Serikali ya Zanzibar haioni kwamba inawajibika kuwafanyia kitu watu wa Field Marshall John Okello?

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Nov 22, 2022
1,689
3,259
Mapinduzi ya Zanzibar yaliendeshwa na bwana John Okello. Hili halina ubishi. Mapinduzi yalianza saa tisa za usiku yakiongozwa na Okello na watu mia kadhaa wakiwa na silaha za jadi.

Walivamia vituo vya polisi na huko ndiko walikopata bunduki. Kufika saa moja asubuhi Okello akatangaza redioni kuhusu mapinduzi huku akijitambulisha kama Field Marshall. Wakati huo wote Karume alikuwa yuko huku Tanganyika.

Kufupisha stori: Baada ya Karume kushika madaraka Okello alifukuzwa Zanzibar kwa kuzuiwa kuingia Zanzibar akitokea Tanganyika. Akaenda Kenya na baadaye Uganda akiwa kapuku.

Naelewa kwa nini Karume alimfukuza Okello, hata mimi ningefanya hivyo. Kwanza alikuwa mtu mkatili sana, mwenye kuongea maneno ya kikatili hasa. Wakati wa mapinduzi alikuwa akipiga kelele watu waue na kuchinja waarabu. Inasemekana waarabu zaidi ya 20,000 waliuawa. Wanawake walibakwa vibaya na kuuawa. Kuwa na mtu mkatili kama kichaa ni hatari sana. Alifaa kufukuzwa.

Waarabu waliochinjwa wakati wa mapinduzi.
1704993837675.png

Pia jamaa alifaa kufukuzwa sababu hakuendana kabisa na jamii ya wazanzibari, alikuwa ni wa kuja hasa. Alikuwa anapiga kelele akidai ni mkombozi wa kikiristo huku akiwa na lafudhi yake nzito ya Uganda. Kwa Zanzibar ambayo majority ni Waislamu hawakumuelewa kabisa swaga zake.

Sababu za kumfukuza Okello zinakubalika kabisa. Lakini mchango wake kwenye mapinduzi ya Zanzibar ni mkubwa sana. Huyu ndiye aliyewakomboa Wazanzibari kutoka ukandamizwaji wa serikali ya Sultani. Ndiye aliyewatoa unyonge wanahitaji kumshukuru. Serikali ya Zanzibar haioni kuwa inahitajika kuwafanyia kitu watu wa familia ya bwana Okello.
 
Historia mpya ya udini, watu 20,000 kwa wakati huo ni wengi sana kwani Dar haikua na watu zaidi ya 15,000, pia tuwe wakweli mauaji hayo hayakutokea na kama yalitokea makaburi yako wapi, propaganda za kijinga kwani Okello na ukristu wake asingeweza kuchinja watu wote hao.
 
Okello alikuwa kama kichaa(Wanamapinduzi wengi huwa namna hiyo) Idadi ya waliouawa bado inabishaniwa ila ukweli ni kuwa watu wengi walichinjwa. Si udini ila Okello alikuwa anajiona kama nabii mchinjaji.
 
Hao waarabu 20,000 waliochinjwa waweza share nasi makaburi yao walipozikwa?
 
Mapinduzi ya Zanzibar yaliendeshwa na bwana John Okello. Hili halina ubishi. Mapinduzi yalianza saa tisa za usiku yakiongozwa na Okello na watu mia kadhaa wakiwa na silaha za jadi. Walivamia vituo vya polisi na huko ndiko walikopata bunduki. Kufika saa moja asubuhi Okello akatangaza redioni kuhusu mapinduzi huku akijitambulisha kama Field Marshall. Wakati huo wote Karume alikuwa yuko huku Tanganyika. Kufupisha stori: Baada ya Karume kushika madaraka Okello alifukuzwa Zanzibar kwa kuzuiwa kuingia Zanzibar akitokea Tanganyika. Akaenda Kenya na baadaye Uganda akiwa kapuku.

Naelewa kwa nini Karume alimfukuza Okello, hata mimi ningefanya hivyo. Kwanza alikuwa mtu mkatili sana, mwenye kuongea maneno ya kikatili hasa. Wakati wa mapinduzi alikuwa akipiga kelele watu waue na kuchinja waarabu. Inasemekana waarabu zaidi ya 20,000 waliuawa. Wanawake walibakwa vibaya na kuuawa. Kuwa na mtu mkatili kama kichaa ni hatari sana. Alifaa kufukuzwa.

Waarabu waliochinjwa wakati wa mapinduzi.
View attachment 2868847

Pia jamaa alifaa kufukuzwa sababu hakuendana kabisa na jamii ya wazanzibari, alikuwa ni wa kuja hasa. Alikuwa anapiga kelele akidai ni mkombozi wa kikiristo huku akiwa na lafudhi yake nzito ya Uganda. Kwa Zanzibar ambayo majority ni Waislamu hawakumuelewa kabisa swaga zake.

Sababu za kumfukuza Okello zinakubalika kabisa. Lakini mchango wake kwenye mapinduzi ya Zanzibar ni mkubwa sana. Huyu ndiye aliyewakomboa Wazanzibari kutoka ukandamizwaji wa serikali ya Sultani. Ndiye aliyewatoa unyonge wanahitaji kumshukuru. Serikali ya Zanzibar haioni kuwa inahitajika kuwafanyia kitu watu wa familia ya bwana Okello.
Naunga mkono hoja
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Okello alikuwa kama kichaa(Wanamapinduzi wengi huwa namna hiyo) Idadi ya waliouawa bado inabishaniwa ila ukweli ni kuwa watu wengi walichinjwa. Si udini ila Okello alikuwa anajiona kama nabii mchinjaji.
Inakuongezea nini kwenye uislamu wako, Okello aliwezaje kuwachinja wazanzibari ambao walimpindua mwarabu! Huu ni ujinga na upumbavu, nia ni kumfanya mkristu mmoja aonekane aliwaua wazanzibari 20,000!
 
mjadala huu unakuwepo kila mwaka na wala hakuna suluhisho.
Historia mpya ya udini, watu 20,000 kwa wakati huo ni wengi sana kwani Dar haikua na watu zaidi ya 15,000, pia tuwe wakweli mauaji hayo hayakutokea na kama yalitokea makaburi yako wapi, propaganda za kijinga kwani Okello na ukristu wake asingeweza kuchinja watu wote hao.
mauaji yalitokea kweli ijapokuwa idadi haijulikani, na wala usipinge kwani hata Okello mwenyewe kwenye kitabu chake aliandika, sasa wewe kama unataka makaburi kamuulize yeye mwenyewe huko aliko kwenye kaburi lake.

Huo ugalatia sijui umetokea wapi lakini hata wale waliopiga picha za hao maiti walikuwa ni wataliana, ilitokea tu kwamba walikuwa wanaandika documentary kuhusu Afrika (Africa addio?) na walikuwepo kwenye eneo la Afrika ya Mashariki ndiyo wakachukua filamu hizo. Na hiyo ndiyo filamu pekee iliyoko kuhusu mapinduzi.

Sasa hao wataliana nao walikuwa ni waislamu?
 
hata wale waliopiga picha za hao maiti walikuwa ni wataliana,
Documentary zipo nyingi nyingine zimefichwa wewe hauwezi kuonyeshwa wamechukua wakaenda kuzificha, Ila kuna kitu kimefichwa kwenye haya Mapinduzi siku moja kitawekwa wazi maana naona km kuna watu wanahisi wao ndio walioonewa yaan wao ndio waliopinduliwa sio Sultan Ila Sisi kiini macho tunaambiwa Sultan ndie aliepinduliwa
 
mjadala huu unakuwepo kila mwaka na wala hakuna suluhisho.

mauaji yalitokea kweli ijapokuwa idadi haijulikani, na wala usipinge kwani hata Okello mwenyewe kwenye kitabu chake aliandika, sasa wewe kama unataka makaburi kamuulize yeye mwenyewe huko aliko kwenye kaburi lake.

Huo ugalatia sijui umetokea wapi lakini hata wale waliopiga picha za hao maiti walikuwa ni wataliana, ilitokea tu kwamba walikuwa wanaandika documentary kuhusu Afrika (Africa addio?) na walikuwepo kwenye eneo la Afrika ya Mashariki ndiyo wakachukua filamu hizo. Na hiyo ndiyo filamu pekee iliyoko kuhusu mapinduzi.

Sasa hao wataliana nao walikuwa ni waislamu?
Hoja yangu ni idadi ya watu 20,000 Zanzibar kwa wakati huo ni kubwa sana karibu ya nusu ya idadi ya watu Dar es Salaam kwa wakati huo.
 
Back
Top Bottom