Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Kuna huyu member KingY , keshasema vya kutosha kwa maoni yangu. You guys back and forth was somewhat entertaining. Wote mko vizuri sana kwa vijembe, but then again, the topic is not all of that.
yapite kabisa mkuu
 
Nawafahamu hao Kisinane mkuu. Actually nadhani amekuwa underestimated. Huyu alikuwa na pesa kabla hata ya hao kina Mengi.

BTW Reginald Mengi pia ana mdogo wake anaitwa Benjamin Mengi nayeye pia ana miradi kadhaa na ana pesa. Hata kule Shanty town ana hotel moja siyo mbaya pametulia kiaina.

Upo sahihi mkuu! Alikua ni agent pekee wa beer toka kenya na alikua na vision kubwa sana.
 
Duuh!Haruni! Alikuwa lambalamba sana jamaa. Yeye ulevi wake mkubwa Zaidi ya hiyo kuberi ni mademu. Alikuwa hakosi Safary Rally, enzi hizo mara zote akipata nafasi ya kwanza na gari yake ikiwa namba 1. Kuna wakati pia Babu Sambeke aliingia na yule chotara walikuwa wakimuita John Jeep. Waliikuwa naamba 4. Walipata ajali mbaya sana. Ndipo chanzo cha sura ya babu Sambeke kuwa na makovu. John Jeep yeye alitenguka kiuno. Ila wote pia walikuwa wanapita na mademu kwa kasi ya ajabu. Walikuwa players mbaya.
Waliingia kwenye mashindano yale wakiendesha Jeep la John, mmoja akiwa dereva na mwingine navigator

Jeep yenyewe ilikua wazi juu na walileta msisimko mkubwa katika mashindano yale yaliyofanyika baada ya kua yamesitishwa kwa muda mrefu

Ila wanawake wa Moshi walikua wanawashobokea sana hawa ma player, na walitafunwa haswaa kuanzia wanafunzi wa sekondari hadi mademu wa kitaa
 
Hivi kwanini Wachaga enzi hizo walipenda kuziita bar zao majina ya Stereo,ukikuta baa imeandikwa sijui sterio jua ya Mchaga,Kinondoni Stereo
Kipindi hicho nadhani ndio zile radio za Stereo za kijapani Panasonic na Hitachi ndio zilikuwa zinaingia miaka tisini mwanzoni na zilikuwa maarufu na aghali. Mfano Super Stereo Bar Temeke Hospital ndio likazaa jina la soko la Super Stereo
 
Ninachojua unahitaji sentensi hii kama ya Yesu "watu huninenaje"
kuna aina flani ya vijimisemo vina viashiria vya dharau (huenda hujijui)
ndio maana nimetanguliza hilo swali la Yesu kwa wanafunzi wake, unajua alitakaje?
Alitaka kupata ushuhuda kuwa watu wanamwelewaje kwa;
- usemi
- matendo
-na maisha kwa ujumla
unaweza kujiona umekamilika sababu tu una Elimu nzuri, mali nk
lkn watu wanakuelewaje?

Angalia haya;
Timu fafafa
Umesema Weruweru wote hawakuwa saizi yako na ukachomokea neno flani..rudia kusoma pale?

Je? umejiuliza
Hawa timu fafafa watajisikiaje?
hivi wanavyoandika ndivyo walivyo?
wengine komediani but wana maisha yao?

Sky Eclat wajua kasoma mwakani pale Weruweru?
Nikushauri kitu, unaweza kuwa na PHD but ukishindwa kuwa ma ULIMI wenye munyu na kuvutia hadhira/ jamii inayokuzunguka hujaelimika.
Ukiwa na mali ukakosa mvuto na heshima kwa jamii si chochote.
Ok am sorry to her,to you and all
Ila naye amekosea
Ukisoma comments zake kwa jicho la 3 utaelewa nachosema
Kwann nireact kwake tu?
I don't know her
Msuluhishi mzuri atajiuliza hilo na atatafuta chanzo
Inshort she provoked me
yameisha but soma vizuri utaelewa nachosema
 
Sio Babu anaitwa "Bob Sambeke" Huyu Jamaa nilifahamiana nae Mwaka 2012 Nakumbuka nilikuwa Kidato cha Nne, Nilifahamiana nae Baada ya Kukatiza uwanja Mdogo wa Ndege wa soweto (Nikiwa natoka TPC,Kupitia Dar es Salaam Street), Kukatiza Pale tukakamatwa na walinzi wa Airport pale, wakatuonesha Sheria na ibara kibao za Uchukuzi wa Anga wakidai tulipe Dola 200 wakati ule kama 400K, tulikuwa wanne.. Ndipo akatokea Huyo mtu anaitwa Bob Sambeke Wakati ule Bob alikuwa mtu wa makamo na alikuwa akimiliki ndege Mbili zilizokuwa zikipaki Pale uwanja wa Ndege SOweto.. Bob alikuwa mtu Mkorofi.. Katika Hali yake akaanza kutupigisha story (Bob Hadi walinzi walikuwa Wakimwogopa).. Kilatini kuna Msemo unasema "In Vino Veritas" yaani katika Pombe/Kilevi kuna ukweli..Muhusika lazima Aongee ukweli Fulani!
Bob akasema yeye hawezi kufa kwa ugonjwa, Kifo chake kinatakiwa kiwe cha Risasi au Ajali ya Ndege!
Baada ya Bob kuondoka Ndipo Yule Mlinzi akafunguka kuwa Bob alishawahi kuwa Jambazi na Mali zake alizichuma kwa Njia hiyo hasa hasa, pia ikumbukwe Bob alishawahi Kuwa Mwanajeshi...Alikuwa Tajiri Mkubwa Mno!
Muda Mchache Baadaye Nahani 2012/2013 Bob alipata crash ya Ndege Uwanja wa Ndege Arusha Pale..Bob Alifariki (Mungu Amrehemu)
Alikuja Kuzikwa Pale Parokia ya Karanga Moshi..Kanisa lililokuwa karibu sana na Bweni letu... Sikuhudhuria Misa ila niliona Barabara yote inayoelekea Kanisani kama 1 KM ilijazwa na Magari... Nasikia Kanisani hawakuficha kusema Kuwa Bob aliwahi kuwa Jambazi!

Kwako Mtoa Mada!

Point of correction well presented!
 
Una uhakika mnamzungumiza mtu mmoja? Kuna jamaa mwenye kiwanda Nigeria ambaye yeye mjengo wake wa nguvu sana upo kwenye ile njia panda ya kuelekea KCMC kama unatokea YMCA
Pale njia panda ya Chuo cha Ushirika,CCP na Shanti opposite na Shule ya JK Nyerere?Mimi sizungumzii Mimi nazungumzia njia ya Rau ukitokea YMCA kupitia Keys Hotel na St Mary Goreth
 
Back
Top Bottom