Ukiwa na ubongo ulio hai lazima utashangaa kwanini CCM ishindwe kumsaidia mtu aliyewasaidia kukidhohofisha chama chake mwenyewe, Dr Slaa hakuisaliti CHADEMA bali aliamua kusimamia kile anachokiamini.
Waafrika tuna shida kubwa ya kutokuwa na misimamo na ndio maana tumekuwa vigeu vigeu ktk mazungumzo na matendo yetu ya kila siku.
In fact hatujazowea kuwa na wanasiasa wanaosimamia kile wanachokiamini mwanzo mwisho,tumeshazowea uswahili uswahili na kwasababu hiyo basi wengi wenu mlitaka Dr Slaa afanye siasa za kiswahili swahili.
Dr Slaa angekuwa anafanya siasa za namna hiyo toka zamani nadhani CHADEMA wangepotea sana, ilihitajika kiongozi mwenye misimamo kama Dr Slaa kuweza kuivusha CHADEMA salama ktk misuko suko na dhoruba kali za kisiasa ilizokumbana nazo huko nyuma. Ila nyinyi wafuasi wa Mbowe hamuwezi kuyajua haya, very soon you are going to find out what you lost.