Mbowe na tafakuri zake...

Mbowe na tafakuri zake...

Ibrah,
Karibu sana kijiwe hichi. Kama unavyojionea mwenyewe kuna wale wanaopenda kukata issues, na kuna wengine wenye husda wanaopenda kuwabeza na kuwakashifu wenzao.Ndivyo tulivyo, lakini karibu sana.
 
Duh!!

Watu wazima inabidi tukae kando na kuangalia mambo.... maana hamna la maana la kuchangia, From character assasination to kukata issues.
Tunawasoma...

FD
 
napenda kwanza kuweka record za mwanasiasa sawa kusema kuwa mgombea wa CUF tunduru Mazee Rajab Mazee ni mwanachama wa kawaida ni kuudanganya umma kwani Mazee ndio mkurugenzi wa blue guard CUF Taifa na anaishi Dar maeneo ya magomeni hivyo kusema kuwa hata makao makuu yake hajafika ni kudanganya ama kuupotosha ukweli kwa makusudi.
Mazee ndio nguzo ya ulinzi wa cuf muulize Tambwe atakuambia jinsi ambavyo mazee alimshughulikia hata akaupoteza ukurugenzi wake hadi kukimbilia ccm.
nitajadili yaliyojiri tunduru kwa kirefu kesho asubuhi.
 
naomba kuweka record sawa ili kumjibu mwanasiasa .
pamoja na ukweli kuwa huwa namheshimu sana mwanasiasa na mchango wake humu ni kuwa Mazee Rajab Mazee ni kiongozi wa ngazi ya Taifa cuf na huyu ni mkurugenzi wa kurugenzi ya ulinzi kule cufd.
pia ni nguzo ya cuf muulize Tambwe atakuambia jinsi mazee alivyomfukuzisha ukurugenzi wake na hivyo kusema kuwa ni mwanachama wa kawaida sio kweli.
Anaishi magomen dar na hivyo kusema hajafika hata makao makuu ya chama chake ni uwongo soma katiba ya cuf uone jinsi mkurugenzi wa ulinzi alivyo na nguvu kwenye vikao vyote vya chama.
ni mtu wa mwisho kushauri chama kuhusu viongozi wa kitaifa hivyo anaweza hata kumfanya Lipumba kupoteza cheo chake.
 
Mzee Mkuki,

Samahani mzee, heshima mbele nitakurudia maana nakiona kiporo changu hapo kwenye post yako kuna ishu za kuzikata, shughuli ndugu yangu zimenikaba lakini nitakurudia, subira kidogo lakini maneno yako mazito!

Wenzangu wengine hapo,

Yaaani huruma kweli, masikini ya Mungu!
 
Tanzanianjema: Nimesoma post zako mara tatu; nakubali mwenzangu hilo ni somo zito. Endelea kuelimisha, wenye macho na masikio wataona na kusikia!

Mswahili: Ndugu yangu kujigamba kuwa CUF ni bora zaidi ya CHADEMA ni kujiingiza kwenye mtego wa CCM wa kuhakikisha vyama vya upinzani vya upinzani havinawiri. Kama kweli wewe ni mwanachama wa CUF au chama chochote cha upinzani au kama nin mojawapo ya watu wanaopenda demokrasia ya vyama vingi ikuwe katika nchi yetu, hupaswi kuwa na mawazo haya. Sisi sote ambao ni wananchama wa vyama vya upinzani tunapaswa kuendelea kujiuliza ni kwa nini viongozi wetu hawataki kuunganisha nguvu japokuwa wanajua kabisa kuwa wakienda kwenye uchaguzi moja moja tutashindwa? Sasa badala ya kujiuliza maswali magumu, nawe umeingia kwenye mtego wa CCM wa kuvishindanisha vyama vya upinzani!

Sio siri kuwa vyama vya CUF na CHADEMA ndio vyama vikubwa vya upinzani kwa Tanzania sasa hivi. Lakini ni kweli pia kwamba hivi vyama vina udhaifu wa asili ambao ni kikwazo kikubwa katika kukua kwao. CUF wana dhambi ya asili kwamba ni chama cha udini na cha upemba. Sasa inawezekana hii sio kweli, lakini ndio taswira walio nayo. Nasi CHADEMA tuna dhambi ya asili kwamba hiki ni chama cha wachaga na kwamba ni cha kifamilia. Inawezekana pia kwamba hili sio la kweli, lakini ni ukweli pia kwamba hii ndio taswira ya chama chetu. Kwenye siasa taswira ya nje wakati mwingi ni muhimu kuliko kilichopo ndani! Kwa maoni yangu dawa moja kubwa ya kuvunja hizi dhambi za asili zinazokabili hivi vyama viwili ni kuunganisha nguvu. Kwa CHADEMA na CUF kuja pamoja, madai ya uislamu na ukabila yatakakuwa ndio mwisho wake. Kuendelea kutunishana msuli kwa hivi vyama hakusaidii zaidi ya kuthibitisha taswira iliyopo kwa jamii.

Kuna watu wengi wamekuwa wakidai kuwa eti hivi vyama haviwezi kuungana kwa kuwa vina itikadi, falsafa na agenda tofauti. Hili sio kweli. Ukisoma katiba na sera zao, vyama vyote viwili hivi ni vyama vya mlengo wakati ambao ni liberalism. Kuna kipindi vyama vyote pia huegemea kidogo katika mlengo wa kati kushoto. Ukiangalia falsafa zao pia zinafanana kwa kiasi kikubwa ukiacha mbwembwe za slogans.

Kwa hiyo kikwazo cha kuungana sio sera wala itikadi, bali ni ubinafsi na ushabiki wa kijinga wa baadhi ya viongozi na wanachama kama wewe Mswahili unayeshabikia kuwa eti CUF ina nguvu kuliko CHADEMA. Nguvu gani hizo wakati chama hakina mbunge hata moja katika majimbo zaidi ya 200? Are you serious au unafurahisha baraza? Hatuwasaidii viongozi wa vyama vyetu kwa kushabikia ujinga. Inakuwa ni ujinga zaidi pale ambapo ushabiki wa namna hii unafanywa na wanachama wa vyama vya upinzani. Unless Mswahili uniambie unafanya kazi ya CCM, nitakuelewa; vinginevyo nakuomba urudi nyuma kidogo, shika tama, then angalia haya mambo kwa sura pana. Kushindanisha vyama hivi viwili ni sawa na kushindanisha wagonjwa badala ya kuwatafutia dawa wapone ili wakashindane na mpinzani wao CCM!

Mwansiasa unajenga hoja vizuri na kwa ufasaha sana. Endelea na makamuzi mpaka kieleweke! Ila kwenye suala la muungano wa vyama natofutiana na wewe.

Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa wemekuwa na mtazamo kwamba vyama vya upinzani havifanyi vizuri katika chaguzi kwa sababu ya kutoungana! Kwa mtazamo wangu siamini kuwa muongano wa vyama vya upinzani ni suluhisho,bali ni kituko kingine kwenye medani za siasa Tanzania.

Muungano ni jambo lenye mantiki, lakini nikitafakari zaidi linaniumiza kichwa.Vikiungana kichwa kichwa bila malengo tutakua hatujafanya lolote, kuiondoa CCM ni jambo moja kuiletea Tanzania maendelo ni jambo jingine.


Lazima malengo yawe zaidi ya kuiondoa CCM. Chukulia CUF inajitambulisha kama chama cha Kileberali, CHADEMA social democrats(mlengo wa kati) NCCR naona wana mguso wa kijamaa sasa je wakiuangana hicho chama kitafuata sera zipi? Hatuoni kama tutakuwa tunadumaza uwanja mpana wa mawazo?Itapendeza tukiwa na vyama vinne au vitano imara, tuweze kufaidika na mawazo toka itikadi na falsafa mbalimbali.

Cha msingi ni jamiii ya kitanzania kuamka zaidi ya vyama kuungana. Hakuna haja kuilazimisha jamii kuchagua nyeusi na nyeupe tu, jamii itambue kuna nyekundu, bluu na kahawia pia.Tuondoe dhana ya uwili, CCM na upinzani, ndio na hapana, ukweli na uongo! huu ni utupu, ujinga, ukale na ujima! Jamii ya kisasa haitarajiwi kuwa na mtazamo chakavu kama huu.


Kunatakiwa kuwepo ushindani wa fikra, hoja nzito/sera mbadala.Tusitengeneze NARC nyingine Tanzania ambayo malengo yalikuwa kuondoa KANU pekee. Vyama viungane kama malengo, maono au itikadi zinauwiana na si kwa lengo la kuitoa CCM pekee. Hofu yangu ni kuwa, huu muungano wenyewe utakuwa ni ulafi, ya kwamba badala ya vyama vilivyoungana kujadali sera na mambo ya msingi ya kuliendeleza Taifa wakaishia kujadili majimbo mangapi wagawane, kila chama kitapata mawaziri wangapi badala ya kuanagalia sera za kuongoza hizo wizara, hii ni vurugu.


Ndio maana Mrema aliwahi kubeza muungano wa vyama akisema, vyama vya upinzani vikiungana vinaunganisha nini? Je kwa matokeo ya kura ya 2005,2000 na 1995 tukiunganisha kura za upinzani zingeweza kuiondoa CCM?


Tatizo la msingi liko kwa wapiga kura na mfumo mbaya wa uchaguzi(tume ya uchaguzi, katiba n,k).Haya ndio mambo ya kuyashambulia sasa. Vyama vya upinzani, jumuiya za kiraia na wananchi makini waunganishe nguvu zao kudai katiba na tume huru ya uchaguzi ili hatimae tuwe na uchaguzi wa kidemokrasia ifikapo 2010.
 
Mzee ES nasubiri majibu na maoni yako katika hili!!...Usiwe na hofu wewe piga mzigo, maana kazi ndo kipimo cha utu na maendeleo ya kweli -the secret of being ahead, is getting started-wahenga (wa kizungu) walisema.... Ila kweli kwa mtizamo wangu na upeo wangu mdogo wa kuielewa siasa ya nchi yetu...., siku ambayo CCM itaruhusu wagombea binafsi basi nitajua kweli CCM imedhamiria kujenga demokrasia ya kweli katika taifa letu (si taifa changa tena maana tuna nusu karne ya uhuru-atleast wa bendera!!
 
Hili bado sijalielewa.. kwanini tunapenda kuwadiscuss watu binafsi... tuulize alilala na nani, wapi, alikunywa nini, na msalani alienda wapi.. why why why!!!

HALI YAKO, BWANA KAKA! NAONA MZEE MAMO YAMEKUWA MAMBO LEO.

KATIKA UWANJA WA HENGA LEO AMEINGIA KIJARUBA.....KWA WATANI WANGU WA PWANI. VVIPI KAKA MWANAKIJIJI? IMEKUWAJE TENA.....

NAKUMBUKA KUNA SIKU , BWANA MMOJA JINA NIMELISAHAU ALIZUNGUMZIA KWAMBA WATU WENGI WANATAKA KUJUA HABARI ZA WATU. NA KAMA SINTOKOSEA ILIKUWA NI KATIKA TOPIC YA BWANA DITOPILE. ALIYEKUWA AKIJADILIWA ALIKUWA NI BWANA JAKAYA KIKWETE NA UHUSIANO WAKE NA BWANA DITTO .

ANGALIA LEO, LIMEGEUKA , BWNA KAKA!

NAOMBA UNIELELWE KATIKA HILI. SISEMI KWAMBA WEWE ULISEMA KITU ILA ULIPASWA KUKANYA WATU LAKINI HAUKUFANYA HILO. SASA ANGALIA LEO LIMEMJIA CHIEF MBOWE TOKA UCHAGANI, NAONA WEWE UMERUKIA . VIPI MWANANGU KULIKONI?
 
Ndugu zangu:


Nimeanza rasmi kujibu hoja kuhusu „Family Bussiness na Viti maalum ‚mpaka kieleweke’!. Lakini niseme bayana kwamba baada ya kumaliza kujibu hoja za suala la Familia na viti maalum. Nitaacha kuchangia mara kwa mara katika JF. Hii ni kutokana na ushauri wa baadhi ya wanaforum humu. Huwa nasisitiza sana kwamba sipendi kuchangia michango mifupi sana kutokana kwa kuepuka kutoeleweka ama kueleweka vivyosivyo. Hivyo nitachangia mara chache hapa JF pale ambapo itabidi kuchangia. Otherwise, niwaachia ndugu wengine hapa mchangie. Endeleeni kukata issues kwa maslahi ya Taifa.

1. Kwa kuanzia kufafanua suala la familia hoja ya uchagga umejitokeza sana. Naomba nirejee tamko la chama ambalo linajibu hoja za wote waliosema kwamba CHADEMA ni chama cha familia ya wachaga(Hoja ya CHAGA BUSSINESS)

Kwa akili za kawaida, shutuma kwamba CHADEMA imejaa wachaga maana yake ni kwamba CHADEMA ina viongozi na wanachama wengi wachagga kuliko kabila lolote hapa Tanzania. Je ni kwa kiasi gani kauli hiyo ina ukweli?.

Katika safu ya juu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA yenye viongozi sita: wenyeviti na makatibu mchaga ni mmoja tu-Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe. Viongozi wengine wanatoka makabila mengine kama MuIraq, Myao, Mpemba na MuUnguja.

Aidha katika sekretariati ya chama taifa ambacho ndio chombo kinachosimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za chama kikiwa na kurugenzi 9, kati ya wakurugenzi wake mchaga ni mmoja tu. Na wasukuma ni watatu. Kwa nini hawasemi kwamba CHADEMA ni chama cha wasukuma?

Kadhalika mpaka sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameteua wajumbe wanne wa kamati kuu, kati yao hakuna na mchaga hata mmoja na kati yao wawili ni wahaya, Profesa Mwesiga Baregu na Balozi Ngaiza. Kwa nini hawakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wahaya?

Kwa upande mwingine kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita, jimbo ambalo CHADEMA iliongoza kwa uwingi mkubwa zaidi wa kura ni Tarime ikiwa asilimia zaidi ya 64. Kama CHADEMA ni chama cha wachaga kwa nini jimbo la kwanza lisingekuwa la mkoa wa Kilimanjaro?
Kati ya majimbo kumi ambayo CHADEMA ilifanya vizuri zaidi, jimbo la Kilimanjaro ni moja tu la Moshi mjini huku mikoa kama Kigoma, Rukwa ikiwa na majimbo mawili ambayo CHADEMA imefanya vizuri zaidi. Kama CHADEMA ingekuwa chama cha wachaga si ingefanya vizuri zaidi katika majimbo ya Kilimanjaro?
Je, wanataka kutuambia kuwa Mara, Kigoma, Rukwa na mikoa mingine ambayo CHADEMA imefanya vizuri kote kumejaa wachaga?

Kwa mantiki hiyo basi, si kweli kwamba CHADEMA ni chama kilichojaa wachaga. CHADEMA ni chama cha kitaifa. Kinachojumuisha wanachama na wapenzi wa asili na hali mbalimbali. Lakini swali la kujiuliza ni je wachaga hawana haki ya kuwa sehemu ya viongozi katika taifa na wanachama wa CHADEMA?

Zaidi ya hayo tunawashangaa wakitoa hoja kwamba CHADEMA imejaa wachaga. Lakini tunawashangaa zaidi kwa kuwa hatukuwasikia akisema chochote pale Rais Kikwete alipoteua wachaga na watanzania wenye asili ya Kilimanjaro wengi zaidi katika baraza la mawaziri kuliko makabila mengine. Je, kwa mantiki ya wazushi kama hao serikali ya Kikwete ni ya wachaga? Je, kwa kuwa wachaga ndio kabila lenye wabunge wengi zaidi kati ya wabunge wa viti maalumu wa CCM na CHADEMA, Je kwa kigezo hiki tu tuseme kwamba CCM na CHADEMA ni vyama vya wachaga? Je, kwa CCM kuwa na wabunge wa viti maalum wachaga hata katika mikoa mingine ya nchi yetu zaidi ya Kilimanjaro wanapotoka wachaga je, kwa uchambuzi wa wazushi kama hao wanaweza kusema kwamba CCM ni chama cha wachaga?

Hatukupenda kujadili viongozi kwa kutazama makabila yao. Lakini tumeamua kutoa uchambuzi huu kwa sababu suala la ukabila ni nyeti sana kwa mustakabali wa nchi yetu na kwamba kwa kutoa mifano hai tutathibitisha wazi uzushi wa watu hawa. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuasa kwamba kufanya dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha.

Sisi tunaamini kauli za wazushi kama hawa zinapandikiza mbegu ya ubaguzi miongoni mwa watanzania na kuwashawishi watu kutazamana kwa misingi ya makabila yao. Tukiwaruhusu watu kama hawa tutaweka mashakani mshikamano na amani yetu hapa nchini. Tunatoa mwito kwa watanzania kupuuza na kukumea kauli za viongozi kama hawa. CCM inaendelea kukumbatia wazushi hawa na uzushi wao, watanzania watakuwa na kosa gani wakianza kuamini kwamba chama tawala kinapandikiza mbegu za ubaguzi? Na kwa upande mwingine, tunatoa rai kwa vyombo vya habari kuchambua kwa kina kauli za watu kama hawa kwani uwongo ukisemwa sana wananchi wanaweza kuaminishwa kwamba ni ukweli.

Katika taarifa yake CCM imeinukuu shutuma ya wanaotoka upinzani ya kulalamikia tabia za ubabe na udini ndani ya CHADEMA? Ni ubabe upi huo? Ni udini upi huo ulioko katika CHADEMA? Hivi katika vyama vikuu vya siasa hapa nchini kuna chama ambacho safu yake ya kitaifa ina uwiano wa kidini kama CHADEMA? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema pia kwamba katika kutafuta uongozi kuna watu wanaweza kutumia vigezo vya kijinga kama udini na ukabila kujihalalisha ili kufikia malengo yao na ndivyo wanavyofanya watu jamii hii.“

Nitaendelea na hoja zinazofuata za Family Bussiness na Uteuzi wa Viti maalum

JJ
 
Mwansiasa unajenga hoja vizuri na kwa ufasaha sana. Endelea na makamuzi mpaka kieleweke! Ila kwenye suala la muungano wa vyama natofutiana na wewe.

2010.

Eric: Kuhusu muungano wa vyama, nitarejea, bahati mbaya sijapata muda mwafaka. Natambua uzito wa hoja zako, japokuwa baadhi sikubaliani nazo, hasa hii ya muungano. Nikipata muda nitarejea soon kwenye hili.
 
Mzee Mnyika,

Heshima yako mkuu, swali langu lilikuwa kuhusu wadhamini tu waliotajwa na Mwanasiasa, ambao wote ni kutoka mkoa mmoja na kabila moja, haikuwa wanachama wote wa Chadema,

Pamoja na kwamba niliridhika na majibu ya Mwansiasa, sitajali ukiweka nyongeza only on wadhamini!


Halafu njoo tukate ishu hapa, unashauriwa vipi wakati taifa liko njia panda? Hivi unajua uongo usipojibiwa kwa muda mrefu hugeuka ukweli? Na hasa uongo wa siasa? Kijana njoo tukate ishu hapa acha hizo za kushauriwa, sisi forum tunakushauri uje ukate ishu kama ndogo au kubwa wananchi wataamua, wewe ni kutwanga mahindi tu hapa, manake sasa tumeamua kutwanga kiroho mbaya!!

Ahsante Mkuu! anyway wazee wengine kote tutarudi kesho ndugu zangu kukata ishu!
 
Fikiraduni,
Pole kijana. I am with you.Eti wanakata issues, eh?
 
Mzee Es:

Nikiri kuwa Mbowe alikidhamini chama kwenye kampeni 2005. Lakini si Mbowe peke yake-wanaCHADEMA wengi ambao nisingependa kuwataja kwa majina mmoaja mmoja. Nadhani mwanasiasa amemtaja Mbowe kwa kuwa his amount is considerable. Lakini kumbuka kuwa alikuwa pia mgombea urais na Mwenyekiti wa chama Taifa. Kwa hiyo hata ungekuwa wewe, ungechanga zaidi aidha toka kwako au wapenzi wa chama kupitia wewe. Lakini pia hawa wawili Mbowe na Ndesamburo pamoja na watu wengine kadhaa walikubali kukopesha chama kufanikisha uchaguzi na hatimaye tumeongeza viti na na kura na kukuza ruzuku ya chama. Ni kama uko wa Sykies ulivyofanya wakati wa kuanzishwa kwa TANU-walipanda Mbegu ya harakati ikiwemo kwa kuchapa kadi za kwanza. Baada ya hapo wananchi wakufuata!Kwa maneno mengine kwa ruzuku yetu ya sasa tunameeshaanza kutenga fungu kwa ajili ya uchaguzi ujao. Hivyo tegemea katika uchaguzi ujao fungu kubwa la kuanzia kuanza kutoka katika chama chenyewe!. Ndesamburo ametoa pia mchango wake kwenye jimbo la Moshi mjini na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla. Lakini hapa alitimiza wajibu wake kama mgombea na Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro-Udhamini wa namna hii ukihesabika basi wadhamini tuko wengi mimi nilidhamini pesa zangu Ubungo na majimbo baadhi ya DSM. Balozi ngaiza alifanya hivyo Karagwe, Mzee Makani alifanya hivyo shinyanga, Chacha Wangwe alifanya hivyo kwake kama Mwenyekiti wa mkoa wa Mara...orodha ni ndefu kwa kweli.......kwa maneno mengine...hakuna element ya ukabila katika hii michango....kila mtu ametimiza wajibu wake kwa nafasi yake na uwezo wake...

JJ

Kama hili la uchaga limekwisha niendelee na hoja ya Viti maalum
 
Mnyika,

Nimekusikia bro, hamna haja ya kuendelea na huu mjadala tena I mean on my behalf nafikir majibu ya Mwanasiasa bado yanasimama kuwa ni authority kwangu, wewe ninaona ni spinning tu lakini ahsante kwa kunijibu,


Shukrani bro, tuhamie ishu zingine sasa!
 
KWEMYE HILI

Mzee ES niko na wewe

credibility ya JJ iliondoka pale alipoanza kudodge kujibu maswali mepesi mpaka akaja mwanasiasa kumjibia
 
I hope kuwa Freeman kasha submit coursework yake huko Hull maana next week watu wanaenda Easter break
 
Why would you bother hadi utake kujua hili kama vile wewe u mwalimu wake ? Ratiba zake na mipango ya shule yake na maisha yake ya kila siku yana kuhusu nini ?

Wewe mbona na harakati za mkutano wa Uchaguzi UK na mengine uliyajua umeyafanya lakini hatukutaka kusema lolote la kukuonyesha kwamba unapashwa na hukupashwa kufanya vile kwa unibafsi wako badala ya matakwa ya wengi ?
 
Umh!

Atleast bado kuna mtu mmoja kama wewe usiedanganyika. It is the empty vessel that make the most noise. Yours is excessive.You should display this courage in Tanzania notr on the media.

We moght be wadanganyika, but I think I better be one than a coward. Mageuzi hayaletwi kwa maneno tuu kwenye forum.

Belt up or shut up!!!
 
Back
Top Bottom