Mjue John Okello aliyeongoza mapinduzi matukufu ya Zanzibar. - Sylvanus Kamugisha

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,882
155,863
1705055804318.jpg

MWANAMAPINDUZI JOHN OKELLO

John Okello ambaye aliongoza Mapinduzi ya Zanzibar alizaliwa mwaka 1937 huko Uganda katika kabila la Lang'o ambalo pia ni la Rais wa Zamani wa Uganda Milton Obotte. Alizaliwa akiitwa John Gideon Etuku. Wazazi wake walifariki Akiwa bado mdogo na kulazimika kwenda kulelewa na mjomba wake pamoja na wadogo zake wawili lakini kutokana na utukutu wake hakuweza kuishi kwa mjomba sababu alikuwa akipigwa na akakimbia kwenda kuanza vibarua huko Soroti katika Gineri ya kuchambua pamba. Inasemekana alitaka kwenda kujiunga na jeshi lakini hakufanikiwa kutokana na umri mdogo.

Katika harakati za kutafuta maisha alifika hadi Nairobi nchini Kenya na kuendelea hadi Mombasa ambapo alikuwa ukifanya kazi za vibarua. Alichukia kiuitwa boy , mtumishi, au mtumwa . Mwaka 1955 aliwekwa gerezani huko na akiwa humo alikutana na wapiganaji wa maumau waliokuwa wakipinga Ukoloni nchini Kenya kutoka kwao alipata hamasa ya Kupambana na ukoloni na ukandamizaji.

Mwaka 1959 akiwa na rafiki yake Mluo walienda Pemba katika eneo la Vitongoji na akawa anafanya kazi ya kugonga na kuuza mawe. Huko alipendwa na kuwa na ushawishi na ndipo alipoanza kuonesha nia yake ya kuuondoa utawala wa Sultan. Wakati anaondoka Pemba alipatia chama cha ASP nyumba yake ili waifanye ofisi ya chama.

Mwaka 1963 alihamia Unguja na kuanza kufanya kazi za kupaka rangi nyumba pamoja na kufanya kazi katika kiwanda cha kuoka mikate na akaendelea na vuguvugu la kisiasa.

Kumekuwa na Tetesi kuwa aliwahi kuwa mwanajeshi na askari polisi na askari wa Mau mau lakini pia kuwa aliwahi kupigana wakati wa vita vya pili vya Dunia, dhana zote hizo si za kweli. Ukweli ni kuwa Okello hakuwahi kuwa mwanajeshi au kupata mafunzo ya kijeshi. Majigambo yake kuwa alikuwa na uzoefu wa kijeshi yalikuwa ni mbinu tu ya kumsaidia kuongoza mapinduzi

Alifanikiwa kuanzisha chama cha Mafundi rangi wa Unguja na Pemba na kupitia chama hicho aliweza kupenyeza ushawishi wake wa kufanya mabadiliko ya kumuondoa Sultan

Baada ya kufanikisha Mapinduzi aalimkaribisha Karume kuongoza serikali. Tatizo la Okello hakuwa na back up ya kisiasa na hakuweza kuaminika. Akatupwa na kufukuzwa bila shukrani. Mwanzoni alipelekwa Kenya lakini akafanya jitihada za kutaka kurudi nchini akakamatwa Mwanza na kufungwa. Lakini baadae akarudi Uganda.

Wakati Idd Amini alipompindua Obotte mwaka 1972 alikwenda kumpongeza. Lakini baadae akawa na Mawasiliano na kundi la Obotte lililokuwa Tanzania, katika harakati za kutaka kujiunga na kundi hilo alikamatwa na kuuwawa na Idd Amin.

Kwa hiyo tunaona kuwa Okello alikuwa Mwanamapinduzi. Kuongoza na kushiriki Mapinduzi ya Zanzibar haikuwa kwa ajili ya Mshahara, bali ilitokana na nia yake ya dhati ya kupinga ukoloni na ukandamizaji.
 
Asante kwa Bandiko lenye Historia ndani yake.

TUMEJIFUNZA NA TUNAKUSHUKURU.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
View attachment 2869637

Thanks for this.
P
 
Katika hali ya kushangaza sasa; huwezi kuwasikia wahafidhina wa Mapinduzi matukufu wakimtaja mahali popote pale huyu mwamba John Okello!

Na badala yake, sifa zote wanamwagiwa mtu ambaye nasikia alikimbilia na kujificha nyumbani kwa Mwalimu; siku hayo Mapinduzi yalipofanyika.
 
Back
Top Bottom