Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango wakati anawasilisha Bajeti ya 2023/2024 amesema kutokana na ukuaji wa teknolojia, biashara nyingi zinafanyika mtandani na hivyo matangazo yanayofanywa kukuza bishara hizo kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook, Twitter na blogs mbalimbali imekua maradufu.
Kutokana na hayo, Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi, inatarajia kuanzisha mfumo wa kidijitali wa kufuatilia na kuhakikisha kodi husika za Serikali zinalipwa kwa wakati. Hii itajumuisha matangazo ya Biashara ambayo huwekwa na watu maarufu (digital influencers) na biashara za mtandaoni zinazofanyika nchini.