Sikuwahi kufikiria kwamba akina
Crashwise watakuja kumkejeli Dr Slaa na kumuabudu Lowassa kwa jinsi ambavyo huyu mzee alitumia juhudi na maarifa mengi ktk kukiimarisha hiki chama.
Mara hii wamesahau yote mazuri ambayo Dr Slaa aliyafanyia CHADEMA, eti wanamwita msaliti,mtu aliyekaa na CHADEMA kwa zaidi ya miaka 30,akikihudumu chama kama katibu mkuu kwa zaidi ya miaka 20 leo asiaminiwe halafu kuaminiwa mtu ambaye maisha yake yote alikuwa na CCM,kwa zaidi ya miaka 40. Kajiunga juzi tu na CHADEMA mara hii yeye ndio limegeuka kuwa Mungu ndani ya chama, kila goti la mfuasi, kada na mwanachama wa CHADEMA kwake litapigwa.
Kweli fedha ni sabuni ya roho, ukiwa mpigania uadilifu na ukweli kama Dr Slaa utadharaulika, ukiwa mtu mwenye tuhuma nyingi za ufisadi kama yule jamaa yetu maadamu una pesa basi hata magoti utapigiwa.