Mzee Mwanasiasa,
Heshima mbele, nimezisoma kwa makini hoja zako na za Katibu tarafa,
(1). Nimeridhika na majibu kuhusu "HISIA ZA UKABILA", kwa mtu kama wewe ambaye sio kada wala mpenzi wa chama hicho, ni maneno mazito sana nafikiri mwenye macho ameyaona maswali yangu na majibu yako on ukabila, sasa ni uamuzi wa wananchi, lakini mimi nimeridhika nayo.
(2). CCM tunao utaratibu wa kuuuliza maswali, lakini katiba yetu inatubana kuuliza kwenye vikao rasmi vya chama chetu kwa mujibu wa katiba zetu, ndio maana huwa hatusutani kwenye vyombo vya habari kama Mbunge Zitto alipoamua kupumzika, tunafahamu kuwa chama kilisoma kwenye media zetu, hakukuwa na kikao cha yeye kueleza uamuzi wake, na kutolewa to the public na msemaji wa chama au wa mwenyekiti, kama Mwingira, sijui huko upande wa pili msemaji wa chama ni nani?
(a). CCM tuna utaratibu mzuri wa kusema machungu yetu na kusikilizwa na viongozi wa juu na wa serikali yetu, na kufanyiwa kazi kwa mfano nitaaanza na ya awamu ya nne kwanza,
- Balozi wetu wa zamani huko Italy, alipatikana na tuhuma za kuhusika na ubadhirifu wa pesa za walipa kodi, yaani wananchi, wewe na mimi, katika kikao cha kwanza kamati kuu ya CCM kilichofanyika Ikulu Dar Mwenyekiti wa CCM alishambuliwa na wanakamti kuhusu kitendo hicho cha balozi, na wiki iliyofuatia mwenyekiti huyo ambaye pia ni rais wa jamhuri, alimfukuza kazi balozi huyo na aliporejea nyumbani balozi huyo alifunguliwa mashitaka rasmi na serikali ya jamhuri, na kesi hiyo bado inaendelea, hii ni pamoja na CCM kuheshimu "The Rule of Law" ishu ambayo hata wenzetu Zimabbwe majuzi wamekumbushwa na the Mighty South Africa's Government, kuheshimu hilo, sisi CCM hatuna tatizo na hilo!
-Wabunge wa CCM walipokuja juu sana kuhusu Richmond, serikali ya CCM ya awamu ya nne haikusita kuwaondoa mara moja wale wote waliohusika kutoka katika madaraka yanayohusika na masuala ya umeme na richmond, that is leadership yaani "rapid response" as opposed na maneno ya mnadani kwenye nyama, hiyo ni spinning at its best!
-Majuzi taifa letu limeshudia ishu ya Manji/Mengi ikitatuliwa bungeni bila ya woga, tumejionea spika wa bunge letu akitoa uamuzi wa haki kwa kufuata maoni ya wabunge wawili Anna Kilango/Sendeka (CCM) waliokuwa minority katika kamati ya bunge iliyokaa kama mahakama, na spika huyo hakuishia hapo tu ameikabidhi PCB tume ya kuzuia rushwa kulishughulikia suala hilo kwa mujibu wa sheria nchi yetu, Mengi ndiye aliyekuwa na haki katika kesi hiyo ambayo mbunge Malima alishindwa kuthibitisha madai yake kwamba Mengi hujipendela kwenye TV zake na kudharau viongozi, hujiweka dakika kumi na kuwapa viongozi wakuu wa nchi dakika moja au sekunde, baada ya tepu kuonyeshwa ndani ya bunge ikagundulika kuwa ni uongo, pamoja na mbinu zote zilizofanywa na kiongozi mmoja wa juu wa CCM ku-pre matokeo on Manji behalf, haikuwezekana, kwetu CCM sheria ni msumeno CCM,
nenda IIP uuulize siku ya hukumu kutolewa na spika jinsi Mengi na wafanya kazi wake walivyolia kama watoto, maana walikuwa na mawazo kama yako kuwa uamuzi utategemea njama zilizofanywa na kiongozi huyu mkuuu mmmoja wa CCM, CCM tunaheshimu haki za wananchi hata kama ni Mengi! na tunaheshimu mawazo ya wabunge wetu hata kama ni wawili against wenzao, muulize Mzee Ndesamburo, jinsi moto ulivyokuwa ukiwaka ndani ya vikao hivyo vya mahakama,
(3). Kuhusu swali langu la mwisho ninakubali kuwa ni tooo broad kujibiwa kwa mara moja, hivyo ninakupa the benefit of the doubt, lakini as we go on tutaendelea kuuulizana zaidi.
Mzee Katibu Tarafa,
Heshima yako mkuuu, maneno yako mazito ingawa kuna sehemu flani ni misguided, kwa mfano CCM kutumia a goodwill ya the past chama kimoja, hapana si kweli maana kuna wabunge wa upinzani kama Mheshimiwa Dr. Slaa wameweza kuishinda CCM, tena kwa kura nyingi, pamoja na hiyo gooodwill kuwepo, Mheshimiwa Kabwe Zitto pia ameidhinsa CCM, kwa hiyo hoja ina walakini ndugu yangu, ingawa umeitoa kwa nia njema kabisa I can see that.
But, on the other hand una a valid point kwenye "wananchi wenye uwezo mdogo wa kujua nini maana ya mfumo wa vyama vingi", lakini again hiyo haiwezi kuwa the final authority on the ishu kwa sababu bado unahitaji kufafanua how wananchi waliweza kuichagua CUF kule Pemba yote under hiyo circumstances za uwezo mdogo wa kuelewa, na pia waliwezaje kuwachagua kina Dr. Slaa na Zittto, kwa sababu ni understatement kusema kuwa wananchi wa Kigoma, Mbulu, na Pemba ndio peke yao wenye uwezo mkubwa wa kuelewa mifumo ya vyama vingi, katika Tanzania, otherwise heshima zangu za dhati kwa uwezo wako mkubwa wa kujadili taifa letu.
Kwa wenzangu wengine samahani, muda wa kujibu hoja za pua hatuna tena, halafu forum ni forum, na redio ya mwanforum sio ya forum tusichanganye mambo, mpaka tutakap[oambiwa officially, kuwa hiyo redio ni part ya hii forum!
Mzee Lunyungu, kama kawaida heshima mbele bro, RESPECT, wengine tupunguze hasira life is too good!
Ahsanteni Ndugu Zangu! Tutaonana kesho majaliwa!