Kutoka Pemba: Sura Isiyofahamika ya John Okello

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,260
KUTOKA PEMBA: SURA USIYOIJUA YA ‘’FIELD MARSHAL’’ JOHN OKELLO

Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964 haiwezi kukamilika bila ya kumtaja John Okello.

Ukweli ni kuwa historia ya mapinduzi ipo na kwa miaka mingi imekuwa ikizungumzwa bila ya kutajwa John Okello.

Lakini wako wengi ambao hawatajwi lau kama wanatakiwa kutajwa na watambuliwe kama washiriki katika historia ya mapinduzi.

Wanamapinduzi wanayaita ‘’Mapinduzi Matukufu.’’

Wapinzani wa mapinduzi wanayaita, ‘’Mavamizi.’’

Katika miaka ya hivi karibuni katika mitandao ya kijamii John Okello anatajwa na wengine wanakwenda mbali kufikia kumwita, ‘’Baba wa Taifa wa Zanzibar,’’ ‘’Che Guevara wa Afrika,’’ nk.

Sifa hizi wanazitoa tu bila ya kufikiri kwani John Okello yuko nje kabisa ya kuwa muasisi wa Zanzibar iliyopo achilia mbali kuwa anaweza kufananishwa na Che Guevara.

Lakini hawa wenye kumpa lakabu hizo si Wazanzibari wengi wao huwa watu kutoka Tanzania Bara na hawana uelewa wa historia yoyote ila wanasukumwa na hamaki ndani ya nyoyo zao.

Labda tujiulize kwa nini iwe watu kutoka iliyokuwa Tanganyika ndiyo yanawatoka maneno hayo isiwe Wazanzibari wenyewe wenye mapinduzi yao?

Wanafanya hivi kwa chuki.

Wanadhani wakimnyanyua John Okello kama kiongozi wa mapinduzi watawaudhi Wazanzibari na hili pia litakuwa jibu kwa historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo kwa kiasi kikubwa ilitawaliwa na Waislam ndani yao akiwemo Mufti wa Tanganyika wa miaka ile Mzanzibari, Sheikh Hassan bin Ameir.

Haya ni mambo mapya yaliyokuja miaka hii ya hivi karibuni pamoja na uandishi wa kusahihisha historia iliyokuwapo.

Wakati wa Mwalimu Nyerere na Mzee Karume historia hii haikuwapo.

Hapakuwa na watu wenye ujasiri wa kumtukuza John Okello wala kuandika historia kinyume ya historia rasmi iliyokuwapo wakati viongozi hawa wamekalia viti vyao.

Kwa nini haya hayakuwapo?

Ukiondoa uoga sababu nyingine ni kuwa ilikuwapo hali ya utulivu baina ya Wazanzibari na Watanganyika na watu wa pande zote mbili za muungano waliikubali hali iliyokuwako.

Ilitaka moyo mgumu sana kwenda kinyume na Mwalimu Nyerere au Mzee Karume kwa lolote lile lililowagusa wao au kuigusa Tanzania.

Viongozi hawa walikuwa na nguvu na wakitawala unaweza kusema kwa upande mwingine kwa mkono wa chuma.

Wakisemacho na wakitakacho wao huwa na ndiyo sheria.

Ikiwa hawa hawakutaki katika historia yao hakuna wa kukuingiza.

Mzee Karume hakumtaka Abdallah Kassim Hanga awepo katika historia ya mapinduzi na kwa hakika kabisa Hanga hayumo katika historia ya mapinduzi.

Mwalimu Nyerere hakutamtaka Oscar Kambona katika historia ya uhuru wa Tanganyika na kwa hakika Kambona hayumo katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mwalimu Nyerere na Mzee Karume hawakumtaka John Okello awe sehemu ya historia yao na hakuwa.

Katika katika hali hii John Okello ikawa kama vile hakupata kuwako katika maisha ya siasa ya viongozi hawa.

Hili lilidumu kwa miaka mingi sana.

Mabadiliko ya siasa Tanzania khasa baada ya kuja mfumo wa vyama vingi mlango wa kughitilafiana ukafunguka na mlango huu
ukakaribisha mengi ambayo yalikuwa hayasemwi kabla sasa yakawa yanasemwa waziwazi kila mtu kuyasikia.

Yale yaliyokuwa ‘’nyeti’’ na ‘’mwiko’’ kusemwa yakapata nafasi katika vyombo huru vilivyokuja pamoja na mabadiliko haya.

Magazeti huru yakawa na pupa yakishindana kuchapa habari zilizokuwa zimefunikwa kwa miaka mingi.

Kubwa katika mapinduzi haya ya siasa ilikuwa ujio wa kupashana habari kupitia mitandao.

Katika hali kama hii ya uhuru wa kupitiliza ndipo lilipojitokeza jina la John Okello.

Katika hali ya kutaka kumtukuza John Okello aliyejipa cheo cha Field Marshal akaongezewa cheo kingine kikubwa kuliko Field Marshal, John Okello, wakatokea waandishi katika mitandao bila hofu yoyote wakamwita ati ni ‘’Baba wa Taifa la Zanzibar.’’

Hili limezua mjadala mkali kupita kiasi.

Historia ya John Okello katika mapinduzi ya Zanzibar ni historia ya umwagaji damu mkubwa uliotokea katika mapinduzi.

Hii ndiyo historia ya Zanzibar.

Dr. Harith Ghassany katika kitabu chake, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ (2010) kaeleza hili kwa kirefu na kawataja wahusika wote kwa majina yao.

Historia ya John Okello ni historia ya hotuba zake kali kupitia Sauti ya Unguja hotuba ambazo ndizo zilizomfanya ajulikane ndani na nje ya mipaka ya Zanzibar.

Hivi ndivyo anavyokumbukwa John Okello na wale ambao walioshuhudia mapinduzi.

Bila ya hotuba hizi John Okello anakuwa mtu kama walivyokuwa wanamapinduzi wengine katika orodha ya waliofutwa kwa makusudi katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar.

Bila ya hotuba hizi John Okello anakuwa sawasawa na wale Wamakonde waliovushwa kutoka Pwani ya Kipumbwi kuingia
Zanzibar kuja kusaidia kuiangusha serikali ya Waziri Mkuu Sheikh Mohamed Shamte.

Haya ndiyo yaliyopo katika historia ya mapinduzi.

Nimefika Pemba na nimekuwa na hamu kubwa sana ya kuona wapi John Okello aliishi alivyofika katika kisiwa hicho kutafuta maisha.

Wakati huo District Commissioner au kwa jina lingine, Mudir wa Pemba alikuwa Suleiman Mbaruk.

Familia hii bado ipo Pemba sehemu inayoitwa Mkanjuni na nimepata bahati ya kzungumza na baadhi yao.

Tunaweza kusema familia hii ndiyo iliyompokea John Okello Pemba mwaka wa 1959.

Nimeonyeshwa nyumba aliyokuwa akiishi Suleiman Mbaruk aliyekuwa Liwali wa Pemba maarufu inaitwa, ‘’Nyumba ya Kasuku,’’
kwa kuwa kulikuwa na kasuku barazani ambae alikuwa mtu akipata atamtolea maneno ya kumnanga.

Kwa ajili hii inasemekana watu walikuwa wanaogopa kupita mbele ya nyumba hiyo kwa kumuogopa kasuku yule kwani kasuku huyu anaweza kusikika akikusema, ‘’Muone hata viatu hakuvaa,’’ na ikasadifu kuwa hakika mtu huyo hakuwa na viatu.

Lakini umaarufu wa nyumba hii si tu kwa ajili ya huyu kasuku mropokaji na kuwa ilikuwa nyumba ya Liwali, la hasha, umaarufu wake ulikuwa Sultan wa Zanzibar, Khalifa bin Haroub alikuwa akija Pemba kufanya ziara anafikia hapo nyumbani kwa Liwali Suleiman Mbaruk ingawa alikuwa analala kwenye meli yake iliyotia nanga baharini.

Kuwa John Okello, mtu dhalili kutoka Uganda alikuja kuingiliana na watawala wa kisiwa cha Pemba hapana maelezo ila kusema ilikuwa Qadar ya Allah.

Mwenyezi Mungu alipanga iwe hivyo.

Watu ambao walimjua John Okello katika siku zake za mwanzo akiwa anafanya kazi za ujenzi kama kibarua kujipatia rizki yake wengi wao wametangulia mbele ya haki.

Lakini familia iliyopata kuishi na John Okello alipofika Pemba na wakampatia mahali pa kukaa ni familia ya Mohamed Nassor Mazrui na aliishi kati ya jamii hii hapo Mkanjuni hadi alipoondoka kuelekea Unguja mwaka wa 1963.

Bahati mbaya nyumba aliyokuwa akiishi John Okello haipo na imeanguka miaka hii ya karibuni.

Kwa hakika haikuwa nyumba bali banda.

Banda hili aliloishi John Okello kama lingehifadhiwa ingekuwa sehemu muhimu ya historia ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na pengine ingesababisha na nyumba ya Mudir Suleiman Mbaruk nayo ihifadhiwe kama sehemu muhimu katika historia ya Pemba.

Nyumba ya Kasuku ya Liwali Suleiman Mbaruk Bedui bin Salim bado ipo lakini ni gofu imehamwa hakuna anaeishi hapo na si muda mrefu itakuwa nayo vilevile haipo, italala mchangani na mchanga utazolewa na mvua na kusukumwa Bahari ya Hindi kubakiza kiwanja kitupu.

Wakati huu ilikuwa ikijengwa shule, Seyyid Khalifa Secondary School na John Okello alikuwa kibarua hapo kama mbanjuaji wa kokoto zilizokuwa zinatumika katika ujenzi.

Mjenzi wa shule hii alikuwa Ahmed Nassor Mazrui na bila shaka hii ndiyo ikawa sababu ya John Okello kupata kazi katika ujenzi wa shule hii ya Seyyid Khalifa ambayo baada ya mapinduzi ikabadilishwa jina jina ikaitwa, ‘’Fidel Castro,’’ jina la kiongozi wa mapinduzi ya Cuba.

John Okello ndiyo huyu akiwa sehemu ya historia ya Pemba akiishi kama waivyoishi wengi waliokwenda Pemba kutafuta maisha katika kuchuma karafuu na kazi nyingine.

John Okello akaondoka Pemba mwaka wa 1963 kwenda Unguja kujaribu kuboresha maisha yake.

Bila ya shaka yoyote nyumba aliyopewa John Okello na Mazrui ilipata kukaliwa na vibarua wengine kama yeye na wao pia walikaa hapo na wakaondoka na wengine wakaja na yawezekana hawakurejea tena Pemba.

Si John Okello.

John Okello alirejea Pemba mwaka wa 1964 baada ya miezi miwili kutokea mapinduzi

John Okello hakurejea Pemba kama kibarua.

John Okello alirejea Pemba akiwa ‘’Field Marshal’’ akisindikizwa na askari wake.

Hapa haijalishi kama John Okello alikuwa kweli ni Field Marshal kama Joseph Tito wa Yugoslavia aliyepigana Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) au vinginevyo.

Bila shaka asubuhi ya kuamkia mapinduzi, wahisani na wenyeji wa John Okello pale Mkanjuni walisikia sauti yake katika Sauti ya Unguja akitangaza kupinduliwa kwa serikali ya Zanzibar.

Nakuachia wewe msomaji ufikirie wale waliokuwa wanamjua John Okello kama foreman mbanja kokoto akijenga shule ya Seyyid Khalifa bin Haroub hali yao ilikuwaje?

Hebu fikiri mshangao wao ulikuwa mkubwa kwa kiasi gani?

Tumekaa na mpashaji habari wetu Sheikh Abdallah Nassor Suleiman, mjukuu wa Liwali Suleiman Mbaruk ndani ya Msikiti wa Ibadh wa Mkanjuni baada ya Sala ya Ijumaa msikiti ukiwa mtupu tuko peke yetu pembeni.

Sheikh Abdallah Nassor Suleiman katuteka kwa ufasaha wake wa kuzungumza akitueleza historia hii ya baba na babu zake na John Okello.

Sheikh Abdallah anasema John Okello alifika nyumbani kwao miezi miwili baada ya mapinduzi kwa vishindo vikubwa akiwa kafuatana na askari wa mapinduzi lakini vishindo vile havikuwa vya shari.

Ugeni huu wa Field Marshal utakuwa mwezi wa March, 1964.

John Okello aliingia uwanjani akipiga hodi na kuita majina ya wazee wake kwa furaha na bashasha, ’Yuko wapi Mzee Ahmed Nassor wakasalimiana kwa adabu pamoja na mkewe Bi. Mariam, akatoka akaenda kwa Mzee Mohamed Suleiman akamsalimu.’’

Kote humu anapita askari wa mapinduzi wanamfuata nyuma.

John Okello akawaambia askari wake kuwa wale ni wazee wake na ameishinao kwa wema wasibughudhiwe.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Watu hawa hawakupata kumnyanyasa John Okello.

Waliishi na yeye kwa salama na amani.

Askari wakatoa stengun wakapiga mfulilizo wa risasi juu kama ishara ya furaha na uwanja mzima ukajaa watu na watoto wadogo wanafurahia kuwaona askari na kusikia mlio wa risasi.

Hawa aliokuja kuwasalimua na kuwahakikishia usalama wao na kuwaita wazee wake ni ‘’Waarabu’’kama walivtyokuwa ‘’Waarabu,’’ wengine waliouliwa Unguja lakini John Okello anasema hawa wa Mkanjuni waliompa kazi na mahali pa kuishi walikuwa watu wema.

Hapa panafikirisha.

Tunaweza kusema wale ‘’Waarabu’’ wa Unguja waliokuwa mashamba ambako wengi ndiko walipouawa laiti wangelipata fursa ya kuishi na wale Wamakonde kutoka Kipumbwi na wao wangeliushuhudia wema wao na kutokana na wema huo wangenusurika kuuawa.

Huu ni upande wa pili wa John Okello ambao wanahistoria bado hawajaueleza.

Hapa panahitaji utafiti.

Gramafoni za wanaomwandika John Okello zimekuwa zikipiga na kusikiliza upande mmoja tu wa santuri za His Master's Voice (HMV).

Okello hakurejea tena Pemba baada ya safari ile kwake ilikuwa kama kaja kuwaaga nduguze na akayasema maneno hayo ya shukurani kwa kinywa chake tena hadharani.

John Okello aliporejea Unguja hakukaa sana alifukuzwa Zanzibar akarejeshwa kwao kwa idhara kubwa na wale waliomtumikisha na kumsabilia radio kutangaza mapinduzi.

Baada ya mapinduzi mwezi January hadi kufika March John Okello baada ya kupita miezi miwili akawa muhamiaji asiyetakiwa Zanzibar.

Siku moja ni nyingi katika siasa sikwambii miezi miwili.
1692008255984.png

1692008300496.png

1692008359351.png

1692008420312.png

PICHA:
1. John Okello
2. Sheikh Abdallah Mohamed Nassor kushoto aliyeegemea ukuta
3. Mabaki ya nyumba ya Liwali Suleiman Mbaruk naarufu kwa jina la "Nyumba ya Kasuku."
4. Nyumba ya Mazrui kama ilivyo hivi sasa
5. Shule ya Fidel Castro (zamani Shule ya Seyyid Khalifa bin Haroub)
 
Napenda kusoma makala zako ,zinanipa mwanga fulani kwenye historia ya nchi. Ila kuna element fulani za kuwa obssessed na mambo ya dini . Sijui kwanini
 
Mc...
Ndiyo historia yenyewe si dini bali Waislam.

Waasisi wa African Association: Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Kleist Abdallah Sykes, Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Wanahistoria waliwafuta hawa.

Chama walichoasisi hawa 1929 ndicho kilichozaa TANU 1954.

Kama nisingewataja historia hii ingepotea.

Wangetajwa mimi ningekuwa kimya na wewe usingetaabishwa na "dini."
 
Okay nimekuelewa. Nataka kufahamu je kile kitabu cha kwaheri ukoloni kwaheri uhuru ... Jina la mwandishi limenitoka kidogo, je kipo sensadi hapa Tz? Nimetafuta kwenye maduka mengi kipindi fulani sijafanikiwa kupata copy yake
 
Kipo Tanzania Publishing House.
 
Asante Mzee MS kwa historia hii.

Mimi sioni kama waarabu wote walikuwa wabaguzi na wakatili dhidi ya Waafrika. Lakini ukweli wa picha jumla, kwa sababu ya mfumo wa kibaguzi uliojengwa, Waarabu wametesa sana watu weusi. Ni kama tu wajerumani walivyotesa wanama na waherero kule Namibia. wewe kuishi na kujamiiana na waarabu ambao wamekuwa wema kwako kuna kufanya upofushwe kutokuukubali udhalimu wa kihistoria wa waarabu, ndio maana hata makala yako hii iko very apologetic kwa 'waarabu'.
 
Huyo mzee ni muumini mzuri sana wa waarabu
 
KUTOKA PEMBA: SURA USIYOIJUA YA ‘’FIELD MARSHAL’’ JOHN OKELLO

Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964 haiwezi kukamilika bila ya kumtaja John Okello.

Ukweli ni kuwa historia ya mapinduzi ipo na kwa miaka mingi imekuwa ikizungumzwa bila ya kutajwa John Okello.

Lakini wako wengi ambao hawatajwi lau kama wanatakiwa kutajwa na watambuliwe kama washiriki katika historia ya mapinduzi.

Wanamapinduzi wanayaita ‘’Mapinduzi Matukufu.’’

Wapinzani wa mapinduzi wanayaita, ‘’Mavamizi.’’

Katika miaka ya hivi karibuni katika mitandao ya kijamii John Okello anatajwa na wengine wanakwenda mbali kufikia kumwita, ‘’Baba wa Taifa wa Zanzibar,’’ ‘’Che Guevara wa Afrika,’’ nk.

Sifa hizi wanazitoa tu bila ya kufikiri kwani John Okello yuko nje kabisa ya kuwa muasisi wa Zanzibar iliyopo achilia mbali kuwa anaweza kufananishwa na Che Guevara.

Lakini hawa wenye kumpa lakabu hizo si Wazanzibari wengi wao huwa watu kutoka Tanzania Bara na hawana uelewa wa historia yoyote ila wanasukumwa na hamaki ndani ya nyoyo zao.

Labda tujiulize kwa nini iwe watu kutoka iliyokuwa Tanganyika ndiyo yanawatoka maneno hayo isiwe Wazanzibari wenyewe wenye mapinduzi yao?

Wanafanya hivi kwa chuki.

Wanadhani wakimnyanyua John Okello kama kiongozi wa mapinduzi watawaudhi Wazanzibari na hili pia litakuwa jibu kwa historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo kwa kiasi kikubwa ilitawaliwa na Waislam ndani yao akiwemo Mufti wa Tanganyika wa miaka ile Mzanzibari, Sheikh Hassan bin Ameir.

Haya ni mambo mapya yaliyokuja miaka hii ya hivi karibuni pamoja na uandishi wa kusahihisha historia iliyokuwapo.

Wakati wa Mwalimu Nyerere na Mzee Karume historia hii haikuwapo.

Hapakuwa na watu wenye ujasiri wa kumtukuza John Okello wala kuandika historia kinyume ya historia rasmi iliyokuwapo wakati viongozi hawa wamekalia viti vyao.

Kwa nini haya hayakuwapo?

Ukiondoa uoga sababu nyingine ni kuwa ilikuwapo hali ya utulivu baina ya Wazanzibari na Watanganyika na watu wa pande zote mbili za muungano waliikubali hali iliyokuwako.

Ilitaka moyo mgumu sana kwenda kinyume na Mwalimu Nyerere au Mzee Karume kwa lolote lile lililowagusa wao au kuigusa Tanzania.

Viongozi hawa walikuwa na nguvu na wakitawala unaweza kusema kwa upande mwingine kwa mkono wa chuma.

Wakisemacho na wakitakacho wao huwa na ndiyo sheria.

Ikiwa hawa hawakutaki katika historia yao hakuna wa kukuingiza.

Mzee Karume hakumtaka Abdallah Kassim Hanga awepo katika historia ya mapinduzi na kwa hakika kabisa Hanga hayumo katika historia ya mapinduzi.

Mwalimu Nyerere hakutamtaka Oscar Kambona katika historia ya uhuru wa Tanganyika na kwa hakika Kambona hayumo katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mwalimu Nyerere na Mzee Karume hawakumtaka John Okello awe sehemu ya historia yao na hakuwa.

Katika katika hali hii John Okello ikawa kama vile hakupata kuwako katika maisha ya siasa ya viongozi hawa.

Hili lilidumu kwa miaka mingi sana.

Mabadiliko ya siasa Tanzania khasa baada ya kuja mfumo wa vyama vingi mlango wa kughitilafiana ukafunguka na mlango huu
ukakaribisha mengi ambayo yalikuwa hayasemwi kabla sasa yakawa yanasemwa waziwazi kila mtu kuyasikia.

Yale yaliyokuwa ‘’nyeti’’ na ‘’mwiko’’ kusemwa yakapata nafasi katika vyombo huru vilivyokuja pamoja na mabadiliko haya.

Magazeti huru yakawa na pupa yakishindana kuchapa habari zilizokuwa zimefunikwa kwa miaka mingi.

Kubwa katika mapinduzi haya ya siasa ilikuwa ujio wa kupashana habari kupitia mitandao.

Katika hali kama hii ya uhuru wa kupitiliza ndipo lilipojitokeza jina la John Okello.

Katika hali ya kutaka kumtukuza John Okello aliyejipa cheo cha Field Marshal akaongezewa cheo kingine kikubwa kuliko Field Marshal, John Okello, wakatokea waandishi katika mitandao bila hofu yoyote wakamwita ati ni ‘’Baba wa Taifa la Zanzibar.’’

Hili limezua mjadala mkali kupita kiasi.

Historia ya John Okello katika mapinduzi ya Zanzibar ni historia ya umwagaji damu mkubwa uliotokea katika mapinduzi.

Hii ndiyo historia ya Zanzibar.

Dr. Harith Ghassany katika kitabu chake, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ (2010) kaeleza hili kwa kirefu na kawataja wahusika wote kwa majina yao.

Historia ya John Okello ni historia ya hotuba zake kali kupitia Sauti ya Unguja hotuba ambazo ndizo zilizomfanya ajulikane ndani na nje ya mipaka ya Zanzibar.

Hivi ndivyo anavyokumbukwa John Okello na wale ambao walioshuhudia mapinduzi.

Bila ya hotuba hizi John Okello anakuwa mtu kama walivyokuwa wanamapinduzi wengine katika orodha ya waliofutwa kwa makusudi katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar.

Bila ya hotuba hizi John Okello anakuwa sawasawa na wale Wamakonde waliovushwa kutoka Pwani ya Kipumbwi kuingia
Zanzibar kuja kusaidia kuiangusha serikali ya Waziri Mkuu Sheikh Mohamed Shamte.

Haya ndiyo yaliyopo katika historia ya mapinduzi.

Nimefika Pemba na nimekuwa na hamu kubwa sana ya kuona wapi John Okello aliishi alivyofika katika kisiwa hicho kutafuta maisha.

Wakati huo District Commissioner au kwa jina lingine, Mudir wa Pemba alikuwa Suleiman Mbaruk.

Familia hii bado ipo Pemba sehemu inayoitwa Mkanjuni na nimepata bahati ya kzungumza na baadhi yao.

Tunaweza kusema familia hii ndiyo iliyompokea John Okello Pemba mwaka wa 1959.

Nimeonyeshwa nyumba aliyokuwa akiishi Suleiman Mbaruk aliyekuwa Liwali wa Pemba maarufu inaitwa, ‘’Nyumba ya Kasuku,’’
kwa kuwa kulikuwa na kasuku barazani ambae alikuwa mtu akipata atamtolea maneno ya kumnanga.

Kwa ajili hii inasemekana watu walikuwa wanaogopa kupita mbele ya nyumba hiyo kwa kumuogopa kasuku yule kwani kasuku huyu anaweza kusikika akikusema, ‘’Muone hata viatu hakuvaa,’’ na ikasadifu kuwa hakika mtu huyo hakuwa na viatu.

Lakini umaarufu wa nyumba hii si tu kwa ajili ya huyu kasuku mropokaji na kuwa ilikuwa nyumba ya Liwali, la hasha, umaarufu wake ulikuwa Sultan wa Zanzibar, Khalifa bin Haroub alikuwa akija Pemba kufanya ziara anafikia hapo nyumbani kwa Liwali Suleiman Mbaruk ingawa alikuwa analala kwenye meli yake iliyotia nanga baharini.

Kuwa John Okello, mtu dhalili kutoka Uganda alikuja kuingiliana na watawala wa kisiwa cha Pemba hapana maelezo ila kusema ilikuwa Qadar ya Allah.

Mwenyezi Mungu alipanga iwe hivyo.

Watu ambao walimjua John Okello katika siku zake za mwanzo akiwa anafanya kazi za ujenzi kama kibarua kujipatia rizki yake wengi wao wametangulia mbele ya haki.

Lakini familia iliyopata kuishi na John Okello alipofika Pemba na wakampatia mahali pa kukaa ni familia ya Mohamed Nassor Mazrui na aliishi kati ya jamii hii hapo Mkanjuni hadi alipoondoka kuelekea Unguja mwaka wa 1963.

Bahati mbaya nyumba aliyokuwa akiishi John Okello haipo na imeanguka miaka hii ya karibuni.

Kwa hakika haikuwa nyumba bali banda.

Banda hili aliloishi John Okello kama lingehifadhiwa ingekuwa sehemu muhimu ya historia ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na pengine ingesababisha na nyumba ya Mudir Suleiman Mbaruk nayo ihifadhiwe kama sehemu muhimu katika historia ya Pemba.

Nyumba ya Kasuku ya Liwali Suleiman Mbaruk Bedui bin Salim bado ipo lakini ni gofu imehamwa hakuna anaeishi hapo na si muda mrefu itakuwa nayo vilevile haipo, italala mchangani na mchanga utazolewa na mvua na kusukumwa Bahari ya Hindi kubakiza kiwanja kitupu.

Wakati huu ilikuwa ikijengwa shule, Seyyid Khalifa Secondary School na John Okello alikuwa kibarua hapo kama mbanjuaji wa kokoto zilizokuwa zinatumika katika ujenzi.

Mjenzi wa shule hii alikuwa Ahmed Nassor Mazrui na bila shaka hii ndiyo ikawa sababu ya John Okello kupata kazi katika ujenzi wa shule hii ya Seyyid Khalifa ambayo baada ya mapinduzi ikabadilishwa jina jina ikaitwa, ‘’Fidel Castro,’’ jina la kiongozi wa mapinduzi ya Cuba.

John Okello ndiyo huyu akiwa sehemu ya historia ya Pemba akiishi kama waivyoishi wengi waliokwenda Pemba kutafuta maisha katika kuchuma karafuu na kazi nyingine.

John Okello akaondoka Pemba mwaka wa 1963 kwenda Unguja kujaribu kuboresha maisha yake.

Bila ya shaka yoyote nyumba aliyopewa John Okello na Mazrui ilipata kukaliwa na vibarua wengine kama yeye na wao pia walikaa hapo na wakaondoka na wengine wakaja na yawezekana hawakurejea tena Pemba.

Si John Okello.

John Okello alirejea Pemba mwaka wa 1964 baada ya miezi miwili kutokea mapinduzi

John Okello hakurejea Pemba kama kibarua.

John Okello alirejea Pemba akiwa ‘’Field Marshal’’ akisindikizwa na askari wake.

Hapa haijalishi kama John Okello alikuwa kweli ni Field Marshal kama Joseph Tito wa Yugoslavia aliyepigana Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) au vinginevyo.

Bila shaka asubuhi ya kuamkia mapinduzi, wahisani na wenyeji wa John Okello pale Mkanjuni walisikia sauti yake katika Sauti ya Unguja akitangaza kupinduliwa kwa serikali ya Zanzibar.

Nakuachia wewe msomaji ufikirie wale waliokuwa wanamjua John Okello kama foreman mbanja kokoto akijenga shule ya Seyyid Khalifa bin Haroub hali yao ilikuwaje?

Hebu fikiri mshangao wao ulikuwa mkubwa kwa kiasi gani?

Tumekaa na mpashaji habari wetu Sheikh Abdallah Nassor Suleiman, mjukuu wa Liwali Suleiman Mbaruk ndani ya Msikiti wa Ibadh wa Mkanjuni baada ya Sala ya Ijumaa msikiti ukiwa mtupu tuko peke yetu pembeni.

Sheikh Abdallah Nassor Suleiman katuteka kwa ufasaha wake wa kuzungumza akitueleza historia hii ya baba na babu zake na John Okello.

Sheikh Abdallah anasema John Okello alifika nyumbani kwao miezi miwili baada ya mapinduzi kwa vishindo vikubwa akiwa kafuatana na askari wa mapinduzi lakini vishindo vile havikuwa vya shari.

Ugeni huu wa Field Marshal utakuwa mwezi wa March, 1964.

John Okello aliingia uwanjani akipiga hodi na kuita majina ya wazee wake kwa furaha na bashasha, ’Yuko wapi Mzee Ahmed Nassor wakasalimiana kwa adabu pamoja na mkewe Bi. Mariam, akatoka akaenda kwa Mzee Mohamed Suleiman akamsalimu.’’

Kote humu anapita askari wa mapinduzi wanamfuata nyuma.

John Okello akawaambia askari wake kuwa wale ni wazee wake na ameishinao kwa wema wasibughudhiwe.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Watu hawa hawakupata kumnyanyasa John Okello.

Waliishi na yeye kwa salama na amani.

Askari wakatoa stengun wakapiga mfulilizo wa risasi juu kama ishara ya furaha na uwanja mzima ukajaa watu na watoto wadogo wanafurahia kuwaona askari na kusikia mlio wa risasi.

Hawa aliokuja kuwasalimua na kuwahakikishia usalama wao na kuwaita wazee wake ni ‘’Waarabu’’kama walivtyokuwa ‘’Waarabu,’’ wengine waliouliwa Unguja lakini John Okello anasema hawa wa Mkanjuni waliompa kazi na mahali pa kuishi walikuwa watu wema.

Hapa panafikirisha.

Tunaweza kusema wale ‘’Waarabu’’ wa Unguja waliokuwa mashamba ambako wengi ndiko walipouawa laiti wangelipata fursa ya kuishi na wale Wamakonde kutoka Kipumbwi na wao wangeliushuhudia wema wao na kutokana na wema huo wangenusurika kuuawa.

Huu ni upande wa pili wa John Okello ambao wanahistoria bado hawajaueleza.

Hapa panahitaji utafiti.

Gramafoni za wanaomwandika John Okello zimekuwa zikipiga na kusikiliza upande mmoja tu wa santuri za His Master's Voice (HMV).

Okello hakurejea tena Pemba baada ya safari ile kwake ilikuwa kama kaja kuwaaga nduguze na akayasema maneno hayo ya shukurani kwa kinywa chake tena hadharani.

John Okello aliporejea Unguja hakukaa sana alifukuzwa Zanzibar akarejeshwa kwao kwa idhara kubwa na wale waliomtumikisha na kumsabilia radio kutangaza mapinduzi.

Baada ya mapinduzi mwezi January hadi kufika March John Okello baada ya kupita miezi miwili akawa muhamiaji asiyetakiwa Zanzibar.

Siku moja ni nyingi katika siasa sikwambii miezi miwili.
View attachment 2717050
View attachment 2717051
View attachment 2717052
View attachment 2717055

PICHA:
1. John Okello
2. Sheikh Abdallah Mohamed Nassor kushoto aliyeegemea ukuta
3. Mabaki ya nyumba ya Liwali Suleiman Mbaruk naarufu kwa jina la "Nyumba ya Kasuku."
4. Nyumba ya Mazrui kama ilivyo hivi sasa
5. Shule ya Fidel Castro (zamani Shule ya Seyyid Khalifa bin Haroub)
Mimi naamini kabisa una tatizo fulani kwenye namna ya kuwaza kwasababu hata hao wakoloni ambao baba yako Sykes na wenzie waliwapachika majina mabaya je unataka kuniambia hakukuwa na wakoloni wemA ?
 
Back
Top Bottom