Mbowe na tafakuri zake...

Eric Ongara

Senior Member
Sep 19, 2006
165
8
Tumegeuka taifa la vipofu
Freeman Mbowe

KWA wengi, nimekuwa kimya. Kimya kina tafsiri nyingi. Kila mtu kwa uelewa wake na pengine matamanio yake. Leo nimeamua kuandika tena. Na nitaendelea kuandika "mpaka kieleweke." Nakiri ni muda mrefu sijaandika. Sababu ni nyingi. Naamini katika subira.

Naandika kwa mara ya kwanza kupitia vyombo vya habari - baada ya Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2005. Nilishiriki kama mgombea urais. Nilipigana, niliumia lakini jumla ya kura haikuniwezesha kuongoza nchi.

Sijutii ushiriki wangu. Naushangilia na kuuona kama mchango wangu wa ‘damu' kwa Watanzania wenzangu wa leo na kesho. Nimekomazwa na kuimarishwa katika dira, dhamira na hata mbinu za harakati.

Kwa wenye dhamira safi, uchaguzi una malengo mawili ya msingi. Yote ni sehemu ya mchakato wa harakati. La kwanza ni nia ya kupewa ridhaa ya kuongoza na la pili ni fursa ya kufikisha mawazo na fikra mbadala kwa wale wanaoombwa ridhaa husika. Naamini ujumbe ulifika japo haujatosha.

Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kushiriki uchaguzi ule. Nawashukuru wale wa chama changu walioniamini na kunitwisha msalaba ule. Watanzania wengi walinisikiliza – kwenye mikutano na kwenye vyombo vya habari – nawashukuru kwa subira yao!

Wako walioniombea usiku na mchana! Wako walionisaidia kwa hali na mali zao! Wako walionipa kura zao (zilizohesabiwa na zilizoyeyuka). Nawapa asante sana na nawaombea sana kwa Mwenyezi Mungu kwani sina uwezo wa kulipa fadhila na upendo wao kwangu.

Wako niliowakwaza ama kwa kauli au kwa vitendo katika mchakato ule! Nawaomba wanielewe! Naam, wako walioninyima kwa sababu mbalimbali za haki na zisizo. Hawa nao nawatakia heri! Wako walioniibia kura zangu! Hawa …..!

Nilishiriki kupokea matokeo yaliyomtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi. Nilimpongeza Kikwete kwa kumkumbatia. Niliwachanganya wengi, hasa wale wengi jasiri walioumia na walioshuhudia uhuni wa kutisha kutoka kwa mamlaka zilizopewa wajibu wa kusimamia haki, amani na usalama kwenye chaguzi na hata maisha yetu ya kawaida. Ni kweli rafu ilichezwa sana – hata Kikwete na timu yake wanajua uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Si Kikwete wala wenzake wenye ujasiri wa kulikiri hili.

Nilipata moyo huo kwa sababu moja tu: Naipenda nchi yangu! Naamini katika mabadiliko ya mbinu na mazoea. Naamini katika subira. Utamaduni wa kukubali matokeo ni mojawapo ya mbinu za mapambano.

Kuna msemo wa Kiingereza unaosema "to retreat is not to surrender but rather, a war strategy", yaani "kurudisha majeshi nyuma si ishara ya kujisalimisha bali ni mkakati wa kivita." Niliamini kuwa mabadiliko ni mchakato, na mchakato ni tunda la muda!

Sawa, tuliibiwa, lakini tuna sababu ya kukiri pia kuwa tulikuwa na udhaifu wetu uliosababisha tukaibiwa! Hili nitalijadili siku za usoni!

Siku ya kupokea matokeo pale Diamond Jubilee, kundi kubwa la wanahabari lilinivaa na kunihoji: "Mheshimiwa Mbowe, kwa matokeo haya huoni kuwa wapinzani mmeshindwa sana?" Nilifadhaishwa na swali hili na nakumbuka kujibu: "Kwanza mimi si mheshimiwa ila ni kamanda…. Wa kujuta kwa matokeo haya siyo wagombea na viongozi wa vyama vya upinzani pekee, bali ni Watanzania wote…… Wana CCM wengine wanashangilia bila kujua msiba huu unawahusu ….. pengine wenye sababu ya kushangilia ni kundi dogo la viongozi wa CCM, serikali yake iliyopita na inayokuja na washirika wao ambao wana hakika ya hifadhi ya uchafu wao na mwendelezo wa ufisadi wao wakitumia mgongo wa mfumo wa vyama vingi."

Baada ya kauli ile, wanahabari wengi walitawanyika kwani wengi wao nao walikuwa katika mkumbo wa ulevi wa ushindi wa Kikwete na CCM. Wengi hawakujua kuwa, baadhi yao wameibaka taaluma na hivyo nchi. Walikuwa wamemaliza kazi ‘waliyotumwa' na hivyo wana sababu ya kukaa mkao wa kula! Wengi walijiona na wengine bado wanajiona sehemu ya utawala!

Leo zaidi ya mwaka umepita baada ya uchaguzi – wengine wanasema haukuwa uchaguzi bali ‘mnada wa kura.' Hukumu ya kama neema imeonekana nawaachia Watanzania. Mengi yanasemwa lakini moja linaendelea kunisononesha. Watanzania wengi wanauliza "Wapinzani wako wapi? Mbona kina Mbowe na wenzake hatuwasikii?

Maovu mengi yanafanyika mbona wao wamekaa kimya?"

Ukweli ni kuwa hawajakaa kimya. Wapinzani wamesema na wanasema sana, ila watawala, na baya zaidi Watanzania walio wengi bado wanawasaliti!

Watanzania wenzangu! Hata wapinzani ni binadamu wenye kupata maumivu na mfadhaiko. Kuna makundi mengi ya wanaharakati yanayopigania haki na ustawi katika nchi yetu. Najipa ujasiri kusema katika makundi yote haya, kundi la vyama vya upinzani (pamoja na kuwapo ‘waganga njaa' miongoni mwao) limejitoa mhanga kuliko makundi mengine yote!

Wengine wanadai kufanya siasa za upinzani Tanzania ni lazima uwe na ‘uendawazimu' kidogo. Hii ni kutokana na mazingira magumu ya maisha ya kiuchumi na kijamii kwa wengi yanayoambatana na harakati hizi.

Pamoja na upungufu wake, viongozi wa upinzani ni watu wenye kuhitaji kuungwa mkono na kusaidiwa mzigo huu na jamii. Jamii ina wajibu wa kututia moyo na siyo kubeza! Maisha yetu na familia zetu tumeyaweka rehani na kila siku kukicha salama tunamshukuru Mungu!

Kosa letu nini? Kutetea haki na ustawi katika nchi yetu na watu wake wakiwamo hao waliogeuzwa mawakala wa kutudhalilisha! Ninawaheshimu wote wenye mamlaka ya uongozi wa taifa letu. Kamwe sitasita kuwapongeza wafanyapo mema.

Hata hivyo, nakataa kufanywa kondoo. Nakataa kuwa mnafiki. Nakataa kubariki dhuluma, wizi, ufisadi na unafiki unaofanywa na wengi tuliowapa dhamana ya kuongoza maisha yetu ya leo na hata vizazi vijavyo.

Mbali na wajibu tuliopeana kikatiba, kwa kuwa katika nchi moja, yaani jamii moja tuna mkataba wa asili ambao wanafalsafa wanauita ‘social contract.' Kwa social contract hii, sisi kama Watanzania tumekubali kuachia baadhi ya uhuru wetu asilia na kukubali kutii mamlaka (na hivyo sheria) tukitegemea kuwa kwa kufanya hivyo, mamlaka itatuwezesha kupata uhuru zaidi unaoambatana na haki na ustawi.

Uchaguzi leo umekwisha lakini maisha yetu hayajakoma. Lazima tuendelee kujiuliza kama wale tuliowapa dhamana ya kutuongoza wanatekeleza wajibu wao kama sehemu ya ‘social contract' hii.

Mimi kama Mtanzania na zaidi kama kiongozi ninayeongoza kundi kubwa la Watanzania ni wajibu wangu kuendelea kuhoji utekelezaji wa ‘social contract' baina ya wananchi na viongozi. Naelewa hautakuwa ujumbe mzuri kwa wale wenye madaraka! Harakati ni zoezi la kudumu hasa pale haki inapokuwa inahubiriwa kinafiki kwa maneno lakini inabezwa kwa matendo na watawala.

Najua wengi wataingiwa hofu na maneno haya! Lakini sihitaji kujikomba kwa yeyote. Ndiyo, mimi si malaika au mtakatifu. Kama binadamu wengine, nami nina udhaifu wangu, lakini hauondoi ukweli na umuhimu wa kuhoji utendaji na dhamira ya wale wanaotuongoza. Kufanya hivyo ndiyo kuendeleza unafiki uliotufikisha Watanzania tulipo! Najua wengine watasema Mbowe anafanya kazi ya uchochezi! Ni kweli, sina sababu ya kukataa ukweli huu.

Sioni sababu ya kutochochea Watanzania waamke, wajijengee ujasiri kudai haki badala ya kuendelea kuiomba na kuona kuwa ni fadhila! Tuna sababu gani ya kutii mamlaka kama haitelelezi sehemu yake ya mkataba?

Utawala uliopatikana kwa njia chafu utatawala hivyo hivyo. Waliojitwalia madaraka kwa kutumia vibaya sheria (safi na chafu); vyombo vya dola yakiwamo majeshi ya ulinzi na usalama na hata usalama wa taifa; tume isiyo huru na isiyo ya haki; fedha za ufisadi; utajitakasa vipi kutenda yaliyo mema bila kukiri uharamia uliotumika kwenye uchaguzi?

Hivi kweli kiongozi mwadilifu anaweza kujisifu kwenye ushindi mchafu? Nina hakika viongozi wetu nao wanapenda kusifiwa. Sina hakika ni wangapi wanaambiwa ukweli kavu kavu kama huu! Mimi nitawaambia na maisha yangu nayakabidhi kwa Mungu!

Nchi inafadhaisha. Viongozi wanashangilia umaskini wetu na ujinga unaotujengea woga na hofu! Watanzania tunajengwa kuwa tegemezi kwa serikali kifikra na kiuchumi. Tumefungwa mnyororo wa fikra! Bado tuna usingizi wa kudhani Kikwete na Lowassa ndio wana ufunguo wa suluhisho la matatizo yetu! Ndiyo sababu kila kukicha utasikia "serikali itusaidie lile, Kikwete tukomboe, Lowassa tupia jicho lile!' Eti wanaombwa wakati ni wajibu wao kujua.

Tabia ya kutukuza viongozi na serikali imeendelezwa hata bungeni. Utasikia wabunge "tunaiomba serikali…., tunamwomba waziri n.k.'' Tumejikabidhi jumla kama makinda! Kikwete anapeta Ulaya sisi tunamngojea! Siku akirejea, mawaziri kazi hawafanyi – wote wakiongozwa na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, mawaziri, mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, meya na wengine kibao lazima waache kazi, wachome mafuta ya misafara ya magari wakajipange uwanja wa ndege kumpokea ‘messiah' mwenye muarobaini wa matatizo ya Watanzania!

Huu ndiyo unafiki na ukondoo na si itifaki wala nidhamu! Ni udhaifu unaoukuta nchi za Afrika tu! Leo kuna watu wazima tena wasomi wanaamini bila CCM hawawezi kuishi! Nani kasema bila CCM hakuna maisha? CCM ya nini kama imeshindwa kutekeleza wajibu wake katika ‘social contract?'

Tupende tusipende, katika jamii yoyote kuna matabaka ya watu. Daraja la juu, la kati na la chini. Mara nyingi Tanzania tunajidanganya, hatuna matabaka haya! Pengine liliwezekana kidogo enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Daraja la juu leo lina viongozi wa juu serikalini, washirika wao ambao ni wafanyabiashara wakubwa na hasa wawekezaji wa nje. Katika nchi yetu, kundi hili ni dogo sana na nina diriki kusema halifiki watu 250! Katika nchi yoyote, kundi hili ndilo hufaidi nchi na lenye neema. Halipendi mabadiliko kwani tayari uzuri au ubora uliopo kwao ni neema!

Daraja la kati (working class) ndiyo mara nyingi huleta mabadiliko katika nchi. Kundi hili hujumuisha viongozi wa dini, wasomi – yaani wanataaluma mbalimbali, watumishi wa serikali (civil servants), viongozi wa kijamii wakiwamo waandishi wa habari - (civil society), viongozi wa kisiasa (political leaders) na wafanyabiashara wa kati.
 
Hili ndilo kundi linalotoa viongozi na lenye uwezo wa kuitayarisha jamii kuleta mabadiliko! Kwa nchi yetu kundi hili ni la wastani, pengine linaweza kufikia Watanzania laki mbili.

Kundi hili lina uhakika wa mlo. Lina uelewa wa kutosha. Kwa idadi ya nchi yetu, ni kundi lililostahili kuwa kubwa zaidi. Lingestahili kufikia Watanzania milioni 10. Hii ni sehemu ya umaskini wetu wa kujitakia ambao wengi wa kundi hili hawaelekei kuujutia.

Kundi la mwisho ndilo la Watanzania walio wengi. Hawa ndio sehemu kubwa ya Watanzania wenzetu, wengi wao wakiishi vijijini (wakulima na wafugaji) na wengine wao sasa wamekimbilia mijini wakitafuta ‘hifadhi’ ya maisha. Maisha yao ni ya mlo hadi mlo! Ukweli hawa ni wote waliobakia. Hawa ‘wamepigika’ kweli kweli na ni wa kuonea huruma na ndio wanaostahili kupiganiwa!

Kundi hili halina fedha, lina nguvu ya kutisha. Nguvu ya uasi au ya kura! Leo linatumiwa vibaya, iko siku litatumiwa vizuri ……!

Changamoto yetu kubwa leo ni kujiuliza kundi hili la kati liko upande gani katika kudai ustawi wa taifa letu?

Tatizo la Tanzania ni kuwa kundi hili mara nyingi limejivika hisia ya kuwa sehemu ya kundi la juu, ama kwa rushwa ndogo tu ya kujuana na viongozi, kupelekwa ng’ambo kwa kufuatana na Rais na kuitwa ‘wafanyabiashara’, ahadi za ajira na vyeo vya hapa na pale.

Hili ndilo kundi ambalo kwenye nchi za wenzetu, hutoa dira ya mwelekeo wa taifa na huwashikisha adabu viongozi mafisadi. Hawa huongoza harakati na kamwe hutegemei kundi hili liwe ndilo la upambe kwa watawala.

Kwa Tanzania kundi hili ndilo limesaliti vizazi vilivyopigania uhuru wa taifa hili na linaviponza vizazi vijavyo. Naomba nieleweke, wapo Watanzania katika kundi ili wanaotekeleza matarajio yao! Lakini ni wangapi?

Mara nyingi lawama zimetupwa upande wa ‘vyama vya upinzani.’

Jamii yetu yote leo inalalamika. Hata makada wa CCM – ambao awali walijiona washindi leo wanalalamika!! Viongozi wetu na washirika wao sasa wana haki ya kulewa sifa na fedha! Watanzania tumewalemaza! Sasa hawana hofu tena. Wana uhakika wa ‘amani na utulivu.’

Wamefanikiwa (japo kwa muda) kujijengea uhalali wa kuipeleka nchi kama wanavyotaka wao na washirika wao. Kilio cha wananchi sasa ni upepo wa kupita. Wanajiona salama kwa kuwa madarakani. Wapambe wao nao wanajisikia sehemu ya utawala!

Tumegeuka taifa la vipofu. Tumekuwa taifa lisilojua haki zake!

Tukutane wiki ijayo.

Source:http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/1/24/makala5.php
 
Nakubaliana na mambo Mengi Mbowe aliyosema dhahidi ili suala la viongozi wote kukimbilia uwanja wa ndege wakati mheshimiwa anaporudi jamani huu ni ukosefu wa kazi au upungufu wa akili ? Aingii akilini kwa viongozi wote wa serikali kukimbilia uwanja wa ndege kwenda kumpokea Rais kama anaenda kutoa posa .
 
Maisha bora kwa kila mtanzania bila kufanya kazi ni ndoto, ni kweli viongozi wetu wanapoteza muda mwingi sana kwa mambo yasiyo na manufaa, hata rais aitoka mwanza au kilimanjaro pale uwanjani ni utitiri wa viongozi, kaeni ofisini mfanye kazi tujenge nchi.

hawa jamaa wakikaa ofisini itapunguza na tatizo la foleni, kwani kila mara ving'ora, barabara zinafungwa kisa VP anakwenda uwanja wa ndege kulaki mheshimiwa, mara vingora tena PM nae huyo njia moja uwanjani, mnatutesa jamani kwani kila mpitapo shart barabara zifungwe kuwapisha watukufu mpite.
 
Ni kweli unafiki na njaa njaa ndizo zinazowaponza wengi hata wasomi ambao wanakubali kugeuzwa kasuku kuushangilia utawala mbovu.Halafu pia ujasiri hatuna watz i mean nidhamu ya woga imetutawala.Leo hii mtu amesoma lakini bado anaogopa kudai haki yake.Kama huku India watu wanasoma kwa mkopo lakini wanalazimishwa kusoma kozi flani na student minister wa hapo ubalozini.Anatishia eti MNADHAMINIWA NA SERIKALI HALAFU MNATUPANGIA CHA KUSOMA!!Rejea constitution yetu inasema vipi kuhusu elimu
 
Ni kweli unafiki na njaa njaa ndizo zinazowaponza wengi hata wasomi ambao wanakubali kugeuzwa kasuku kuushangilia utawala mbovu.Halafu pia ujasiri hatuna watz i mean nidhamu ya woga imetutawala.Leo hii mtu amesoma lakini bado anaogopa kudai haki yake.Kama huku India watu wanasoma kwa mkopo lakini wanalazimishwa kusoma kozi flani na student minister wa hapo ubalozini.Anatishia eti MNADHAMINIWA NA SERIKALI HALAFU MNATUPANGIA CHA KUSOMA!!Rejea constitution yetu inasema vipi kuhusu elimu


Sasa nyie ndo mnashida kweli kama mpaka mnachaguliwa msome nini! Kwani mlipoondoka nyumbani hamkujua mnaenda kusoma nini huko India? Kama mliingie mkataba na serikali kuwasomesha katika fani nanyi mlipofika huko mkabadilisha fani, hapo serikali ina haki ya kuwakaba koo na wala sio swala la constitution tena, ni mkataba wenu wa kusomeshwa unasemaje!
 
Manen haya ni mazito na si rahisi kusikia JK kakaa na kuandika mwenyewe mambo kama haya . Huyu Mbowe bwana basi tu ila jamaa anajua kwa nini alikuwa anagombea Urais .
 
Manen haya ni mazito na si rahisi kusikia JK kakaa na kuandika mwenyewe mambo kama haya . Huyu Mbowe bwana basi tu ila jamaa anajua kwa nini alikuwa anagombea Urais .


Huyu mbwa kama sio yeye basi ana washauri wazuri...huwa anapotoka hapa na pale lakini akipewa nafasi atapelekea Tanzania katika kupiga hatua kubwa kimageuzi. Mageuzi katika nchi yetu ni safari ndefu sana...mfano hapo juu amezungumzia matabaka hayo 3 kwa mmachinga wa uwanja wa karume ukimueleza hilo itakuwa ngumu sana kukuelewa. Nampa Mbowe hongera nyingi sana kwa kujaribu na kuendelea kujaribu. Namtakia kila la kheri one day..just one day wadanganyika watafunguka macho na kumuelewa.
 
Leo Mbowe kajibu hoja ya wengi kwamba wapinzani wako haya yanatokea Tanzania .Tunakimbilia kuandika hapa lakini mkiwa hapa TZ mkasikia maandamano hamtashiriki . Ws just ast week Wapinzani wamejitoma mtaani angalia ni wangali walio jitokeza kuwapa support.They still dream of changes chini ya JK na kusikiliza maneno ya Mzee Muhuni Makamba kachokla kabisa hata akili . Hao ndiyo ma Think tank wa CCM ambao tuna ambiwa wengine tumewaona wamelala pale uwanjani sasa sijui ule ndiyo U think tank wenyewe . Wengine wanaenda kupokea wageni uwanjani kwa jila la wana pesa na hao ndiyo ma think tank wa CCM. Kazi kubwa tunayo
 
Tatizo la Tanzania ni vyama vya siasa ambavyo havina strategy nzuri ya kuing'oa CCM kwenye madaraka. Inabidi viungane sasa kabla ya mwaka 2010 kwenye uchaguzi na kuondoa hii tamaa ya madaraka ya mmoja mmoja.
 
Ole vyama siasa ni nani ? Nini mchango wako katika kuiondoa CCM na kujaribu mtawala mwingine ? Jamani mbona Mbowe kasema hapo na mimi nasema Tanzania ni ya wote si si yale ama hao . Wewe unasimama wapi katika kusaidia kupata ukweli ?
 
Sasa ndio tunarudi pale pale unaniuliza mimi nini mchango wangu? Wewe mchango wako uko wapi? Vyama vya siasa ninaposema ni kwamba tayari vimeanza na wanapoungana ndio wengi wanaingia, shida moja wapo wengi kwenye vyama tofauti na wengine hatuna vyama lakini wakati wa uchaguzi tumo, kama mgawanyiko ndio huu hawa viongozi walafi hawatakwisha.

Kuandika hapo chini unajiunga na Chadema sio nyenzo ya kusema wewe una mchango mkubwa kuliko mimi. Na mpaka sasa hivi bila kuungana CCM ni vigumu kuiondoa.
 
Ole usiogope maandiko tafadhali . Kuingia kwenye Chama si kwamba mtu una haki sana zaidi ya mpenzi japokuwa utofauti upo ndiyo . Lakini naamini unaweza kusaidia zaidi Chama ama kitu ukiwa nje ya kundi .Mfano hapa JF tunamwaga nondo ambazo ni moto kushikwa na watawala wetu wa TZ ni msaada kwa taifa ka njia nyingine . Cause they hear us and let them know that we know their blunders nk .

Sheria ya kuungana vyama Tanzania haipo. Na wanategemea kuipeleka mwaka huu Bungeni kama sikosei . Pia nakubaliana nawe kwamba tuujenge upinziani uwavutie watu safi na wenye nia safi na TZ na si watu aina ya Tambwe na Nsanzugwako .

We are doing that now and the message is reaching them. Tuna kazi kubwa kuwafanya akina Mrema waelewe kwamba tuua vyama tuache vichache vyenye sauti ili tushike Bunge Urais tuwachie CCM. Waopinzani wakisha shika majimbo means Bunge basi tunaondoa mambo ya kuteaua Wabunge kama vile kuna uhaba wa Wabunge .

Tuendelee
 
Mwanasiasa Unauliza kama niko India peke yangu?Tupo wengi, ila peke yangu nimeamua kuufichua huu uozo.Hata hapa JF tupo wengi labda pengine itafikia muda kila mtu ataamua kujisajili kwani wengi ni wasomaji tu kama nilivyokuwa msomaji mimi
 
Muungano ni jambo lenye mantiki, lakini nikitafakari zaidi linaniumiza kichwa.Tukiungana kichwa kichwa bila malengo tutakua hatujafanya lolote, kuiondoa CCM ni jambo moja kuiletea Tanzania maendelo ni jambo jingine.

Lazima malengo yawe zaidi ya kuiondoa CCM. Chukulia CUF inajitambulisha kama chama cha Kileberali, CHADEMA social democrats(mlengo wa kati) NCCR naona wana mguso wa kijamaa sasa je wakiuangana hicho chama kitafuata sera zipi? Hatuoni kama tutakuwa tunadumaza uwanja mpana wa mawazo?Itapendeza tukiwa na vyama vinne au vitano imara, tuweze kufaidika na mawazo toka itikadi na falsafa mbalimbali.

Cha msingi ni jamiii ya kitanzania kuamka zaidi ya vyama kuungana. Hakuna haja kuilazimisha jamii kuchagua nyeusi na nyeupe tu, jamii itambue kuna nyekundu, bluu na kahawia pia.Tuondoe dhana ya uwili, CCM na upinzani, huu ni utupu.

Kunatakiwa kuwepo ushindani wa fikra, hoja nzito/sera mbadala.Tusitengeneze NARC nyingine Tanzania ambayo malengo yalikuwa kuondoa KANU, tuungane kama malengo, maono au itikadi zinauwiana na si kwa lengo la kuitoa CCM pekee. Hofu yangu ni kuwa, huu muungano wenyewe utakuwa ni ulafi, ya kwamba badala ya vyama vilivyoungana kujadali sera na mambo ya msingi ya kuliendeleza Taifa wakaishia kujadili majimbo mangapi wagawane, kila chama kitapata mawaziri wangapi badala ya kuanagalia sera za kuongoza hizo wizara, hii ni vurugu.

Ndio maana Mrema aliwahi kubeza muungano wa vyama akisema, vyama vya upinzani vikiungana vinaunganisha nini? Je kwa matokeo ya kura ya 2005,2000 na 1995 tukiunganisha kura za upinzani zingeweza kuiondoa CCM?

Tatizo la msingi liko kwa wapiga kura na mfumo mbaya wa uchaguzi(tume ya uchaguzi, katiba n,k).Haya ndio mambo ya kuyashambulia sasa.
 
Na ili jamii ya kiTanzania iamke, siyo kuwaachia wapinzani tu waende majukwaani. Uhamasishwaji wa jamii uanzie kwa ndugu, jirani, kaya, kata nk.

Wahamasishaji wawe ni wewe na mimi ambao tunakutana hapa kwenye forum na kupashana lipi ni jipya na ni nini kinatokea na tunabadilishana mawazo ya nini kifanyike.

Ni wachache katika jamii wanaoelewa mfumo mzima wa utawala, wachache mno wanaotambua kwamba pesa wanazofuja hawa tuliowapa kura ni mali yetu. Mishahara wapatayo hawa watawala inatokana na jasho letu. Hamasa ya kuwatoa usingizini katika hili inaweza kuleta matunda.

SAMBAMBA na hamasa,tupinge mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kuwa mtangazaji pekee wa matokeo ya uchaguzi. Kura zihesabiwe huko huko kwenye vituo vya kupigia kura ili zijumuishwe bila zengwe na mshindi ajulikane. Na ni wakati mwafaka wa tume hiyo kuwa na wawaklilishi wa upinzani.
 
A quick scan on Mr. Mbowe's article shows that Kikwete is mentioned 8 times, CCM 7 times and Serikali 8 times. CHADEMA? Not even once. That simple observation sums up the plight of the opposition and its leadership in the country. They spend lifetime talking about what others are doing or not doing instead of articulating their agenda.

For Mr. Mbowe, the number of women dying from childbirth is not important but the number of Ministers receiving the President at the airport from overseas visits. Petty politics unworth of the person who wants to be our President. Mr. Mbowe find it important to remind us that he was brave, and that aliwashangaza mamia alipomkumbatia JK pale Diamond Jubilee, but do not see that, for many of us, shortage of places in Secondary schools for our kids is what is pressing at the moment, and alternative strategy, from what the government is doing at the moment, is what we would welcome the most from him – not self-promotion rhetoric.

Sidhani kama hili ni kosa la kimkakati, nadhani ni suala la uwezo mdogo wa "kitafakuri". To say that you are representing an alternative view is one thing, and to actually do it is another. "Mawazo mbadala" zitabaki porojo tu.

For all the flight time in the helicopter, and the "shock and awe" that it brought to the peasantry, what has stuck in people's mind about CHADEMA's agenda ni u-majimbo. And how does CHADEMA account for that?: distortions by CCM. It is always about "them". In his article, Mr. Mbowe attributed his 2005 defeat to rigging! I can understand that because if you are dependent on those unsuspecting whites for your party funding, you have to create an impression that you come from a repressive African country where rigging is rampant! It fits their prejudices about Africa. Funny that Mr. Mbowe is making this accusation now and not immediately after the election. Coffers dried up?

I re-read the article again and again and was struck by the "u-mimi" tone in it. It is one thing for Mr. Mbowe to say anajenga Chama-Taasisi and it is entirely another matter for him to tame that humungous ego and see his 2005 shot at the Presidency beyond vanity, ambition and self-promotion.

One day, perhaps, the sort of our political leadership will be irrelevant in whether or not we prosper (look at the United States of America). But it is remarkable achievement for our democracy and openness that a person of Mbowe's background, education, abilities and indeed ethics, can pose as a potential leader of this country and actually get a platform. Or perhaps it is a mark of our naiveté.

One member here was so uncharitable as to see CHADEMA as a SACCOS. Come to think of it, that is a compliment. SACCOS has a purpose of collective development. CHADEMA has individuals bent on personal development. Mr. Mbowe speaks of a personal sacrifice he is taking in joining politics but he goes out to get a couple "drive-by" degrees. How can you be a student of Mwalimu, as Mbowe brands himself, without understanding sacrifice? Sacrifices is not about coming over from England, fly around the country for a week, call a press conference and flee back to London. You cannot speak in Mwalimu's tone but fail to emulate his hard political work in building the party (as he did when he handed over the reigns to Mzee Kawawa immediately after independence). That is sacrifice. For Mr. Mbowe, personal sacrifice constitutes negative articles about him on newspapers and not putting off efforts for personal enrichment by cutting off dubious business ties with the people he is condemning.

And what's with the class rhetoric in the article? Is it a new CHADEMA policy to drive a wedge between people based on where they work and how much they earn (Which is how Mr. Mbowe really defined his classes). So, the party of Mzee Mtei, capitalist par excellence, finds fault in having a group of people in the country with a lot of money. For me, this confusion is a result of Mr. Mbowe getting into politics without sufficient intellectual maturity. Even Issa Shivji wouldn't go that low in politics of classes. Mr. Mbowe, not all theories on politics you are currently reading have relevance to Tanzania. But then, this is politics – just as others take shortcuts to affix PhD after their names, others think they can score political points by regurgitating Hobbes after a binge of cramming in adulthood. This is college stuff and Mbowe did not go to college. But the desire to be seen as well read is evident. How intoxicated by eliticism!

Leaders do not emerge by chance. A spoiled kid, who failed in school, turned into a Disc Jockey – and then failed as an entrepreneur cannot, all over a sudden, find passion in running the country simply because there is an opportunity and simply because he is aggrieved that his generational peers are dropping crumbles for him from the spoils of their political power or connections. Public service is a lifetime commitment – it has to be in you, either as a volunteer or the President. Be afraid of a person who failed in everything else but think he has to be President to serve his country.

Shame that Mr. Mbowe did not, in his article, mention his 'thanksgiving tour' mikoani recently. You know why? Because it was a big flop. No media attention, no momentum, and, of course, no new agenda. And it is for this reason that he is branding his article as "breaking the silence". Mr. Mbowe, you were not silent: you toured the country, you had press conferences, you wrote here at JF. Breaking the silence is a lie. You were simply inaudible. And the problem is your stale, uninspirational, and hateful message - not the means you are using to convey it. Let us see how this new effort of weekly articles pans out.

Mbowe thought a smart way to use a helicopter this time is to circle around towns first and pull/push people to the rally grounds. People came – to look at the ride. But they would not be taken for a ride. Hate speeches, delivered as performances, are a turn-off to many Tanzanians.

Mr. Mbowe: if you really want to build your party, abandon your "drive-by" MBA course (yes, I know it is important to one-up Amina Chifupa), take a Landrover, a motorbike, a boat and travel around the country, and listen to the people, do not perform by showing-off your recently-acquired mastery of Plato to the peasantry. I know it is difficult to resist hearing yourself.

What is tragic about all this is that people seeking alternative direction for the country, which it seems to me are the majority here, have pinned their hope on a fake. Although it has happened before, with Mrema escaping scrutiny until he crumbled, the heartbreak and disappointment of a Mbowe melt will be crushing because first, as a person, he is a nice guy, secondly, he has managed to convince smart people that he is for real, and thirdly, he at least knows who Annete Benning is.

Finally, I can predict a response to this article: another hit-job by CCM. It is always about them! Mr. Mbowe, welcome to the Major League. You cannot expect to continue to be coddled in a virtual republic that most of your supporters live in.
 
Mugongo mugongo
Naona umeamka baada ya Mbowe . Ila nina swali .Ujumbe huu umelenga wazungu ama watanzania ? Ujumbe wa Mbowe utafika hadi kijijini kwetu na wako utaishia hapa hewani kwa wasomi .Vipi kutawaliwa na wazungu namna hii ?
 
Muungano ni jambo lenye mantiki, lakini nikitafakari zaidi linaniumiza kichwa.Tukiungana kichwa kichwa bila malengo tutakua hatujafanya lolote, kuiondoa CCM ni jambo moja kuiletea Tanzania maendelo ni jambo jingine.

Lazima malengo yawe zaidi ya kuiondoa CCM. Chukulia CUF inajitambulisha kama chama cha Kileberali, CHADEMA social democrats(mlengo wa kati) NCCR naona wana mguso wa kijamaa sasa je wakiuangana hicho chama kitafuata sera zipi? Hatuoni kama tutakuwa tunadumaza uwanja mpana wa mawazo?Itapendeza tukiwa na vyama vinne au vitano imara, tuweze kufaidika na mawazo toka itikadi na falsafa mbalimbali.

Cha msingi ni jamiii ya kitanzania kuamka zaidi ya vyama kuungana. Hakuna haja kuilazimisha jamii kuchagua nyeusi na nyeupe tu, jamii itambue kuna nyekundu, bluu na kahawia pia.Tuondoe dhana ya uwili, CCM na upinzani, huu ni utupu.

Kunatakiwa kuwepo ushindani wa fikra, hoja nzito/sera mbadala.Tusitengeneze NARC nyingine Tanzania ambayo malengo yalikuwa kuondoa KANU, tuungane kama malengo, maono au itikadi zinauwiana na si kwa lengo la kuitoa CCM pekee. Hofu yangu ni kuwa, huu muungano wenyewe utakuwa ni ulafi, ya kwamba badala ya vyama vilivyoungana kujadali sera na mambo ya msingi ya kuliendeleza Taifa wakaishia kujadili majimbo mangapi wagawane, kila chama kitapata mawaziri wangapi badala ya kuanagalia sera za kuongoza hizo wizara, hii ni vurugu.

Ndio maana Mrema aliwahi kubeza muungano wa vyama akisema, vyama vya upinzani vikiungana vinaunganisha nini? Je kwa matokeo ya kura ya 2005,2000 na 1995 tukiunganisha kura za upinzani zingeweza kuiondoa CCM?

Tatizo la msingi liko kwa wapiga kura na mfumo mbaya wa uchaguzi(tume ya uchaguzi, katiba n,k).Haya ndio mambo ya kuyashambulia sasa.



Bravo Ongara,

Kwa kuongezea tu, hivi vyama kwa sasa vinaweza kuungana katika kutoa elimu ya umma kuhusu mageuzi na kuweka mshikamano kwenye mabadiliko ya katiba. Malengo 2 muhimu short term kushikiza serikali ibadili katiba; long term kuelimisha umma kuhusu mageuzi.
 
Back
Top Bottom