Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,279
23,052
Huyu ni Mmoja wa Mashujaa wa miaka ile aliyeshiriki kuwaondoa Makoloni huko Zanzibar. Kama ambavyo Bara nao walikuwa wameondoa wao.

Anasimulia mzee wangu ambaye alikuwa Mwalimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka hiyo Che Guavera alikuja Tanzania mwaka 1965. Anasema Che alijaribu kuulizia habari za Mwanamapinduzi aliyesaidia kuipatia Zanzibar Uhuru wake John Okello.

Kwa his disappointment alishtuka kuambiwa the Man alifukuzwa mara baada ya kumaliza jukumu lililomleta Zanzibar kuwaondoa Waarabu waliokuwa wakiitawala Zanzibar.Aliwaokoa Waafrika kutoka kutawaliwa walipopata tu uhuru wakamfukuza.

John Okello Baba wa Taifa la Zanzibar ataendelea kukumbukwa kila tutakapoadhimisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Baada ya hapo John Okello alirudi kwao kwenda kuendeleza mapambano dhidi ya udhalimu na hatimaye alikuwa kama mtu wa kawaida tu pasipo makuu. Hakulipwa yeye wala familia yake. Kabla ya Mwaka 1967 Che Guevara kufariki aliwahi mtumia mzee wangu barua akimtaka amtafute John Okello wajiunge naye kwenye harakati huko Msumbiji na Angola.

Mzee hakujua aanzie wapi.

Pia Soma https://www.jamiiforums.com/threads...a-taifa-huru-la-zanzibar-john-okello.1579821/
 
Wazanzibar wanaona nishai kwamba alitokea mjaluo mmoja toka Uganda akaja akawakomboa toka Kwa waarabu.

Niliwahi kusoma mahala kwamba baada ya Okello kuwafurusha wajomba zake Chief Hangaya, alipewa madaraka ya kiulinzi (sikumbuki exact jina la cheo) ila akaanza kujikweza sana hata akavuliwa mamlaka hayo ndipo akaakuamua kwenda zake Kenya.

Akumbukwe John Okello.
 
Wazanzibar wanaona nishai kwamba alitokea mjaluo mmoja toka Uganda akaja akawakomboa toka Kwa waarabu.

Niliwahi kusoma mahala kwamba baada ya Okello kuwafurusha wajomba zake Chief Hangaya, alipewa madaraka ya kiulinzi (sukumbuki exact jina la cheo) ila akaanza kujikweza sana hata akavuliwa mamlaka hayo ndipo akaakuamua kwenda zake Kenya.

Akumbukwe John Okello.
City...
Mzee wetu Mohammed anasemaje juu ya hili?
City...
Okello anabebeshwa mzigo si wake.

ASP haikuwa na uwezo wa kupindua serikali.

Mipango yote ilifanyika Dar es Salaam ikisimamiwa na Oscar Kambona na Abdullah Kassim Hanga.

Waliweka kambi Kipumbwi ambako waliwaweka Wamakonde kutoka shamba la Mkonge la Sakura kwa ajili ya kuwavusha kuingia Zanzibar kuIpigIa kura ASP na kushiriki katika mapinduzi.

Kambi hii ilikuwa chini ya Ali Mwinyi Tambwe akiwa District Commissioner wa Tanga na Regional Commissioner Jumanne Abdallah.

Waliopewa kazi ya kuchagua vijana wa kuletwa kambini Kipumbwi walikuwa Victor Mkello kiongozi wa chama cha wakata mkonge na Mohamed Omar Mkwawa kijana wa Kidigo kutoka Tanga aliyepatakuwa mwanachama hodari wa ASP.

Ali Mwinyi Tambwe wakati wa ukoloni aliwatumikia Waingereza kama "mole" wao ndani ya TAA kisha TANU.

Mkwawa yeye ndiye aliyekuwa akiwavusha hawa Wamakonde kuwaingiza Zanzibar usiku kwa majahazi wote wamevaa kama wavuvi wa Kidigo.

Kipumbwi yote ilikuwa imezuiwa kwa watu kuingia ovyo.

Hawa Wamakonde ndiyo walioua Waarabu wengi wakulima wa kawaida tu waliokuwa mashambani Zanzibar.

Mpango huu ulifanyika kwa siri kubwa sana.

Mzanzibari aliyepata kufika Kipumbwi inasemekana ni Jimmy Ringo ambae aliuliwa baada ya mapinduzi kama walivyouliwa wana ASP wengine.

John Okello hakuwa katika mipango hii.

Kilichompa umaarufu ni kule yeye kupewa radio kutangaza kuwa serikali imepinduliwa na Karume arejee Zanzibar kukalia kiti chake.
 
City...
City...
Okello anabebeshwa mzigo si wake.

ASP haikuwa na uwezo wa kupindua serikali.

Mipango yote ilifanyika Dar es Salaam ikisimamiwq na Oscar Kambona na Abdullah Kassim Hanga.

Waliweka kambi Kipumbwi ambako waliwaweka Wamakonde kutoka shamba la Mkonge la Sakura kwa ajili ya kuwavusha kuingia Zanzibar kuIpigIa kura ASP na kushiriki katika mapinduzi.

Kambi hii ilikuwa chini ya Ali Mwinyi Tambwe akiwa District Commissioner wa Tanga na Regional Commissioner Jumanne Abdallah.

Waliopewa kazi ya kuchagua vijana wa kuletwa kambini Kipumbwi walikuwa Victor Mkello kiongozi wa chama cha wakata mkonge na Mohamed Omar Mkwawa kijana wa Kidigo kutoka Tanga aliyepatakuwa mwanachama hodari wa ASP.

Ali Mwinyi Tambwe wakati wa ukoloni aliwatumikia Waingereza kama "mole" wao ndani ya TAA kisha TANU.

Mkwawa yeye ndiye aliyekuwa akiwavusha hawa Wamakonde kuwaingiza Zanzibar usiku kwa majahazi wote wamevaa kama wavuvi wa Kidigo.

Kipumbwi yote ilikuwa imezuiwa kwa watu kuingia ovyo.

Hawa Wamakonde ndiyo walioua Waarabu wengi wakulima wa kawaida tu waliokuwa mashambani Zanzibar.

Mpango huu ulifanyika kwa siri kubwa sana.

Mzanzibari aliyepata kufika Kipumbwi inasemekana ni Jimmy Ringo ambae aliuliwa baada ya mapinduzi kana walivyouliwa wana ASP wengine.

John Okello hakuwa katika mipango hii.

Kilichompa umaarufu ni kule yeye kupewa radio kutangaza kuwa serikali imepinduliwa na Karume arejee Zanzibar kukalia kiti chake.
Ohh nahisi.
Je mzee Karume alikuwepo kisiwani wakati wa mapinduzi akishiriki bega kwa bega?
Pengine hakuwepo! Ndio maana anaskika okelo akimwita, je alikuwa wapi?
Na kwanini amekimbia?
Na Ni kwanini aitwe yeye badala ya wengine ?
 
Ohh naisi.
Je mzee Karume alikuwepo kisiwani wakati was mapinduzi akishiriki bega kwa bega?
Pengine hakuwepo! Ndo maana anaskika okelo akimwita.je alikuwa wapi?
Na kwanini amekimbia?
Na Ni kwanini aitwe yeye badala ya wengine ?
Sela...
Okello alichaguliwa kutoa tangazo la kuanguka kwa serikali ya Mohamed Shamte kwa sababu ya lafidh yake ambayo si ya Kiunguja.

Karume, Babu na Hanga wote walikuwa Dar es Salaam.

Sauti ngeni kwa Wazanzibari iliwatia wananchi hofu.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom