Mbowe: Tozo ya Matangazo kwenye Facebook itawapunguzia Vijana Kipato na Fursa za Kujiajiri

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,981
Mwenyekiti wa Chadema Mbowe anesema Tozo/Kodi inayotarajiwa kuwekwa kwenye Matangazo ya Facebook itawapunguzia Vijana Kipato na Fursa za Kujiajiri.

Mbowe anesema Maisha ya Vijana wa Tanzania ni ya kuungaunga hayana Afya yoyote hivyo ni vema Serikali ikawaangalia kwa jicho la Huruma.

Jumaa Mubarak 😀

=======

Mbowe.png

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kitendo cha Serikali kukusudia kuanza kuwatoza kodi wafanyabiashara wanaoweka matangazo madogomadogo mitandaoni kusaka wateja ni kuwarudisha nyuma kiuchumi.

Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni miezi michache imepita tangu Serikali kutangaza kufanya mabadiliko ya sheria ya kodi ili kuruhusu kukusanya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilima mbili hata kwa kampuni zisizo na ofisi nchini.

Kampuni zinazotoa huduma za kidijitali nazo zitaguswa na utaratibu huo utakapoanza kutekelezwa.

Kulingana na tangazo hilo lililotolewa na Serikali Julai mwaka huu, kodi hizo zitaiwezesha Serikali kukusanya zaidi ya Sh4.8 bilioni kwa mwaka.

Tayari Kampuni ya Meta (zamani Facebook) imetoa taarifa kwa wateja wake kuwa kuanzia Desemba Mosi, mwaka huu matangazo yatatozwa kodi ya VAT ya asilimia 18 ya thamani husika.

Jana akitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na X (zamani Twitter), Mbowe alisema kwa mtu aliyejielimisha kuhusu mapinduzi ya nne ya viwanda duniani, ataelewa kuwa mabadiliko haya yanaanza na biashara ndogo zinazoanza mitandaoni na hukomaa na kuingia kwenye mifumo rasmi baadaye.

“Muuza mitumba anayetafuta elfu mbili au tatu anatarajia kufungua maduka siku moja, anatumia mitandao kutangaza na kutafuta wateja, dalali wa nyumba na viwanja, wauza simu na vifaa vya umeme mfano ac, friji na makochi yaliyotumika.

“Wauza nguo na vitambaa, wauza chakula, siwezi kuwataja wote hapa ila itoshe kuwa mtandao ni ulimwengu halali uliopo na biashara inashamiri. Hii ni hatua ya kwanza kuelekea urasimishaji wa biashara,” alisema.

Alisema Serikali inayotoa kipindi cha mpito kulipa kodi kwa kampuni zenye mitaji ya mabilioni, ndiyo Serikali hiyohiyo imegoma kuwapatia wananchi wake ahueni.

“Vijana wengi ambao wamejiajiri kupitia mitandao ya kijamii, kuwatoza kodi kwa matangazo madogo wanavyofanya kutafuta wateja ni kung'oa mizizi ya biashara ambazo ndio kwanza zinachipukia,” alisema na kuongeza;

“Serikali hii inaendelea kujaza kodi kila sehemu huku ikishindwa kwa kiwango cha kutisha kuibiwa na kufanya anasa nyingi kwa kodi ambazo Watanzania wamelipa kwa jasho na damu na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali amethibitisha kwa miaka mingi.

"Kila upenyo unaoweza kuwa na manufaa kwa mwananchi wa kawaida kwao ni chanzo cha tozo na kodi, ndiyo maana ni ngumu kwa kijana kutoboa kwa jitihada zenu binafsi,” alisema Mbowe.

Katika kuhitimisha andiko lake, Mbowe alisema Serikali imechoka, imeshindwa kuendesha nchi, na njia pekee ni kuipumzisha mwaka 2025 ili tutoe fursa kwa viongozi mbadala kupitia chama kilichojipambanua bila kuogopa kubaguliwa, kuteswa, kudhalilishwa na kuogopwa, viongozi wanaojua shida za nchi na kuthamini mchango wa kila mmoja wenu kwenye kuleta mabadiliko chanya kwa nchi yetu.

Hata hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi alipoulizwa na Mwananchi jana kuhusu mtazamo huo wa Mbowe, alisema hayo ni maoni yake, huku akieleza masuala yote yanayohusiana na vyombo vya habari, ikiwemo mitandao ya kijamii yatagusiwa na ripoti ya kamati ya kutathimini hali ya uchumi wa vyombo vya habari.

“Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye mwishoni mwa mwezi Novemba na ripoti itaangazia mambo yote hayo tuwe na subira,” alisema

Gazeti hili lilizungumza na muuza kompyuta wa Dar es Salaam, Peter Cyril aliyesema mitandao hiyo inakuza biashara na wanaofanya shughuli hizo kwa asilimia kubwa hawana mitaji mikubwa, hivyo kiasi kile kidogo walichonacho kupitia mitandao wanawafikia wateja bila kuwa na ofisi.

“Ukisema mtu huyo atoe kodi na bado unatafuta ujikomboe kiuchumi ulipe kodi ya pango, mtandao inakuwa haijakaa sawa, mamlaka ziangalie namna gani zinaweza kukusanya kodi kwenye bidhaa kupitia mifumo ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA),” alisema

Naye Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk Timoth Lyanga alisema anachokisema Mbowe si sahihi kusema kutawadidimiza vijana, isipokuwa mfumo huo unalenga kuwajenga wajue wajibu wao.

“Wanapaswa waweze kuwajibika kulijenga Taifa lao kupitia vyanzo vyao na mikono yao, kusipojengwa kwa taifa la namna hiyo tutaendelea kuwa ombaomba,” alisema.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Sayansi ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Abel Kinyondo alisema kutokana na umuhimu wa kodi katika uchumi wa nchi, kinachotakiwa si kuwapa muda bali kunapaswa kutengenezwa usawa.

“Tusiseme kwa sababu anaanza kufanyabiashara asilipe kodi ni lazima kuwekwe utaratibu kuonyesha kiasi fulani anayeanza na bahati mbaya nchi yetu wanaolipa kodi ni wachache na ni waliopo kwenye mfumo rasmi,” alisema.

Mwananchi
 
Walipe Kodi au tozo Kwa sababu wamepunguziwa hela ya kujisajili sana Sasa Kwa nini wasilipie Kodi?

Hii tabia inayoanza kuzuka kudhani kwamba Kuna watu Fulani wanatakiwa kulipa Kodi Ili wengine wale ikome mara Moja.

Kila mtu alipe Kodi kulingana na urefu wa kamba yake.
 
Serikali imewekeza nini Facebook mpaka itake tozo huko?
 
Mwenyekiti wa Chadema Mbowe anesema Tozo/Kodi inayotarajiwa kuwekwa kwenye Matangazo ya Facebook itawapunguzia Vijana Kipato na Fursa za Kujiajiri.

Mbowe anesema Maisha ya Vijana wa Tanzania ni ya kuungaunga hayana Afya yoyote hivyo ni vema Serikali ikawaangalia kwa jicho la Huruma.

Jumaa Mubarak 😀
Mbowe ni mlipa kodi mzuri hivyo anajua anachokiongea
 
Sio swala la kuwekeza Facebook bli ni swala la Kila anaeingiza kipato ndani ya mipaka ya JMT anatakiwa kulipa Kwa shughuli yeyote.

Vinginevyo hamia Facebook utoke Tzn hapa maana naona unaongea ujinga as if hutumii Huduma za Tanzania.
Huduma karibia zote watu wanalipia pesa moja kwa moja na pia bado wanalipa kodi kwa kila bidhaa wanayonunua. Hapo bado hatajazungumzia madini, bandari, vitalu vya uwindaji n.k
 
1700205155579.png

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kitendo cha Serikali kukusudia kuanza kuwatoza kodi wafanyabiashara wanaoweka matangazo madogomadogo mitandaoni kusaka wateja ni kuwarudisha nyuma kiuchumi.

Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni miezi michache imepita tangu Serikali kutangaza kufanya mabadiliko ya sheria ya kodi ili kuruhusu kukusanya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilima mbili hata kwa kampuni zisizo na ofisi nchini.

Kampuni zinazotoa huduma za kidijitali nazo zitaguswa na utaratibu huo utakapoanza kutekelezwa.

Kulingana na tangazo hilo lililotolewa na Serikali Julai mwaka huu, kodi hizo zitaiwezesha Serikali kukusanya zaidi ya Sh4.8 bilioni kwa mwaka.

Tayari Kampuni ya Meta (zamani Facebook) imetoa taarifa kwa wateja wake kuwa kuanzia Desemba Mosi, mwaka huu matangazo yatatozwa kodi ya VAT ya asilimia 18 ya thamani husika.

Jana akitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na X (zamani Twitter), Mbowe alisema kwa mtu aliyejielimisha kuhusu mapinduzi ya nne ya viwanda duniani, ataelewa kuwa mabadiliko haya yanaanza na biashara ndogo zinazoanza mitandaoni na hukomaa na kuingia kwenye mifumo rasmi baadaye.

“Muuza mitumba anayetafuta elfu mbili au tatu anatarajia kufungua maduka siku moja, anatumia mitandao kutangaza na kutafuta wateja, dalali wa nyumba na viwanja, wauza simu na vifaa vya umeme mfano ac, friji na makochi yaliyotumika.

“Wauza nguo na vitambaa, wauza chakula, siwezi kuwataja wote hapa ila itoshe kuwa mtandao ni ulimwengu halali uliopo na biashara inashamiri. Hii ni hatua ya kwanza kuelekea urasimishaji wa biashara,” alisema.

Alisema Serikali inayotoa kipindi cha mpito kulipa kodi kwa kampuni zenye mitaji ya mabilioni, ndiyo Serikali hiyohiyo imegoma kuwapatia wananchi wake ahueni.

“Vijana wengi ambao wamejiajiri kupitia mitandao ya kijamii, kuwatoza kodi kwa matangazo madogo wanavyofanya kutafuta wateja ni kung'oa mizizi ya biashara ambazo ndio kwanza zinachipukia,” alisema na kuongeza;

“Serikali hii inaendelea kujaza kodi kila sehemu huku ikishindwa kwa kiwango cha kutisha kuibiwa na kufanya anasa nyingi kwa kodi ambazo Watanzania wamelipa kwa jasho na damu na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali amethibitisha kwa miaka mingi.

"Kila upenyo unaoweza kuwa na manufaa kwa mwananchi wa kawaida kwao ni chanzo cha tozo na kodi, ndiyo maana ni ngumu kwa kijana kutoboa kwa jitihada zenu binafsi,” alisema Mbowe.

Katika kuhitimisha andiko lake, Mbowe alisema Serikali imechoka, imeshindwa kuendesha nchi, na njia pekee ni kuipumzisha mwaka 2025 ili tutoe fursa kwa viongozi mbadala kupitia chama kilichojipambanua bila kuogopa kubaguliwa, kuteswa, kudhalilishwa na kuogopwa, viongozi wanaojua shida za nchi na kuthamini mchango wa kila mmoja wenu kwenye kuleta mabadiliko chanya kwa nchi yetu.

Hata hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi alipoulizwa na Mwananchi jana kuhusu mtazamo huo wa Mbowe, alisema hayo ni maoni yake, huku akieleza masuala yote yanayohusiana na vyombo vya habari, ikiwemo mitandao ya kijamii yatagusiwa na ripoti ya kamati ya kutathimini hali ya uchumi wa vyombo vya habari.

“Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye mwishoni mwa mwezi Novemba na ripoti itaangazia mambo yote hayo tuwe na subira,” alisema

Gazeti hili lilizungumza na muuza kompyuta wa Dar es Salaam, Peter Cyril aliyesema mitandao hiyo inakuza biashara na wanaofanya shughuli hizo kwa asilimia kubwa hawana mitaji mikubwa, hivyo kiasi kile kidogo walichonacho kupitia mitandao wanawafikia wateja bila kuwa na ofisi.

“Ukisema mtu huyo atoe kodi na bado unatafuta ujikomboe kiuchumi ulipe kodi ya pango, mtandao inakuwa haijakaa sawa, mamlaka ziangalie namna gani zinaweza kukusanya kodi kwenye bidhaa kupitia mifumo ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA),” alisema

Naye Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk Timoth Lyanga alisema anachokisema Mbowe si sahihi kusema kutawadidimiza vijana, isipokuwa mfumo huo unalenga kuwajenga wajue wajibu wao.

“Wanapaswa waweze kuwajibika kulijenga Taifa lao kupitia vyanzo vyao na mikono yao, kusipojengwa kwa taifa la namna hiyo tutaendelea kuwa ombaomba,” alisema.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Sayansi ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Abel Kinyondo alisema kutokana na umuhimu wa kodi katika uchumi wa nchi, kinachotakiwa si kuwapa muda bali kunapaswa kutengenezwa usawa.

“Tusiseme kwa sababu anaanza kufanyabiashara asilipe kodi ni lazima kuwekwe utaratibu kuonyesha kiasi fulani anayeanza na bahati mbaya nchi yetu wanaolipa kodi ni wachache na ni waliopo kwenye mfumo rasmi,” alisema.
 
Mbowe anaacha kumuunga mkono Mwabukusi kupigania katiba mpya kivitendo,anakuja kupick easy fight ya tozo ya matangazo.

Haya madogo hayawezi kuisha hadi kubwa lao la katiba mbovu lipatiwe ufumbuzi.
Harakati za kodi na tozo ndio raia wengi wanaweza kuelewa kuliko mambo ya katiba.
 
Kuendekeza wanyonge ndo sababu nchi haiendelei.
Watu walipe kodi
Kumtoza kodi mnyonge na masikini ni kuendeleza umasikini. Nchi haindelei kwa sababu watu hawawezi kukuza biashara zao kwa kasi.
 
Huduma karibia zote watu wanalipia pesa moja kwa moja na pia bado wanalipa kodi kwa kila bidhaa wanayonunua. Hapo bado hatajazungumzia madini, bandari, vitalu vya uwindaji n.k
Na hiyo walipie kwani hawaingizi kipato?
 
Back
Top Bottom