Masikini Dr. Slaa, Nyumba yake yapigwa mnada

Masikini Dr. Slaa, Nyumba yake yapigwa mnada

Angalia Gazeti lili report habari hii !
Kwa wanaofahamu washa elewa zamani sana
 
Huo ndyo mshahara wa dhambi mbaya ya usariti
 
Kwa ujumla wake, hii bi mbinu ya kutakatisha pesa au ya kuibia benki.

Slaa hajashindwa kulipwa mkopo asilani.

Tukumbuke yule mkewe alisema wana mpango kujenga shule.

Connect .....
Ndio hivyo tena Ndama mtoto wa ng'ombe mjukuu wa Papaa Msofe kashanunua mjengo wa Dr. Slaa.
 
Mbowe siku hizi ni Bank? Mtu anapewa nyumba halafu anamwachia mchumba akope hela Bank bila kusimamia hiyo biashara kisha mlitaka Mbowe aje tena amlipie na deni?
kumbe nyumba aliweka rehani?hapo ndo nimeelewa,
 
Ambaye hana deni au mkopo anyooshe kidole juu
Huwezi kulinganisha watu wote na kiongozi wa kitaifa aliyefanya kazi miaka kibao tangu enzi za chama kimoja mpaka sasa kafikia umri wa kustaafu kimsingi.

Dr. Slaa kuwa na deni la nyumba mpaka leo ni ishara ya uzembe na kutoweza kuongoza.

Kiongozi anatakiwa kuwa mtu wa kutoa mfano. Anatakiwa kuwa mtu aliyekwishaidhinda dhiki ndogondogo ya kukosa sehemu ya kukaa, jwa sababu kiongozi mwenye dhiki ndogondogo, hata vishawishi vinavyoweza kunuondolea imani ni vidogo vidogo.

Mimi nina wadogo zangu wamemaliza chuo kikuu miaka mitano iliyopita na wanahamia kwenye nyumba zao.

Huyu babu mzima mpaka leo hajalipa mkopo wa nyumba tu?

Au alifikiri kila kitu atalipiwa na chama mpaka kufa?
 
Nikiwa nasikiliza Habari za magazetini asubuhi hii nimesikia Nyumba ya aliyekuwa katibu wangu Nyumba yake imeuzwa kwa mnada baada ya kuchukua Mkopo.

Nikajiuliza, ina manaa walikuwa wakimchukulia ndege special kutoka South Africa kipindi cha kampeni na kumlipia gharama kubwa hotelini na Ulinzi mkubwa, Leo wanashindwa kumlipia deni mpaka Nyumba inauzwa?

Ina maana pesa zote zimeisha au wamemrusha?

Ushauri wangu kwa Dr. Slaa, awaombe msamaha wana-Chadema na nina uhakika wataunganisha nguvu kuokoa jahazi.
View attachment 319457
Hakuna kitu kibaya kama usaliti. Huyu alisaliti kaniaa, akasaliti mke na watoto, akasaliti chama. Unategemea nini? He should expect worse
 
Hii ni style ya dk slaa ya NITOKE VIPi. Trust him NOT....
 
Kwa hiyo umepatwa na furaha kwa sababu nyumba ya Dk. Slaa inapigwa mnada?

Furaha yote ni kwa sababu hakumsaidia fisadi Lowassa kuingia Ikulu?

Moral and Human principle is more than material gain!

Dhehebu lake linasema, heri wenye moyo safi...

Dk. Slaa aliamua kuwa na moyo safi!
Moyo safi wa Slaa uliosafishwa kwa sabuni ya CCM. Uko sahihi ila Slaa ana roho mbaya na malipo ni hapa hapa.
 
Ukiwa na ubongo ulio hai lazima utashangaa kwanini CCM ishindwe kumsaidia mtu aliyewasaidia kukidhohofisha chama chake mwenyewe, Dr Slaa hakuisaliti CHADEMA bali aliamua kusimamia kile anachokiamini.

Waafrika tuna shida kubwa ya kutokuwa na misimamo na ndio maana tumekuwa vigeu vigeu ktk mazungumzo na matendo yetu ya kila siku.

In fact hatujazowea kuwa na wanasiasa wanaosimamia kile wanachokiamini mwanzo mwisho,tumeshazowea uswahili uswahili na kwasababu hiyo basi wengi wenu mlitaka Dr Slaa afanye siasa za kiswahili swahili.

Dr Slaa angekuwa anafanya siasa za namna hiyo toka zamani nadhani CHADEMA wangepotea sana, ilihitajika kiongozi mwenye misimamo kama Dr Slaa kuweza kuivusha CHADEMA salama ktk misuko suko na dhoruba kali za kisiasa ilizokumbana nazo huko nyuma. Ila nyinyi wafuasi wa Mbowe hamuwezi kuyajua haya, very soon you are going to find out what you lost.
Macho yako yamefumbwa na uCCM kiasi ambacho kazi iliyopo mbele yako ni kuitawadha CCM hata kama harufu chafu imezagaa.

CHADEMA vs Slaa si suala tena maana ushahidi wa usaliti wa Slaa ulikuwa wa bei nzuri ni kinyume cha matarajio kuwa anaweza kupoteza asset bila msaada hasa wa alichofikia bei. Labda iwe zuga
 
Sikuwahi kufikiria kwamba akina Crashwise watakuja kumkejeli Dr Slaa na kumuabudu Lowassa kwa jinsi ambavyo huyu mzee alitumia juhudi na maarifa mengi ktk kukiimarisha hiki chama.

Mara hii wamesahau yote mazuri ambayo Dr Slaa aliyafanyia CHADEMA, eti wanamwita msaliti,mtu aliyekaa na CHADEMA kwa zaidi ya miaka 30,akikihudumu chama kama katibu mkuu kwa zaidi ya miaka 20 leo asiaminiwe halafu kuaminiwa mtu ambaye maisha yake yote alikuwa na CCM,kwa zaidi ya miaka 40. Kajiunga juzi tu na CHADEMA mara hii yeye ndio limegeuka kuwa Mungu ndani ya chama, kila goti la mfuasi, kada na mwanachama wa CHADEMA kwake litapigwa.

Kweli fedha ni sabuni ya roho, ukiwa mpigania uadilifu na ukweli kama Dr Slaa utadharaulika, ukiwa mtu mwenye tuhuma nyingi za ufisadi kama yule jamaa yetu maadamu una pesa basi hata magoti utapigiwa.
Umetumia viashiria gani kutoa maoni utetezi na kashfa?

Kwa vile misimamo yako ni wazi wewe ni mpuuzi tu kama Slaa
 
Mwenzako yuko Marekani anasoma wewe endelea kula vumbi kwenye majukwaa ya Chadema halafu hata ubunge wa viti maalum hujapewa!

Hivi Tanzania Daima ni gazeti la kufanyia reference?
Kwani wewe ni mbunge wa viti maalum wa CCM? Mbona hubanduki kwenye kuitetea CCM na kuinanga CHADEMA?
 
Dr Slaa mwenyewe alishawahi kukiri kuwa nyumba anayoishi alisaidiwa kununua na Mbowe,naona Mbowe kaamua kuchukua nyumba yake;Mbowe una roho mbaya sana yaani umeshindwa kufikiria nguvu za Dr Slaa katika kukikuza chama mpaka umemkomoa kwa kumpokonya nyumba yake?
Alikuza chama kweli lakini kafikia bei na CCM. Mbowe anaingiaje hapa kwani Slaa ni mfugo wake?
 
Back
Top Bottom