Masikini Dr. Slaa, Nyumba yake yapigwa mnada

Masikini Dr. Slaa, Nyumba yake yapigwa mnada

Mwenzako yuko Marekani anasoma wewe endelea kula vumbi kwenye majukwaa ya Chadema halafu hata ubunge wa viti maalum hujapewa!

Hivi Tanzania Daima ni gazeti la kufanyia reference?
 
Sikuwahi kufikiria kwamba akina Crashwise watakuja kumkejeli Dr Slaa na kumuabudu Lowassa kwa jinsi ambavyo huyu mzee alitumia juhudi na maarifa mengi ktk kukiimarisha hiki chama.Mara hii wamesahau yote mazuri ambayo Dr Slaa aliyafanyia CHADEMA, eti wanamwita msaliti,mtu aliyekaa na CHADEMA kwa zaidi ya miaka 30,akikihudumu chama kama katibu mkuu kwa zaidi ya miaka 20 leo asiaminiwe halafu kuaminiwa mtu ambaye maisha yake yote alikuwa na CCM,kwa zaidi ya miaka 40,kajiunga juzi tu na CHADEMA mara hii yeye ndio limegeuka kuwa Mungu ndani ya chama,kila goti la mfuasi,kada na mwanachama wa CHADEMA kwake litapigwa.Kweli fedha ni sabuni ya roho,ukiwa mpigania uadilifu na ukweli kama Dr Slaa utadharaulika,ukiwa mtu mwenye tuhuma nyingi za ufisadi kama yule jamaa yetu maadamu una pesa basi hata magoti utapigiwa.

Mkuu, ni yeye mwenyewe aliyekisaliti chama alichoshiriki kukijenga. Sasa wewe unailaumu Chadema tena kwa nini?
 
Safi sana Dr. Slaa...una saikoloji ya Juu sana sana sana...bora nyumba iuzwe tuu kwa njia ya mnada kwasababu wangekusakama sana sana,Pia hata kiusalama ungekuwa ni Mdogo kama ungerudi pale....Umetumia akili kubwa sana...umeruka mtego wa kusubiriwa urudi kisha ungeingia tuuu...maneno yangeanza....Hii nimeipenda kwa Jicho la 3.
 
Mwenzako yuko Marekani anasoma wewe endelea kula vumbi kwenye majukwaa ya Chadema halafu hata ubunge wa viti maalum hujapewa!

Hivi Tanzania Daima ni gazeti la kufanyia reference?
Miaka yote hiyo bado anasoma?? Wenzake wamepumzika na wajukuu sasahivi yeye bado anahangaika kusoma ili aajiriwe hehehe.. Kweli elimu ni bahari
 
DSC00447.jpg
 
Dr Slaa mwenyewe alishawahi kukiri kuwa nyumba anayoishi alisaidiwa kununua na Mbowe,naona Mbowe kaamua kuchukua nyumba yake;Mbowe una roho mbaya sana yaani umeshindwa kufikiria nguvu za Dr Slaa katika kukikuza chama mpaka umemkomoa kwa kumpokonya nyumba yake?
 
Kweli Mshumbuzi ni noma., kamwingiza chaka mzee wa watu hadi nyumba yake inapigwa mnada...mahaba niuwe ni noma!
 
Ukiwasoma vijana wa Chadema kwenye thread kama hizi ....unahitaji kuwa mwendawazimu kuwa sehemu yao katika mapambano ya kutetea wanyonge wa nchi hii ....wameshaandika kejeli na matusi juu kwa headlines za magazeti tu ....
 
Dr Slaa hayupo sawa ni swala la kumuombea kwa Mungu kama binadamu mwingine kwa yanayompata ili aende sawa..binadamu hatujakamilika yanayompata Slaa yeyote yanaweza kumpata..
 
Sikuwahi kufikiria kwamba akina Crashwise watakuja kumkejeli Dr Slaa na kumuabudu Lowassa kwa jinsi ambavyo huyu mzee alitumia juhudi na maarifa mengi ktk kukiimarisha hiki chama.Mara hii wamesahau yote mazuri ambayo Dr Slaa aliyafanyia CHADEMA, eti wanamwita msaliti,mtu aliyekaa na CHADEMA kwa zaidi ya miaka 30,akikihudumu chama kama katibu mkuu kwa zaidi ya miaka 20 leo asiaminiwe halafu kuaminiwa mtu ambaye maisha yake yote alikuwa na CCM,kwa zaidi ya miaka 40,kajiunga juzi tu na CHADEMA mara hii yeye ndio limegeuka kuwa Mungu ndani ya chama,kila goti la mfuasi,kada na mwanachama wa CHADEMA kwake litapigwa.Kweli fedha ni sabuni ya roho,ukiwa mpigania uadilifu na ukweli kama Dr Slaa utadharaulika,ukiwa mtu mwenye tuhuma nyingi za ufisadi kama yule jamaa yetu maadamu una pesa basi hata magoti utapigiwa.

We unataka kusema hukuliona kosa la Dr.Slaa kabla hajakimbilia nje MZEE ?!. Dr ilitakiwa abaki kimya alivyoamua mwanzo. Lakini alipoiruhusu CCM kumuandalia Press na midahalo kukikandia chama chake !! Ulitegemea wana CDM nao wasimgeuzie kibao ?

Hebu angalia Mkama alivyokatwa na nafasi yake kujazwa na Kinana amesema nini mpaka leo ?! Kimya. Na WaTz tulivyo wanafki hatukuliona kama jambo kubwa, lakini leo pamoja na Dr kuisuta CDM watu mnadai kosa lake lisiguswe, hii si sawa hata ukiwa maarufu lakini usinyee kambi yako iliyokulisha.
 
Dr Slaa mwenyewe alishawahi kukiri kuwa nyumba anayoishi alisaidiwa kununua na Mbowe,naona Mbowe kaamua kuchukua nyumba yake;Mbowe una roho mbaya sana yaani umeshindwa kufikiria nguvu za Dr Slaa katika kukikuza chama mpaka umemkomoa kwa kumpokonya nyumba yake?
Kwani mkopo kachukua Mbowe au Josephine?
 
Back
Top Bottom