Mbivu na mbichi za Wagombea Uspika wa CCM kujulikana leo Januari 19, 2022

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Mchakato huo unaendelea pia kwenye Chama cha ADC ambacho ni kati ya vyama vya upinzani chenye mgombea, Maimuna Kassim, aliyejitokeza kuchukua fomu ya kuwania kiti hicho kilichoachwa wazi.

Wateule ndani ya CCM watajulikana baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kupitisha majina matatu yatakayopelekwa kwa hatua zaidi.

Kamati hiyo iliyokutana Januari 18 na leo, Januari 19 ndiyo inayokamilisha mchakato huo baada ya kupokea majina yaliyopitiwa na sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Sekretarieti hiyo ilikutana Januari 17, mwaka huu, kujadili na kuishauri Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa wagombea waliojitokeza kuomba kiti hicho.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa awali Januari 9, mwaka huu na Katibu Idara ya Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka, urejeshaji fomu ulikamilika Januari 15, mwaka huu.

Kabla ya kupigiwa kura na wabunge wote, Janauri 21 hadi 30 (wiki ijayo) kikao cha chama cha wabunge wa CCM (caucus), kitapiga kura kumpata mgombea ambaye atakwenda kuomba kura bungeni.

Hadi sasa wanachama wa CCM 71 wameomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi hiyo ya u-Spika. Miongoni mwa waliojitokeza kwenye kijany’anyiro hicho ni Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia Simba na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mbunge wa Jimbo la Bariadi (CCM) kwa muda mrefu, Andrew Chenge.

Makada wengine waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni wabunge mbalimbali akiwamo Joseph Kasheku maarufu Msukuma, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Bunge la Afrika (PAP) na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele na mwingine ni msomi aliyejinasibu ana shahada tisa, Baraka Byabato.

Baada ya kukamilika kwa mchakato ndani ya chama hicho, jina litakalopitishwa litawasilishwa bungeni Februari mosi, mwaka huu, kwa ajili ya wabunge kuchagua Spika atakayepigiwa kura kushika nafasi hiyo.

Vile vile, mgombea huyo atakayepitishwa na CCM atashindana na wagombea wa vyama vingine kwa wingi wa kura za wabunge baada ya kujinadi mbele yao wakati wa vikao vya bunge.

Mchakato wa kumpata Spika mpya umeanza baada ya Spika Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo Januari 6, mwaka huu, baada ya kauli yake ya kupinga mikopo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua taharuki hali iliyosababisha baadhi ya watu kushinikiza ajiuzulu nafasi hiyo kwa kile kilichoonekana kupingana na kiongozi wake.

Chanzo: Nipashe
 
Spika anatokea Saigon.

Je, unamjua?
Huyu hapa

Makofi_kidogo_kwa_Mh_Spika_wa_Bunge_mtarajiwa_%F0%9F%A4%A3_hii_Nchi_ina_Vituko_aisee.jpg
 
Chenge na mwenzie Sofia watatumia nguvu ya pesa achilia mbali msukuma, Tulia na Steve watakaotumia mizizioloji.

Huyo wa chama cha upinzani nampa heko sana amedhubutu
 
Naatabiri watatu kuteuliwa ugombea uspika kupitia CCM ni Tulia Ackson, Masele na Azzan Zungu

Sababu ya kwanza Zungu kuwakilisha waislamu

Tulia kuwakilisha wakristo

Masele kuwakilisha Sukuma gang lililokabidhi kiti kwa Mama Samia wasukuma wengi wamechukua fomu mwakilishi wao atakuwa Masele

Wote hao wana uwezo na uzoefu na kashfa zero

Wanafaa yeyote kati yao
 
Back
Top Bottom