Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,380
8,301
Mwaka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.

Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.

Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.

Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]

Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?

Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?

1332A8BF-A6E5-4160-B936-43321E10066E.jpeg


==============
Siku Field Marshal John Okello ‘alipotimuliwa' Zanzibar

YAFUATAYO ni masimulizi mafupi ya kipindi kifupi cha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari, 1964 yaliyoipindua serikali ya ubia ya chama cha Zanzibar Nationalist (maarufu Hizbu) na kile cha Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP). Tunaangazia nini hasa kilitokea usiku wa Jumamosi Januari 11, yaliyojiri siku ya pili yake na mwezi mzima wa Januari, mwaka 1964 .

Tumeyakusanya masimulizi haya baada ya kuzungumza na walioshiriki katika Mapinduzi hayo ambao baadaye walisaidia kudhibiti madaraka na kuunda taasisi zilizoziba pengo la Serikali iliyopinduliwa ya Waziri Mkuu, Muhammed Shamte Hamadi.

Usiku wa manane wa Januari 11, makada wapatao 200 wa Umoja wa Vijana wa Afro-Shirazi (Afro-Shirazi Youth League) walielekea kwenye kambi ya polisi ya Ziwani, nje kidogo ya mji huko Unguja.
Wakiongozwa na Yusuf Himid wapinduzi hao hawakukabiliwa na upinzani walipofika Ziwani ila waliikuta ghala ya silaha iko wazi na wakazinyakua silaha na kukimbia nazo hadi kwenye uwanja ulio nje ya jengo la Raha Leo.

Hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache na ndipo wapinduzi walikokuwa wakipewa silaha. Studio za redio ya Serikali pia zilikuwa hapo.

Moja ya sababu zilizoyafanya Mapinduzi yafanikiwe haraka ni uamuzi wa viongozi wa Serikali iliyopinduliwa - Sheikh Muhammed Shamte na Sheikh Ali Muhsin Barwani - kuwataka wafuasi wao wasitumie nguvu kuyapinga.
Hivyo, mbali na mapigano yaliyozuka saa za asubuhi ya Jumapili Januari 12, mbele ya Steshini ya Polisi Malindi, hapajazuka mapigano Unguja kati ya waliopindua na waliopinduliwa. Pemba nako pia hakukuwa na upinzani ijapokuwa kisiwa hicho kilikuwa ngome ya vyama vya ZNP na ZPPP.

Wengi wa wapiganaji waliokuwa kwenye Stesheni ya Polisi ya Malindi walikuwa wakuu wa polisi Wakiingereza. Wakipigana na makada wa Umma Party ambao ndio pia waliouteka uwanja wa ndege, bandari pamoja na kituo cha mawasiliano ya nje cha Cable & Wireless, kilichokuwa kwenye jengo ambalo sasa ni Hoteli ya Serena Mji Mkongwe.
Kwa hakika, kinyume cha baadhi ya watu walivyoandika hapakutokea mauaji ya kimbari. Aliyeanzisha uvumi huo alikuwa John Okello aliyeandika kwenye kitabu chake kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kwamba watu zaidi ya elfu kumi waliuliwa. Okello aliongeza kwamba aliamrishwa na Yesu Kristo kuwakomboa ‘Waafrika' wa Zanzibar kutoka kwa ‘wageni'.

Tutamrejelea Okello na wengine waliokuwa Raha Leo baadaye. Kwanza tukumbushe kwamba mkesha wa Januari 12, mwaka 1964, Zanzibar haikuwa na jeshi. Kulikuwa polisi waliokuwa wakiongozwa na Waingereza. Wengi wa askari polisi walikuwa raia wa Tanganyika. Serikali iliyopinduliwa ilikataa kuandikiana mkataba wa kijeshi na Uingereza kwa sababu ikihisi mkataba kama huo utaonekana kuwa wa kikoloni.
Hatuwezi kusema ni nani hasa aliyepiga risasi ya mwanzo au ya mwisho katika Mapinduzi. Naitoshe tusemapo kwamba kwa vile hakukuwa na upinzani, Serikali iliyokuwa madarakani iliporomoka kama ‘nyumba ya karata'.

Tuwarejelee sasa waliokuwa Raha Leo, makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache. Kwanza tumuangalie Okello ambaye sauti yake ndiyo iliyokuwa ikivuma kwenye Redio Zanzibar.
Hatuna uhakika nani alimpeleka Okello Raha Leo. Wengine wanasema ni Yusuf Himidi. Wengine wanasema ni Seif Bakari aliyetoa rai atumiwe kutoa matangazo kwenye redio kwa vile sauti yake ilikuwa na lafudhi ngeni ya kutisha.
Uhakika tulio nao ni kwamba Okello alipotokea Raha Leo na mabastola yake, Aboud Jumbe alishtuka na akauliza: "Nani huyu? Katokea wapi?"

Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 27 hakujulikana kabla ya Mapinduzi. Alikuwa mtu asiyejua kuandika wala kusoma na akili zake zikimtosha mwenyewe. Hakuwa na sifa za uongozi na wala hakushiriki katika vuguvugu lolote la kisiasa.

Akijibandika cheo cha kijeshi cha Field Marshall ni yeye aliyetangaza kwamba serikali ya ZNP/ZPPP imepinduliwa.
Kwa hakika, kazi hiyo ya kutangaza kufanikiwa kwa Mapinduzi kwanza alipewa Ramadhan Haji, mmoja wa wapinduzi. Lakini alikataa. Jina la Okello lisingelisikika lau Ramadhan Haji angekubali kutangaza kwamba Serikali imepinduliwa na kwamba wapinduzi waliidhibiti nchi.

Waliokuwa wakiongoza mambo Raha Leo tangu Mapinduzi yaanze, hadi Jumatatu Januari 13, walikuwa Aboud Jumbe, mmoja wa viongozi wa chama cha Afro-Shirazi (ASP), Thabit Kombo (Katibu Mkuu wa ASP) na Badawi Qullatein wa Umma Party. Muda wote huo, Sheikh Abeid Amani Karume (kiongozi wa ASP), Abdulrahman Babu (mwenyekiti wa Umma Party) na Abdalla Kassim Hanga (ASP) walikuwa Dar es Salaam.
Mnamo siku hizo hizo liliundwa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri lililokuwa na mamlaka kamili ya kuiendesha Zanzibar. Mabaraza hayo mawili yalikuwa taasisi kuu za Serikali ya kimapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Na sio ile iitwayo ‘Kamati ya Watu Kumi na Nne' ambayo baadhi ya watu wanasema kuwa ndiyo iliyoandaa Mapinduzi.

Okello akipenda kujigamba kwamba ndiye aliyeyapanga na kuyaongoza Mapinduzi. Alikuwa akitoa matamshi ya kushtusha na ya ajabu-ajabu kwenye Redio Zanzibar. Kwa mfano, siku moja alidai kwamba alipwe mshahara mkubwa zaidi ya aliokuwa akilipwa Rais Karume. Siku nyingine akasema kwamba kasri zote alizokuwa akitumia sultani kupumzikia apewe yeye.

Kuna siku aliyotoa hukumu kwamba mzee mmoja wa zaidi ya miaka 60 afungwe kwa miaka 99. Alisema kama huyo bwana atakufa gerezani basi mwanawe afungwe ili kuendeleza kifungo na mwanawe akifa basi mjukuu wake afungwe mpaka itimie miaka 99.

Nyakati nyingine aliwaonya watu wazitie moto familia zao na wao wenyewe mpaka wafe ‘kabla ya majeshi yangu kuja.' Alikuwa akitoa vitisho visivyowahi kamwe kusikika Zanzibar.
Kuna siku alitangaza kwamba wakazi wa eneo moja ambako alikuwa apite, wajipange foleni barabarani wakiwa wamevaa chupi tu.

Okello alikuwa ni adha, kitisho, kichekesho na fedheha kwa Zanzibar. Viongozi wapya wa nchi walichoka naye na wakaamua kumchukulia hatua. Salim Rashid, mmoja wa viongozi wa Umma Party aliyekuwa katibu wa Baraza la Mapinduzi anasema kwamba, kwanza alilizungumza suala la Okello na Sheikh Karume. Halafu akalizungumza na Brigadia Yusuf Himid na mwisho yeye, Yusuf Himid na Kanali Ali Mahfoudh wakalitafutia dawa.

Ilisadifu kuwa siku moja Okello alisafiri kwenda Dar es Salaam akifuatana na Jaha Ubwa, aliyekuwa katibu wake. Walipokuwa wanatarajiwa kurudi Zanzibar, Karume, Yusuf Himid, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walikwenda uwanja wa ndege kumsubiri.

Siku hiyo anaikumbuka vizuri Luteni Hashil Seif aliyekuwa ofisa wa zamu kwenye kambi ya jeshi huko Migombani karibu na uwanja wa ndege. Alipigiwa simu akitakiwa aende kwa haraka uwanja wa ndege. Hakuambiwa anaitiwa nini.
Alipofika ndipo alipoambiwa kwamba kuna ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya Mashariki iliyokuwa inakuja kutoka Dar es Salaam ndani yake wakiwemo pia Okello na Jaha Ubwa. Akaelezwa kwamba awaruhusu abiria wote pamoja na Ubwa washuke, lakini amzuie Okello asishuke. Halafu amwambie rubani ampeleke Okello Kenya.

Hashil naye akampigia simu komredi mwenzake Luteni Amour Dugheshina kumwita aende uwanja wa ndege amsaidie. Maluteni wote wawili walikuwa na bunduki za aina ya ‘machine gun'.

Ndege ilipotua walipanda ndani ya ndege, wakampokonya silaha Okello na kutekeleza amri waliopewa. Rubani wa ndege alikasirika sana. ‘Uso wake ulighadhibika, utafikiri mnyama aliyekosewa risasi,' alieleza Hashil.
Lakini rubani hakuwa na la kufanya ila kuiwasha ndege na kuelekea Kenya.
Huku nyuma Salim Rashid akampigia simu Oginga Odinga, Makamu wa Rais wa Kenya, kumuarifu kwamba wamemfukuza Okello na ‘wanamrejesha' Kenya. Alifanya hivyo kwa makosa kwa sababu kutokana na jina lake akifikiri kuwa Okello ni Mjaluo kutoka Kenya.

Kumbe alikuwa mtu wa kabila la Acholi aliyezaliwa Uganda na alikwenda Unguja kabla ya kuhamia Pemba ambako alikuwa mwashi, mtiaji rangi nyumba na mpasuaji mawe.

Swali la kujiuliza hapa ni; je, iwapo kweli Okello alikuwa ‘kiongozi mpendwa wa Mapinduzi' ilikuwaje wafuasi wake na wanamapinduzi wenzake wasimtetee alipoadhiriwa uwanja wa ndege na kufukuzwa nchini? Ilikuwaje akafukuzwa kwa urahisi hivyo?

Kuna uzushi mwingi kuhusu kipindi hiki kifupi cha historia ya Zanzibar. Kwa mfano, kuna filamu ya kubuni ya Wataliana inayoonyesha maiti chungu nzima za watu waliopigwa risasi. Filamu hiyo ilikuwa na lengo moja tu; kuonyesha ‘ukatili na unyama wa Waafrika.'
Hakuna ithibati yoyote kwamba watu waliouawa katika siku za mwanzo za Mapinduzi walifika elfu kumi. Ukweli ni kwamba jumla ya watu waliouawa siku hizo haipindukii 200, katika sehemu za mjini hawazidi 25.

Uzushi mwingine ni kwamba walipelekwa Watanganyika, Zanzibar wakiwa na silaha kwenda kupindua. Na si kweli kwamba Mapinduzi yalikuwa na msisitizo wa kikabila. Katika kipindi cha mwanzo cha Mapinduzi msisitizo ulikuwa wa kitabaka. Nyimbo zilizokuwa zikiimbwa kwenye Redio Zanzibar zikiwazungumzia ‘wakwezi na wakulima' na wafanyakazi kwa jumla na si makabila.

Mapinduzi ya Zanzibar yalianzisha taasisi mpya za utawala zikiwa pamoja na Baraza la Mapinduzi, Baraza la Mawaziri na ofisi ya Rais. Taasisi hizo zilikuwa zifanye kazi kwa muda wa mwaka mmoja tu kwa vile ilikwishaamuliwa kwamba Januari 1965 pafanywe uchaguzi wa kulichagua Bunge la Katiba, lililokuwa litunge Katiba ya kudumu ya Zanzibar.
Baraza la Mapinduzi la Zanzibar pamoja na Serikali mpya zilianza kwa ubia baina ya chama cha ASP na Umma Party.

Ingawa wanachama wa ASP ndio waliofanya Mapinduzi waliutambua mchango wa wafuasi wa Umma Party na hasa mchango wa makada wao waliopata mafunzo ya kijeshi nchini Cuba.
Vijana hao wa Umma walizitia wasiwasi serikali za Marekani na Uingereza na kuzifanya ziamini kuwa utawala mpya wa Zanzibar ulikuwa wa ‘kikomunisti'. Dhana hiyo ndiyo iliyosababisha kuchukuliwa hatua ya kuyachimba na kuyagandamiza Mapinduzi ya Zanzibar yaliyodumu kutoka Januari 12, hadi 26 Aprili, mwaka 1964.

Ahmed Rajab RAIA MWEMA 22-February, 2012


Video ikimwonesha Okello,Karume na Babu masaa machache baada ya Mapinduzi

 
Last edited by a moderator:
Philemon umesema ukweli,

Historia ya Tanzania imekuwa na tabia ya kufuta michango ya wale ambao hawakupendwa na wakubwa: John Okello akiwa mmoja wao.

Ingawa sijasoma maandiko yaliyopo kuhusu historia ya Tanzania kwa muda mrefu ukweli wa kuwa majina kama ya Okello, Kambona, na Kanali Mahafudhi yamefutika kabisa katika historia ya Tanzania. Bibi Titi Mohammed alipata bahati baada ya kurudi CCM na hivyo kurudisha jina lake katika historia lakini nalo lilikuwa limeshapotea.

Tutafute utaratibu wa kutunza historia kamilifu ya nchi bila kujali uhusiano wa wahusika na "ukoo wa mfalme" ulikuwaje.
 
Wakati huo huo tusisahau kuwa wengine ambao tunalazimishwa kuwasahau ni
Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu, Tewa Said Tewa, Ali Migeyo , Suedi Kagasheki, Dossa Azizi, Abdulkarim Karimjee,Chifu Abdieli Shangali wa Machame, Kleist Sykes, Ally Sykes na Abdulwahid Sykes.

Kwa uchache sasa huyo Okello alikwa ni just one in a million na at least eyey leo anazungumzwa.
 
Maprofessa mahiri wetu mko wapi kwa historia ya kweli,upo wapi haroub othman,proffesa mazrui, baregu na wengine tele wasomi..wanazuoni.

Historia ya mataifa yetu hapa afrika mashariki imepindishwa, andikeni upya.
kwa nini tunawafundisha watoto uwongo?
 
phillemon mikael said:
Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa zanzibar ...john okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio zanzibar,...baada ya siku chache mzee karume anamfukuza zanzibar kama mbwa ...


YAITWAYO "MAPINDUZI"

John Okello alitoka kwao Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka Tanganyika, na kuivamia nchi huru usiku wa manane wa kuamkia tarehe12 Januari 1964. Wananchi, mafisadi kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao hawakuhisi uchungu kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza roho za wazee wao, za ndugu zao na za marafiki zao. Kwa mujibu wa kitabu cha huyo aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi' ya Januari 12, 1964, John Okello, amesema kuwa watu waliyokufa katika 'mavamizi' hayo ni 13,000. Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja.

Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi vilivyokuwa na ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata kuhadithika. Wengi waliokuwa wanaijua Zanzibar, waliona taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia yametokea Zanzibar kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'. Ilifika hadi, siku hiyo ya 'mavamizi' washenzi na makatili hao kuwanajisi maiti wa kike.

Kitendo hicho hakijawai kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni zenye ubinaadamu na ustaarabu wake. Lenye kuzidi kushangaza na kusikitisha ni kumsikia mwananchi mwenye kujulikana kuwa yeye ndiye mwongozi wa hao wenye kujiita "progressives" akasema kuwa, watu waliyouliwa katika hayo yenye kuitwa 'mapinduzi' ni 491! Duh!

Mwenyewe Okello alieongoza hayo mauwaji amesema kuwa wamekufa wananchi 13,000. Hata wangekuwa watano tu, bali ni binaadamu, ni wananchi, jee, ndio wawe wamestahiki kuuliwa kwa kuvamiwa nchi yao na wageni ambao wewe na wenzio kama wewe mmechanganyika na hao wageni katika kuifisidi nchi na wananchi wake? La kustaajabisha zaidi - ni pale ilipojulikana kuwa haya yote yalipangwa kabla - kwa siku 30 tu yaaani Desemba 10 mpaka Januari 11 ilitosha kujuwa uovu wa Serikali hata ikastahiki kupinduliwa? Hata ingelikuwa ni ovu hivyo, bali njia za kuiondowa za kikatiba zilikuwepo ambazo zingaliweza kutumika, khasa na hao Wapinzani. Haikuhitaji hata kidogo kutumia nguvu. Lakini hakika khasa ni kuwa mambo yalikwisha pangwa zamani, hayo yalikuwa ni matekelezo tu!!
 
drwho,

Good question. Atupe source yake siyo kuandika tu yale anayoyafikiria moyoni mwake. Kama asemavyo rafiki yangu FD lazima uangalie kila upande wa shillingi, lakini toa source.
 
Maana kuna watu kibao walikuwa mashujaa wa Tanzania waliachwa ka kusudi wakati wanaandika historia sasa hizi kelele za Okello naona haziishi

Iweje watu kama akina Suedi Kagasheki na Dosa Aziz wasipewe kipaumbele wakati Okello mnataka kumfanya Mungu Mtu?

Charity begins at home na tunao our sons and daughters ambao walipigania na kumwaga damu zao pale lakini husikii kitu.
 
Okello was a foreigner lakini kazi yake ilipokwisha akaambiwa kuwa muda wake ushaisha aanze

Sasa kuna jopo linaanza ku re write history

Huko nyuma walifanya hayo na leo hii wanarudia hayo hayo.
 
Besty,

Tulia kwanza, are you allright?!?, tunazungumzia utaifa, Znz ni taifa sio kabila, dalili za kupenda ukabila ni dalili za ubinafsi na ufinyu wa kufikiri.

FD

Kuna sehemu ambayo nimezungumzia ukabila? au umeshindwa kuelewa nilicho andika? Fikiri kabla ya kujibu tafadhali, kina Chief Mkwawa, Mangi Sina, Mangi Mandara, Wakina Chief Songea Mbano na Chief Chabruma wa kule Ruvuma, au Saidi Milambo wa tabora, wakina Isike, Kinjekitile, au Chief Masanja, Chief Mataka wa kule kwa wayao hawa ni alama ya taifa letu la Tanzania na ndio hawa tunapaswa kuwaenzi, watu hawa walionyesha uzalendo wa hali ya juu kulitetea Taifa letu la Tanganyika.
 
Mzee Philemon ahsante kwa kutoa topic hiii.Kwa ukweli mchango wa Okello katika mapinduzi ya waafrika umesahaulika sana.Inatakiwa ijengwe sanamu kubwa ya Okello kwa kuwa naamini kuwa huyu ni shujaa na jasiri mkubwa kuliko wote afrika ya mashariki,sidhani kama kuna mwanamapinduzi yoyote anayemkaribia huyu.

Bahati mbaya mafanikio yake yametekwa na karume na wengine....lakini naamini Tanzania na Zanzibar tutamkumbuka mtu huyu miaka ijayo..wakati wanahistoria wetu watakapoacha mtindo wao wa kuchanganya historia na siasa.

Ndio watu wengi walikufa,lakini revolution sio tea party,watu wanakufa lakini mafanikio ya kuondoa tabaka la makupe ambao waliwatweka wazanzibari mika zaidi ya 500 ya utumwa sio mchezo.

Cha kushangaza, 'wanahistoria' wetu wa so called udsm no one among them has ever written anything on Okello,wenywewe huangalia 'mashujaa' wa nje tu.

Ni aibu kubwa kwa watanzania!!!

Ahsante Phil kwa insight yako!!
 
kina Chief Mkwawa, Mangi Sina, Mangi Mandara, Wakina Chief Songea Mbano na Chief Chabruma wa kule Ruvuma, au Saidi Milambo wa tabora, wakina Isike, Kinjekitile, au Chief Masanja, Chief Mataka wa kule kwa wayao hawa ni alama ya taifa letu la Tanzania

Kweli machifu wetu hawa walionyesha uzalendo halisi , bila influence yeyote ya nje, licha ya kuwa jamii zao ziliishi kwenye 'ujima' (afrika ya leo, wapinzani/wanaharakati wengi, hubebwa na wageni). Chifu tuliyefundishwa kumtukana, Mangungo wa Msovero, aliyeuza ardhi kwa wageni, leo hii warithi wake tunawasifia kwa kuinua uchumi:mad: :D
 
[URL="home.globalfrontiers.com/zanzibar/nine%20hour%20revolution.htm"]home.globalfrontiers.com/zanzibar/zanzibar_revolution.htm[/URL]

Please members, go through these catches above. I am afraid to say that Mapinduzi yanayosheherekewa lewa its just a nightmare, I dont see anywere unless in zanzaibar gorvernment side of story the role of abeid karume and fellows in revulution, walijificha hadi kina Okello walipomaliza kazi ndio wakaibuka. Revolutionarry gorvernment should come out watuambie kwa nini hawataki kumsikia okello na pia inaonekana wwaliopigana kikweli hawajaenziwa.
 

Similar Discussions

38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom