Maulidi Kitenge aacha kazi ITV/Radio one

Sijui kwanini watanzania hatupendi kuondoka sehemu kwa amani na bila kurusha mane no? Hivi ninani aliyemlazimisha kusign mkataba name IPP miaka yote hiyo?
Hivi kwanini tusiondoke kimya kama tulivyo ajiriwa kimya?kwanini tusishukuru? Kwakweli haya matangazo ni kukosa busara kabisa.

Si alisema anakwenda kujiajiri? Mbona Millard na Salama waliacha bila maneno? Kwani alilazimishwa kuendelea na ITV miaka yote hiyo?
Hivi ni mshahara gani utamtosha kwa hao wake wote+watoto?

Kutaka attention tu na kuandikwa kama hivi kuna watu huwa wanapenda sana. Miaka yote aliyokaa sikuwahi kuwaza jana alupoweka barua yake ya kuacha kazi kwenye media hata Kayanda na Regina walienda BBC ndio tulijua ila hatukuona wakirusha mambo yao binafsi na waajiri wao kwenye media this is awful sikuwahi kuwaza kabisa mtu unaweka hadi barua hadharani duh.
 
no big deal, people always change work places for greener pastures!!!
 
Ndiye huyo huyo mkuu. unafiki wake ni nini hasa? kama kuna mifano tafadhali.

Deo anakubalika sana na uongozi wa juu wa ITV/Radio One kutokana kuwa na sauti nzuri ya utangazaji...(of course huu ni ukweli).

Lakini sasa kwa kuwa ndugu yetu yule elimu yake ni ndogo amekuwa ni mtu wa kutegemea majungu ili aweze kupanda madaraja.

Haoni shida hata kidogo kukukandia mbele ya mama (Joyce Mhaville) ili tu upigwe chini au uundiwe zengwe lolote lile, na kwa kupitia mbinu hii chafu imemuwezesha bwana Deo hadi leo hii kuwa Mkurugenzi wa Radio One...
 
Kutaka attention tu na kuandikwa kama hivi kuna watu huwa wanapenda sana. Miaka yote aliyokaa sikuwahi kuwaza jana alupoweka barua yake ya kuacha kazi kwenye media hata Kayanda na Regina walienda BBC ndio tulijua ila hatukuona wakirusha mambo yao binafsi na waajiri wao kwenye media this is awful sikuwahi kuwaza kabisa mtu unaweka hadi barua hadharani duh.

Hata Salama na Millard waliondoka lakini si kwa stahili hii kutaka kuharibiana biashara.
Huyu mtu amekosa busara.
 
Hio Message yake amekosea ama ?

Sababu anasema baada ya kutumika kwa miaka 14... hii inatoa maana nyingine kabisa ukilinganisha na kutumikia

Hapo kwenye red color nami pamenipa ukakasi kidogo. Naomba labda wajuzi wa lugh watuwekee sawa maana yake kimantiki.

kutumika?
kutumikia?

Nikiangalia huyu mtangazaji anavyo andika naishia kucheka tuu!
Kuna mambo najiuliza kwanini ameamua kutangaza ameondoka? kulikuwa kuna ulazima wa kusema hayo yote?

Ni wazi MTU akisoma alivyo andika atajua fika huyu mtu analengo Fulani na anataka watu wamuone mwajiri wake mbaya au kumuaribia biashara.

Pamoja na umahiri wa kitenge kwenye utangazaji wa habari za michezo kwa sisi wasikilizaji wa radio one na watazamaji wa ITV bado kumebaki watangazaji wazuri kama Amri masali,Katanga hi yo sikweli patapwaya!

Hivi kumbe busara aliyonayo Millard Ayo imewashinda wengi kiasi hiki? Hivi ukiondoka kimya kama ulivyo ajiriwa kimya kuna kosa? IPP media naona ndio kiwanda cha kuzalisha watangazaji Tanzania na ni ngumu kuwalipa kila mtu kulingana na matakwa yake!

Hivi kuondoka kwa matangazo ni busara?hadi Leo pamoja na Allan laki,Adrian stepp kuondoka kwa kuutangazia umma sikuwai kuona mapengo yao mpaka Leo, kuondoka kwa matangazo mengi kunachukuliwa kama njia ya kutaka kuharibu.

Ukiona mtu anaondoka kwa matangazo ujue hana busara na anataka muajiri wake aonekane mbaya na anataka kumharibia biashara.
Kijana Millard Ayo ana busara sana.
Mgurusi Ruttashobolwa, nakubaliana kabisa na wewe kwa 100%. Kiukweli hata kuandika 'KUTUMIKA' kwenye barua yake si kimakosa bali alidhamiria kabisa ili kurusha kijembe kwa mwajiri wake IPP. Ila pia kwenda kutangaza tena kwenye redio ya mtu mwingine (si yake, kwa maana ya kwamba amebadilisha mwajiri) bado namhurumia tu kwani hata kama mshahara ni mkubwa bado 'KUTUMIKA' kupo pale pale tu! Kama angejiajiri kwa kweli ningekubaliana na neno 'KUTUMIKA' aliloliandika kwenye barua yake! Hata hivyo hongera zake kwani yeye binafsi ndiyo anayoyajua yaliyokuwa kati yake na IPP Media!
 
Last edited by a moderator:
Wewe Kama Hujaamka Na Bange Ya Longido Basi Utakuwa Umepata Kitu Cha Tarime. Mwenzako Ameacha Kazi Na Wewe Unamwambia Rest In Peace..........!!!!!!!!!!!!! Hakika JF Kuna Mkusanyiko Wa Akili Za Ajabu Ajabu.

Hilo jina lako duuu, mwanangu kadungwa 7, Kitenge badala ya kusema anaacha kazi yeye anadai kajiuzulu. Mbona sasa anafanya kazi ileile efm.
 
Mgurusi Ruttashobolwa, nakubaliana kabisa na wewe kwa 100%. Kiukweli hata kuandika 'KUTUMIKA' kwenye barua yake si kimakosa bali alidhamiria kabisa ili kurusha kijembe kwa mwajiri wake IPP. Ila pia kwenda kutangaza tena kwenye redio ya mtu mwingine (si yake, kwa maana ya kwamba amebadilisha mwajiri) bado namhurumia tu kwani hata kama mshahara ni mkubwa bado 'KUTUMIKA' kupo pale pale tu! Kama angejiajiri kwa kweli ningekubaliana na neno 'KUTUMIKA' aliloliandika kwenye barua yake! Hata hivyo hongera zake kwani yeye binafsi ndiyo anayoyajua yaliyokuwa kati yake na IPP Media!

Serikalini kuna utumishi, kwenye makampuni na mashirika ni utumishi pia, wafanyakazi wote wa sehemu hizo ni watumishi, wanatumikia serikali na makampuni, kutumika ni utumwa ambapo unamtumikia mtu binafsi bila ujira.

Lete muktadha wako muuza ubuyu
 
Umeeleza vizuri mkuu.
Sio busara kuwafuatilia watu lakini kwa usikilizaji wangu kidogo wa redio huyu ana mashabiki wengi na ukiangalia alichoandika na historia yake unagundua kuwa uelewa wa mashabiki wake wengi unafanana naye.
Hitimisho la haraka ni kuwa Tanzania bado sana kama upeo wenyewe wa mambo ndio huu.

Kuondoka kwa kitenge redio one sio tatizo kwani ni mambo ya kawaida sana kwa wafanyakazi hasa waliopo dar kubadilisha waajiri. Wengine huwa kila baada ya miezi sita wanabadili mwajiri!! Ila jinsi alivyotangaza kuondoka kwake kupitia media mbalimbali nadhani nia ilikuwa kuiharibia redio one (iliyompa jina) na kumpa kick mwajiri mpya efm. Sijawahi ona mfanyakazi anasaini mkataba wa kazi mbele ya media zaidi ya wachezaji wa simba na yanga. Inawezekana mojawapo ya masharti ya mkataba katika ajira mpya ya efm yalitaka atangaze kwenye media zote anaacha kazi radio one ili kudraw attention ya anapokwenda efm. Kama ndiyo hivyo atakuwa kawakosea sana radio one angeondoka tu kimya kimya ndivyo wafanyavyo waungwana jamani maana huwezi jua ya kesho unaweza kutumika tena halafu ukaachwa barabarani na kuna watu yaliishawakuta.
 
Wake wanne? Mimi nilisikia
ni wawili. Nampongeza kwa kuwa na wake wawili. Kuwa na mke mmoja na
michepuko kibao ni gharama kuliko wake wawili wanaotambulika

Michepuko bado anayo tena mmoja alimpangishia kawe mjimpya ila kwa sasa kamuamishia sinza tena ni mfanyakazi mwenzie,hapo unategemea mshahara wa sh ngapi kulingana na majukumu aliyokuwa nayo
 
Serikalini kuna utumishi, kwenye makampuni na mashirika ni utumishi pia, wafanyakazi wote wa sehemu hizo ni watumishi, wanatumikia serikali na makampuni, kutumika ni utumwa ambapo unamtumikia mtu binafsi bila ujira.

Lete muktadha wako muuza ubuyu
Mkuu bowlibo, wala sikatai hayo yote uliyoyaandika ndiyo ninayoyafahamu! Tatizo kwa jamaa yangu nadhani ametoka ITV/Redio one kwenda kwenda EFM, huku akirusha kijembe cha 'kutumika' kwa huyo mwajiri wake wa zamani wakati pia anaenda pia 'KUTUMIKA' sehemu nyingine EFM! Pole zake, kwani mie naona hapakuwepo haja ya kuandika kwa style hiyo na pia kurusha kwenye media barua ya ku-terminate contract of employment! Kifupi jamaa naona hana tofauti na Juma Nkamia (Mzee wa kusema siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa!)
Kwa kweli ningekubaliana naye kama angekua anaenda KUJIAJIRI, tofauti na hivyo hata huko aendako anaenda 'KUTUMIKA'!
 
Last edited by a moderator:
Hivi issue ni umaarufu ama nini kinaingia mfukoni mwisho wa siku watoto Wapate kwenda chooni? Think Big ww..

Refer Tahadhari ( Maono yangu Binafsi ) na wewe unayethinki Bigi unayako Binafsi na Akili zako Mwaya ....
don't take life too serious wakati mwingine acha to thinki low :closed_2:
 
Kuondoka kwa kitenge redio one sio tatizo kwani ni mambo ya kawaida sana kwa wafanyakazi hasa waliopo dar kubadilisha waajiri. Wengine huwa kila baada ya miezi sita wanabadili mwajiri!! Ila jinsi alivyotangaza kuondoka kwake kupitia media mbalimbali nadhani nia ilikuwa kuiharibia redio one (iliyompa jina) na kumpa kick mwajiri mpya efm. Sijawahi ona mfanyakazi anasaini mkataba wa kazi mbele ya media zaidi ya wachezaji wa simba na yanga. Inawezekana mojawapo ya masharti ya mkataba katika ajira mpya ya efm yalitaka atangaze kwenye media zote anaacha kazi radio one ili kudraw attention ya anapokwenda efm. Kama ndiyo hivyo atakuwa kawakosea sana radio one angeondoka tu kimya kimya ndivyo wafanyavyo waungwana jamani maana huwezi jua ya kesho unaweza kutumika tena halafu ukaachwa barabarani na kuna watu yaliishawakuta.

WORD ! ameshindwa kugoogle hata jinsi ya kuandika Barua ya kuacha kazi kwa sababu ya haraka ! :A S 109:
 
Anawaharibia hata watoto wake maana kwa mtindo huo hata watoto wake hawawezi pokelewa ITV! Dunia iko hivyo mtu anaweza akakupa kazi kwa vile amefanya kazi vizuri na baba/mama/kaka/dada yako etc
 
Mkuu bowlibo, wala sikatai hayo yote uliyoyaandika ndiyo ninayoyafahamu! Tatizo kwa jamaa yangu nadhani ametoka ITV/Redio one kwenda kwenda EFM, huku akirusha kijembe cha 'kutumika' kwa huyo mwajiri wake wa zamani wakati pia anaenda pia 'KUTUMIKA' sehemu nyingine EFM! Pole zake, kwani mie naona hapakuwepo haja ya kuandika kwa style hiyo na pia kurusha kwenye media barua ya ku-terminate contract of employment! Kifupi jamaa naona hana tofauti na Juma Nkamia (Mzee wa kusema siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa!)
Kwa kweli ningekubaliana naye kama angekua anaenda KUJIAJIRI, tofauti na hivyo hata huko aendako anaenda 'KUTUMIKA'!

I can guess ni elimu ndogo (sijui ana elimu ya kiwango gani, but can guess kwa hicho alichokifanya). As long as you are employed, you are under impoverishment. What matters is the degree of impoverishment- relative or absolute impoverishment. Ndio maana nasema elimu yake ya ku-intergrate na ku-differentiate mambo ni questionable!
 
Back
Top Bottom