Kisa cha Al Habib Umar bin Sumeyt na ''Field Marshal John Okello''

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
Siku chache zilizopita niliandika hapa kuhusu John Okello na pia nikaweka na video inayoeleza safari ya Okello Pemba mwezi Machi 1964 baada ya mapinduzi.

Sharif Mohamed Yahya kutoka Tanga kaniandikia hayo maneno hapo chini na kaandika kwa herufi kubwa tupu.

Nami nabakisha hivyo hivyo herufi kubwa kama nilivyopokea:

KUNA JAMBO JENGINE HALIZUNGUMZWI PIA KUHUSU AMRI ZA OKELLO.

PALE ALIPOTOA AMRI KALI KUHUSU MTAA WA MALINDI WAJITOKEZE WAMEPIGA MAGOTI NA YEYE ATAPITA HUKO KUKAGUA.

HABIBU UMAR BIN SUMEYT AKAWA WA KWANZA KUTOKA NA KUPIGA MAGOTI.
WAKAMNASIHI WATU ARUDI NDANI AKAGOMA.

WAKAENDA KWA KARUME, KARUME AMTUMA BABU AKAMUONDOE NA ZIARA HIYO IKAFUTWA.
WAMESEMA WENYE KUSEMA KUWA HAPO NDIO ULIKUWA MWANZO WA MWISHO WA OKELLO.

1692788060830.png

Asante sana kwa kisa hiki na taarifa hii

P
 
P,
Taarifa hii haiko sawa Jussa amenifahamisha nami nakuwekea aliyoniandikia:

"Ni kweli John 0kello alitoa tangazo kuwa watu wote wa Malindi watoke na wajipange barabarani na kwamba atapita hapo yeye na akipita wamsujudie.

Habib Omar bin Sumait na yeye akatoka. Watu wengi walimwambia yeye asitoke lakini akasema ilivyokuwa amri ni kwa watu wa Malindi na yeye ni mmoja wao basi atatoka. Akatoka yeye na aila yake (wakiwemo alokuwa akiwalea).

Isipokuwa yeye alipotoka watu walimwekea kiti ili asisimame. Akawa amekaa kwenye kiti.

Waliokuwepo wanasema ilikuwa taharuki kubwa kumuona Habib Omar bin Sumait na yeye ametoka nje na ikawa wanawaza itakuwaje atakapopita John Okello.

Kabla ya Okello kuja, akapita Mussa Maisara akiwa kwenye gari na alipoona ile hali, akatangaza kuwa watu wote warudi majumbani.

Habib Omar hakupiga magoti kwa mtu yeyote.

Kisa hichi mimi kwanza nilisimuliwa na bibi mmoja aliyelelewa na Habib Omar na ambaye walikuwa pamoja barabarani pamoja na watu wengine wa aila ya Habib Omar siku hiyo ya tukio. Na baadaye nikaja kukisoma kwenye kitabu cha Bi Fatma Mohamed Salim Jinja 'Gone With The Tide'."

Fasihi simulizi vs fasihi andishi,
maadam Sharif Mohamed Yahya amekuandikia na wewe uliwahi kusoma mahali, then fasihi andishi ndio the correct details, taarifa ya Jussa ni fasihi simulizi, fasihi andishi is more trustworthy than fasihi simulizi, ndio maana bado tunasisitiza mashuhuda ndio wasimulie, waandishi waandike toka kwa mashuhuda na sio wasimuliwa!.
Hakuna ubishi kuhusu Habib Omar bin Sumait alitoka nje, jee ni akasimama, alikaa kwenye Kiti au alipiga magoti?.

Pascal...
Muhimu katika kadhia hii ni kule Okello kufikia kibri cha kiasi kile.
 
Kiburi sii muungwana!, nilisikikiza zile amri zake za matangazo ya Redio pale Karume House, wakati akitangaza Mapinduzi ya Zanzibar, kiukweli... tuache tuu.

Ila pia kiukweli Tanzania tuna dini Kuu mbili, viongozi wetu wakuu wa dini fulani, always ni waugwana sana, na wa dini fulani ni viburi!, angalia sasa viburi walipo na waungwana walipo!.

Hata humu JF, watu tunapaswa kujifunza, baadhi ya sisi viburi, tupunguze viburi kwenye minikasha yetu, tujitahidi kuwafuata waungwana wetu humu, wewe Maalim ukiwa ni mmoja wa waungwana wakuu humu.
Ubarikiwe sana
P
 
Siku chache zilizopita niliandika hapa kuhusu John Okello na pia nikaweka na video inayoeleza safari ya Okello Pemba mwezi Machi 1964 baada ya mapinduzi.

Sharif Mohamed Yahya kutoka Tanga kaniandikia hayo maneno hapo chini na kaandika kwa herufi kubwa tupu.

Nami nabakisha hivyo hivyo herufi kubwa kama nilivyopokea:

KUNA JAMBO JENGINE HALIZUNGUMZWI PIA KUHUSU AMRI ZA OKELLO.

PALE ALIPOTOA AMRI KALI KUHUSU MTAA WA MALINDI WAJITOKEZE WAMEPIGA MAGOTI NA YEYE ATAPITA HUKO KUKAGUA.

HABIBU UMAR BIN SUMEYT AKAWA WA KWANZA KUTOKA NA KUPIGA MAGOTI.
WAKAMNASIHI WATU ARUDI NDANI AKAGOMA.

WAKAENDA KWA KARUME, KARUME AMTUMA BABU AKAMUONDOE NA ZIARA HIYO IKAFUTWA.
WAMESEMA WENYE KUSEMA KUWA HAPO NDIO ULIKUWA MWANZO WA MWISHO WA OKELLO.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P
 
Back
Top Bottom