JohnGalt,
Kwanza karibu jf, pili Dkt. Harith Ghassany mwenyewe ni memba humu, alishakileta humu hicho kitabu, kilichambuliwa kama karanga!.
Wanazuoni wa JF walimbana mwandishi kwa hoja left, right and centre, alishindwa kuzijibu hatimaye aliishia kukimbia!.
Kwa kukusaidia tuu, mimi ni mmoja wa waliokisoma hicho kitabu,kama ningekuwa ndio msimamizi wa thesis ya Ph.D ya huyu Dr, asingeipata ng'o kwa kujenga premise based on fasihi simulizi na kuigeuza fasihi andishi, wakati akifanya research yake,tayari ilishajijengea picha fulani kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,hivyo aliamua kuihalalisha picha hiyo kwa simulizi alizoziona ziko favaurable na mind opinion yake.
Mimi nilisema, napenda sana kusoma hadithi hivyo nilimshukuru mwandishi kwa kuwa ni story teller mzuri.
Hoja moja muhimu ambayo nilimpongeza ni kwa kuandika something kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, mengi hayajaandikwa na makovu hayajapona hivyo hitaji la truth and reconciliation commission lilikuwepo japo limeshapoozwa na GNU!.
Asante kutukumbushia, jf inasajili member wapya kila kukicha, hivyo acha wapya pia wapate na wasome.
Wakati huo huo tusisahau kuwa wengine ambao tunalazimishwa kuwasahau ni
Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu, Tewa Said Tewa,Ali Migeyo , Suedi Kagasheki,Dossa Azizi,Abdulkarim Karimjee,Chifu Abdieli Shangali wa Machame, Kleist Sykes,Ally Sykes na Abdulwahid Sykes
kwa uchache sasa huyo Okello alikwa ni just one in a million na at least eyey leo anazungumzwa
Huyu mtu aitwaye John Okello alikuwa ni mercenary, Kwa Kiswahili sanifu anaitwa Mamruki...! Sasa ni nchi gani ambayo imetumia majeshi ya kimamruki kupindua nchi kisha wakaitwa mashujaa!?
Ninavyojuwa mimi mamruki wote ukodiwa kwa kazi chafu yoyote na wakishalipwa biashara inakuwa imekwisha, sasa John Okello yeye alitaka kulowea kabisa na kutaka kutawala, sasa aliposhtukiwa ndio kama hayo yaliomkuta.
Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.
Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.
Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.
Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]
Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?
Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?
Pasco
asante kwa kuja na kuniweka sawa lakini kuna couple of things.
1. Nimetafuta threads zenye kuonyesha kitabu kilivyochambuliwa kama karanga sijazoja hata moja zaidi ya threads ambazo zinasema watu wakisome au wanarefer kama reference
In otherwords sijaona critical review of the book au thesis ya Ghassany
2. Naomba unipe walau mwelekeo wa hao wana zuoni wa JF maana at least naweza kuwauliza hata kwa PM wanionyeshe hizo post ambazo walizotoa kama ulivyosema hapo juu yaani LE,RIGHT & CENTRE
3. Je unaweza kunifafanulia at what point did Ghassany run away from hao "wanazuoni" wa Jamii Forum (baada ya kutolewa hoja gani?
4. Umesema kuwa wewe ni mmoja kati ya waliokisoma hiki kitabu na ungekuwa msimamizi wa thesis ya hii P/h D usigeitoa/ kwa sababu:
a) Thesis ilikuwa based on fasihi simulizi
b) Fasis simulizi kugeuzwa kuwa andishi
c) wakati akifanya research yake,tayari ilishajijengea picha fulani kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar
d)aliamua kuihalalisha picha hiyo kwa simulizi alizoziona ziko favaurable na mind opinion yake.
Mimi ninachosema ni kuwa kwanza ningependa kusoma Critical literary review yako on this book ili tuweze kuwa sambamba. Sasa kwa sababu hii ni scholarly work tena ameifanya akiwa mwanafunzi toka kwenye Chuo ambacho ni credible (HARVARD) sidhani kama hao waliomsupervise na hilo jopo la baraza lilokaa naye wakati anatetea hii academic work yake ni watu ambao hawakujua jinsi alivyofanya research yake na mwishowe wakamu award hiyo Doctorate yake. Mind you hii ni kazi ambayo ni NON-FICTION hivyo maswali ambayo obviously ile panel waliyafanyia kazi ili kujua yalikuwa ni:
1. Je Subject ilikuwa ni nini na hiki kitabu kilikuwa kinadeal na period gani?
2. Je how thorough Ghassany amekuwa katika research yake?
3. Je alitumia sources zipi?
4. Je hizo simulizi zilikuwa in broad/detailed?
5. Je style ya uandishi ni wa kigazeti gazeti (reportorial ) au ile ya interpretive writing? (ambayo inampa msomaji uelewa na ufafanuzi zaidi wa matukio)
6. Je thesis yenyewe iilikuwa na maana gani?
7. Je treatment ya hii thesis ni superficial au profound?
8. Je walengwa wa hiki kitabu walikuwa akina nani? ( vyuo vya elimu ya juu au ndio wale wale wasoma riwaya kama zile tunazozisoma magazetini?}
9. Kwa sababu ni kitabu kinachozungumzia mapinduzi je kuna biographical writing toka kwa Ghassany kwenye hiki kitabu?
10. Je Ghassany ameweka emphasise yoyote kwenye social or political history ?
11. Je tarehe zimetumiwa barabara ?
13. Je zipo maps, illustrations, charts, etc. kwenye kitabu if so je jopo la Harvard lilippitia au lilifanyia evaluation?
Kwa uelewa wangu mdogo hayo ndio machache ninayoyakumbuka nilivyofundishwa na mwalimu wangu (nakumbuka nilifanya mambo ya environmental Political Theory) na ilikuwa mara yangu ya kwanza kuambiwa nifanye critical review ya journal article fulani. Anyway tatizo kubwa ambalo nimeliona humu JF so far ni hili la kuwa BIASED based solely on prejudice na feelings ambalo kiini chake naona ni huko mashuleni ambako wanafunzi wetu wanatokea. It would be interesting kama hii forum ikawa na members wachache lakini inakuwa ni Agora ya mijadala yenye marefu na mapana kuliko the current trend ya kuogopa controversy (as long as watu wako within the Forum guidlines sioni sababu ya kufuta au kufunga threads) Maana kila thread niliyotafuta yenye posts za hiki kitabu ilikuwa imefungwa!
Sasa najua utakuwa uko bize na mimi hapa natazama hili panga la DFID kwa akina Lesotho, India na Burundi lililotangazwa jana.
Inaonyesha una utaalamu mkubwa juu ya masuala ya uandishi ingawa sijabahatika kuona kitabu chako chochote.
Haya unayoeleza/ unayouliza pengine ni masuala ya msingi lakini kwa sisi tuliobahatika kukisoma na kwa sababu yako tulioyashuhudia, tumeridhika kuwa ni kazi well done.
Kwanini hii kazi usiifanye wewe kama uko that much interested kuliko kuachia wengine kuifanya?
Hapa naona dalili za wivu lakini pia si mbaya sana.
"Kuuzunguka mbuyu si kazi, kazi kuukumbatia"
Wakati mwalimu wangu ananifundisha somo la historia nikiwa darasa la nne alitufundisha kwamba kiongozi wa mapinduzi ya zanzibar alikuwa field marshal john okello ambaye kwa asili yake alitokea uganda. Mwalimu wangu huyu alitueleza kwamba usiku wa mapinduzi huyu karume hakushiriki kamwe kwani alikuwa amejificha. Lakini katika kufuatilia historia ya mapinduzi ya zanzibar ni wazi karume hausiki na wala hastahili kuhenziwa kama shujaa wa mapinduzi yale. Ukweli utabaki, john okello ndiye kiongozi na shujaa wa mapinduzi ya zanzibar ya januari 1964. Hawa wanaohenziwa ni maghumashi tu ukizingatia historia halisi ya tanzania imefisadiwa kwa kiwango kikubwa.
hizi ndo shukran za viongozi wetu-maana wanachoweza wao ni kugeuza ukweli kuwa uongo,karumke hana mchango wowote kwenye mapinduzimwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru john okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.
Baada ya mapinduzi kufanikiwa john okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa zanzibar mzee karume na babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza john okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.
Baada ya hali kutulia okello anamtangaza karume rais na abdulrahman babu kuwa waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.
Baada ya siku chache mzee karume akamfukuza zanzibar kama mbwa john okello [field marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]
naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya john okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?
Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la field marshal dedan kimathi...mbona wapenda hitoria zanzibar na tanganyika kwa jumla hamumtendei haki john okello [fieldmashal]?