Dr. Slaa: Si mimi wala mke wangu aliyechukua Mkopo Benki, Nyumba yetu haijapigwa mnada

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
2.jpg

Katibu Mkuu wa Zamani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa ametoa majibu kuhusu taarifa zinazoandikwa kwenye baadhi ya magazeti nchini pamoja na mitandao kuwa nyumba yake iliyoko Mbezi jijini Dar es Salaam inauzwa baada ya kushindwa kulipa mkopo wa Benki ikidaiwa kuwa mkewe aliuchukua na kumpa mwanaume mwingine.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Mke wa Dk. Slaa, Josephine alichukua mkopo wa shilingi milioni 300 katika moja kati mabenki nchini na kushindwa kuirudisha fedha hiyo.

Dk. Slaa ambaye yuko nchini Canada akijiendeleza kimasomo, amekanusha taarifa hizo na kueleleza kuwa yeye na mkewe Josephine hawajawahi kuchukua mkopo katika benki yoyote nchini.
“Nataka nikuambie na uwajulishe Watanzania kwamba wala si mimi Dk. Slaa wala mke wangu, Josephine kwa wakati wowote ule hatujawahi kuchukua mkopo benki,” Dk. Slaa aliliambia gazeti la Mtanzania kwa njia ya simu.

“Tangu nitoke Bungeni sijawahi kuchukua hata senti moja benki, achilia mbali propaganda ya shilingi milioni 300.

" Hivyo, ni vizuri waliokupa taarifa wakupe undani ni benki ipi nilikopa au Josephine alikopa na ni shilingi ngapi na kwa nyaraka zipi.

"Na ni vema ukafuatilia benki husika pia kama walikuwambia ni benki gani,”Mwanasiasa huyo mkongwe alieleza.

Dk. Slaa ambaye alitangaza mwaka jana kustaafu siasa, alisema kuwa anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote walioandika habari hizo.
 
Hahahahaha, Hivi katika hali ya kawaida, mtu maarufu kama Dkt Slaa, nyumba yake ikipigwa mnada...tunadhani itakuwa siri!?

Maana minada yote hapa mjini inajulikana....hilo gazeti limeshindwa kuweka wazi taarifa za kutosha ikiwemo benki iliyokopwa, kampuni inayopiga mnada na hata picha tu ya nyumba yenyewe bila kusahau plot no.

Kwa sisi wazoefu wa kuandaa propaganda....tulielewa tu kuwa ni uzushi na hatukutaka kuchangia kwa namna yoyote katika uzushi huo. Nilicheka sana kuona Manyumbu yameingizwa choo cha kike.....Nayo yaliingia kirahisi sana. Teh Teh Teh.
 
Katibu Mkuu wa Zamani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa ametoa majibu kuhusu taarifa zinazoandikwa kwenye baadhi ya magazeti nchini pamoja na mitandao kuwa nyumba yake iliyoko Mbezi jijini Dar es Salaam inauzwa baada ya kushindwa kulipa mkopo wa Benki ikidaiwa kuwa mkewe aliuchukua na kumpa mwanaume mwingine.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Mke wa Dk. Slaa, Josephine alichukua mkopo wa shilingi milioni 300 katika moja kati mabenki nchini na kushindwa kuirudisha fedha hiyo.

Dk. Slaa ambaye yuko nchini Canada akijiendeleza kimasomo, amekanusha taarifa hizo na kueleleza kuwa yeye na mkewe Josephine hawajawahi kuchukua mkopo katika benki yoyote nchini.

“Nataka nikuambie na uwajulishe Watanzania kwamba wala si mimi Dk. Slaa wala mke wangu, Josephine kwa wakati wowote ule hatujawahi kuchukua mkopo benki,” Dk. Slaa aliliambia gazeti la Mtanzania kwa njia ya simu.

“Tangu nitoke Bungeni sijawahi kuchukua hata senti moja benki, achilia mbali propaganda ya shilingi milioni 300.

" Hivyo, ni vizuri waliokupa taarifa wakupe undani ni benki ipi nilikopa au Josephine alikopa na ni shilingi ngapi na kwa nyaraka zipi.

"Na ni vema ukafuatilia benki husika pia kama walikuwambia ni benki gani,” Mwanasiasa huyo mkongwe alieleza.

Dk. Slaa ambaye alitangaza mwaka jana kustaafu siasa, alisema kuwa anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote walioandika habari hizo.
 
Mashariki ya mbali Ni nchi kama China Japan na Korea,Dr Slaa yupo Canada huko Ni Marekani Kaskazini
Kiwavi hiyo Ni Jiografia ya darasa la tatu

Usiwe kama Nyumbu, bila kujali yupo Magharibi au Mashariki lengo ni kuonyesha yupo mbali na Tanzania.
 
Propaganda za ukawa, kuna kijarida flani nimeona title yake leo imeandika, mke wa slaa alicmchukulia mkopo mwanaume mwingine, vile vile ukaja uzushi mwingine kua anaseek asylum huko canada, kumbe kaenda kusoma, UFIPA ni kiwanda cha kutengeneza uongo.
 
Hivi kwani ikiwa ni kweli nyumba yake inapigwa mnada unadhani atasema? Ila namheshimu sana dr
 
Back
Top Bottom