Mwanasheria Dkt. Nshala Rugemeleza: Mkataba wa bandari ni wa kiuhaini, Umevunja katiba ya nchi na utakwenda kuvunja sheria za nchi

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
"Mkataba uliosainiwa ni "Binding Agreement" hakuna namna ya kujitoa, kuna propaganda zinasema eti tungoje HGA, this is nonsense, itategemea vipi HGA wakati IGA unasema hauna namna ya kujitoa na ukitaka kujitoa uende katika mahakamani za kimataifa, angalia ibara ya 10, 18 na 27 ya mkataba huo ndio utagundua waliosaini mkataba huo walikuwa na dhamira ya kuuza nchi," Mwanasheria Rugemeleza.

Yote yanayofanywa sasa na Serikali ni propaganda kiwaaminisha watu walichofanya ni sahihi, na kilikuwa na nia njema, sasa hatuwezi kuruhusu nia njema kuuza rasilimali zetu-Mwanasheria Rugemeleza.

"Namshukuru Daktari Slaa kwa kulisemea hili, nawashukuru wote waliosimama kuhesabiwa kulisemea jambo hili la kuuzwa kwa rasilimali zetu, nilitegemea Bunge lingeweza kumuwajibisha Rais,kwa maana hakuna aliye juu ya sheria, lakini haikuwa hivyo," Mwanasheria Rugemeleza.

"Mtu mwenye hulka ya wizi lazima atatuibia, mtu mwenye uwezo mdogo wa akili haiwezekani leo ageuke mwenye busara" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba uliosainiwa kwa kuuangalia tu kama hauna majeraha ya akili na akili yako iko sawasawa utagundua ule ni mkataba batili, ule ni mkataba haramu, ule ni mkataba usio weza kutetewa na mkataba wenyewe umejivika madaraka kuwa juu ya sheria ya nchi katika ibara ya 27" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba uliosainiwa kwa kuuangalia tu kama hauna majeraha ya akili na akili yako iko sawasawa utagundua ule ni mkataba batili, ule ni mkataba haramu, ule ni mkataba usio weza kutetewa ni mkataba unaovunja katiba yetu ya nchi moja kwa moja na mkataba wenyewe umejivika madaraka kuwa juu ya sheria ya nchi katika ibara ya 27," Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba uliosainiwa unajiweka juu ya sheria ya nchi, mkataba unajiweka juu ya katiba ya nchi, unagandisha sheria za kodi, halafu niliwasikia watu kama kina Tulia wakifokea fokea watu, mtoto mdogo unafokea fokea watu, nilichogundua hajui sheria za mikataba ya kimataifa," Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba utaisha siku shughuli za bandari zitakapokwisha, mkataba hausemi manufaa ya uwekezaji huo, ni lipi andiko limeandika manufaa ya uwekezaji huo na kusema tunamuhitaji mwekezaji huyu, mkataba utatumia sheria za kodi za siku iliyosainiwa, hautalipa tozo, halafu Mbarawa anatueleza mkataba huu una manufaa, ni yapi hayo manufaa ikiwa mkataba utakuwa juu ya sheria zote za nchi yetu?" Mwanasheria Rugemeleza.

"Viongozi matumbo wamefanya maamuzi ya vizazi vijavyo bila kuzingatia usawa,Wajukuu wetu watakuwa wanaiangalia bandari kama wanavyomuangalia Mama Mkwe na wasifanye lolote, Mkataba wa Rio unasema kufanya maamuzi juu ya vizazi vijavyo kwa kuzingatia usawa, Mkataba unasema utaisha siku,Mwenyezi Mungu akisema Dunia imefika mwisho,tutatawaliwa na Dubai hadi siku Dunia ikifika mwisho," Mwanasheria Rugemeleza.

"Viongozi awa ndio tunawapisha barabarani kwenye misafara yao, Rais aliapa kuilinda na kuitetea katiba, je, alichofanya ndicho!!?? sicho, amepoteza uhalali wa kuwa Kiongozi wetu" Mwanasheria Rugemeleza

"Kitendo cha bunge kupitisha mkataba ule ni aibu, ni dharau kwa nchi, awa watu wameisaliti nchi yetu, wote waliosaini na kupitisha ule mkataba majina yao yaandikwe msaliti, mhaini, tuwakemee watu awa kwa hasira maana wameisaliti nchi yetu," Mwanasheria Rugemeleza.

"Na kuhusu suala la Katiba Mpya,nashauri tukae tuchague watu wa kwenda kutuandikia katiba yetu lakini sio awa waliopo" Mwanasheria Rugemeleza

"Ibara ya 14 kuhusu fidia (Prompty and adequate compassition) utalipa fidia ya hasara ya Sasa na ya mbeleni iliyopotea inapingana na ibara ya 24(2) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema alipwe fidia inayostahili, inapingana na ibara ya 4 na ibara ya 2 la Umoja wa mataifa ya International investment law inayosemwa alipwe fidia inayostahili, Mimi PhD yangu ni ya International investment law na nimesomea Havard, na Mimi sio Mwanasheria uchwara, huu mkataba umeiuza nchi na kukiuka katiba ya nchi yetu," Mwanasheria Rugemeleza

"Mkataba uliosainiwa ni "Binding Agreement" hakuna namna ya kujitoa, kuna propaganda zinasema eti tungoje HGA, this is nonsense, itategemea vipi HGA wakati IGA unasema hauna namna ya kujitoa na ukitaka kujitoa uende katika mahakamani za kimataifa, angalia ibara ya 10, 18 na 30 ya mkataba huo ndio utagundua waliosaini mkataba huo walikuwa na dhamira ya kuuza nchi," Mwanasheria Rugemeleza.

"Spika alikuwa anakuja kwetu kama mwanafunzi wa kujifunza intern kuulizia haya mambo ya International investment law, Leo anajifanya yeye anajua sana, hii ni kejeli, dharau na jeuri, hii inatuonesha sisi Watanzania hatujawafundisha viongozi wetu kutuheshimu, zile kanuni za Tanu wao hawajazisoma, kwa hiyo sisi wanatufanya watwana wao, ndio maana licha ya ibara 27 kusema Tanzania itawajibika kwa Dubai, wao wanakata mayenu wanasema mkataba huu uko sawa sawa," Mwanasheria Rugemeleza.

"Ukiangalia ibara ya 28 uhaini mkubwa umefanyika dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mkataba huu wa bandari na hili nalisema bila kumung'unya maneno haya yamefanywa na Kiongozi namba moja, bunge na wote waliosaini," Mwanasheria Rugemeleza

"Viongozi wetu hawana uhalali wa kuendelea kukaa madarakani, wenzetu waislamu kama umemtendea baya lazima akuoneshe alivyochukia, Watanzania lazima tuoneshe tulivyochukia, hapa lazima tuvue gloves, kama kupigwa basi zipigwe kavu kavu kuonyesha jinsi tulivyochukia," Mwanasheria Rugemeleza.

"Mimi sio mtoto mdogo tena, nimepata miaka yangu yote ya kuishi na nimepata akili nyingi juu ya sheria za nchi na kimataifa, namshukuru Mungu, Sasa siwezi kuruhusu mtoto wangu au mjukuu wangu aishi katika ujinga namna hii, huu ni mkataba haramu, danyanyifu, mkataba wa kuuza nchi, mkataba uliovunja katiba"Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba huu umevuja kwa namna ya ajabu sana, je mikataba mingapi haijavuja na kuna madudu kama, uliposainiwa mkataba huu ilisainiwa mikataba mingine mingi hapo Dubai, kwa hili lililotokea tutawaamini vipi awa viongozi wetu, wamepoteza uhalali wa kuaminiwa na Wananchi," Mwanasheria Rugemeleza.

Pia soma > Askofu Mwamakula: Dkt. Rugemeleza Nshala amedai yupo hatarini baada ya kutoa maoni kuhusu mkataba wa Bandari na DP World

 
Ni kweli kabisa.

Kuunga mkono mkataba huu bila ya kuufanyia marekebisho muhimu kwanza yanayohitajika, ni Usaliti mkubwa sana kwa nchi, wananchi pamoja na maslahi yao yote. Watanzania wanaounga mkono mkataba huu ni wasaliti wakubwa, siyo wenzetu hata kidogo.Wamekosa kabisa uzalendo kwa nchi, na wananchi wenzao, roho haziwaumi kabisa kuuza nchi kwa raia wa kigeni.

Kitendo walichofanya ni sawa na "kutoboa meli ambayo tunayosafiria" ili kusudi maji yaingie ndani ya meli. Wote tunajua matokeo yake kuhusu kitakachofuata baada ya maji kuingia kwenye chombo.
 
Ni kweli kabisa.

Kuunga mkono mkataba huu bila ya kuufanyia marekebisho muhimu kwanza yanayohitajika, ni Usaliti mkubwa sana kwa nchi, wananchi na maslahi yao yote
 
Kinachotafutwa hapa ni kimoja tu nadhani na hawakisemi!!

Ni pale mabaka yatakapo shawishiwa kuwa eti hatuna imani nae kwasababu ya uhaini wa mipaka uliofanyika!!

YAANI aape mwingine kutuvusha!! Aiseh Bas ngoja tuone hatma!

"Mtu mwenye akili ndogo""!hilo ni tusi kubwa sana,ina MAANA mamlaka umeacha wataalam wamtukane mwenye mamlaka!!?
 
Back
Top Bottom