SoC01 Manka binti mrembo, Mzaliwa wa Machame na mkazi wa Tandale alivyobahatika kuacha ukahaba mpaka kuwa dereva Ikulu

Stories of Change - 2021 Competition

Amina68

JF-Expert Member
Jul 16, 2021
298
545
Kwa majina naitwa Manka, Mzaliwa wa Moshi Machame, mkazi wa Tandale Dar es salaam.

Nilifanikiwa kuanza masomo yangu ya msingi Dar, na kufanikiwa kujiunga masomo ya Sekondari shule wanafunzi wenye vipaji maalumu Tabora Girls, ambapo nilisoma mpaka kidato cha nne, na kufanikiwa pia kuendelea na masomo yangu hapo hapo shule ya wasichana Tabora Girls kidato cha sita.

Kiukweli niliishi maisha ya raha sana kutokana na wazazi wangu wote kuwa wafanyakazi mama akiwa mfanyakazi Wizara ya Mambo ya nje na baba akiwa balozi wa Tanzania nchini Australia.

Maisha yalikuja badilika baada ya baba angu mzazi kupata ajali ya gari akitokea uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akielekea Machame nyumbani ambapo aligongana uso kwa uso na roli. Baada ya taarifa kufika nyumbani mama nae alipata mshtuko akafariki kwa ugonjwa wa moyo, hivyo nikapoteza baba na mama kwa wakati mmoja. Niliumia sana, na hapo maisha yangu yakaanza kubadilika rasmi.

Baada ya wiki moja ndugu wenye tamaa walikuja nyumbani na kuanza taratibu za kuchukua Mali mpaka nyumba yetu iliuzwa ndani ya miezi mitatu tu, kumbuka wakati huo nilikuwa katika utaratibu wa kujiandaa kwenda chuo kikuu udsm kusomea uhandisi wa Umeme. Niliumia sana,nilifukuzwa pia nyumbani nikawa sina pa kuishi wala pa kula.

Nilianza kuishi mitaani,na Kama unavyojua maisha ya Dar ni magumu sana, ilinilazimu kujiingiza katika maisha ya ukahaba ili tu maisha yaweze kwenda.

Wakati wa ukahaba wangu, nimewahi kukutana na changamoto mbalimbali sana Kama kulala njaa kwa kukosa chakula maana Kuna siku unaweza toka uspate hata mwanaume mmoja, na Kuna baadhi ya siku nilikuwa nasafiri mpaka morogoro msamvu kusaka wateja,maisha yalikuja magumu sana i

Siku moja nikiwa nimekaa zangu, sehemu niliyokuwa nimepangisha Mtoni kijichi,mida ya saa 4 asubuhi Mara ikaja gari moja, ikasimama mbele ya nyumba ile, wakashuka watu wawili wote wanawake wakanifata wakanisalimia na wakaniuliza, samahani wewe ndio manka Anthony Mushi, nikawajibu ndio Mimi.

Wakajitambulisha wametokea ofisi ya Rais utumishi na utawala bora,ninahitajika na bosi wao ofisini nilishtuka sana,na nikawauliza huyo bosi wao ananijua? Wakanijibu wao wamepewa maelekezo ya kunitafuta na ndipo walipojua ninapoishi.

Nilijiandaa nikaondoka zangu,huku nikiwa na mawazo akilini kwangu,je huyu bosi niliwahi kutoka nae? Au Ni mteja wangu? Ila nilipiga moyo konde nikaenda na kusema nitajua huko huko.

Nilifika na kupelekwa moja kwa moja ofisini kwa huyo bosi.baada ya kufika sikumkumbuka ,ila akajitambulisha kuwa yeye Ni katibu ofisi ile iliyopo Mjini Dar es Salaam.aliniuliza maswali mengi sana na mwisho wa siku akaamua kupasua ukweli.

Akanambia kwamba ofisi yake imeanza kunifatilia tangu nilipochaguliwa kidato cha kwanza tabora girls na wamenifatilia nyendo zangu kwa muda wa miaka 9, na ndipo Leo imekuwa tamati na ninatakiwa kujiunga nao ili na Mimi nianze kufatilia watu,sikumuelewa ila nilipiga moyo konde nikasema liwalo na liwe.

Waliniruhusu nirudi nilipopanga nikachukue vitu vyangu vya muhimu nirudi pale,baada ya hapo nilipelekwa kwenye nyumba Safi na siku 3 zijazo nikapelekwa jeshi la kujenga taifa, nikaanza mafunzo na nilipomaliza, nilipangiwa kwenda kozi maalumu kurasini,na baada ya hapo nilipewa first appointment ikulu.

Hivyo napenda kuwaasa ndugu zangu hasa wadada, usikate tamaa, Hujui kusudi la maisha yako hapa duniani.

Thanks
 
..mbona hakuna balozi anaitwa anthony mushi?

..pia sina kumbukumbu ya Tanzania kuwa na ubalozi Australia.
 
Unasema hao wageni wako walikuambia kuwa wamekufuatilia toka ukiwa form one mpaka wakati huo.. na bila shaka walijua kuwa umefiwa, umezurumiwa mali, unajiuza, na unaishi maisha ya hovyo.. yaani pamoja na yote hayo bado wakakuacha usote bila ya kukusaidia? Nieleweshe tafadhali..
 
Sikuuliza chochote ,nilihisi Mungu kaona mateso ninayopitia!
 
Manka siyo jina la kupewa bali ni title ya kuzaliwa yaani mtoto wa pili wa kike, kwa hiyo hii title huwa haitumiki rasmi kama jina na Wachagga hatuna huo utaratibu eti mtu aandikishwe au ajitambulishe kama, mfano, Manka Mushi. Badala yake atajitambulisha kwa jina rasmi la kupewa na siyo title ya kuzaliwa. Kwa hiyo hata story inakuwa kidogo inakosa uhalisia
Hii ni chai yenye tangawizi nyingi na kitafunio mabumunda
 
Me nilisoma nilipofika kwenye ilo neno la ubalozi nimegota hapo nikasikitika jf kuruhuru huu uzi nimepoteza hata radha ya shindano.
Eti hakuna ubalozi Australia,leo Madam president ,kateua balozi JF?
 
Eti hakuna ubalozi Australia,leo Madam president ,kateua balozi JF?
Balozi wetu ambae kituo chake ni Japan ndio anatuwakilisha Australia, New Zealand na Papua New Guinea. Hatuna ofisi ya ubalozi Australia kama vile nao hawana ofisi ya ubalozi kwetu.

Amandla...
 
Manka siyo jina la kupewa bali ni title ya kuzaliwa yaani mtoto wa pili wa kike, kwa hiyo hii title huwa haitumiki rasmi kama jina na Wachagga hatuna huo utaratibu eti mtu aandikishwe au ajitambulishe kama, mfano, Manka Mushi. Badala yake atajitambulisha kwa jina rasmi la kupewa na siyo title ya kuzaliwa. Kwa hiyo hata story inakuwa kidogo inakosa uhalisia
Ok, nilikuwa sijui.Mtoto wa kwanza wa kike anaitwa nani
 
Ok, nilikuwa sijui.Mtoto wa kwanza wa kike anaitwa nani
Hana jina la kitamaduni ila cheo cha ukuu yaani "Mbe" na hii ipo pia kwa mtoto wa kwanza wa kiume. "Mbe" hutumika Sana kama kivumishi. Mfano unamuita "Neema Mbee", "Daud Mbee" "Baba Mbee" au kushukuru "aika Mbee" yaani asante.

Hata kwenye kusali tunaita "Mungu Mbowe" Yesu Mbee
 
Unamaanisha mbowe =mbee?
 
Sijui kwa nini nimewaza hivi Ila sijui Kama ndio hivi basi Nyumba yangu ni nyeupe Hadi uvunguni😢😢😢😢
 
Back
Top Bottom