa ya Jaji Chande lakini nao kimya. Wananchi wameamia sana.

3. Kwamba Magerezani kwenyewe hoi

Uwe ulifungwa kwa haki au kuonewa, nenda gerezani sasa anasema Jaji Chande; utabloo wanasema vijana. Pakulala pabovu, chakula kibovu. Kwa nini lakini? Why? Bado sisisi askari magereza hatujatesa wafungwa na kuwatia udhalili! Ni jinai baada ya jinai. Hakuna namna. Tubadilike.

4. Ujeshi tu kila mahali

Hili nalo limenistusha. Sijui wenzangu. Yani leo taasisi hata ya kutupa huduma ya kusafiri nje na kurudi inakuwa “Jeshi la Uhamiaji?” Watu wanaotakiwa kuokoa maisha ya watu kwa kumwagilia moto maji usiteketeze mali nao wanahangaika kuwa wanajeshi. Kwani hatuwezi kutatua shughuli za kijamii hadi tuwe jeshi? Mbona wenzetu wanavikosi vya zima moto, upelelezi, majanga n.k na sio Jeshi?

Nimeishi sana Marekani huwezi kukuta Idara ya Kupambana na Majanga (Federal Emergence Managamenet Agency-FEMA) ni jeshi, never). Kama kuna mtu alipita jeshi humo sawa sio shida lakini Idara ya kuhudumia watu sio lazima iwe jeshi.

5. Kwa hiyo Ndio Jino kwa Jino?

Jaji anasema bado sisi Tanzania tuna adhabu ya kifo yaani tunaendeleza ile jino kwa jino. Katika ripoti anatuhoji hakuna adhabu nyingine mbadala? Lazima kifo kimoja kiondoke na watu wawili? Naamini jamii italitazama hili kwa kina. Yani kwa sababu yoyote ile iwayo jazba (provocation) au makusudi (with malice aforethought) mama kamuua baba, ndio baba nae anauawa, maana hakuna option nyingine, kisha watoto wanabaki na nani??

6. Nimesikia Kuhusu Kila Mtu Mpelelezi!

Hakika Ripoti ya Jaji imechambua kwa kina tunapokosea. Hivi mtaalamu hasa ni nani polisi, majeshi, Takukuru, dawa za kulevya kila mtu mpelelezi. Nani Mkuu? Ndio maana kuna mda wenyewe wanabishana. Katika dunia yenye maswali magumu twende kama wenzetu FBI tu tuwe na chombo chenye wabobezi wa kuchunghuza makosa makubwa haya ya magari sijui mtu kaiba kuku waachiwe polisi!

7. Plea Bargain, Plea Bargain, Plea Bargain

Nimekuita mara tatu ewe rafiki unayeruhusu wakosaji wakiri kosa na kutoa hela na kusepa. Nimeona maoni ya Tume kwamba pia wapo wanaolalamika hata mali zao zilichukuliwa kijinai. Hapana, ripoti ya jinai iondoe jinai hii lakini huu mfumo pia utazamwe upya mbona upo mfumo ndani ya mahakama yenyewe na mshtakiwa kutakiwa kukiri kosa au kukataa (plea of guilty or not), ulikuwa na shida gani??

8. Unakagua Darasa Ukiwa na Jeshi, Polisi, Takukuru!

Niliposikia hili nikasema Mungu ampe maisha marefu huyu Jaji Chande halafu usikute pia huyu Jaji kuna mwalimu wake wa “Mathe” alimwambia hatafika mbali, hapa alipofika ni wapi sasa? Jaji Chande na timu yake hakika wameitendea haki taarifa.

Binafsi nimekuwa nikijiuliza hivi RC au DC katika kazi zake za kila siku anaenda kukjagua shule, hospitali, anakwenda kuona mashamba ya kilimo lazima abebe vyombo vyooote vya dola tena wakuu watupu na wasaidizi wao? Hawa jamaa wanafanya kazi lini katika ofisi zao? Jaji Chande ubarikiwe. Umefika na utafika mbali. Tunasubiri sasa tamko la Serikali lini wanapigwa marufuku hawa watu rasmi.

9. Kwamba Eng. Haujamaliza Mradi Ndani?

Kiukweli tumetoka mbali, yani mkandarasi ameingia mkataba ambao uko chini ya sheria ya mikataba ambazo ni sheria za madai (civil law), hajamaliza mkataba iwe kwa sababu zake au upande wa pili au mambo yaliyo nje ya uwezo (force majure), RC au DC hajui hilo, anaona mwenge unakaribia anataka sifa siku ya mwenge, anakuja, anaagiza unakamata mkandarasi unaweka ndani! Hii ni haki ya wapi? Hii ni jinai yetu wenyewe. Lazima tukiri.

10. Kumbe Juu ya Juu Kuna Juu

Nimeeleza sana hapa jinsi Ripoti hii ya Jaji Chande bila wengi kujua inavyoweza kuja kugeuka limbuko kwa haki za wananchi. Ni ripoti ambayo sio haki tu bali hata mchango wake katika udemokrasia (democratisation) hautamithilika.
Lakini, hata kama hatupendi, maono na nia yote ya kubadili haya inatoka kwa mtu husu Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Sisi watu wa masuala ya asasi za kiraia tunasubiri kwa hamu utekelezaji maana yote yaliuyotajwa tulilia sana, tuliyaandikia sana na tuliyalalamikia sana. Tunamtakia kheri Rais katika kuyatolea mwelekeo na maagizo ya kiutekelezaji.

Lakini nihitimishe kwa kutoa wito kwetu sote Watanzania wenzangu kujitazama tena na tena maana tuliosababisha jinai na makosa yote haya ni sisi wananchi, sisi polisi, sisi wanajeshi, sisi wanaharakati hivyo jinai hii ni yetu sote sasa tuikatae.

Nimeona mahali wanasema jinai sasa basi. Hakika.
 
Ukiona adui yako anakusifia,Jitafakari…
 
Back
Top Bottom