jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,375
- 25,453
Umechanganya na uongo mwingi. Hajawahi kuwa mwanajeshi, mwanawe Jamal Sambeke ndo mwanajeshi.Sio Babu anaitwa "Bob Sambeke" Huyu Jamaa nilifahamiana nae Mwaka 2012 Nakumbuka nilikuwa Kidato cha Nne, Nilifahamiana nae Baada ya Kukatiza uwanja Mdogo wa Ndege wa soweto (Nikiwa natoka TPC,Kupitia Dar es Salaam Street), Kukatiza Pale tukakamatwa na walinzi wa Airport pale, wakatuonesha Sheria na ibara kibao za Uchukuzi wa Anga wakidai tulipe Dola 200 wakati ule kama 400K, tulikuwa wanne.. Ndipo akatokea Huyo mtu anaitwa Bob Sambeke Wakati ule Bob alikuwa mtu wa makamo na alikuwa akimiliki ndege Mbili zilizokuwa zikipaki Pale uwanja wa Ndege SOweto.. Bob alikuwa mtu Mkorofi.. Katika Hali yake akaanza kutupigisha story (Bob Hadi walinzi walikuwa Wakimwogopa).. Kilatini kuna Msemo unasema "In Vino Veritas" yaani katika Pombe/Kilevi kuna ukweli..Muhusika lazima Aongee ukweli Fulani!
Bob akasema yeye hawezi kufa kwa ugonjwa, Kifo chake kinatakiwa kiwe cha Risasi au Ajali ya Ndege!
Baada ya Bob kuondoka Ndipo Yule Mlinzi akafunguka kuwa Bob alishawahi kuwa Jambazi na Mali zake alizichuma kwa Njia hiyo hasa hasa, pia ikumbukwe Bob alishawahi Kuwa Mwanajeshi...Alikuwa Tajiri Mkubwa Mno!
Muda Mchache Baadaye Nahani 2012/2013 Bob alipata crash ya Ndege Uwanja wa Ndege Arusha Pale..Bob Alifariki (Mungu Amrehemu)
Alikuja Kuzikwa Pale Parokia ya Karanga Moshi..Kanisa lililokuwa karibu sana na Bweni letu... Sikuhudhuria Misa ila niliona Barabara yote inayoelekea Kanisani kama 1 KM ilijazwa na Magari... Nasikia Kanisani hawakuficha kusema Kuwa Bob aliwahi kuwa Jambazi!
Kwako Mtoa Mada!
And yes, ni Babu Sambeke vilevile, ndo jina lake toka home, ila wengine walikuwa wakimuita hivyo "Bob Sambeke".
Kumbuka "Bob" ni jina linalotokana na Robert. Yeye alikuwa akiitwa Ernest Sambeke Mallya.
Kule uchaggani ilikuwa kawaida kwa watoto kupewa jina la “Babu”
