DR Kamala Amefikiria hutuba yake? (Slaa atupiwa makombora) Habari leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DR Kamala Amefikiria hutuba yake? (Slaa atupiwa makombora) Habari leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by david2010, Oct 20, 2010.

 1. d

  david2010 JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  AHADI zinazotolewa na baadhi ya wagombea uongozi nchini katika kampeni zinazoendelea za uchaguzi mkuu zikitekelezwa, huenda zikawaweka Watanzania pabaya, imebainika.

  Taarifa ya kitaalamu imebaini, kwamba kuna wagombea urais ambao wamekuwa wakiwaahidi Watanzania kuondoa kodi katika saruji watakapochaguliwa kuingia Ikulu.


  Taarifa ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, iliyotolewa jana na Waziri mwenye dhamana, Dk Diodorus Kamala, ilisema ahadi hiyo inapotosha wananchi na kuwapa matumaini ambayo hayatekelezeki.


  Alisema chini ya kifungu 2(4)(c) cha Itifaki ya Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki, nchi wanachama zilikubaliana kuweka na kutekeleza wigo wa pamoja wa ushuru wa forodha kwa bidhaa zitokazo nje ya Jumuiya.


  Aliongeza kuwa wigo huo ulianza kutekelezwa Januari mosi, 2005 na viwango vilivyokubalika ni asilimia 0 kwa malighafi, pembejeo za kilimo, dawa na mitambo; asilimia 10 kwa bidhaa zilizosindikwa kiasi; na asilimia 25 kwa bidhaa zilizokamilika katika uzalishaji.


  Kamala alisema, bidhaa nyeti ushuru wake ni zaidi ya asilimia 25.


  “Hivyo nchi binafsi mwanachama haina mamlaka ya kurekebisha viwango vya kodi ya forodha … mfumo wa uamuzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hauruhusu nchi moja mwanachama, kufuta ushuru wa forodha wa bidhaa ya aina yoyote ile, ikiwamo saruji.”


  Alisema, kuwaahidi wananchi jambo ambalo halijakubaliwa na viongozi wa nchi zingine wanachama ni kuwadanganya. “Kwa kawaida muungana na mkweli, hatoi ahadi ya jambo ambalo uamuzi au utekelezaji wake unategemea ridhaa ya mamlaka nyingine iliyo juu yake.”


  Alihoji: “Je, ombi la kufuta ushuru likikataliwa na nchi zingine wanachama itakuwaje? Je, mhusika atawarudia wapiga kura na kuwaambia kuwa alitoa ahadi hewa au isiyo na mantiki?”


  Alisema, saruji ni miongoni mwa bidhaa zilizowekwa katika kundi la bidhaa nyeti, ambazo wazalishaji wa nchi zinakotoka, hupewa ruzuku ambapo wazalishaji wa EAC hawapewi ruzuku hiyo, lakini wanaweza kuzalisha kwa ufanisi.


  Hatua hiyo alisema kuwa inachangia katika maendeleo ya viwanda, ajira, mapato ya Serikali na kuokoa fedha za kigeni, ambapo pia kuweko kwa ruzuku kwa wazalishaji wa nje huku wa ndani wakikosa, kunaweka mazingira ya ushindani usio sawa katika soko la Jumuiya dhidi ya wazalishaji wa Afrika Mashariki.


  Alisisitiza, kwamba kwa upande wa saruji, kuanzia Januari mosi 2005 ushuru wake ni asilimia 55 na nchi wanachama zilikubaliana ushuru huo ushuke kila mwaka hadi asilimia 35 kuanzia Januari mwaka huu na ubaki katika kiwango hicho.


  Alitaja bidhaa zingine katika kundi hili na kiwango cha ushuru kwenye mabano, kuwa ni sukari (100%), mahindi (50%), ngano (35%), mchele (75%), maziwa (60%), tumbaku (35%), sigara (35%), khanga, kikoi, kitenge (50%), mashuka (50%), magunia ya jute (50%), viberiti na betri za redio (35%).


  “Kwa hiyo kufutwa ushuru si tu kutasababisha viwanda kufa, lakini mapato ya serikali na ajira vitapungua sambamba na uanachama wa Tanzania katika Jumuiya kuwa shakani.


  “Sina hakika kama misamaha ya kodi inaendana na ahadi dhaifu za elimu na afya bure kwa Watanzania zinazotolewa na wapinzani.


  Huwezi kutoa elimu bure na afya bure na wakati huo huo, usamehe ushuru wa forodha,” alisema Kamala.


  Alisisitiza pia kuwa, hatua ya kupunguza ushuru wa forodha kwenye saruji ilichukuliwa kitambo, lakini kufutwa kukashindikana kutokana na hali halisi iliyobainishwa awali.


  “Mwaka 2005 ushuru ulikuwa asilimia 55 ukapunguzwa hadi asilimia 25 ya sasa … hatua hii ilichukuliwa kutokana na maandalizi ya Kombe la Dunia, Afrika Kusini na Olimpiki, China.


  Alisema, wakati huu ambao ushuru kwa muda umeshushwa hadi asilimia 25 huku ikifikiriwa kama utarejea asilimia 35, tayari wazalishaji saruji wameanza kulalamika kuwa wenzao wa nje hususan Misri, wanapata ruzuku na hivyo kuiuza kwa bei ndogo katika Jumuiya.


  “Kwa maana hiyo kufutwa kabisa kwa ushuru, kutasababisha viwanda kufa na dhana ya kuwapa wananchi saruji ya bei nafuu kufa pia … bei ya bidhaa yoyote duniani, hutegemea upatikanaji wake na mahitaji ya soko.


  “Pindi viwanda vya saruji vya Afrika Mashariki vikifa, wazalishaji kutoka nje ya Jumuiya, watashawishika kupandisha bei, kwa kuwa sasa watakuwa wamejengewa ukiritimba katika soko kwa kukosa mpinzani wa ndani,” alisema Waziri.


  Katika kampeni zake nchini, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa, amekuwa akiwaahidi wananchi kuwa akiingia Ikulu atapunguza bei ya saruji hadi Sh 5,000 kwa mfuko wa kilo 50, ili wananchi wajijengee nyumba bora za kisasa.


  Je ndugu zangu inamaana Tanzania hatna Chetu Tena mpaka Jumiya iamue kumbe ndo maana Dr P.W. slaa amesema watanzania hawajafundishwa kuhusu Jumiya ya EAC.

  Haya ndi maaoni ya wanaoipenda nchi yao wewe wasemaje?


  Jumla Maoni (17)

  Hakuna maelezo ya maana hapo. Suluhisho ni kujitoa EAC. Hatudanganywi sasa hivi. Samahani mheshimiwa waziri Maoni Mheshimiwa Kamara ni mbabe na kamwe huwa hafati taratibu za kikazi kufanya kazi.Anapotembelea mahali hutisha watumishi wa Serikali kwa cheo chake kwa uwaziri wake wa A.Mashariki. Nina mifano mingi ambayo ctaki kuitaja.

  Mr Kamala LEAD DON'T DRIVE. Maoni kamara ni kibaraka wa kikwete kwahiyo tuzichukulie kauli zake zaidi za kisiasa kuliko kitaalam. kenya na uganda haziwezi kuipangia Tanzania viwango vyake vya kodi na hii ndio baadhi ya mambo ambayo watanzania tunapinga EAC haukutokana na wananchi wenyewe bali viongozi wachache wanaojitafutia umaarufu. viwango vya kodi vinatokana na uwezo wa kiuchumi wa nchi husika . kenya ina uchumi mzuri kuliko TZN kwahiyo viwango vya TAX vya TZN ilibidi viwe vya chini ili kuruhusu kukua kwa uchumi.

  Poleni sna mana mnachokiongea hamkijui,ila ni ushabiki wa kisiasa.Inawezekana na saruji itashuka bei,mbona anayoaidi kikwete hamyasemi?.

  Bora ushirikiano ufe lakini Watanzania tupate saruji kwa bei nafuu kuliko kutetea jumuiya halafu Watanzania tunaumia kwa bei ya saruji. Ni moja ya ushirikiano ulioingiwa bila kujali Wananchi watafaidi vipi na hiyo jumuiya.

  Mh. Kamara unataka kutafanya kwamba sote atuna akili ! iweje kuboresha maisha yetu itegemee ridhaa ya nchi nyigine? alafu unasema kwamba viwanda vitakufa!! kiwanda kinakufa kikipewa nafuu ya kodi!! hiyo PHD ulipewa au uliandika Thesis au umerukwa na akili kipindi hiki cha uchaguzi.au ndo unafukuzia U-RC kwa kupiga porojo nashangaa ata wandishi waliokuoji ata maswali awajakuliza! Mh.kamara siyo kila sheria inatenda haki.Ok rudi kwenu ukalime ndo maana walikunyima ubunge.

  Ina maana waziri anataka kutuambia kuwa sasa hivi tanzania hatuwezi kujiamulia mambo yetu wenyewe mapaka tuamuliwe na nchi nyingine.....CCM na hii jumuiya yenu ya EAC ovyo kabisa....hatuwataki wote!

  Muheshimiwa Camara! Inawezekana Kupunguza bei ya cement kwa kupunguza ushuru kwa viwanda vya ndani na cement ikauzwa kwa bei nafuu sana kama uganda. Kupunguza ushuru wa forodha katika vifaa vya ujenzi sidhani kama inaweza kuinyima mapato serikali. Mwalimu alisomesha watanzania kwa korosho na katani sasa tuna Madini kama Tanzanite, Gold, Diamond, na tuna uranium pia, gas, jamani why tusisome bure? Cheo cha uwaziri ni kikubwa mno na unaposimama kwa public ni vizuri ukijipanga ili utoe kitu chenye mantik usidhani odience wote ni wale wa mwaka 47 kwa sasa wasomi wengi na wengine umetufundisha wewe. Ni mtazamo tu Maoni Ndugu kamala wewe umeshindwa kwenye kura ya maoni ya Ubunge wananchi wa Nkenge hatuakuridhika na utendaji wako tukakupumzisha. Na umefoji ukajiita dokta lakini wasomi tukakuondoa, nakushauri uende ukasome ujue kujenga hoja. Siyokupiga blaa blaa. Rais wetu mpya Slaa, atajua jinsi ya kulipa hizo kodi, kutokana na madini yanayopelekwa bure. Maoni iyo itifaki ya umoja wa forodha sio msaafu kwamba hawezi badilika nchi kama inaona wananchi wake hawapati manufaa yoyote na izo kodi kiongozi wa nchi ana wajibu wa kurise alram kwa nchi husika .kamara anaongea as if ,ayo ni maneno matakatifu ambayo hayawezi kubadilika.yeye hana uchungu na watu wake ndo maana wananchi wa nkenge wamekataa kumrudisha bungeni yeye kama mbunge na waziri mwenye zamana alitakiwa alione ilo .mfuko wa cement kwa mkoa wa kagera na kigoma kwa sasa ni sh 22000/=.kwa bei iyo wananchi wangapi watamudu kujenga makazi bora?na ayo maisha bora kuna siku kweli yatapatikana?tatizo viongozi wengi walioko madarakani wengi wao uwezo wa kufikiri na kuwa creative umefikia mwisho ndo maana tunaitaji mabadiliko waje wenye kuweza au ata kuthubutu kutenda sio kila siku tunasikia eti ili haliwezekani mbona yasiyo kuwa na maana kwa wananchi yanawezekana? Maoni Dr kamala,unakosea tena sana kusema ahadi za slaa na chadema hazitekelezeki! Jibu maswali yafuatayo kisha uamue mwenyewe ni ahadi zp haztekelezeki
  1: hospitali 7 za rufaa inawezekana? Kivp?
  2.Viwanja vya ndege vya kimataifa vitatu inawezekana? Kivip?
  3.Machinga complex nne dar inawezekana? Kivip?
  4.Meli kubwa mpya ziwa victoria,tanganyika,na nyasa inawezekana? Kivip?
  Ahadi za ccm ni nyingi kuliko maelezo na zinahitaji matrilioni ya pesa na kamwe hazitekelezeki.Tuambie hizo pesa za kutekeleza anachoahidi bosi wako kikwete mtatoa wapi?
  Maisha bora kwa kila mtanzania yanaanza kwenye elimu na malazi zaidi sana chakula,jambo ambayo chadema wanazungumzia nyie mwawakejeli mkisema ahadi hzo ni ngumu,je zenu? Maoni Hayo ndiyo maelezo ya kitaalamu yanayotakiwa kutolewa na watu makini, itambulike kuwa Tanzania si kisiwa kinachoweza kujiendesha chenyewe, hongera waziri kueleza ukweli na kuwaumbua hao wanaotoa ahadi zisizokuwa na utafiti wala ukweli wowote ili wapigiwe makofi Maoni Unajua mwalimu nyerere alishasema umasikini wa fikra ni umasikini mkubwa na mbaya kabisa, Je mabilioni mangapi ya EPA yamepotea,Je Rada wanasema bil ngapi zilipotea,je madeni tunayowapa tunawaita wahisani ni mabilioni mangapi,Tanzania tumejengewa ukoloni wa jinsi ya ajabu sana,Pale mkuu wa kaya anapokosa watu wa kumshauri namna ya kupata kile tunachokihitaji kutokana na kile tulichonacho na kutwa nzima tukienda uko na uko kuemea.Je kamara aoni kwamba hata kura za wananchi wa Nkenge wanaona hafai,licha Tanzania nzima. vyote anavyosema silaa vinawezekana mpeni nafasi mwone.Kama mmeona upande fulani haufai kwa nini msijaribu upande mwingine,kuliko kulz=azimisha kule kule kusikofaa. Maoni Ninawachukia wnasiasa wanaojidai kutoa ufafanuzi wenye kuponda wakati slaa anapoahidi wakati kikwete anongopa wazi mnakaa kimya! Hivi kweli kujenga reli kutoka Mwanza hadi Dar kupitisha treni ya mwendo kasi ndani ya miaka 5 inawezekana? Umeme wa kuendeshea uko wapi! Waheshimiwa mumekaa kimya. Mambo yanayozungumzika mnayashikia bango! Katiba ya Afrika mashariki ni Msahafu usioweza kubadilishwa jambo? Maoni Nawachukia wanaomini kuwa kuna kiongozi akingia madarakani atakuwa mwokozi wa TZ. Halipo hilo hizo ni ahadi tu ambazo yeyote anaweza zifanya ili apate hiyo kula ingawa watu wengi tunafikiri kura. Hakuna anayetaka nafasi au ajira kwa maslahi ya mwananchi kama tunavyojidanganya, ila kwa ajili ya kuendesha maisha yake kwanza next follows. Hivyo udhaifu uliojitokeza kwa kikwete pia utakuwepo kwa huyo slaa. Kwani kiongozi bora ni yule anaependa kubadilika na asiyejiona anajua kila kitu. Asiyefikiri kwa makini ataamini kila kitu. Maoni raisi wetu docter silaa ni mtu makini sana alipo taja mafisadi watu walimcheka nakusema huyo ni muongo na wengine kudiliki kusema tutamshitaki sasa,mpaka leo hakuna aliyemshitaki na ukweli umejulikana
  naamini amefanya utafiti wa kutosha,hayo yote mnayosema anayajua,hana historia ya kudanganya tunaamini anayo tuahidi yanatekelezeka. Maoni HUYU KAMARA HANA ELIMU YA PHD, HAJASOMA CHUO CHOCHOTE KILE DUNIANI NA KUPEWA PHD. YEYE AMEJIPATIA HIYO PHD KWENYE INTERNET. UWEZO WAKE WA KUFIKIRI NI MDOGO HIVYO HATA HOJA ZAKE NI NYEPESI SANA. HII INATHIBITISHWA NA WANANCHI WA JIMBO LA MKENGE AMBAO WALIMPIGIA KURA ZA HAPANA BAADA YA KUMUUNA HANA UWEZO WA KUWA MBUNGE. SASA KAMA WATU WA JIMBO LAKE WALIMUONA HANA UWEZO WA KUWA MBUNGE HATAWASHAWISHI VIPI WATANZANIA WOTE KUWA ANA UWEZO WA KUFIKIRI NA KUJENGA HOJA?
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Naona analinda position yake
   
 3. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Huyu ni majeruhi wa kura za maoni .Sasa ni mwendo wa kujikomba ili angalau apewe kacheo ka ukuu wa Wilaya na JK. Asamehewe kwani hajui atendalo
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Ni vyema Dr. kamara akaelewa ya kuwa tanzania ni nchi huru na haiwezi kuruhusu masilahi ya raia wake yapangwe na EAC ambayo viongozi wake hawajachaguliwa na raia.

  Huyu jamaa alishindwa kura za maoni na yupo hap na uwaziri wake kumshikia Dr. Slaa kwa muda tu sasa Kamara atawezaje kumpa mipasho hiyo the future president? Kweli ni kichekesho hicho..............................
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  EAC ni moja kati ya mikataba ya kifisadi, haina tofauti na Buzwagi.Dr.slaa akiingia lazima umoja huo uangaliwe upya.Ndiyo maana juzi juzi Makamu wa Rais wa kenya kadai bado wanamhitaji Kikwete aendelee ili alinde mkataba tata wa EAC.Ni wizi mtupu
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,763
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mwaka 2005 ushuru ulikuwa asilimia 55 ukapunguzwa hadi asilimia 25 ya sasa … hatua hii ilichukuliwa kutokana na maandalizi ya Kombe la Dunia, Afrika Kusini na Olimpiki, China.
  Hilo kombe linatuusu nini sisi kama hufanyi kwa ajili ya wananchi wako!
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Kamala uwezo wa kuchambua mambo mdogo ndiyo maana WAHAYA walimpiga china hana vision
   
 8. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unafikiri wahaya wanakopesha ukisha kuwa fisadi au wakigundua Dr fake umeliwa. Muulize Kamala mwenye na kandamunagi (sorry Karamagi)!
   
 9. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,057
  Likes Received: 3,984
  Trophy Points: 280
  kwani je subsidizing cement hairuhusiwi pia? kama hivyo hiyo EA na ifie mbali kwavile haiwezekani nchi kama hii yenye limestones na other raw materials all over halafu cement izidi 10,000 huku ni kukosa maarifa
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wakuu nadhani Kamala hajui watanzania wengi hawana raha na huyu mdudu EAC,saruji lazima iteremshwe bei suala la mikataba itabidi wamtafute Muungwana ndiye aliyesaini bila kutazama maslahi ya nchi.
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Mbona mimi naona anajichanganya mwenyewe. Hivi kiwanda kitakufaje kwa ajili ya kupunguziwa ushuru?? Asichanganye ushuru na ruzuku. Kama viwanda vyetu vingekuwa vinategemea ruzuku then vingeweza kufa kama ruzuku ingeondolewa kama ilivyokuwa NMC n.k.
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Chinese kweli kweli.
  Yaani akili yake si ya kwake imechakachuliwa na dawa za kichina
   
 13. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  mbaya zaidi na hizo dawa za kichina zimechakachuliwa....yaan hapo ni full michakachuo!!
   
 14. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Halau waungwana mimi sijawahi kuona jumuiya ambayo viongozi wanatia saini bila wanachi kuridhia, sehemu zote palipo na jumuiya huanyika kura ya maoni kama wananchi wake wanakubali kujiunga nayo au la, sasa hii mbona wamejiamulia wenyewe bila kuwahusisha wananchi, hii nini jamani? Halafu jamaa kamala ni kilaza sana, iweje ushuru ukipungua kiwanda kinakufa, huu ni uchambuzi, make navojua kwa elimu yangu ndogo kwenye masuala ya kodi ni kwamba kodi huongeza garama za kutengeneza bidhaa, as a result kodi ikipungua then ile garama inapungua and then na bei pia hupungua, yeye alisoma wapi?

  Mtu kama huna point unakaa kimya and let other people analyse the whole aspect, sema tu watanzania ukiwa waziri basi ndo unajua kila kitu, hicho kipindi kilishapita, tupo kwenye zama nyingine, stone age is gone, acha data za kodi wazungumzie wanaojua kodi, Dr. Slaa hakukurupuka tu, vijana walifanya tathmini kwanza na manipulate implications zote na ndio maana akawambia watanzania tunaumizwa pasipo sababu. Au kwa sababu yeye nyumba alijengewa na mafisadi so hajui hata garama ya cement?
   
 15. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  jamani naomba tu nimcheke kamala maana hata wananchi wake wameonesha kuwa ni kilaza. poleni wana jamii forum haya naanza.....hahhahaha hahahha mbembbebembebe mmbahahajkkkssks manaa a mbuuuaa hahahahaahahahahhaaaaaaaaa. Poleni kwa makelele wana jf.
   
 16. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hawana jipya!kila kitu kwao hakiwezekani!kinachowezekana kwao ni kufanya ufisadi tu na si kuwaletea wananchi maendeleo!
   
 17. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  KAMALA NDO BADO ANASOMA PhD. HAJAWA DOCTOR, REKEBISHA TITLE. HATA HIVYO ANA MSONGO WA MAWAZO. KAMALA (BUMALA) MAANA YAKE 'SUMU YA KUWEKA KWENYE MISHALE'. MUONEENI HURUMA.
   
 18. minda

  minda JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ilishawekwa katika 'hukumu' ya tendwa kwa tafsiri yake pana ya sheria ya uchaguzi pamoja na mengine kwamba ahadi ni muhimu katika kampeni hizi.
  ni wazi hata bosi wake ameahidi mengi au tuseme ndio anampinga?
  mi naona kama anajichanganya mwenyewe kwa sababu yeye mwenyewe ni sehemu ya hizo 'litania' za ahadi katika kampeni.
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lakini pia inaelekea Dk kamala amesahau kuwa hiyo EAC protocol ni makubaliano ambayo si Biblia au Koran... kuna uwezekano wa kuibadili na kukubaliana mengine pia
   
 20. M

  MJM JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Jamaa kapauka kichwani balaa. Kamalaaaaaa Advanced Diploma in Economic Planning, Masters ya Uchumi na PhD fake kumbe ni fake kiasi hiki?
  1. Nani alimdanganya kinachopandisha bei ya bidhaa ni ushuru wa forodha tu?
  2. Hizo tax relief, incentives wanazotoa kwa wachumia tumbo (wawekezaji) na kodi bambikizi kwa watanzania zikirekebishwa kwa viwanda vya ndani bei haishuki?
  3. Kwani ameambiwa kila bidhaa lazima itoke nje ya nchi anakoongelea ushuru wa forodha?

  Poor Kamala. Rest in Political Peace. Rudi ukashike chalk. Lakini uanzie shule ukasome mwenyewe kwanza maana utaaibishwa kama ndiyo haya utakwenda kufundisha
   
Loading...