Hadithi: Mwanaheri binti wa kijakazi

mireille

JF-Expert Member
Mar 4, 2020
523
568
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 1

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

MWANAHERI Ni binti alielelewa na mzazi wake mmoja ambae Ni mama yake baada ya baba yake mzazi kufariki miaka mitano iloyopita, maisha ya mama mwanaheri na mwanae yalikuwa Ni maisha ya shida Sana, mama mwanaheri aliamua kufanya kazi kwenye majumba ya watu Kama kufua na kufanya usafi ilimladi wapate kuishi na mwanae.

Japo walikuwa na Hali ngumu na kipato duni mama mwanaheri alijitahidi Sana kumsomesha binti yake mpaka akamalizia kidato Cha nne , mwanaheri alifaulu vizuri lakini mama yake alishindwa kabisa kumsomesha ikabidi mwanaheri akae nyumbani kumsaidia mama yake kazi ndogo ndogo Kama vile kuuza vitumbua na maandazi . Kutokana na ucheshi na kuongea Sana pia kauli nzuri ilifanya biashara kwenda vizuri.

" Haya haya mama zamda toka nje uje ununue andazi lililokandwa kwa Nazi bila kusahau hiriki andazi Lina lika kwa kinywaji chochote ukija Sasa hapo kwenye kitumbua kimechambuka sio ugali Kama Cha mwafulani njooni kwa wingi jamani nikishapita ndio imetoka hiyo. Watu walikuwa wanamiminika kuwahi kununua
" Huyo ndio mwanaheri anavyojua kupiga debe Sasa.

" Sio kupiga debe tu bidhaa zangu zinajitangaza wewe unatafananisha vitumbua vyangu na vile vya Bibi Pili mishavu.
" Basi utasikuwa we mtoto utuletee balaa hapa
" Kumbe na nyie mnaogopa kuchambwa .

Badae ya kuishi maisha ya kubangaiza mama mwanaheri alibahatika kupata kazi kwenye jumba moja la kifahari alilipwa mshahara mzuri kidogo maisha yao yalibadilika , hatimae siku zilienda na maisha yakaendelea

Siku moja usiku mama mwanaheri alipata homa ya ghafla akamwambia mwanae
" Mwanaheri mwanangu naumwa sijui Kama kesho nitaweza kwenda kazini
" Sasa kazini utaendaje na hiyo hali ona unavyotetemeka utaenda kufanya kazi gani huko?
" Lakini kesho Kuna kazi nyingi mtoto wa boss wetu anamvalisha mchumba wake Pete Sasa sijui Kama nitaeleweka.

" Kwanini asikuelewe Sasa kwani wao hawajawahi kuumwa au ndio kwasababu masikini hatuna pesa tunafanya kazi Kama punda.

" Sio hivyo mwanangu nilifikiria Kama itawezekana ungeenda kwaajili yangu
" Khaaa mama Sasa naanzaje kwenda wakati na Mimi Nina Mambo yangu
" Hayo Mambo yako hayana faida kesho tutaenda pamoja nitakukabidhi kwa mfanyakazi mwenzangu ili msaidiane alafu Mimi nitaenda hospital.

" Sawa Ila Mimi Mambo yakurudi jioni sitaki Mambo ya mtaani yatanipita
" Mwanangu huo umbea wa mtaani unakusaidia Nini kutwa kucha Ni kusutana unajua sipendi hiyo tabia Basi tu hujui .
" Basi tusifike huko unaumwa pumzika hapo kesho nitaenda kwenye hiyo kazi yako .

Usiku ule walilala kulipokucha mama yake alimuamsha
" Mwanaheri amka kumekucha mwanaheri aliamka kivivu huku akijinyoosha
" Ndio uamke uache uvivu wako

" Nimeshaamka mama wewe nenda kajiandae. Mama mwanaheri alipotoka chumbani mwanaheri alirudi kulala aliporudi akakuta ndio kwanza mwanaheri anavuta shuka

" Jamani mtoto mvivu wewe hebu amka haraka . Aliongea mama yake huku akimpiga kibao mwanaheri aliamka na kujishika alipopigwa

"Mamaa Sasa ndio nini kunipiga asubuhi subuhi kwani hujui vibao vya asubuhi vinavyouma
" Nimekwambia amka haraka muone unachojua wewe Ni umbea tu nyooo. Mwanaheri aliamka akiwa kanuna akaenda kujiandaa alipomaliza waliondoka na mama yake mpaka kwenye Hilo jumba la kifahari

" Kumbe hapa ndipo unapofanyia kazi ? Aliuliza mwanaheri huku akiangaza macho kuangalia mazingira yakuvutia ya Ile nyumba kabla mama yake hajajibu alitokea mama mwenye nyumba na kuwasalimia
" Habari za asubuhi ! Mama mwanaheri akaitikia
" Salama mmeamkaje?
" Salama
" Mama Taliq huyu Ni binti yangu anaitwa mwanaheri. Mwanaheri alimsalimia mama Taliq
" marahaba jamani kumbe una binti mrembo hivi, karibu Sana mwanaheri

" Asante nimekaribia Leo nipo hapa mpaka jioni .mama Taliq aliachia tabasamu
" sawa Tena imekuwa vizuri leo tunasherehe ya Taliq anamvalisha Pete mchumba wake.
" Sawa Sasa mama si uombe hiyo ruhusa uwahi hospital Mimi ndio nimeshafika
" Kumbe mama mwana unaumwa Sasa si ungepumzika

" Nimekuja kuomba ruhusa alafu kwakuwa kutakuwa na kazi nyingi nimemleta mwanaheri aje asaidie saidie kidogo.

" Umefanya vizuri Basi mwanaheri nenda kule utakuta wenzio watakuelekeza Nini Cha kufanya
" Sawa. mwanaheri alienda alipoelekezwa akawaacha mama yake na boss wakiongea mama Tariq alitoa kiasi Cha pesa na kumpa

" Chukua hii kwaajili ya matibabu. Mama mwanaheri alisita kupokea
"Usiogope chukua . Alipokea na kumshukuru Kisha akaondoka .

Mwanaheri alipoingia ndani alianza kushangaa alisogelea kwenye kabati la kioo lililokuwa pale sebleni
" Jamani matajiri siwawezi kumbe wao hawana shida yakununua samaki wanafuga wenyewe ona walivyokuwa wazuri . Mwanaheri alifurahishwa na wale samaki waliokuwa wakizunguka ndani ya yale maji
" Mbona hii inavutia kuangalia ona wamepanda mpaka majani . Alitaka kuingiza mkono Mara akasikia anaambiwa
" Oya unafanya Nini hapo? Mwanaheri alishituka akageuka kumuangalia aliyemuongelesha

 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 2

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Mwanaheri aligeuka na kumuangalia aliemsemesha
" Nilikuwa naangalia Hawa samaki ,kwan vip?
" Wewe ni nani?
" Naitwa mwanaheri na wewe unaitwa nani?
" Kwani wewe ni mfanyakazi wa hapa?
" Hapana nimekuja kumshikia mama yangu
Af subiri kidog mbona unaniuliza tu maswali kama tupo kituo cha police kwani unataka nini kwangu na maswali yangu ninayo kuuliza hata hunijibu.
Tariq alimuangalia mwanaheri akauliza tena
" Mama yako ni kijakazi hapa?
" Ni mfanyakazi sio kijakazi .
" Sasa Kuna tofauti gani hapo?
" Samahani Kaka nimekuja kufanya kazi sio kujibu maswali yako nielekeze nielekee wapi?
" Kamuulize boss wako. Mwanaheri alirudi nje akamfuata mama Tariq
" Samahani nimefika sebleni nimekutana na Kaka mmoja kanichanganya kwa maswali sijajua nielekeze wapi
" Ahaa ngoja nikupeleke . Mwanaheri na mama taliq waliongozana mpaka jikoni akamkabidhisha kwa wafanyakazi wengine wawili.

" Jamani huyu ni mwanaheri mtasaidiana nae hapa.
" Sawa karibu mwanaheri
" Asante . Mama Tariq aliwaacha na wao wanaendelea na kazi.
Kuna muda mwanaheri aliiagizwa ndani kwenda kuchukua baadhi ya viungo kwaajili ya kupikia Mara akakutana na mama Tariq akiwa kashika nguo mkononi
" Afadhali nimekuonea shika hizi nguo mpeleke Tariq chumbani kwake
" Lakini sijui chumban chake ni kipi

" Nenda mlango ule pale . Mwanaheri alizipokea zile nguo na kwenda mpaka kwenye mlango alielekezwa alipofika aligonga mlango lakini hakuitikiwa aliendelea kugonga zaidi ya Mara mbili bila kukaribishwa akaamua kufungua na kuingia kumbe wakati huo Tariq alikuwa bafuni anaoga , mwanaheri aliweka nguo kitandani na kuanza kushangaa movie iliyokuwa inaendelea kwenye TV iliyokuwepo pale chumbani , akiwa bado anashangaa huku kasimama Tariq alifungua mlango wa bafuni na kutoka akiwa kajifunga taulo kiunoni mwanaheri alipomuona alishituka na kuanza kucheka cheka

" Niliagizwa nikuletee nguo nimepiga Sana hodi haukufungua
" Sasa Kama haujakaribishwa unaingiaje je ungekuta sijavaa nguo ingekuwaje?

" Bahati haijawa hivyo . Mwanaheri aligeuka haraka na kutaka kutoka Mara akagonga na mguu chupa iliyokuwa imewekwa chini na kusababisha kuvunjika , mwanaheri aligeuka kumuangalia tariq, nae Tariq alimkata jicho Kisha akasogea kwenye kioo Cha dressing table akawa anajiangalia . Mwanaheri akataka kuondoka akasikia anaambiwa

" Wewe unaenda wapi?
"Naenda kufanyakazi zangu kwani unataka nikae hapa wakati unataka kuvaa
" Nenda kachukie vifaa vya usafi uje usafishe fanya haraka
" sawa nakuja . Mwanaheri alibinua mdomo na kwenda kuchukua ndoo yenye maji na kwenda kusafisha alipofika mlangoni alisimama na kuuliza
" Niingie au bado unavaa?

" Ingia . Mwanaheri aliingia na kukuta Tariq anaendelea kuvaa
" Jamani si ungemaliza kwanza kuvaa ndio uniruhusu kuingia
" Wewe endelea na kazi yako Mimi kuvaa na wewe kufanya usafi Kuna uhusiano gani kila mtu afanye linomuhusu
" Kaka wa hkvyo huyu looh. Tariq alimgeukia akamuuliza
" Unasemaje?

" Sijasema kitu.
Mwanaheri alimaliza kufanya usafi wakati anataka kutoka aligeuka kumuangalia Tariq ambae alikuwa bize anajipulizia pafyum
" Kaka nimemaliza kusafisha .
" Una uhakika umetakatisha?
" Kwani unavyoniona unahisi siwezi kufanya kazi njoo Basi ukague.
" Nenda kaendelee na shuhuri zako. Mwanaheri alibeba vifaa vyake alipiga hatua chache Mara aliangusha Ile ndoo na kupiga kelele
" Aaaaaaaah. Tariq aligeuka haraka akamuona mwanaheri kanyanyuka mguu
" Una nini wewe? Aliuliza Tariq huku anamfuata alikuta mwanaheri anatokea na damu mguuni kipande Cha chupa kilikuwa kimemkata

" Ona sasa umeumia kwa uzembe wako mwenyewe nilikuuliza Kama umesafisha vizuri ukasema ndio .
" Lakini nimesafisha nikazoa chupa zote
" Sasa hiki kipande kulichokukata kimetoka wapi?
" Sijuikimetoka wapi labda ulinitegeshea mimi nitajuaje. Tariq alitaka kutoa kipande kilichong'ang'ania mguuni kwa mwanaheri , mwanaheri akavuta mguu wake
" Wewe unataka kufanya Nini?

" Nataka kutoa hicho kipande Cha chupa
" Niache nitakitoa mwenyewe taratibu . Tariq alimtegea na kukivuta Kisha akaenda kuchukua pamba akam safisha
" Wewe Kaka kwani wewe Ni daktari? Tariq alitingisha kichwa akimaanusha hapana
" Kwanini Sasa usingekuwa daktari Kama hizi kazi unazijua maana huna hata huruma . Tariq hakumjibu aliendelea kumsafisha Kisha akamfunga kidonda
" Haya nyanyuka uende.
" Niondoke nisisafishe?

" Wewe nenda kamwambie sauda aje asafishe.
Mwanaheri alinyanyuka akawa anatembea kwa kuchechemee Kisha akasimama
" Vipi mbona umesimama?

" Nashindwa kutembea nasikia maumivu makali. Tariq aliacha alichokuwa anafanya akaenda kumshika na kumsaidia kumtoa pale chumbani . Wakati wanashuka ngazi Kuna Dada mrembo aliekuwa anatabasamu Ila baada ya kumuona Tariq kamshikilia mwanaheri taratibu tabasamu lilianza kutoweka hakusubiriwashuke chini aliamua kuwafuata, Tariq alimpokea kwa tabasamu akamuachilia mwanaheri wakakumbatiana. Wakati wanakumbatiana yule Dada alimsukuma mwanaheri akayumba na kutaka kuanguka. Mwanaheri alisimama vizuri na kuwaangalia moja kwa moja alijua Ni mwanamke wa Tariq . Yule mwanamke alimuangalia kwa dharau mwanaheri Kisha akauliza.

" Baby huyu ni nani na mbona ulikuwa umemshika vile?
" Naina mpenzi punguza wivu Mimi Ni wako peke yako huyu ni mtoto wa mama mmoja mfanyakazi wa hapa ?
" Sasa yeye kafuatanini hapa?
" Hebu tuachane na hayo twende tukaongee. Walishikana mikono wakashuka ngazi huku mwanaheri akiwaangalia

" Muone na matege yake na ningeanguka ndio angezijua rangi zangu nisingemuogopa huyo mwanaume wake Wala nisingejali Kama nipo ukweni kwake shubamit na huyo kanitelekeza Sasa nitashukaje hapa. Mwanaheri alishuka taratimu Mara Tariq alikuwa anaelekea chumbani kwake akamkuta bado anajivuta pale kwenye ngazi.
" Oooh sorry kumbe nimekutelekeza hapa twende nikupeleke ukapumzike Tena hizo kazi usifanye unatakiwa utulize huo mguu. Tariq alimshika na kumpeleka jikoni akamkalisha kwenyu kiti Kisha akachukua miguu ya mwanaheri akaiweka juu ya kiti kingine alipomaliza akaondoka Ile anatoka tu aliingia Naina na kusimama mbele ya mwanaheri

" Wewe umekuja kufanya kazi au kuchukua mabwana za watu? Mwanaheri alimuangalia na kucheka Naina alizidi kupandwa na hasira

 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 3

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688157169

Mwanaheri aliendelea kucheka kwa dharau Naina akapandwa na hasira
" Nyamaza unachekacheka Nini?
" Khaaa wewe dada hebu niache mwenzio nicheke niongeze siku za kuishi alafu kumbuka Leo Ni siku muhimu Sana kwako hivyo usije ukasababisha nikakuharibia siku . Naina alimfyonza Kisha akamwambia
" Yani wewe kijakazi uniharibue siku Mimi ?
" Kwani kijakazi Hana mdomo wa kuongelea hebu nenda kwa huyo bwana ako nisije nikakuchamba ukaanza kulialia hapa , kwanza mtu gani hujiamini eti bwana angu ,mume wangu hata paka ana bwana ndio maana anazalishwa .
" Alafu wewe nakuweka kiporo acha siku ya Leo ipite .
" Raha ya mchuzi unywewe wamoto bwana ukipoa hauna Radha . Mara Tariq alienda jikoni akawakuta
" Baby kumbe upo huku nilikuwa nakutafuta . Naina alimfuata Tariq wakaondoka
Huku wameshikana mikono Naina akageuka nyuma kumuangalia mwanaheri Kama vile anamringishia .
" Kione kilivyo kama kisungura Sasa anafikiria nawaonea wivu kwa taarifa yake sijamtamani huyo mwanaume wake na ningekuwa nimemtamani mbona ningemkomesha nimgemuonyeshea mauzauza mpaka aombe po.

Maandalizi yakaendelea hatimae wageni walianza kufika sherehe ikaanza Dada mmoja mfanyakazi wa pale alimfuata mwanaheri akamwambia
" Twende kwenye sherehe .
" Sina hamu yakwenda huko maana hakuna maajabu yoyote Bora ungeniletea msosi nile maana njaa inaniuma sioni hata wa kuniuliza mko bize na hao wageni . Yule Dada alitabasamu
" Basi naenda kukuletea chakula
" Utafanya la maana Sana na vipilipili usisahau kuweka alafu hii Ni sherehe haikosi vinywaji naomba uniletee tafadhali. Mwanaheri alitengewa chakula akaanza kula alipomaliza alinyanyuka taratibu kuelekea kwenye sherehe alisimama pembeni kuangalia yanayoendelea
" Sasa ndio sherehe gani imepoa mziki unaopigwa ni wakizungu Kama tupo ulaya watu wanaigiza uzungu wanataka kupoteza tamaduni zetu hapa ingefaa waweke kisingeli watu tujichanganye Sasa hapa mtu Kama Mimi naanzia wapi kucheza mziki una this,this,that,that hapa Bora niwe mpenzi mtazamaji.

Baada ya Tariq na Naina kuvalishana Pete watu walienda kuwapa hongera , mwanaheri alifikiria kitu Kisha akatabasamu taratibu aliwasogelea akaanza kwa Tariq
" Hongera Sana boss Mungu akutangulie kwenye safari yako ya Mapenzi .
" Asante. Mwanaheri alimsogelea Naina akataka kumkumbatia Naina akarudi nyuma Kisha akamuangalia Tariq akakuta Tariq anamuangalia ndio akajituliza mwanaheri akamkumbatia akasogeza kichwa chake karibu na sikio la Naina akamwambia
" Sasa nimejua kwanini una wasiwasi wa kuibiw a mpenzi wako nimegundua nimzuri Sana anaweza kumvutia mwanamke yoyote hivyo sio kosa lako Ila endelea kuwa makini . Mwanaheri alimuachia Naina Kisha akamuangalia usoni huku anatabasamu akamalizia kwa kumpa hongera Kisha akaondoka huku Naina akiwa anamuangalia kwa hasira.

Sherehe ilipoisha watu walianza kuondoka mwanaheri alimfuata mama Tariq akamwambia
" Boss Mimi naomba niondoke kwa hii Hali yangu siwezi kufanya kazi yoyote alafu sijui mama yangu anaendeleaje huko nyumbani .
" Sawa usijali unaweza ukaenda . Mwanaheri alijivuta taratibu akaenda jikoni akamkuta yule Dada aliempa chakula
" Samahani dada naomba uniwekee chakula kwenye huu mfuko nimpelekee mama yangu so unajua mgonjwa atakuwa hajapika.
" Haina haja yakuweka kwenye mfuko nitaweka kwenye hotpot . Yule Dada alichukua hotpot akampakulia chakula na kuweka kwenye ule mfuko alafu akampa
" Asante Sana acha nimuwahi .
" Sawa Mpe pole . Mwanaheri aliondoka huku akichechemea alipofika maeneo ya getini Tariq alimuona akataka kumfuata Naina akamuuliza
" Unaenda wapi mpenzi .
" Naenda kumpatia nauli mwanaheri.
" Achana nae bwana kwani kakuomba ?
" Hajaniomba lakini na Ile Hali yake hawezi kufika kituo Cha daladala . Tariq alimfuata mwanaheri huku Naina akimfuata nyuma walipomkaribia Naina akamuita
" wewe kijakazi mdogo hebu subiri . Mwanaheri alisimama huku akitafakari jibu la kumpa alipogeuka akiwa kakunja uso akakutana uso kwa uso na Tariq . Tariq alijua mwanaheri hajapenda kuitwa vile akamgeukia Naina akamwambia
" Huyu sio mfanyakazi wetu alikuja kumsaidia mama yake.
" Oooh samahani binti wa kijakazi . Naina aliongea huku akiwa anaukumbatia mkono wa Tariq .
" Nawasikiliza wapendanao. Tariq alitoa hela akampatia mwanaheri.
" Hii utafanya Kama nauli . Mwanaheri aliipokea na kumshukuru
" Asante.
" Hela kidogo unatoa Asante kubwa hivyo. Naina aliropoka
" Tariq naomba Sana umfundishe adabu huyu limbukeni wa mapenzi naona anajiona kamaliza kukupata kijana mtanashati Kama wewe Ila ipo siku wapo warembo wanaovutia watakukamata na kumuacha akibweka Kama anavyobweka hapa . Mwanaheri alimaliza na tabasamu Kisha akaondoka
" Tariq unamsikia huyu mjinga anavyonikashifu na wewe husemi kitu
" Unataka nifanye Nini na wewe ndio ulieanza ukorofi. Tariq alirudi ndani Naina akasimama kumuangalia mwanaheri aliekuwa anampungia mkono

 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 4

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Siku moja jioni mvua ilikuwa inanyesha mama mwanaheri alishindwa kuondoka akawa anasubiri mvua ikatike , Tariq alimuona akamuuliza
" Mbona umejibanza hapa?
" Nasubiri mvua ipungue niondoke . Baada ya kuambiwa hivyo Tariq alipiga hatua chache akiingia ndani Mara akasimama na kurudi pale aliposimama mama mwanaheri.
" Naweza nikakupeleka nyumbani kwako?
" Kama una safari yakutoka sawa .
" Sawa Basi twende. Tariq alijifunika mwamvuli na mama mwanaheri akajifunika kitenge chake wakaenda mpaka parking ya magari wakapanda kwenye gari la Tariq safari ya kuelekea kwa mama mwanaheri ikaanza. Kwenye gari Tariq alianza kumuuliza maswali mama mwanaheri
" Hivi mwanao anajishuhurisha na nini?
" Mmmh unamuulizia mwanaheri?
" Ndio
" Yupoyupo tu mtaani Hana kazi ya maana
" Na amesoma Yani anajua kusoma na kuandika?
" Ndio anajua kasoma mpaka form 4 Ila ndio hivyo sikuwa na hela ya kumuendeleza kimasomo.
" Ok nikimpatia kazi kwenye ofisi yangu anaweza kufanya ?
" Ndio baba nitashukuru Sana ukifanya hivyo utakuwa umenisaidia mno .
" Basi nitaenda kuongea nae Kama atakubali ataanza kazi maana tuna uhaba wa wafanya usafi pale kazini
" Hiyo kazi inamfaa kabisa.

Mama mwanaheri akawa anamuelekeza ilipo nyumba yake walipofika alisimamisha gari wakashuka ,Tariq alichukua mwamvuli wake akajifunika wakaingia kwenye geti dogo lililotengenezwa kwa mabati walimkuta mwanaheri akiwa katikati ya mvua akiwakaloana , mama yake akamwambia
" Wewe mjinga unafanyanini kwenye mvua ? Mwanaheri aligeuka kumuangalia mama yake alishituka kumuona Tariq akaanza kuvuta vuta nguo yake kwa aibu maana ililowa na kung'ang'ania mwilini ikawa inaonyesha baadhi ya maumbile yake mama yake alimrushia kile kitenge alichokuwa kajifunika mwanaheri akajifunika haraka
" Tariq karibu ndani.
" Asante. Mama mwanaheri na Tariq waliingia ndani na kumuacha mwanaheri akiwa kasimama anawaangalia
" huyu boss mtoto kafuata Nini hapa kwetu Tena mama kamuingiza ndani nitapitaje kwanza hata siingii ngoja niendelee kuchota zangu maji . Mara akasikia anaitwa na mama yake
" Mwanaheri unafanya Nini huko hebu njoo bwana .
" Nachota maji
" Nimekwambia toka kwenye mvua ingia ndani haraka . Mwanaheri aliingia ndani akiwa kalowana akapita pale sebleni akaingia chumbani akabadilisha nguo Kisha akatoka sebleni .
" Mwanaheri mwanangu nimekuja na Tariq anataka kuongea na wewe .... Kabla hajamalizakuongea mwanaheri akadakia
" Mama Kama kuhusu kuwa kijakazi Mimi sitaki kabisa maana najijua mwenyewe naweza nikamfanya vibaya yule mwanamke wake anaeshindania tuzo ya mapenzi . Tariq alitamani kucheka alijikaza akaishia kutabasamu
" Sio kazi hiyo nataka nikupe nafasi ya kufanya usafi kule kazini kwangu je upo tayari? Kabla mwanaheri hajajibu mama yake akamjibia
" Lazima awe tayari
" Sawa vipi Kama muhusika hatakuwa tayari
" Mama kasema kwanini nikatae na vipi kuhusu mshahara utanilipa shilingi ngp?
" Hilo tutaliongea naomba jumatatu ufike pale ofisini kwetu.
" Sasa nitapajuaje hapo kazini kwako ? Mama mwanaheri akamjibu
" Tutatoka hapa mapema nitakupeleka ndio na Mimi niende kazini .
Baada ya makubaliano Tariq aliwaacha akaondoka
" Mwanaheri mwanangu safari hii nakuomba usichezee hii kazi imekuja kwako kama bahati .
" Nimekuelewa .
" Sio unielewe kwa juu juu nielewe vizuri maana umeshakuwa mkubwa inabidi ubadilike achana na Makundi ya kijinga kila siku kusutana huko mitaani haitakusaidia chochote
" Nimekuelewa mama yangu kipenzi hiyo kazi nitafanya lakini na Mimi naomba kitu kimoja tu
" Kitu gani hicho?
" Hapo kwenye Mambo ya kusutana hapo mtu akiingia kwenye anga zangu au akienda kusema umbea sitaacha kumsuta kwasababu mashoga zangu wenyewe wananielewa Mimi ndio kamanda mwenye vyeo kwenye kusutana
" Yani wewe ipo siku utaelewa kwanini nakataza haya Mambo ya kusutana kibao kimoja kitakuja kukugeukia ukisutwa na kupigwa sitaingilia hatanikute unasutwa hapo nitakupita Kama sikujui
" Hahahaha mama acha Basi kwani hunijui mwanao kwanza huyo wa kunisusha nani ,cheo changu Cha ukamanda ajipange. Wakiwa bado wanaongea alikuja mtu akawa anamuita mwanaheri
" Mmmh kumekucha mwanaheri hutoki hapa ?
" Sasa sitoki vipi hujui hata anaeniita Ni Nani na anashida gani unanizuia , acha nikamsikilize kwanza mbona huniamini hivyo mama yangu? Mwanaheri alitoka akamuona shoga yake Maimuna kajibanza mlangoni
" Wewe Mai na mvua hii unataka Nini ?
" Wewe nae nimeshindwa kuvumilia shoga yangu ikabidi nitoke na hiki kimvua nije nikuletee umbea .
" Hayo ndio nayataka hebu nipe mambo.
" Ni kuhusu Said yule bwana uliekataa posa yake ....
" Mfyuuu Sasa habari za Sadi Mimi zinanihusu Nini ?
" Tulia Bibi nikupe kitu kamili kikukae rohoni . Ni hivi Sadi kamchumbia Asma mahari imeshatolewa na harusi yao mwezi ujao na sale imeshakatwa upo nyonyo?
" Weweeeee Sasa hapo sio pakukosa na Mimi nataka hiyo sale . Mai aliduwaa huku akimshangaa
" Nini unanishangaa sare ipo kwa Nani ?
" Mwanaheri inamaana huumizwi na hili
" Khaaaaa ndio maana ukaja mbio na umbea wako ukajua utaniharibia siku Sasa nakwambia hivi sijashituka Wala sijaumia hata kidogo kwenye hiyo harusi nitaenda na sare nashona na pilau lao nakula Tena ikiwezekana na kubeba nitabeba na hizi taarifa kawafikishie wambea wenzio najua mlikaa mkanijadili , kwaheri nenda kwenu usije ukapata homa na hii mvua kajitulize nyumbani kwenu kwaher

 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 5

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Mwanaheri aliingia ndani Mai aliendelea kusimama akishangaa
" Kwani huyu ana moyo wa jiwe hajaumia hata kidogo ndio kwanza anaulizia sare mmmh sijawahi kuona nilijua atakuwa mdogo kwa wivu lakini ndio kwanza yamenishuka Mimi mleta habari looh.

Ilifika siku ya jumatatu mwanaheri na mama yake waliamka mapema wakajiandaa Kisha wakaelekea kazini kwa Tariq ,ilikuwa ni mapema Sana ofisi zilikuwa hazijafunguliwa ikabidi mwanaheri akae na mlinzi mpaka utakapofika muda wa wafanyakazi kufika ofisini . Ilipofika mida ya saa mbili na nusu mlinzi alimshitua mwanaheri ambae alikuwa bize anachati na simu yake ndogo
" Dada boss ndio huyo alieingia na Hilo gari
" Ahaaa Asante . Mwanaheri alipiga hatua kumfuata gari la Tariq lilipo park Mara simu yake ikaanza kuita alisimama na kutoa ndani ya mkoba wake akapokea
" Hallow
" Nilikuwa nakwambia leo ndio siku ya kwenda kuchukua sare ya harusi
" Jamani Sasa Mimi sipo nyumbani nisaidie kitu kimoja kanichukulie hiyo sare yangu jioni nitakuja kuchukua kwenu
" Mmm au ndio umeshaanza kuogopa maana watu wanataka kuhakikisha Kama kweli utachukua sare .
" Acha upuuzi tangia lini Mimi nikaogopa wewe kanichukulie Mambo mengine tutaongea badae Sasa hivi nipo sehemu muhimu Sana . Mwanaheri alikata simu akamuona Tariq anaingia kwenye lango kuu la kuingilia ofisinialitembea harakaharaka alipofika hakujua kaingia wapi alianza kuangaza macho kila Kona akimtafuta kwa ndani lilikuwa Ni jengo kubwa kila mtu alikuwa Yuko bize hata waliokuwa wanatembea walionekana kuwa bize
" Sasa hapa naelekea wapi? Akiwa anatafakari Nini chakufanya Kuna Dada mmoja alimfuata na kumsalimia
" Habari dada?
" Salama
" Nimekuona umesimama kwa muda sijui ulikuwa unashida gani ?
" Namtafuta Tariq
" Unamaanisha boss Tariq?
" Huyohuyo
" Una miadi nae?
" Jamani dada mbona maswali mengi Mimi naomba unionyeshe alipo Basi Mambo mengine nitaongea nae yeye
" Sawa lakini Kama hauna miadi nae huwezi kuonana nae .
" Mmh mbona kazi hebu mpigie simu mwambie nipo hapa namsubiri .
" Hebu nifuate nikampigie kwanza simu . Mwanaheri walipiga hatua chache Mara akamuona Tariq anatoka kwenye lift
" Basi dada endelea na kazi zako mtu mwenyewe yule pale
Tariq alikuwa anaongea na simu mwanaheri alimfuata akasimama pembeni yake ,Tariq alimuangalia akaendelea kuongea na simu
" Sasa ndio nini kunisimamisha hivi so angekata hiyo simu yake kwanza anipe maelekezo ya kazi . Alijisemea mwanaheri baada ya kusimama kwa muda kidogo . Tariq alipomaliza kuongea na simu alimuonyeshaa ishara amfuate . Waliongozana mpaka sehemu kwa Dada mmoja
" Habari Queen
" Salama boss .
" Naomba umuelekeze sehemu ya kufanya usafi
" Sawa karibu dada
" Asante
" mwanaheri utafuata maelekezo utakayopewa na Queen.
" Sawa.
Tariq aliondoka akamuacha mwanaheri na Queen
" Naomba unifuate nikupeleke kwa kiongozi wa usafi . Mwanaheri na Queen waliongozana mpaka kwa mama mmoja ambae alikuwa anamalizia kusafisha choo
" Shikamoo mama merry
" Marahaba .
" Huyu Ni mtu wako nimeambiwa nikuletee na boss utampangia sehemu ya kufanya usafi .
" Ahaaa karibu Sana binti
" Asante .
" Haya ngoja niwaache si unajua Tena Mambo ya hapa
" Wahi dada kafanye kazi huyu kafika. Mama merry alianza kumuelekeza sehemu atakazokuwa anafanya usafi na pia alimsisitiza kuwahi kufika unatakiwa wamalize usafi mapema kabla wafanyakazi hawajafika .
" Zingatia kufanya kazi kwa makini boss wetu Ni mkali Sana
" Huyo Tariq ana ukali gani Sasa?
" Mmh labda Ni mpole huko nje lakini hapa kazini huwa hacheki na mtu .
" Mimi namuona yupo kawaida .
" Sawa lakini nimeshakutahadharisha mapema.
Zilipita wiki mbili tangia mwanaheri alipoanza kazi ,watu wengi walimzowea kutokana na uchangamfu wake. Mwanaheri alimshangaa Sana Tariq walipokuwa kazini alikuwa Kama vile hamfahamu pia alikuwa mkali kwa mfanyakazi atakaefanya uzembe kazini
" Mmmh kumbe mama merry alisema kweli hapa na Mimi nijifanye bize nikileta kujuana anaweza akanishushia mbele za watu . Siku moja mwanaheri akiwa kamaliza kufanya usafi akawa amekaa nje na wenzake wanapiga story alifika secretary wa Tariq
" Mwanaheri unaitwa na boss
" Boss gani?
" Mwanaheri acha utani hebu nifuate unajua kasimama dirishani anatuangalia . Mwanaheri alinyanyua macho akamuona Tariq kasimama dirishani anaangalia walipo , secretary na mwanaheri wakaongozana kuelekea ofisini kwa Tariq
" Kwani ananiitia Nini?
" Sijui kaniambia tu nije kukuita Kama Kuna ulilolikoroga unalo maana anaonekana ana hasira Sana
" Kwahiyo hizo hasira zake anataka akamalizie kwangu?
"Sijui Ila Kama ulimkosea lazima hasira amalizie kwako . Walifika wakaingia na kumkuta bado kasimama dirishani
" Boss mwanaheri huyu hapa
" Nenda kaendelee na kazi zako . Yule secretary alitoka, Tariq akaenda kukaa kwenye kiti chake
" Mwanaheri unaweza kutumia kompyuta?
" Nimeitumia wapi mpaka nijue naishia kuziangalia kwa macho tu sijui inafunguliwaje Wala inazimwaje.
" Sawa kuanzia kesho utaachana na kazi ya usafi wa eneo ulilopangiwa utasafisha ofisini kwangu pamoja na kufanya kazi nyingine zinazohusu huku ofisini kwangu.
" Sawa lakini hayo mengine siyajui
" Kila kitu utaelekezwa na Nakaaya secretary wangu .
" Sawa .
" Unaweza kwenda . Mwanaheri alinyanyuka akatoka ofisini kwa Tariq
"Kuwekana hofu tu nikajua sijui nimefanya kitu gani kikubwa kumbe maongezi yanyewe Ni yale. Wakati mwanaheri anaongea mwenyewe akapamiana na Kaka mmoja alipotaka kuanguka yule Kaka akamdaka wakawa Kama wamekumbatiana na wakati huo Tariq alikuwa anatoka ofisini kwake aliwaona akasimama na kuwaangalia

Soma mpaka mwisho kwa 1000 tu

 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 6

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Mwanaheri na yule Kaka walizubaa kwa kushangaana mpaka Tariq akajikohoza kidogo ndipo wakashituka na kuachiana wakamgeukia Tariq yule Kaka aliachia tabasamu na kumfuata Tariq pale alipokuwa kasimama wakakumbatiana wote walionekana kuwa na furaha
" Niambie umeingia lini? Tariq alimuuliza
" Nimeingia Jana jioni
" Nilikukumbuka Sana bro Ila Sameer wewe Ni waajabu Sana unakujaje Bila kunipa taarifa?
" Ni story ndefu Kaka ndio maana nikasema mapema Sana nije kukuona . Mwanaheri alikuwa amesimama akiwashangaa mpaka Tariq akamuuliza
" Mwanaheri unashida gani mbona umeganda hapo? Sameer akadakia
" Samahani dada subiri. Mwanaheri alisimama
" Samahani kwa haraka zangu nikajikuta nakuvamia vipi hukuumia popote?
" Wala sijaumia nipo sawa
" Oooh Safi Sana naitwa Sameer nimefurahi kukutana na wewe mrembo mwanaheri. Tariq alikuwa anamjua vizuri Sana rafiki yake Ni mgonjwa wa wanawake utambulisho na maneno yasingeisha ilibidi aingilie
" Mwanaheri nenda kwa Nakaaya. Mwanaheri alienda kwa Nakaaya huku akijinusa nguo zake
" Huyu Kaka amejimwagia hii pafyumu maana sio kwa kuniachia harufu ya marashi yake. Queen akamuuliza
" Mbona unaongea mwenyewe?
" Kuna Kaka mmoja mzuri amenigonga nilipotaka kuanguka akanidaka Kama wale mastering wa kwenye movie. Queen alicheka
" Bila Shaka Ni Sameer huyo?
" Ndio huyohuyo umejuaje?
" Nilipishana nae .
" Yani sijaamini Kama kanidaka nilikuwa naenda chini
" Kwa bahati ukakutana na steering wa kihindi kuwa makini nae hachekewi .
" Sasa namchekea namjua na ndio kwanza nimemuona leo
" Tuachane na hayo sogea hapa nikuelekeze maana Mambo mengi na muda Ni mchache

Sameer na Tariq waliingia ofisini kwa Tariq
" Nimefurahi Sana kukuona
" Hunishindi Mimi vipi kazi zinaendaje?
" Kama unavyoona tunapambana .
" Naona Mambo sio mabaya ofisi inazidi kupendeza naona na warembo wapya .
" Hujaacha Mambo yako?
" Naachaje Sasa wakati watoto wa zuri Kama mwanaheri ndio ugonjwa wangu
" Unatakiwa kubadilika tabia za uzinzi hazifai
" Eeeee kwakuwa wewe umepata kwa kujistiri ndio unajifanya baba ushauri.
" Bado sijaowa Ila Mambo ya kuchanganya wanawake sio hurka yangu na wewe tafuta mmoja wakuweza kufunga nae ndoa .
" Sawa Ila huyu mwanaheri nazani anafaa kuwa tulizo la moyo wangu.
" Acha ujinga huwezi kumvuruga binti wa watu nenda kawavuruge hao uliowazowea .
" Kwahiyo hutaki na wafanyakazi wako?
" Sameer naomba tubadilishe mada tuongee Mambo ya maana . Waliacha kuongelea Mambo ya wanawake na kuongea Mambo yao mengine .

Mwanaheri alianza kuelekezwa kazi za kufanya pamoja na kutumia kompyuta .
" Mwanaheri unatakiwa kuwa makini Sana na Mambo niliyokuelekeza .
" Sawa nimekuelewa na yote nitazingatia lakini nataka kujua kwanini nifanye hizi kazi ambazo ulikuwa unafanya wewe ikiwa na wewe upo?
" Mwezi ujao naondoka naenda kujiendeleza kimasomo boss kakuteuwa wewe uwe secretary wake .
" Mmmh sawa ngoja nijitahidi kujifunza niepukane na makasiriko . Wakiwa wanaongea Tariq alipiga simu na kuhitaji apelekewe kahawa.
" Boss anahitaji kahawa .
" Kamchukulie so nilishakuelekeza jinsi ya kuandaa. Mwanaheri alinyanyuka akaenda kuandaa alipokuwa tayari aliionja akakunja uso
" Mmm mbona chungu hivi ataweza kunywa . Akachukua sukari akaweka Kisha ajaonja Tena
" Hapa angalau sio Kama mwanzo kwanza sijui wanapendea Nini vitu vichungu Kama mwarobaini. Mwanaheri alibeba na kupeleka ofisini kwa boss Kisha akamimina kwenye kikombe akachanganya na maziwa kidogo .
" Kuna kingine Cha kukuhudumia boss
" Nikihitaji nitakuita kwa Sasa unaweza kwenda . Mwanaheri alipiga hatua mpaka mlangoni kabla hajafungua mlango alisikianatwa
" Wewe ndio umepika hii kahawa?
" Ndio kwani Ina Nini boss?
" Kwanini umeweka sukari?
" Niliona chungu Sana nikaamua kujiongeza nikaweka sukari ili uchungu upungue.
" Hivyo ndivyo Queen alivyokuelekeza ?
" Hapana .
" Toa kahawa yako nahitaji kupikiwa kahawa Kama aliyokuelekeza Queen. Mwanaheri alibeba Ile kahawa akawa anaondoka alipofika mlangoni akataka kufungua mlango ghafla ule mlango ulifunguliwa kwa nguvu na kusababisha viombo alivyobeba vianguke na kuvunjika , Tariq alisimama na kuanza kufoka
" Hivi kwanini hufanyi Mambo yako kwa uangalifu?
" Kosa sio langu ongea na huyu mwanamke wako anaeingia ofisini kwa watu bila hodi.

 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI. 7

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP: 0688156169

" khaa unaongea Nini wewe kijakazi na hapa unafanya nini? Alafu naomba ufahamu hii Ni ofisi ya mpenzi wangu naingia na kufanya nitakalo hivyo usinipangie sawa .
" Heyy naomba msinipigie kelele ofisini kwangu mwanaheri nenda kaendelee na kazi zako na hiyo kahawa siitaki tena, nenda kamwambie mtu wa usafi aje asafishe .
" Afadhali niepukane na hii Shari. Mwanaheri alimpiga kikumbo Naina akaondoka ,Naina alimfuata Tariq
" Baby umeleta kituko gani hapa kazini kwako?
" Hebu kaa kwanza . Naina alikaa kwenye kiti
" Anafanya Nini hapa ?
" Ni mfanyakazi wa hapa
" mmh Yani kutoka kijakazi wa kuosha viombo na kudeki mpaka kuwa mfanyakazi wa ofisini kwa elimu ipi hasa au ndio kubebana ?
" Unakosea Sana kusema hivyo mpenzi wangu kwanza tatizo lako na huyu dada Ni Nini?
" Sipendi uwekaribu nae.
" Kwani unahisi akiwa karibu na Mimi Nini kitatokea ?
" Hakuna Ila sipendi tu . Tariq alitabasamu Kisha akamsogelea Naina
" MKE wangu mtarajiwa Naina hebu achakuwa na mawazo mabovu siwezi kutamani mwanamke yoyote kila ninachotaka nakipata kwako . Naina alijisikia Raha kuambiwa vile .
" Si ndio hapo Sasa huyo mwanaheri mwenyewe hanikuti hata nusu kwa urembo.
" Wewe Ni mrembo mpenzi wangu ndio maana umenikamata
Tariq alikuwa anampasifa mpenzi wake ili ajione Bora kuliko mwanaheri lakini ukweli Ni kwamba mwanaheri alikuwa amejaaliwa shepu tofauti na Naina .
" Sasa mpenzi nimekutia tukapate chai pamoja
"Mmmm kwa Sasa haitawezekana mpenzi ndio kwanza nimeingia ofisini na Nina kazi kibao za kufanya so wewe nenda kanywe .
" Ok lakini naomba lunch tutoke wote.
" Sawa .
" Ok bye ngoja niwahi kazini .
" Ok uwe na kazi njema . Waliagana Naina alitoka pale ofisini na kuelekea alipo mwanaheri ,alikuta queen anamuelekeza vitu kwenye kompyuta alisimama na kuangalia kwa dharau Kisha akasema
" Hivi kwanini unasumbuka kumuelekeza huyu kijakazi naona Kama unajisumbua huyo kazowea kazi za nyumbani . Mwanaheri alimuangalia Kisha akamwambia Queen
" Queen naomba tuendelee achana na huyo fungu la kukosa . Queen alimshangaa mwanaheri alivyomjibu mpenzi wa boss wao bila hata uwoga .
" Tutaona Mimi na wewe Ni Nani fungu la kukosa na ninakupa mwezi huu mmoja wa kukaa hapa . Naina alifyonza akaondoka Queen alimgeukia vizuri mwanaheri
" Unashida gani na huyu dada?
" Simuelewi siku ya kwanza kukutana naealianza kunionyesha mauza uza yake Kani kuta mtu mwenyewe hata sijali lakini akiendelea nitampa kile anachokitaka maana sinaga shoo mbovu.
" Ilakumbuka ni mpenzi wa boss unatakiwa usishindane nae .
" Mimi huyo nivumilie ujinga akiniletea mdomo Wala sitamuacha Nampa vidonge vyake na akiendelea nitamchukua na huyo mwanaume wake anaemfanya anamuonea vivu. Queen alicheka Sana
" Mwanaheri unanifurahisha utamuweza huyo boss hata kucheka hacheki
" Kwani namchukua kwa mapenzi Ni kwaajili ya kumkomesha huyo hayawani wake.
" Hebu acha kunifurahisha tuendelee na Mambo yetu. Waliendelea kuelekezana

Siku moja mwanaheri alipeleka faili kwaajili ya boss kuweka saini Tariq alikuwa bize na kazi nyingine akamwambia aliweke pembeni Kisha amuwekee maji kwenye grass, mwanaheri alikuwa mbali kimawazo akamimina maji yalijaa kwenye grass na kumwagikia mezani na Wala hakushituka aliendelea kumimina mpaka aliposhituliwa na Tariq.
"Wewe huoni Kama una mwaga maji? Mwanaheri alishituka karatasi zilizokuwa karibu zililowana alizitoa na kuzikunguta wakati anawahi karatasi nyingine zisiliwane aliitingusha Ile grass ya maji ,maji yote yakamwagika na Ile grass ikadondoka chini na kupasuka. Muda wote Tariq alikuwa anamuangalia hakumsaidia kusogeza chochote.
" Jamani boss nisaidie Basi kutoa hizo huko kabla maji hayajafika . Tariq alisimama akatoa laptop yake Kisha akaongea kwa hasira
" Hivi wewe upo serious kweli na kazi ?
" Ndio Ni bahati mbaya tu
" Yani wewe kila siku unafanya ujinga alafu unasinguzia bahati mbaya, naomba unisikilize Kama huwezi kufanya kazi kwenye ofisi yangu njia nyeupe unaweza ukaondoka. Mwanaheri hakujibu alijua kakosea aliendelea kufuta Yale maji na Tariq alitoka nje .
" Huyu jamaa kakasirika Sasa na Mimi nimekosea kweli Sasa hapa nafanyaje haya makaratasi yaliyoloana . Mwanaheri alifikiria akapata njia ya kukausha zile karatasi . Alichukua feni mdogo iliyokuwa mezani akaiweka vizuri Kisha akatandaza karatasi zilizolowana Kisha akaiwasha , pembeni kulikuwa Kuna karatasi ambazo hazokulowa zilipeperushwa na upepo wa feni na kuzagaa ofisini
" Mamaaa hii Nini Tena Tariq akikuta hivi siatanimeza . Alizima feni Ile anainama kuokota mlango ulifunguliwa wakaingia Tariq na Sameer walisimama walishangaa imekuwaje karatasi zizagae kila sehemu

 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 8

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Sameer aliamua kumsaidia mwanaheri kuokota makaratasi walipomaliza Sameer alimkabidhi .
" Asante
" Huna haja ya kunipa asante na Wala usijal hiki kilichotokea ni Kama ajali kazini . Tariq aliwaangalia pia mwanaheri alimtupia jicho la uwoga
"Nenda na hizo karatasi kazitoe copy.
" Sawa. Mwanaheri alitoka pale ofisini huku Sameer akiwa anamuangalia na kuachia tabasamu flani kwa mbali .
" Tariq unajua sio vizuri kuwa mkali kwa watoto warembo Kama Hawa unatakiwa kuongea nao kwa upole .
" Upole kwenye kazi zangu hauna nafasi hata kidogo hata huyo Naina akiniletea ujinga kazini kwangu nitakuwa mkali .

Mwanaheri alifanya Kama alivyoagizwa na boss wake huku akiongea mwenyewe
" Sijui nimefanya ujinga gani Sasa hapa nitaanzaje kuomba ruhusa ikiwa nimemkasirisha boss Ila nitajua tu chakufanya siwezi kuikosa harusi ya Sadi maana nikiikosa nitawapa lakuongea wambea wa mtaa utasikia oooh mwanaheri kashindwa kuja kwasababu anaona wivu.

Kesho yake ilikuwa siku ya ijumaa na ndio siku ya harusi ya Sadi , siku hiyo mwanaheri aliamka mapema kabla ya mama yake akakaa kitandani
" Lazima niucheze huu mchezo la sivyo shuhuri itanipita hii. Baada ya muda kwenda mama mwanaheri aliamka na kwenda sebleni anakolala mwanaheri akamkuta kakaa
" Leo umejitahidi umeamka mapema .
" Yani achatu mama hapa nilipo naumwa tumbo kuanzia saa kumi nipo macho sijui Kama nitaweza kwenda kazini
" Hilo tumbo umekula Nini?
" Sijala chochote zaidi y chakula tulichokula usiku. Mwanaheri aliongea huku akiwa ameshika tumbo lake
" Jamani Sasa kwanini usingeniamsha
" Sikutaka kukusumbua , niombee ruhusa kazini.
" Nakuombeaje Sasa wewe si unayo namba ya boss wako mpigie umwambie unaumwa
Hicho ndio alichokuwa anataka kusikia kutoka kwa mama yake alichukua simu yake chini ya mto akatafuta namba ya boss wake na kuipiga , simu iliita bila kupokekewa mpaka ikakata
" Hajapokea ukute yupo kwenye kioo anajiangalia .
" Umejuaje Kama saizi anajiangalia kwenye kioo?
" Anapenda kujiangalia kwenye kioo Kama mtoto wa kike.
" Wewe mdomo huo utakuponza shauri yako uje uropoke akusikie . Mara simu ya mwanaheri ikaanza kuita
" Eheee anapiga Sasa
" Pokea Sasa. Mwanaheri alipokea simu
" Hallow boss habari za asubuhi?
" Salama
" Samahani kwa kukupigia simu asubuhi nilikuwa naomba ruhusa sitaweza kuja kazini naumwa. Tariq alinyamaza kimnya kwa muda Kisha akauliza
" Umeenda hospital?
" Hapana nimeanza kuumwa usiku badae ndio nitaenda hospital
" Sawa ugua pole
" Asante boss nashukuru Sana kwakunipa ruhusa
" Ok ukifika hospital utanijulisha
" Sawa boss. Baada ya kukata simu alimuangalia mama yake
" Kashanikubalia Sasa mama usiwe na wasiwasi nenda kajiandae uwahi kazini.
" Kama unaumwa Sana Basi na Mimi nisiende nibaki kukuuguza
" Hapana mama tumbo tu ndio usiende kazini wewe nenda tu Kama nitazidiwa nitakupigia simu .
" Sawa. Mama yake alipomuacha peke yake alifurahi Sana
" Sasa hapa ndio nitawaonyesha kuwa Mimi ndio mwanaheri mwenye heri zangu sinaga roho ya kichawi na zawadi nimenunua weweeee naona Kama muda hauendi vile .

Hatimae ikifika muda wa ndoa mwanaheri alikuwa bado yupo ndani kwao anajiandaa Mara akasikia kelele hapo nje kwao .
" MKE mwenza tokatoka ukaone mwenzio anavyoenda kupokea Cheti Cha ndoa.
" Mazuzu kweli Hawa wanafikiri Mimi kunguru muoga Sasa ngoja niwaonyeshe . Mwanaheri alitoka akiwa kavalia sare yake ya harusi na kajipodoa mpaka akapodoka . Wenzake walipomuona waliangua kicheko Cha umbea
" Yani bado hamjacheka Naona Kama mmetabasamu tu.
" Haya twende zetu. Mwanaheri alifunga mlango akaongozana na wenzake
Walienda kusheherekea harusi na zawadi alitoa mwanaheri alisheherekea mpaka akasahau Kama alidanganya yeye Ni mgonjwa ilipofika mida ya saa kumi sherehe ilikuwa ndio imenoga watu walicheza singer Kama hawana akili nzuri mmoja wapo akiwa mwanaheri.

Tariq alipiga Sana simu ya mwana hero kwaajili ya kutaka kumjulia hali lakini simu haikupikelewa mwanaheri aliiacha simu ndani kwao. Tariq alipotoka kazini akaamua kwenda kumjulia hali nyumbani kwao alipofika alikuta mlango umefungwa na alipojaribu kumpigia simu iliita ndani , Tariq alipata wasiwasi aliwaza huenda Kuna kitukimempata mwanaheri huko ndani alitaka kumpigia mama yake Mara akatokea Dada mmoja jirani yao akamsalimia na kumwambia
" Wenyewe hawapo
" Mwanaheri kaenda wapi?
" Yupo harusini hapo nyumba ya tatu.
" Ok asante. Tariq aliwaza
" Inamaana kapata nafuu akaenda harusini au alidanganya anaumwa ili aende harusini maana yule akili zake anaziweza mwenyewe . Tariq alienda kupanda gari wakati anaondoka alipofika kwenye nyumba yenye harusi aligeuka kuangalia so ndio akamuona mwanaheri ndani ya sare Tena akiwa bize na kucheza ikabidi apaki gari pembeni akashuka na kumfuata alipofika karibu yake alimshika mkono mwanaheri aliuvuta bila kumuangalia , Tariq aliushikatena mkono wake kwa nguvu
" Wewe vipi? Mwanaheri aliuliza huku akigeuka kumuangalia alishituka kumuona Tariq alitamani kukumbia akashindwa,alitaka kujitetea pia akashindwa wakabaki wanaangaliana Tariq akiwa kakunja uso

 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 9

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Tariq alimvuta wakaenda alipo park gari, watu waliwaangalia huku wakiulizana Nini kinaendelea
" Panda kwenye gari. Walipanda kwenye gari huku mwanaheri alikuwa anatetemeka ,walienda mpaka nyumbani mwanaheri alifungua mlango wakaingia ndani walikaa kwenye Kochi Tariq alimkazia macho mpaka mwanaheri akainamia chini kwa aibu
" Hivi unaumwa kweli wewe? Mwanaheri hakujibu aliendelea kujiinamia
" Naongea na wewe mwanaheri.
" Samahani boss kwakukudanganya Mimi sikuwa naumwa.
' Sasa kwanini udanganye unaumwa na sababu ni Nini?
" Sikiliza Tariq nilikuwa nataka kukuomba ruhusa lakini nikaogopa nikajua hautanikubalia kwasababu Jana nilikukasirisha .
" Ok nipe sababu
" ok nipe sababu ya kukifanya usije kazini ikiwa huna dharula yoyote.
" Ni hivi boss mwanaume wangu wa zamani alikuwa anaowa hivyo ilikuwa lazima nihudhulie harusi yake ili niwafunge mdomo wambea maana nisingeenda hapa mtaani nisingekaa kwa amani . Tariq alitoka tabasamu la mbali Kisha akamuuliza
" Inamaana ulihudhuliwa harusi ya ex wako?
" Ndio lakini nilimkataa ndio maana akaenda kumuowa Esma shoga yangu sijui alijua roho itaniuma .
" Kwahiyo huujaumia hata kidogo?
" Nani Mimi huyo niumie kwangu anaeniletea ujeuri Mimi nakuwa fedhuri ndio maana nikasema sikubali Kama unavyoniona sare nimevaa na zawadi ya Bibi harusi nimenunua nikamkabidhi.
" Mmmh wewe kiboko Ila sijapenda ulivyonidanganya .
" Kwahiyo naomba unisamehe sitarudia Tena pia nakuomba usije ukamsumbua mama
" Kwahiyo nae ulimdanganya? Mwanaheri hakujibu ukimnya wake ukawa Ni jibu kwa Tariq
" Mwana unatakiwa kubadilika wewe sio mtoto tena pia kumbuka haya maisha hayana formula Leo mama yupo kesho hayupo utalian na Nani ikiwa huku nyuma umechezea nafasi ambazo zinaweza zikakutengenezea maisha . Maneno ya Tariq yalimuingia mwanaheri .
" Daaa unavyosema Ni kweli.
" Sasa kuwa makini na hayo unayofanya acha kuchezea sehemu inayokuinguzia kipato hata kama itakuwa Ni mia mbili unatakiwa kuiheshimu .
" Sawa boss nimekuelewa Sana tu.
" Vizuri Kama umenielewa ,vipi kesho utakuja kazini au bado sherehe inaendelea?
" Hapana kesho nakuja .
" Sawa Mimi nilikuja kumuangalia mgonjwa kumbe mgonjwa mwenyewe wa mchongo. Tariq aliondoka mwanaheri alivua Ile sare ya harusi na kujilaza kitandani Kama vile alikuwepo nyumbani .

Siku moja mwanaheri alikuwa anatoka kazini anaelekea nyumbani kwao alishangaa gari linamfuata nyuma kwa mwendo mdogo .
" Huyu dereva Kuna anachokitaka kwani huko kote hajakuona mpaka aje maeneo wanayotemba watu ngoja ajichanganye Sasa napasua vioo vya hicho kigari chake Cha mkopo . Mwanaheri alikazana kutembea Mara Lile gari likaongeza mwendo kidogo likawa saiti yake
" Habari yako mwanaheri! Mwanaheri alipomuangalia alitabasamu
" Kumbe Ni wewe sameer bahati yako maana nilikuwa ninekuandalia bonge la neno.
" Jamani hili neno ningeweza kweli kilimudu?
" Kama moyo wako mwepesi usingeweza kwakweli.
" Njoo Basi upande kwenye gari nikusogeze nyumbani. Mwanaheri hakukataa maana alikuwa bado Sana kufika nyumbani kwao na bado alitakiwa kupanda daladala akaona afadhali kasave nauli yake
Mwanaheri alipanda kwenye gari Sameer alimgeukia na kumuuliza wakaelekea wapi mwanaheri alimuelekeza anapoelekea safari ikaanza, Sameer alikuwa anamuangalia Sana mwanaheri anajifanya Kama hamuoni alipoona anaendelea kumuangalia akamuuliza
" Hivi mtu unaweza kuendesha gari ukiwa unaangalia pembeni ? Sameer alitabasamu
" Kwanini umeniuliza hivyo?
" Nimejisikia tu kukuuliza maana naona kimnya .
" Hamna dereva anatakiwa kuangalia mbele anapoenda
" Ahaaaa Basi dereva anatakiwa kufuata taratibu za barabarani
" Lakini Mimi Ni mzoefu.
" Ninavyojua Mimi vyombo vya Moto huwa havina uzoefu vinahitaji umakini.
" Sawa mrembo . Walipofika nyumbani kwakina mwanaheri , mwanaheri alimshukuru
" Asante Sana .
" Usijali , naomba Kama hutojali unipatie namba yako ya simu ili tuweze kuwasiliana . Mwanaheri alimpatia namba yake na Sameer akampa yake Kisha wakaagana Sameer alifurahi Sana kupata namba ya mwanaheri.

Kesho yake Sameer alimfuata mwanaheri kazini
" Vipi mrembo uko poa?
" Niko poa karibu .
" Asante Ni muda wa lunch huendi kupata lunch?
" Mmmh hapana Mimi siendi
" Kwanini ?
" Huwa siendagi kifupi sijazowea.
" Basi naomba Leo twende wote
" Unataka nikusindikize au?
" Tunaenda kula pamoja .
" Sawa nitakupa kampani . Mwanaheri aliweka vitu vizuri wakaondoka na kwenda restaurant waliagiza chakula wakati wanaendelea kula Tariq na Naina walifika ,Tariq alivyowaona Kama alipata mshituko akasimama na kuwaangalia kwa makini
Tariq alivyowaona alipata Kama mshangao akasimama na kuwaangalia kwa makini Naina nae alisimama akamuuliza
"Vipi mpenzi mbona umesimama ?
" Yule si Sameer? Naina aliwaangalia
"Ni yeye yupo na mwanaheri kwani wanaukaribu ?
" Sijui twende tukakae. Walienda kukaa huku Naina akigeuka kuwaangalia , walikaa kwenye kiti wakisubiria huduma
" Hivi huyu dada umemuajili kwaajili ya kufanya kazi au kuzurura na wanaume ? Naina aliuliza
" Lakini huu Ni muda wa lunch . Muhudumu alifika akawahidumia .

Upande wa Pili mwanaheri na Sameer walikuwa wanaongea na kucheka kile kitendo kilikuwa kinamkera Sana Naina hakupenda kumuona mwanaheri akiwa na furaha pia hakupenda kumuona yupo karibu Sameer

Inapatikana yote kwenye link kwa Bei poa kabisa
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 10

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Sameer alikuwa anamuangalia mwanaheri huku akiwa anaonekana anashauku ya kuongea Jambo , mwanaheri hakujali Sana alimchukulia kawaida maana huwa anamuangalia
" Mwanaheri unajua wewe Ni mwanamke mrembo Sana , mwana une yoyote lijalo anapokuona lazima udenda umtike
" Mmmh wewe Kaka umewaza Nini mpaka ungeniambia maneno hayo?
" Hakuna nipichokiwaza Ila ukweli ndio huo wewe Ni mwanamke mzuri Sana na nikawauda yangu kumpa sifa au kukupa sifa kile kinachostahili kusifiwa huwa siwezi kuficha. Mwanaheri alitabasamu Kisha akasema
" Asante kwakunimwagia sifa .
" Unajua siku ya kwanza tulivyokutana nilitokea kuvutiwa Sana na wewe na nikikumbuka Yale mazingira tuliyokutaniana nahusi Kuna kitu kipo Kati yetu. Mwanaheri alicheka
" Wewe usitake kuniambia unataka kunitongoza saizi.
" Kwani kunatatizo gani Mimi kukutongoza wewe , hebu niangalie kwanza huoni Kama tunapendezana kuwa pamoja?

Kabla mwanaheri hajajibu alikutana macho na Tariq ambae alikuwa anawaangalia mwanaheri alishituka na kumfanya Sameer ageuke kuangalia kule alilokuwa anaangalia mwanaheri, alipomuona Tariq aliachia tabasamu
Kisha akawapungua mkono Tariq na Naina . Alimgeukia mwanaheri akamuuliza
" Vipi unamuogopa boss wako?
" Sameer hapa hapakaliki acha niwahi kazini
" hebu jitulize Tariq Hana shida na wewe kwanza kumbuka upo na Mimi hapa
" Wewe humjui Tariq nikifika kazini ataanza kujisomea lisala zake .
" Kabla hajaanza kujisomea wewe nitakwambia hizo lisala anisomee Mimi maana Mimi ndio sababu ya wewe kuja hapa. Mwanaheri alitulia na kuangalia walipokaawakina Tariq , Naina alikuwa anawangalia Sana huku akimwambia Tariq
" Huyu mwanaheri Wala hafai kuwa secretary wako atakuchafulia jina la ofisi yako
" Kwanini?
" Ona kwa muda mchache aliofahamiana na Sameer kashatoka nae huwezi kujua pengine kashalala nae.
" Hayo Ni Mambo ya mtu binafsi siwezi kuyaingilia . Naina alichukizwa na majibu ya Tariq.
" Kwahiyo unamtetea huyo Malaya . Tariq alikunja uso
" Kwanini unuite mwenzio Malaya na unausibitisho kuwa yeye Ni Malaya ? Naina alinyamaza
" Hebu kula tuondoke mengine hayakuhusu .

Mwanaheri hakukaa kwa Raha alikuwa muoga mpaka Sameer akamwambia
" Naona unamuogopa Sana boss wako.
" Hapana simuogopi namuheshimu Kama boss .
" Ok tunaweza tukaondoka Ila bado nilikuwa Nina mazungumzo na wewe.
" Tutaongea siku nyingine .
" Sawa.

Sameer alienda kulipa bili , mwanaheri aliangalia Tena kwenye meza waliyokaa wakina Naina akakutana na wote wanamuangalia alirudusha macho na kuangalia chini
" Huyu Sameer ameniponza Sasa Kama anajua huu mgahawani ndio anapenda kuja Tariq kwanini akanileta hapa na yule Naina sijui kwanini ananiangalia vibaya vile yule Dada anaroho mbaya sijui hata nimemkosea nini . Sameer alirudi pale walipokuwa wamekaa
" Nyanyuka tuondoke. Mwanaheri alisimama Sameer akavuta kiti
" Twende tukawasalimie
" Mimi nimesha salimiana nao nenda mwenyewe. Sameer alimshika mkono wakaenda mpaka alipokuwa wakina Tariq
" Niambieni wapendanao .
" Safi karibuni tuungane pamoja . Tariq aliwakaribisha
" Asante sisi tumeshamaliza nataka kumuwahisha bibie kazini. Tariq alimuangalia mwanaheri Kisha akaachia tabasamu kwa mbali Naina alikuwa anamuangalia vibaya mwanaheri alitamani waondoke haraka kabla hawajaanza kurumbana .
" Poa Basi tangulieni sisi bado tupo. Waliondoka huku Sameer akiwa kamuwekea mkono begani.

Tariq alipofika kazini alimkuta mwanaheri anaendelea na kazi akampita bila kumsemesha , mwanaheri alipoona kaingia ofisini kwake alishusha pumzi
" Afadhali nilijua atanifokea .

Siku zilizidi kusogea ukaribu wa mwanaheri na Sameer ulizidi . Siku moja ya weekend walitoka pamoja na kwenda kukaa sehemu Sameer akaamua kufungua ya moyoni.
" Mwanaheri unajua unanitesa Sana
" Nakutesa kwa lipi?
" Usinifanyie mtoto mdogo kwani hujagundua nataka Nini kwako?
" Kwani Mimi mfalme njozi mpaka nijue unataka Nini? Sameer aliachia tabasamu
" Acha utani Basi unajua nimetokea kujielewa Sana Yani kifupi nakupenda ,upendo wako Ni mithiri ya matone ya mvua nimeshindwa kutafuta kwa kujibanza nimesimama iniloanishe Mwanaheri aliguna
" Mmmh kwakiyo kuzunguka kote kule Mara umeniletea vizawadi ,kunitia lunch sababu Ni hii kutaka kuja kunitongoza sindio?
" Ni upendo ndio unenisukuma nikufuate nakupenda Sana sipati usingizi mzuri kwaajili yako. Mwanaheri alimuangalia akaanza kucheka
" Kwahiyo unanicheka
" Naijua hiyo Ila hamna shida tunaweza tutaenda sawa.
" Kivipi mbona sijakuelewa. Mwanaheri alikuwa anajua tabia za Sameer watu pale kazini walimpa habari zake
" Hivi Ni kweli umenipenda au umenitamani kwaajili ya kumaliza shida zako.
" Nawezaje kukutumia na kukuacha mwanamke mrembo Kama wewe, nimekupenda toka moyoni niamini kwa hilo
" Sawa nakubaliana na weweila kwa sharti moja. Sameer alikaa tayari kusikiliza Hilo sharti

Ni sharti gani ambalo atapewa na mwanaheri?

Nunua soulmate au mwanaheri upate a boy from London bureeeeeeeeeee
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 11

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Mwanaheri alimuangalia Kisha akaendelea kwakusema
" Sharti langu jepesi Saba ukikubaliana na hili ndio nitajua kweli unamapenzi ya dhati na unania nzuri na Mimi
" Sawa nipe Hilo sharti.
" Sharti langu Ni sitakuwa tayari kukutana kimwili mpaka pale tutakapofunga ndoa . Sameer alimuangalia Kisha akacheka Sana
" Hivi umefikiria Nini mpaka ukanipa Hilo sharti?
" Ni kawaida yangu kutoa ilo sharti kwa kila mwanaume anaetaka tuwe wapenzi.
" Basi sawa kwakuwa nakuhitaji nitafuata sharti lako. Walikubaliana huku kila mmoja akiwa anafikiria kivyake , Sameer alijisemea
" Unajiona mjanja Ila kwangu utanasa tu kwenye mtego wangu hata siku moja sijawahi kushindwa kwenye Mambo ya mapenzi wenzio wananiita asali ya warembo na wewe siku yako Ni moja tu acha nikuvutie Kasi . Mwanaheri nae alikuwa anamfikiria yakwake
" Kama tabia zako ndio zile nilizozisikia hapa umegonga mwamba utafurukuta mwishoe utaachia ngazi Mimi sio Kama hao uliowapitia . Baada ya kila mmoja kufikiria yake waliangaliana na kutabasamu .
Mara kwa Mara Sameer alikuwa anaenda kazini kumchukua mwanaheri na kumrudusha nyumbani kwao pia alijitahidi kumuhudumia na kumpatia kile anachostahiri kupata mpaka baadhi ya wafanyakazi wenzake wakaanza kumsifia
" Shoga mganga wako mkali tuambie ulienda kulogea wapi?
" Kumloga Nani tena
" Tunaona jinsi ulivyomkamata huyo Sameer wenzako waliishia wiki mbili wakaachwa mchana kweupe.
" Hao Ni wao na Mimi Ni mwanaheri mwenye heri zangu Shari zote zinanipitia kando .
" Sawa bwana Ila kabla hizo dawa hazija chuja uwahi uka renew. Baada ya kutaniana na wenzake alienda kuendelea kufanya kazi ,Mara akamuona Naina kasimama mbele yake mwanaheri alimuangalia Kisha akaendelea na kazi zake .
" Hivi wewe hapa umekuja kufanya kazi au umekuja kujinadi huo mwili wako ili wanaume wa watu wakutongize?
" Naina chunga huo mdomo wako usiokuwa na stars hapa nipo kazini .
" Najua upo kazini ndio maana nikaja kukupa ukweli uache kujitongozesha Sameer Ni mwanaume wa mtu atakuchezea akuache .
" kwani nae Ni mwanaume wako wewe au ? Maana nakuona unavyo paparika .
" Sasa endelea na hayo majibu yako ya shombo tutakuonyesha Kama Cha mtu Ni mavi. Mwanaheri aliachia tabasamu Kisha akamwambia
" Kabla haujanionyesha kuwa chamtu mavi nitakuwa nimeshapitia na huyo Tariq ili unionyeshe vizuri. Naina alifyonza akaondoka .
" Naina ,Naina nitakutafuta dozi yako moja tu ambayo itakufanya utulie na kila ukiniona unipishe mbali .
Kitendo Cha Sameer na mwanaheri kuwa wapenzi hakikumpendeza Tariq siku moja alikaana Sameer akamuuliza
" Hivi unampango gani na mwanaheri ?
" Aaah Kaka swali gani Hilo unaniuliza ?
" Sameer nakujua vizuri Sana wewe ni Playboy usije ukamvuruga binti wa watu ukampotezea ramani .
" Sikiliza nikwambie mtu mwenyewe Ni ngumu kamatofali kanipa sharti la kuto kulala nae mpaka tutakapofunga ndoa Sasa ukiniangalia Mimi Ni mtu wakuowa saizi . Tariq alimcheka
"Unacheka Nini Sasa
" Nakucheka wewe kwahiyo kwa mwanaheri umekwama ?
" Najwamaje kirahisi hivyo wakati Mimi ndio kubwa la maaduihapa mpaka kieleweke hakuna mkate ngumu mbele ya chai. Ile kauli ilimfanya Tariq ajisikie vibaya hakutamani kuendeleza Ile mada
Kesho yake alipokuwa ofisini kwake alimuita mwanaheri ofisini kwake mwanaheri alipofika alisimama Tariq akawa bize na kazi
" Boss nimefika
" Nimekuona . mwanaheri valiendekea kusimama akisubiri Tariq amalizie anachokifanya kumbe Tariq hakuwa anafanya kitu Cha maana alikuwa anafikiria aanzue wapi kumkanya kuhusu Sameer Ila hakujua aanzie wapi , mwanaheri alisimama kwa muda huku akimuangalia
"Boss Kama Kuna kazi yakufanya naomba uniambie nimesimama Sana miguu inaniuma . Tariq alimuangalia mwanaheri akaangalia chini
" Sawa unaweza ukaenda.
" Sasa mbona hujaniambia ulichoniitia au nimekosea kukwambia kuwa nimechoka kusimama ?
" Kwahiyo bado unatamani kuendelea kusimama au? Mwanaheri hakujibu aliondoka
" Yani huyu angekuwa sio boss mbona angekoma Leo na hapa nimemstahi tubkwaajili nilimuahidi mama kuwa nitatulia kazini Yani ana bahati Sana .

Tariq alinyanyuka kwenye kiti akaenda kusimama dirishani
" Sasa nimefanya Nini nimeshindwa kuongea nae , natakiwa nimpe tahadhari kuhusu Sameer au atanichukuliaje ataniona ninatabia za kike ? Sitaki kumuona mwanaheri anadumbukia kwenye matatizo . Akiwa anawaza huku anaangalia nje alimuona Sameer akiwa anashuka kwenye gari lake na kuelekea kwenye lango kuu la kuingilia ofisini . Sameer alielekea kwa mwanaheri
" Mambo kichuna wangu .
" Safi karibu . Mwanaheri aliitikia huku akitoa tabasamu Pana
" Asante pole na kazi .
" Asante
" Nimekuleta zawadi . Mwanaheri alipokea mfuko wa zawadi huku akisema
" Jamani hizi zawadi mwaka huu mbona zitanikoma .
" Na kweli zitanikoma maana ndio kwaanza tunaanza hata robo hatujafika . Mwana aliufungua Ile mfuko akakuta gauni zuri
" Waooo nguo nzuri Sana nimeipenda Sana .
" Lazima uipende maana Ni nguo ya Bei ghari nataka uivae siku ya sherehe ya mwaka mpya . ( Kila mwisho wa mwaka kampuni ya kina Tariq huwa wanakodi ukumbi na kukusanyika wafanyakazi wote kwaajili ya kusheherekea)
" Nitapendeza Sana .
" Hicho ndicho ninachokitaka .

Tariq alikaa dakika kumi akisubiri Kama Sameer ataenda ofisini kwake lakini ikawa kimnya akajua lazima atakuwa kwa mwanaheri, alitoka akawakuta wanaongea alisogea mpaka walipo akasalimiana na Sameer Kisha akamuuliza mwanaheri
" Umemaliza kazi niliyokupa?
" Ndio naimalizia
" Ndio unaimalizia au unapiga porojo na huyu jamaa yako . Sameer akadakia
" Lakini nimekuja muda huuhuu
" Sawa lakini ningeomba umuache amalizie hiyo kazi kwanza badae nitakuwa na muda mzuri wa kuongea Mambo yenu.

Jioni wakati mwanaheri anarudi nyumbani alipofika mitaa ya kwao akakutana na wadada wa 4 hapo mtaani walimfusta na kumzunguka
" Nyie nae kulikoni mnanizunguka ? Hawakumjibu walimuangalia kwa dharau Kisha wakaangua kicheko
" Naona menifuata kishari sàna mnataka Nini? Wale wasichana hawakumjibu Mara walitokea Naina na Nice na kwenda kusimama Naina akamwambia nice
" Mtu mwenyewe ndio huyu mshamba mshamba asiejua hata kuoga baada ya kupata mshahara akajiona nayeye ni mwanamke kaanza kuchukua mwabwana za watu . Nice alimkagua juu mpaka chini Kisha akafyonza
" Utakuta kwanini unatembea na Sameer wangu nyie wadada fanyeni kazi yenu.

 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 12

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Wale wadada walianza kumzodoa na kumsuta
" loooh unajifanya unaenda kazini kumbe kazi yako kwenda kuchukua mabwana za watu muone kwanza sura ilivyompauka .alianza kuongea msichana mmoja mwanaheri akawaambia
" Akaaa nyie msifikiri Kama nawaogopa kwa wanaume wa kuvutia mpaka nikawachukua hao mabwana zenu kwanza mbona hamjiamini kama mnajiweza njooni hapa msijitenge huko Kama mafungu ya nyanya mnamatatizo kwanza nawashangaa sijui mnamatatizo gani? Alafu na wewe Pili mwenye mishavu Kama unapuliza Moto wa kuni naomba unyamaze maana yako mengi nayajua nitayasambaza hapa mtaani mpaka ushindwe kwakuweka hiyo sura yako .
" Acha kujifanya unajua wewe Ni Malaya tu mwizi wa wame za watu .
" Ndio nimewaiba mnataka Nini Sasa ?
" Tafuta wako sio kila unapopaona unadandia utakuja kuparamia vibwengo.
Wale wasichana walimchangia kumchamba mwanaheri japo nae hakutaka kushindwa alijibishana nao huku Naina na Nice wakiwa wamekaa pembeni wanacheka , walimfusta na walimnyanganya ule mfuko wa nguo pamoja na kupasuka simu yake . Baada ya hapo Naina akasema
" Kwaleo inatosha atakuwa kajifunza kitu. Aliwalipa hela wale wasichana wakaondoka , mwanaheri aliwasogelea na kuwaambia
"wewe unaejifanya mwanamke wa Sameer kwangu sikumuita alikuja mwenyewe na wewe Naina Ni Kama umenituma nitafanya juu chini nimpate huyo Tariq
" Jaribu uone kitu nitakachomfanya kinyago wewe. Nice alimsogelea akamwambia
" Hiki ulichokiona Ni trela picha unakuja Yani mpaka akili ikukae sawa na mpaka Ile ofisi uione chungu. Naina na Nice walipanda kwenye gari wakaondoka .

Mwanaheri alisimama akaokota simu yake iliyokuwa imevunjika kioo pamoja na pochi ilikuwa imefunguliwa na vitu vyote vilikuwa vimemwagika alivikusanya akaweka kwenye pochi Kisha akaondoka alipofika kwao alilia Sana mama yake akamuuliza
" Unalia Nini?
" Acha tu mama Mimi Ni wakuzalilishwa mtaani kwangu Tena nakuja kusutwa na watu wasioeleweka . Mama mwanaheri alicheka
" Safi Sana nilikwambia achana na mashoga wambea Sasa sijui umeenda kuongea nini mpaka ukasutwa
"Sijaongea chochote Ila yule mwanamke wa Tariq Kuna kitu anakitafuta kwangu na atakipata nasema hawezi kunishusha cheo changu Cha ukamanda lazima nilipize.
" Wewe mtoto umemfanya Nini Naina ?
" Anasema Mimi namchukulia mwanaume wake ona alivyonifanyia kaniharibia simu yangu wakawakodisha na wakina Asha kikojozi , Pili mishavu wanisute mbele za watu.
" Mwanaheri kweli unatembea na Tariq?
" Sijawahi hata kumfikiria yule Kaka . Na nitakuwa mtu wa aina gani niwe na mahusiano na wanaume wawili Tena marafiki.
" Huyo mwingine Ni Nani ?
" Sameer. Mama mwanaheri alimkazia mwanae macho
" Mwanaheri unamahusiano na Sameer?
" Alinitongoza tu ......
" Alafu alivyokutongiza ikawaje?
" Si ndio ikaishia hivyo na Wala sijawahi kumkubali nilikuwa namchunguza tu
" Unamchunguza Nini Kaaa mbali na yule kijana sitaki hata uwe karibu nae ,yule kijana Ni mshenzi ana kila aina ya wanawake hachagui Wala habagui .
" Nalijua Hilo mama nilishaambiwa tokea mwanzo anaanza kunifuatilia .
" Sasa jifanye kunificha utakuja kuumbuka vibaya Tena kwa taarifa tu usije ukaruka huko ukaniletea mimba isiyokuwa na baba na bila kusahau hayo maradhi.
" Mama nae maneno gani unaniambia badala unifariji kwa kilichotokea ndio kwanza unazidi kunichanganya
" Nakufariji kwa lipi na mdomo ndio umekuponza Tena nimefurahi Sana huenda mwanangu ukapunguza umbea . Mwanaheri alinyanyuka na kuingia chumbani

Kesho yake mwanaheri alienda kazini Tariq alipofika alimfuata ofisini kwake
" Habari za asubuhi boss.
" Salama.
" Samahani naweza kuongea na wewe japo kwa dakika chache?
" Ni maongezi marefu Sana?
" Hapana
" Kaa uniambie unachotaka kusema .
" Ni kuhusu Naina wako naomba umkanye na umwambie Mimi Sina mahusiano na wewe huo wivu atafute kwakuupeleka . Tariq alimuangakia huku akiwa kakunja uso na mwanaheri hakukwepesha macho alimuangalia
" Unaongea kitu gani ?
" Inamaana hujui kuwa ugomvi wangu mkubwa na Naina Ni wivu anafikiri Mimi nakutaka Sasa mwambie sijawahi hata kukufikiria na haitatokea Mimi kukupenda Wala kukutana kimapenzi nakuheshimu Kama boss wangu na kile alichokifanya Jana nilimuwekea heshima kwaajili yako.
" Kwani kakufanya Nini? Mwanaheri alitoka simu akaiweka mezani
" Ona walivyoifanya simu yangu. Tariq alichukua na kuiangalia
" Na sio hivyo tu wamenikodishia watu wakanisuta na kunisemea vibaya ,hivi kweli mwanaheri Mimi Ni wakuvuliwa vyeo vyangu mtaani kwangu Mimi hodari wa kusuta Leo nimesutwa Tena kwakukodishiwa watu wenyewe wakina Pili mishavu, afadhali hata huyo Nice kidogo angeongea maana Nina ukaribu na huyo mwanaume wake sio huyu Naina wako anajifanya anawivu wakati hata ukaribu wa hivyo hatuna au nae alikuwa anamta Sameer aliona nafaidi sana
" Basi usijali nenda kaendelee na kazi . Mwanaheri alishangaa Tariq hakuongea kitu ndio kwanza alimwambia akafanye kazi . Mwanaheri aliichukua simu yake kwa hasira Kisha akatoka ofisini kwa Tariq , siku hiyo mwanaheri alishinda kakasirika.
Hata alipoenda kupeleka mafile na vitu vingine ofisini kwa boss wake hakuwa mchangamfu Kama siku zote.

Ilipofika muda wa lunch Sameer alienda kwa Nia ya kumchukua ili watoke pamoja
" Mambo baby
" Afadhali umekuja kabla hasira zangu hazijapoa . Sameer alijua utani akatabasamu
" Leo sitaki kucheka nataka nikwambie kitu kimoja , Mimi na wewe Basi .
" Acha Basi huo utani wako ...
" sitanii nenda kwa huyo nice wako sitaki matatizo na mtu
" haya Ni maswala ya kuyaongea yakaisha Kama nguo na vitu vingine nitanunua
" Ohooo kumbe unajua walichokuja kunifanyia na Ile nguo wakachukua.
" Ndio najua Ila hayo Ni Mambo madogo
" Kwangu Ni makubwa baba ondoka sitaki unininulie chochote . Sameer aliangalia kila upande akaona baadhi ya watu wanawaangalia maana mwanaher alikuwa anaongea kwa sauti .akamsogelea mwanaheri karibu akamwambia
" Unajidanganya mwanaheri huwa sishindwi kirahisi hivyo na sijawahi kukataliwa na mwanamke yoyote Basi nitahakikisha napata kile ninachokihitaji kutoka kwako .
" Utanipata Kama nitakuwa nimelala au Sina ufahamu .
" Tutaona , nakutakia kazi njema . Sameer aliondoka kwa hasira huku baadhi ya wafanyakazi walimuangalia na kucheka kichinichini Tariq pia alikuwa amesijibanza sehemu akasikia kila kitu akawa anatabasamu alifurahishwa Sana na msimamo wa mwanaheri
" Safi Sana mwanaheri Hakuna siku uliyonifurahisha Kama Leo unastahiri zawadi .
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 12

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Tariq aliondoka kwaajili ya kwenda kupata lunch aliporudi alimuita mwanaheri ofisini kwake
" Shika hii.
" Hii Simu ya Nani?
" Simu yako si imeharibika nimekupa hiyo utumie
" Sasa mbona mpya kwahiyo umeenda kuninunulia ?
" Mbona unamaswali mengi au hunashida na Simu?
" Sawa Basi nashukuru nimepata Simu nzuri . Mwanaheri alimuangalia huku anatabasamu Tariq alitoa mfuko akampatia
" Na hii ni gauni utakayovaa kesho kwenye sherehe . mwanaheri alipokuwa na kuangalia nguo ilikuwa nzuri Sana
" Jamani nilikuwa nafikitia nitavaa Nini .
" Basi tumeshamaliza tatizo au Kuna lingine?
" Hapa Kila kitu kipo sawa . Mwanaheri alitoka ofisini kwa Tariq akiwa na furaha .

Kesho yake walitoka kazini mapema kwaajili ya kwenda kujiandaa na sherehe wakati mwanaheri anaagana na wenzake Tariq aliwapita na kwenda kulanda kwenye gari lake aliendesha mpaka nje ya geti akasimama alipomuona mwanaheri anatoka alimpigia honi mwanaheri alisimama na kulisogea karibu
" Unaelekea wapi saizi?
" Naenda kulanda daladala niwahi nyumbani .
" Panda nikupeleke . Mwanaheri alifikiria
" Hapana Kama unasafari zako ungeenda tu .
" Kukupeleka haitaniharibia ratiba zangu . Mwanaheri alipanda kwenye gari
Akampeleka mpaka nyumbani kwao
"Asante boss .
" Ok baadae . Mwanaheri alishuka na kuelekea kwao

Ilipofika jioni mwanaheri aliniandaa na kuelekea shehemu ya sherehe alipofika akakutana na Sameer akiwa anamshuka kwenye gari lake akiwa na Nice , Nice alikuwa kavaa gauni Kama Lile alilokuwa kamnunulia. Mwanaheri hakuwajali alipiga hatua kuelekea kwenye ukumbi uliokuwa umeandaluwa kwaajili ya sherehe kabla haijaingia alisikia anaitwa , alisimama akageuka kumuangalia aliemuita alikuwa ni Nancy mfanyakazi mwenzie
" Waooo umependeza Sana mwana.
" Na uzuri nao unachangia ndio maana watu hawajiamini wanaponiona nipo karibu na wanaume wao wanahisi muda wowote naweza nikawapundua . Mwanaheri aliongea vile makududi baada ya kuona nice na Sameer wapo karibu yao . Sameer alitabasamu nice alitaka asimame aongee kitu ila Sameer alimvuta , kukasirika kwa Nice kulifanya mwanaheri atabasamu pia Nancy alicheka
" Ila wewe kiboko kumbe kuongea vile ulikuwa una maana yako
" Yani wewe acha tu nitawakera mpaka wakome na bado huyo Naina anaejifanya malkia nitahakikisha namfunza adabu .
" Wee kwa Naina acha unajua ukimgusa Naina utakuwa unemchokoza boss ,anampenda sana mpenzi wake
" Asipomkanya Basi nitakula nae sahani moja linapokuja swala la kunidharau huwa sijali na Kama Ni hiyo kazi Bora niache tu.
" Na kweli unayaweza sie wengine waoga
" Mtajua wenyewe na uwoga wenu hebu twende zetu .
Waliingia ukumbini sherehe ikaanza mwanaheri alikuwa amekaa meza moja na wafanyakazi wenzake wanne, watu walikula na kunywa huku wakifurahia huku wakipiga story walisikia Nancy akisema
" Waooo! Kila mtu aligeukia kule alipokuwa anaangalia alikokuwa anaangalia alikuwa ni Tariq pamoja na Naina walikuwa wamependeza Sana watu waliwasifia
" Ila Ni kawaida yake boss kupendeza kila sherehe huwa anakuja kitofauti.
" Ni kweli Ila yule mwanamke wake Mimi ndio anaenichosha anamashauzi sijui ananiona yeye Ni Nani . Mwanaheri akaguna
" Si ananiona mke wa boss ana kila kitu Sasa utambabaisha Nini?
" Ni kweli hatuwezi kujifananisha na mke wa boss. mwanaheri alikuwa anawaangalia huku akiwa anatafakari kitu Mara akashituka aliposikia ananongonezwa sikuoni na Sameer
"Hongera umependeza Sana sikujua Kama Kuna kitu kimejificha ndani yako .
" Nashukuru kwa kutambua urembo wangu lakini hata nice ni mrembo pia hongera kwa kumchagua .
" Achana na Mambo ya Nice kwanza naomba twende pembeni kunajambo nataka tuongee.
" Sameer naomba umuache nenda kaendelee na Mambo yako usiniharibue siku tafadhali . Sameer alitaka kutumia nguvu kumtoa pale mwanaheri alinyanyuka akawa anatoka nje, watu walikuwa wanamuangalia kutokana na umbo lake lilivyokuwa limejichonga na huku nyuma alikuwa majaaliwa mguu ndio usiseme na nguo aliyokuwa ameivaa ilimshika na kuonyesha umbo lake kila alipokuwa anapiga watu waligeuka kumuangalia si wanawake Wala wanaume , alipita sehemu walivyokuwa wamekaa wakina Tariq ,Tariq alipiga na bumbuwazi na kumuangalia bila kukoma, Naina alikasirika hakutegemea Kama mwanaheri angeweza kupendeza kiasi kile mpaka kufanya kila mtu amkodolee macho na alipochanganyikiwa zaidi Ni pale alipomuona Tariq Kama kapagawa flani baada ya kumuona na hakubandua jicho kwa mlimbwende yule
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI. 14

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Mara wakamuona Sameer anatoka nje Naina na Nancy wakaangaliana Kisha Nice akanyanyuka Naina alipotaka kunyanyuka ili amfuate Nice, Tariq alimshika mkono
" Unataka kwenda wapi?
" Namfuata Nice
" Kaa hapo watamaluza wenyewe mambo yao.

Nancy alipotoka nje aliwakuta wamesimama huku Sameer akiwa ameshika mkono mwanaheri
" Hivi unaringa nini ? Kwanza huoni bahati kuwa na mwanaume mzuri na mwenye pesa Kama Mimi wenzako wengi wanaililia hiyo nafasi na wameshindwa kuipata .
" Hebu niachie mkono wangu alafu Mimi kupendana na wewe hiyo Ni ndoto hebu jaribu kujisahau fanya Kama vile hunijui hujawahi kuniona .
" Haitawezekana hata kidogo hata Kama nilisema nakupenda Basi ilikuwa bahati mbaya sijawahi kukupenda
" Ni uongo najua unanipenda najua kilichokuudhi Ni kitendo Cha nice kukufanyia fujo.... Kabla Sameer hajamaliza kuongea nice alifika na kumsukuma mwanaheri mpaka akataka kuanguka .
" Hivi wewe dada unataka nifanye Nini ndio ujue sitaki uwe karibu na mpenzi wangu? Sameer alimuangalia Nice kwa hasira
" Kwahiyo ulikuwa unanifuatilia?
" Unanikosea Sameer Yani Mimi nipo ndani unaniacha na kumfuata huyu Malaya .
" Nisikilize wewe Mimi Sina mpenzi mmoja kwanza nakushangaa unavyonishobokea Kama unaona huwezi kunivumilia unaweza ukasepa sibabaiki na wewe, alafu naomba iwe mwanzo na mwisho kunifuatilia .
Mwanaheri alisimama vizuri na kuanza kumcheka Nice .
" Jamani dunia simama nishuke kumbe hupendwi lakini bado umemganda kama ruba pole Sana kipenzi nilizani ninakazi kubwa ya kupambana na wewe Ila nakuonea huruma kukaa kwenye penzi Kama kivuli na wewe uonekane unamwanaume mzuri . Mwanaheri aliangua kicheko Kisha akaendelea kusema
" Sasa nakuonya utulie Kama vile unanyolewa na kiwembe ukiendelea kuujaribu uvumilivu wangu nitakuonyesha Mimi Ni mtuvwa aina gani maana ninavyowaangalia naona Kama mnanizowea. Mwanaheri alipomaliza kuongea na alimpiga kikumbo Nice Kisha akaenda ukumbini Sameer alikuwa anamsindikiza kwa macho mpaka alipopotea ndipo alipogeuza macho na kumuangalia Nice na kuanza kumcheka
Nice alizidi kupandwa na hasira .
" Unaniangaliaje hivyo ndio ukome kufuatilia Mambo yangu alafu hebu niangalie ki uhalisia Wala huingii kwa mwanaheri kinachokufanya uonekane Ni yako kasura kako kidogo kanamvito na hayo mawigi na vipodozi ndio vinakustiri .
" Wewe Ni wakuniambia hivyo kweli?
" Huo ndio ukweli kwanini nikufiche
" Inatosha Sameer Basi Tena ngoja nikuache na Mambo yako nimechoka kuzalilishwa .
" Daaa itakuwa nafuu kwangu maana uwepo wako unanizibia bahati zangu . Sameer alimuacha Nice akiwa analia Mara Naina alitoka na kumfuata Nice
" Vipi unalia nini?
" Naina ninechoshwa na huyu mwanaume ananidhalilisha amenisema vibaya mbele ya Yule mwanamke wake wa uswahilini hivi kweli Mimi Ni wakudhalilika kila siku kwaajili ya mapenzi?
" Basi usilie ipo siku moja Sameer atatambua umuhimu wako
" Sidhani Sameer hajawahi kunipenda nimelipambania Sana hili penzi lakini nimeshindwa Sameer hajawahi kunipenda ananitumia tu kwashida zake za kimwili, nimemvumilia Sana Sasa inatosha . Nice akilia huku anaongea kwa uchungu Naina alijitahidi kumbembeleza mpaka nice akamnyamaza yakarudi ukumbini kwenda kuendelea na sherehe

Mara kwa Mara Sameer alikuwa anamuangalia mwanaheri na kukaa nae mbali kwaupande wa Tariq ilikuwa hivyohivyo japo kuwa yeye alikuwa anamuangalia kwa mbali jinsi mwanaheri alivyokuwa akifurahia na wenzake Tariq alijikuta akashindwa kuvumilia alinyanyuka na kwenda kwenyemeza walivyokuwa wamekaa wakina mwanaheri .
" Vipi mko poa?
" Tuko poa boss hongera umependeza.
" Ooh Asante na nyie pia nimependeza Sana .
" Ila hatujakufikia wewe. Tariq alitabasamu , Naina alikuwa kanyoosha shingo akimuangalia mpenzi wake .

Tariq akamuuliza mwanaheri
" Vipi unaionaje sherehe maana wewe Ni Mara yako ya kwanza kuhudhulia sherehe zetu.
" Ni nzuri umependeza . Tariq aliachia tabasamu
" Ok karibu Sana
" Asante
" Endeleeni kufurahia . Alipogeuza macho alimuona Naina alivyokuwa anaangalia sehemu alipo ikabidi apite baadhi ya meza na kuwasalimia watu wengine Kisha akarudi kukaa sehemu yake . Ilipofika saa sita kasoro tatu . Alisimama mc na kuwaomba watu wamsikiliz
" Ndugu waalikwa mabibi na mabwana naomba usikivu kidogo. Watu waliitulia kumsikiliza
" Zimebakia dakika tatu tuweze kuingia mwaka mpya nilikuwa naomba wote tunyamaze kinya kwaajiliya kunisubiri mwaka mpya baada ya hapo tutashukuru Mungu kwa kuingia mwaka mpya na kutakiana heri ya mwaka mpya Kisha tutashangilia na kuendelea kusheherekea . Watu wote walifuata maagizo ya mc walinyamaza kimnya ilipofika saa sita kamili kila mmoja alimshukuru Mungu wake kwa kumfikusha mwaka mpya na kutakiana heri ya mwaka mpya , Sameer alimfuata mwanaheri na kumpa mkono
" Heri ya mwaka mpya kipenzi changu. Mwanaheri alimuangalia mkono wa Sameer akaona isiwe tabu nae akampatia wakwake
" Asante nawe pia heri ya mwaka mpya pia nakuombea kwa Mungu katika huu mwaka akubadilishe uweze kuwa kijana mwema na uache tabia zako za ajabu .
" Amin. Aliitikia Sameer huku akiwa anatabasamu
" Lakini umesahau kuniombea kwa Mungu atuwezeshe Mimi na wewe tuwe kitu kimoja .
" Kitu kimoja kivipi?
" Tuwe mke na mume
" Hilo sahau baba Mimi maradhi ya moyo siyawezi hiyo nafasi ungewapa hao ving'ang'anizi.
" Sitaki jibu kutoka kwako nasubiri majibu kutoka kwa Mungu maana kila mwenye kuomba anajibiwa Tena ukizingatia maombe yenye heri Kama haya . Mwanaheri aliuvuta mkono wake na kwenda kutakiana heri ya mwaka na watu wengine
Sameer alimfuata Dada mmoja mfanyakazi mwenzie na mwanaheri wakatakiana heri ya mwaka mpya Kisha wakasogea pembeni walionekana Kama wanateta kitu Kisha wakarudi kuendelea na sherehe , ulipigwa mziki watu wakaenda kucheza Nancy alimlazimisha mwanaheri wakanyanyuka na kwenda kucheza . Yule Dada aliyekuwa anaongea na Sameer hakwenda kucheza kwenye meza yao alibaki peke yake ,alikuwa anawaangalia Sana wenzake alipoona kila mtu Yuko bize kusheherekea alichukua grass yenye kinywaji Cha mwanaheri akaweka kitu Kama unga na kutuangusha vizuri Kisha akaweka juu ya meza Kisha akanyanyuka na kwenda kucheza .

Mwanaheri alipochoka alirudi kwenye meza yao akachukua grass ya kinywaji chake akanywa kinywaji chote pembeni alikuwa alikuwa kasimama Sameer alikuwa aliangalia kinachoendelea
" Safi Sana baada ya dakika kumi utakuwa mikononi mwangu na Leo itakuwa ndio siku yetu.

Kadri dakika zilivyozidi kusogea ndio mwanaheri alizidi kukosa nguvu alikaa kwenye kiti na kujiinamia .yule Dada alimuangalia na kumuuliza
" Mwanaheri unajisikiaje? Mwanaheri hakuweza kumjibu mdomo ulikuwa mzito alimuangalia kwa macho yaliyo legea Kama mtu mwenye usingizi mzito .
" Twende nje ukapunge upepo. Alimsaidia kumnyanyua japo kwa tabu wakatoka nje , wakiwa wanatoka Tariq aliwaona alishituka kumuona mwanaheri yupo kwenye Hali Kama Ile akaamua kuwa fuata kwa nyuma. Yule Dada alienda mpaka sehemu Sameer akatokea na kumsaidia , Tariq alivyomuona Sameer akajua lazima kutakuwa na kitu akajibanza sehemu kuangalia kinachoendelea
" Mtu wako huyu hapa nipe changu . Sameer alitoa kiasi Cha hela na kumpatia Kisha wakaachana Sameer aliondoka na mwanaheri na yule Dada alirudi ukumbini.

Sameer alimchukua mwanaheri mpaka kwenye chumba kimoja Cha hotel huku Tariq akiwa bado anawafuatilia . Sameer alienda kumlaza mwanaheri kitandani wakati anarudi kwenda kufunga mlango akamkuta Tariq kasimama mlangoni
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI. 15

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Sameer alishangaa kumuona Tariq Yuko pale
" Vipi?
" Unataka kufanya Nini Sameer?
" Aaah kwani Nini usichokielewa mwanaheri ni mpenzi wangu.
"Kwanini yupo kwenye Hali hiyo?
" Hali gani huyu kachoka tu.
" Sameer acha Mambo yako ya kihuni Kama mtu hakutaki usilazimishe huoni kumfanyia hivyo Ni kumbaka .
" Sasa nambakaje mpenzi wangu?
" Aisee nisikilize hapa hufanyi chochote
" Tariq wewe Ni wakunifanyia hivi au unamtaka huyu mwanamke?
" Sio namtaka Ila siwezi kuendelea kukuona unazalilisha wanawake na kuanzia Leo nikiona unafanya ujinga nitakuumbua .
" Tariq nakuheshimu naomba utoke .
" Nitaondoka hapa nikiwa na mwanaheri. Sameer alicheka kwa dharau
" Unampeleka wapi?
" Sitaki tupigishane kelele hii Ni sehemu ya watu wastaarabu isitoshe watu wamepumzika ukiendelea kuleta ujinga nitapiga simu polisi.
" Kwahiyo umeamua kunikazia si ndio?
" Ndio .
" Sawa tutaona mwisho wa hili. Sameer aliondoka kwa hasira Tariq alimsogelea mwanaheri Pale kitandani na kuanza kumuita , mwanaheri alikuwa kwenye usingizi mzito alimlaza vizuri na kumfunika Kisha akaenda kukaa pembeni akitafakari amsaidie vipi
Naina alipoona hamuoni Tariq alianza kumtafuta huku akiulizia kwa watu Kama wamemuona ,kila aliemuuliza alimjibu hamjamuona akaamua kumpigia simu , simu ya Tariq iliita bila kupokelewa.
" Huyu atakuwa kaenda wapi na simu hapokei. Naina alirudi kukaa huku alifikiria Mara alikuja Nice na kumuuliza
" Umemuona ?
"Hapana na simu hapokei
" Isije akawa ameondoka na mwanaheri maana nae anauliziwa na wenzake. Naina alihamaki
" Haiwezekani Tariq hawezi kunitelekezea hapa kwaajili ya Yule mjinga asiejua kuoga . Nice alitabasamu
" Anaweza mbona Mimi nimeachwa na Sameer kwaajili yake
" Sameer na Tariq Ni vitu viwili tofauti hivyo usiwafananishe kabisa . Alijibu Naina kwa ukali

Kwakuwa muda ulikuwa umeenda Tariq aliona Bora alale pale hotelini mpaka mwanaheri atakapo amka ,na simu yake ilikuwa inaita kila muda namba tofautitofauti hakuzipokea aliziangalia tu badae akaamua kumpigia Naina
" Tariq mpenzi wangu upo wapi?
" Nimepata dhatula nimetoka hapo Sasa nitamtuma mtu akichukue akurudishe nyumbani .
" Khaaa mbona ghafla Sana na haukuniaga na Ni dharula gani hiyo?
" Naomba tuongee kesho kwasasa siwezi kujieleza. Tariq alipomaliza kuongea alikata simu na kwenda kukaa kwenye Kochi huku akimuangalia mwanaheri.
" Sameer Ni mpuuzi Sana kamzimisha mtoto wa watu ili aje ambake na kesho kutwa Nora ataniambia kwanini kamfanyia mwenzie huu ujinga .

Tariq alilala pale kwenye Kochi lakini hakupata usingizi mzuri mbu walikuwa wakimsumbua pia alikuwa na wasiwasi na Hali ya mwanaheri kila Mara alienda kuangalia Kama anahema na kuangalia mapigo yake ya moyo . Majira ya saa kumi na moja alfajir mwanaheri aliajigeuza huku akiwa anafumbua macho kwa shida aliamka akakaa na kufikicha macho yake alipoangalua vizuri hakujua pale alipo Ni wapi alianza kuangalia kila Kona akamuona Tariq akiwa kalala kwenye Kochi , mwanaheri alishangaa
" Khaaa Tariq anafanya Nini hapa na hapatupo wapi na nimefikafikaje? Alisimama na kuanza kukagua pale chumbani
"Mbona Kama Ni hotelini imekuwaje nipo chumbani na Tariq Mungu wangu mbona sielewi . Alimsogelea Tariq na kumpigam
Piga begani kwa Nia ya kumuamsha Tariq alifumbua macho mwanaheri akashituka ,Tariq alinyanyuka pale kwenye Kochi
" Vipi unajisikiaje?
" Kujusikiaje vipi kwani nilikuwa naumwa ? Na hapa nimefikaje na wewe unafanyanini hapa?
" Mmmm uliza swali moja moja maswali mengi yananichanganya sijui nijibu lipi niache lipi .
" Anza na hili Mimi na wewe tunafanya Nini hapa na umenifanya Nini?
Ilibidi tariq acheke
" Usicheke boss naomba uniambie tumefikafikaje hapa ndani?
" Tumekuja wenyewe unashangaa nini sasa .
" Hapana boss mimi sijaja mwenyewe humu ndani .
"Ulipata shida kidogo ndio maana tupo hapa.
" Shida gani jamani nasaizi ni sangapi?
" Hebu tulia kukikucha nitakupeleka nyumbani kwenu
" Mpaka kukuche tena mimi siwezi kulala nje na nyumbani kwanza sijawahi .
" Leo ndio umelala maana saiz kumeshakucha tunasubiri tu kupambazuke.
" Jamani nitaenda kumwambia nini mama.
" Hebu jitulize mimi nitajua chakwenda kumjibu
" utamjubu jibu gani?
" Nimekwambia niachie mimi. Mwanaheri alienda kukaa kitandani na tariq alirudi kukaa kwenye kochi ,tariq alikuwa anamuagalia mwanaheri kwa kuibia huku mwanaheri alikuwa na mawazo bado alikuwa anajiuliza kimempata kipi mpaka akawa pale.
" Mungu wangu itakuwa kuna kitu nimefanya mpaka hili likatokea sijui nimefanya kitu gani cha ajabu isije ikawa nimetimiza kile nilichomuahidi Naina kuwa nitamchukua mwanaume wake Sasa Kama ndio hivyo huyu Tariq nitakuwa nimemshawishi vipi ?
Pia kwa upande wa tariq akikuwa anafikiria yake .
" Kumbe akitulia ni binti mmoja nzuri sana maskini ningechekewa kidogo Sameer angemfanya kitu kibaya afadhali nilimuwahi .
" Tariq naomba kitu kimoja ukifika kwa mama usimwambie kilichotokea . Tariq alimshangaa
" Wewe mbona unawasiwasi kwani unahisi kimetokea nini Kati yetu?
" Mimi sijui mama yangu hapwndi tabia mbaya .
" Hebu nisikilize wewe Ni mtu mzima Kama ningekuwa nimekufanya kitu chochote lazima ungejua na kuhusu Hali iliyokukuta utajua badae.
" Sawa Ila mama asijue Kama tumekala chumba kimoja . Tariq hakumjibu kitu alitegemea kwenye Kochi usingizi ukampitia baada ya muda mchache mwanaheri nae alilala walikuja kushituka baada ya mlango wao kugongwa. Tariq alienda kufungua mlango akakutana na muhudumu wakasalimiana
" Samahani nimekuja kufanya usafi . Tariq aliangalia saa yake ya mkononi ilikuwa unaelekea saa tano .
" Sawa usijali tunatoka Sasa hivi naomba dakika chache .
" Sawa boss. Tariq alirudi chumbani akamuamsha mwanaheri wakatoka mwanaheri alionekana kuchoka .
" Vipi mbona umelegea hivyo?
" Sijui hata sijielewi nahisi Kama kufakufa hivi. Tariq alishituka alijua pengine madawa aliyowekewa Jana yaneaza kumdhuru
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI. 16

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Tariq alimshika na kumuuliza
' vipi kwani unajisikiaje?
" Nasikia njaa Sana mpaka nahisi kutetemeka . Mwanaheri aliongea kwa sauti iliyojaa madeko, Tariq alimuangalia maana Ile sauti ilikuwa imemvuruga
" Sasa mbona unaniangalia tu Basi nisaidie nikakae kwanza pale chini ya mtu huenda nikapata nafuu kidogo .
" twende mgahawani ukale. Waliingia kwenye mgahawa wacile hotel wakaagizia chakula wakaanza kula mwanaheri hakujivunga alikula kwa kujiachia, Tariq alikuwa anamuangalia huku akiachia tabasamu
" Mbona huku unaniangalia au wewe njaa haijakukamata?
" Usijali endelea kula .
" Mwenzio chango langu haluwezi kuvumilia njaa kabisa na huwa sivungagi kwenye misosi Kama hao wanawake zenu wanaoigiza maisha ya uzungu .
" Ni vizuri nimependa huigizi inaonyesha uhalisia wako Safi Sana .
" Lakini hapa nakula sijui huko nyumbani itakuwaje ?
" Usijali kuhusu Hilo nitaongea na mama yako . Mwanaheri aliacha kula akamuangalia, Tariq akajua anataka kumuuliza maswali yake ya kijinga
" Nini Sasa .....
" Aaaah hebu subiri simu yangu na vitu vyangu vingine viko wapi?
" Kwani ulikuwa una Nini ?
" Nilikuwa na pochi ndogo ndani kulikuwa na hela pamoja na simu.
" Ni hivyo tu au Kuna kingine?
" Vingine vipo lakini havina maana Kama simu na hela
" Kwani hela Ni kiasi gani ?
" Elfu 20.
" Usijali kila kitu kitakuwa sawa
" Nisijali vipi jamani unajua simu yangu naipenda Sana .
" Kila kitu niachie Mimi nitamaliza .

Mama mwanaheri alienda kazini akiwa na wasiwasi kuhusu mwanae
" Mwanaheri atakuja kuniuwa na presha hajarufi nyumbani na kwenye simu hapatikani mbona ananipa mashaka na mtoto mwenyewe Ni mmoja Kama roho. Mara alimsikua Naina anamuuliza mfanyakazi mwingine
" Kwahiyo Tariq hajarudi tangia alivyotoka Jana ?
" Ndio hajarudi.
" Mama yake mwanaheri yupo?
" Ndio yupo jikoni . Mama mwanaheri alishituka aliposikia anauliziwa aliposikia mtu anaelekea jikoni akawa anaendelea na kazi zake, Naina alifika na bila hata salamu alimuuliza
" Jana mwanao alirudi nyumbani?
" Ndio alirudi mapema tu.
Naina alisimama anafikiria Kisha akaondoka
" Inaweze mwanaheri akawa yupo na Tariq? Mama mwanaheri alijiuliza
" Hapana siwezi kusubiri alichukua simu yake na kumpigia Tariq , Tariq alipokea wakasalimiana
" Samahani Jana ukiniona mwanaheri huko kwenye sherehe maana hakurudi nyumbani .
" Nipo nae hapa .
" Uko nae wapi?
" Alipata matatizo kidogo Ila kwa Sasa yupo sawa muda si mrefu nitampekeja nyumbani nampeleka nyumbani.
" Alipata tatizo gani naomba uniambie.
" Usiogope yupo sawa . Walipokuwa wanaongea mwanaheri alijua Ni mama yake akawa anasikiliza kwa makini na walipomaliza kuongea na simu akamuuliza
" Itakuwa mama yangu anawasiwasi Sana naenda nyumbani.
" Nimemwambia uko sawa malizia chakula chako.

Walipomaliza kula walienda mpaka nyumbani kwakina mwanaheri, mwanaheri alichukua funguo kwa jirani yao wakaingia ndani , baada ya dakika Kama 20 mama mwanaheri alifika .
" Mama mbona umerudi mapema unatatizo? Mwanaheri alimuuliza mama yake
" Nimeshindwa kukaa kwa amani ulipatwa na Nini? mwanaheri alimuangalia Tariq . Tariki akajibu
" Mwanaheri alitumia kinywaji kilichokuwa na dawa za usingizi. Mwanaheri na mama yake walishituka
" Kivipi Yani na imekuwaje kiwe na dawa za usingizi?
" Nahisi Kuna mtu aliweka kimakosa lakini Jambo la kushukuru Hakuna kibaya kilichokukuta. Mwanaheri alitamani kuendelea kuuliza maswali Ila akaona anaweza akaharibu .
" Sawa nashukuru kwa kumsaidia mwanangu .
" Usijali hata hivyo naomba niwaache .
" Sawa karibu tena .

Tariq alipoondoka mama mwanaheri alimgeukia mwanae
" Wewe unajua siwaamini kabisa na huyo Tariq hebu niambie ukweli Nini kinaendelea Kati yenu .
" Sasa mama unahisi Nini kinaendelea Tariq Ni boss wangu na Kama alivyokwambia alinisaidia .
" Sasa alipokusaidia alikupeleka wapi?
" Hospital nilipoamka nilijikuta nipo hospital.
" Mmmh kuwa makini maana huyo mwanamke wake anahaha uko na akijua ulikuwa na Tariq sijui itakuwaje
" Huyo Naina Wala hata simuogopi .

Siku ya jumatatu walipokuwa kazini mwanaheri alimfuata Tariq ofisini kwake
" Samahani Sana boss unaweza ukanipa maelezo yaliyojitosheleza kuhusiana na hayo madawa ya usingizi na Ni Nani aliniwekea hayo madawa?
" Kumbe hii Jada haikuisha siku Ile?
" Itaishaje ikiwa Hakuna la maana uliloniambia au Ni wewe ndio ulieniwekea hayo madawa . Tariq alionekana kukasirushwa na maneno ya mwanaheri alisimama na kunisogelea pale aliposimama
" Sikujua kana huna shukrani kiasi hiki .
" Shukrani gani unafikiri kuwa boss ndio unaweza kufanya kile unachojisikia . Tariq alimshika kwenye kidevu na kumbana kwa nguvu huku akiwa kangata meno
" Hivi unanichukuliaje? Au unaniona ninatamaa za kipumbavu Sasa kaa hapo utaujua ukweli . Tariq alimuachia na kwenda kukaa kwenye kiti chake akachukua simu na kupiga akasikika akisema
" Njoo haraka ofisini kwangu . Baada ya dakika chache Lina aliingia ofisini kwa Tariq akamkuta mwanaheri kasimama .
" Ndio boss.
" Hebu muekeze mwanaheri ulichonifanyia siku Ile ya sherehe. Lina alishituka
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 17

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Huku akiwa amemtolea macho boss wake
" Usiniangalie Mimi muekeze mwenzio ulichonifanyia maana Mimi niliona kila kitu. Lina alimuangalia mwanaheri
" Unaniangalia Nini so uniambie Sasa ulinifanyia Nini maana hapa nilipo sijielewi kwanza sijui hata vitu vyangu viko wapi.
" Vitu vyako alivyo Nancy
" Nasubiri umwambie Nina kazi nyingi za kufanya .
" Samahani mwanaheri naomba unisamehe Sana nilishawisgiwa na hela .
" Sasa nakusamehe vipi wakati silijui kosa lako.
" Sameer alinipa dawa nikuwekee kwenye kinywaji chako .....
" Eeeee unasema Nini Lina?
" Nisamehe Ni shetani alinipitia
" Shetani gani huyo wakati wewe ndio huyo shetani sikujua Kama wewe Ni mbaya kiasi hicho kwahiyo ungefurahi baada ya Mimi kubakwa au. Mwanaheri aliongea kwa hasira huku akitaka kumvaa Lina ikabidi Tariq aingilie
" Sitaki mgombane mwanaheri naomba haya yaishe na ulichonifanyia Lina sijakipenda endapo utarudia kufanya ujinga Kama uliofanya nitakufukuza kazi na kufunga nitakufunga
" Naomba unisamehe boss nakuapia sitarudia Tena . Baada ya kusuruhiswa Tariq aliwaruhusu waondoke . Walipofika mlango mwanaheri alirudi.
" Naomba unisamehe boss .
" Tumeshamaliza hayo nenda kaendelee na kazi . Mwanaheri alihisi Tariq kakasirika .
" Unasubiri Nini nenda . Mwanaheri aliondoka
" Yani huyu Lina ababahati amshukuru Sana Tariq Yani nimgemrarua siku nyingine asinifanyie ujinga .
Siku hiyo mwanaheri valikuwa na hasira Sana na Lina Ila alijizuia kutokana na onyo la boss wao. Jioni alipokuwa anarudi nyumbani kwao akakutana na na Pili
" Eheeee afadhali nimekuona Yani hizi hasira zangu nitazimalizia kwako nyamishavu wewe.
" Kwani nimekufanya Nini ?
" Unajifanya unaugonjwa wa kusahau Sasa ngoja nikukumbushe na makofi mawili kwenye hiyo mishavu yako. Mwanaheri aliongea huku akijiandaa kumpiga .Pili alipoona mwanaheri anamaanidha anachokiongea alivua viatu akakimbia
" Unakimbia Nini wewe si hodari wa kusuta unfesimama uone na ukawafikishie salamu zangu hao vibaraka wenzio na hivi viatu navichukua nitaenda hata kuongea . Mwanaheri vakiinama akachukua viatu na kuondoka

Tariq alikuwa bize na Mambo yake hakuwa na maongezi menginevna mwanaheri zaidi ya kazi tu . Siku moja Naina alienda kazini kwao Kama kawaida yake alipitiliza ofisini kwa Tariq
" Baby nimekuja kukupigia tukapate lunch pamoja .
" Leo haitawezekana Kuna kazi natakiwa kuimalizia hapa .
" Tariq mpenzi wangu mbona siku hizi sikuelewi kila ninachokwa mbia lazima uweke kipingamizi .
" Kwahiyo hutaki nifanye kazi kwaajili ya maisha yetu unataka tufuatane Kama kumbikumbu.
" Sijamaanisha hivyo mbona zamani tulikuwa tunatoka pamoja na kazi ulikuwa unafanya
" Zamani na Sasa ni tofauti usiishi kwa kukalili my dear alafu kumbuka natakiwa kutafuta pesa kwaajili ya posa na kuandaa ndoa yetu kwahiyo naomba unipe nafasi ya kupambana hayo Mambo mawili .
" Sawa lakini nifikirie hata weekend moja nimemiss Sana kuwa pamoja na wewe .
" Sawa nitajitahidi . Naina alinyanyuka akamsogekea wakakiss wakaagana Kisha Naina akatoka alipofika mlangoni alimuona mwanaheri anaelekea ofisini kwa Tariq ikabidi Naina asimame kumsubiri . Mwanaheri alipofika karibu alitaka kufungua mlango Naina akamzuia Mwanaheri akamuangalia bila kusema kitu
" Nilikuwa nakufuata imekuwa bahati kukutana hapa
" Ulikuwa unajipya gani?
" Nilikuwa nakupa taarifa jiandae siku yoyote kuanzia Sasa utakuwa huna kazi .
" Unaongea hivyo Kama Nani?
" Heeee unajuzima data hujui naongea Kama Nani?
" Sijajua ndio maana nauliza nimeuliza ili nijue.
" Ok utajua hiyovsiku ikifika .
" Sawa hawara wa boss. Alijibu mwanaheri huku akitaka kuingia ofisini Naina akamsukuma mwanaheri akaanguka kishindo Cha kuanguka kulimfanya Tariq ashituke na kusogea karibu na mlangoni
" Hii Ni trela picha kamili inakuja. Mwanaheri alinyanyuka akakukua mafaili yaliyoanguka
"Siwezi kupigizana kelele na majnuni wote tutaonekana Ni walewale subiri uone kitakachotokea nakwambia Naina nitahakikisha unaumia mara mbili na nihavyoumia Mimi . Naina alicheka Sana
" Mimi na wewe Nani anaepiga kelele au Nani Ni majnuni, hizo dhiki zako zitakutokea puani Mimi sio Nice aliekuachia umchukue bwana ake kirahisi .
" Hata wako naweza kumchukua vilevile.
" Tariq na wewe kinuka mkojo anakupeleka wapi alafu ungejua jinsi anavyokuchukia hataki hata kukuonandio maana soon utatimuliwa hapa . Safari hii mwanaheri alimsukuma Naina kwa hasira , Naina akaanza kulakamika
" Mamaaa unenivunja kiuno . Tariq alifungua mlango akamkuta Naina bado yupo chini na mwanaheri kasimama alimfuata Naina skammsaidia kunyanyuka na kuanza kumfoka
" Mwanaheri umefanya nini?
" Oooh kumbe mkuki kwa nguruwe kimekuuma Sana Mimi kumsukuma huyo nyau wako Mara moja ....
" Nyamaza tambua unaongea na boss wako hivyo kuwa na adabu. Mwanaheri alirudi ofisini kwake
" Nilikuwambua baby huyu sio mtu wa kumuweka hapa ona Sasa alitaka kunivunja mgongo.
" Nawewe usijifanye mwema nimesikia kila kitu na wewe siku zote ndio mkorofi .
" Kwahiyo unamtetea mfanyakazi wako .
" Nadhani unanijua vizur huwa sipendi kutetea ujinga wewe Ni mkosaji na kuanzia leo naomba usikanyage hapa kazini kwangu kuwa mpenzi wangu sio kigezo Cha kutawala na kukufanyia maamuzi kile ninachokimiliki mwanaheri Ni mfanyakazi wangu maamuzi takumfukuza nitafanya Mimi Tena bila ya ushawishi wa mtu yoyote hata akiwa mama yangu mzazi . Naina alibaki kumshangaa
" Naomba uende tutaonana badae. Naina aliondoka akiwa kashika kiunona Tariq alirudi ofisini kwake Mara mwanaheri aliingia
" Vipi Tena kwasasa sitaki mashtaka . Mwanaheri hakumjibu alienda kumuwekea mafaili mezani na barua
" Hiini barua yangu ya kazi nimeamua kuacha kabla hamjafanya maamuzi ya kunifukuza .
" Nimemwambia saa ngapi nakufukuza kazi
" Uliepanganae huo mpango nakutakia kila la heri boss Tariq. Mwanaheri alipiga hatua mbili Tariq akamuita mwanaher alinigeukia
" Haya maamuzi umefanya ukiwa upo sawa au umeongozwa na hasira?
" Nimeshawishiwa na yule mwanamke wako kichaa
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 18

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Mwanaheri akaenda kuchukua vitu vyake akaondoka huku akiwaaga watu kuwa ameacha kazi hatarudi Tena . Tariq alichukua Ile barua aliyoandika mwanaheri kwaajili ya kuacha kazi akaifungua na kuanza kusoma alipomaliza alitabasamu Kisha akaichana na kuitupia kwenye Dustibin.
" Anafikiri nitakubali kirahisi aache kazi , acha kwa leo amalize hasira zake kwanza

Kesho yake asubuhi mama mwanaheri aliamka na kwenda kumuamsha mwanae
" Wewe mbona huamki leo huendi kazini?
" ndio siendi .
" Sababu ya kutokwenda Ni nini?
" Nimeacha kazi . Mama mwanaheri alivuta shuka akaliweka pembeni
" Hebu nyanyuka mpumbavu wewe umeshaanza kunikoroga umeachaje kazi?
" Ndio hivyo mama nimeacha unataka nikujibuje Tena .
" Mwanangu mbona unapenda kunitesa nilijua umebadilika akili imekuwa kumbe bado hivi aliekuloga wewe Ni Nani niende nikamuombe akuopoe .
" Mama Mimi sijarogwa Wala kupigwa hasadi na mtu yoyote Ila tabia ya kunyanyapaliwa na kusema vibaya kisa umasikini wetu Mimi siwezi .
" Nani anaekusema vibaya mbona Tariq Hana tabia ya kumnyanyapaa mtu wewe ndio utakuwa mkorofi wewe Ni damu yangu nakujua bwana .
" Nisikilize mama unajua Naina amekuwa akininyima Sana amani kisa huyo Tariq kila akija kazini ananitukana Mara anisukume alafu huyo mwanaume wake ndio anajifanya anamuonea uchungu Sana mwanamke wake anakuja kunigombeza Mimi niliejitahidi kuushona mdomo wangu na kuzuia hasira zangu .
" Kwahiyo ndio akakufukuza kazi
" Hajanifukuza nimeandika barua ya kuacha kazi .
" Loooh Sasa tutaishije kwa Hali hii na Ile mipango tuliopanga ya kufungua biashara itakamilika kweli?
" Tutaishi Kama zamani mpaka nitakapopata kazi nyingine, na mipango yetu iko palepale .

Baada ya kupita siku mbili Tariq alienda nyumbani kwakina mwanaheri akamkuta yupo nje anaandaa chakula Cha jioni, Tariq alisimama na kumsalimia .
" Vipi mama yupo?
" Yupo ndani .
" Nahitaji kuonana nae.
" Ingia ndani . Tariq alipiga hodi akakaribishwa mama mwanaheri alitoka na kumkaribisha wakaingia ndani.
" Samahani kwa kuja bila taarifa .
" Bila samahani karibu Sana .
" Asante nimekuja kuongee na wewe kuhusu swala la mwanaheri . Mama mwanaheri alikaa vizuri kusikiliza anachotaka kuambiwa.
" Mwanaheri aliandika barua ya kuacha kazi lakini sijaikubali bado namuhitaji kazini .
" Asante Mungu nashukuru Sana hili swala lilikuwa linaniumiza sana akili yangu . Nitashukuru Sana Kama umeamua kumrudusha kazini .
" Sasa tatizo litakuwa kwa mwanaheri nikiongea nae hatakubali naomba uongee nae akikubali nitaomba kesho nionane nae tuweze kuweka mambo sawa .
" Usijali kuhusu Hilo kila kitu kitakuwa sawa sitaki azurule mtaani atarudi kazini atake asitake .
" Sawa yangu Ni hayo tu.
Walimaliza maongezi wakaagana, Tariq alipotoka nje alimuaga mwanaheri Kisha akaondoka na mwanaheri akarudi ndani
" Huyo mtoto wa boss wako alifuata Nini hapa kwetu?
" Kwani yeye kuja hapa Ni dhambi kwanza hebu kaa tuongee Mambo ya maana . Mwanaheri alikaa
" Mmmh niambie .
" Tariq anataka urudi kazini
" Nikafanye Nini na barua ya kuacha kazi nimempa
" Hivi wewe unaakili kweli Yani boss anakuja kukuomba urudi kazini unaleta ujinga wako kwanza umewahi kuona wapi boss akaenda kumbembeleza mfanyakazi ambae hata kusoma hajasoma kwani unafikiri hajaona wakuwapa hiyo kazi
" Kazi za kusumbuana akili siziwezi.
" Nakwambia utaziweza usiniletee ujinga huwezi kunitegemea Mimi kwa kila kitu kwanza tunakoendea Mimi nitachoka nitakuwa nikutegemee wewe Sasa bila kazi utanileaje au ndio utaniacha nife na njaa. Kwanza humuoni yule Amina anavyojituma kwanini usiige mfano kutoka kwake . Mama mwanaheri aliongea Sana na binti yake mpaka akamuelewa
" Sawa mama nitarudi kazini Ila Tariq amkanye Naina maana tunakoendekea nitakuja kumtoa ngeu nimemvumilia Sana Sasa naenda kuchoka
" Sasa hayo utaenda kuongea nae hiyo kesho mtakapoenda kuonana .
" Kuonana wapi Sasa?
" Atakupigia simu atamwambia mkaonane wapi.

Baada ya mama mwanaheri kuongea na binti yake alimpigia simu Tariq na kumpa mrejesho kuwa kila kitu kipo sawa . Kwa upande wa Tariq alijikuta anafurahia Sana maana kwa muda wa siku chache ambao mwanaheri alikuwa haujaenda kazini alikuwa anahisi Kama Kuna kitu kimepungua

Ilipofika majira ya saa tano usiku Tariq alimpigia simu mwanaheri
" Mmmh huyu Tariq anataka Nini saizi? Alijiuliza mwanaheri kabla ya kupokea Kisha akapokea Ile simu
" Hallow
" Hallow habari .ilikuwa ni sauti nzito ya Tariq iliyopenya masikioni kwa mwanaheri na kufanya ahamishie simu sikio la Pili na kuuliza
" Ni wewe Tariq?
" Yah Ni Mimi kwani ulifuta namba zangu?
" hapana ninazo Ila sauti Kama ipo tofauti
" Hahaha mbona sauti yangu ni ileile ya kila siku . Sauti ya Tariq ilikuwa Kama wimbo mzuri unaombembeleza
" Mmmh niambie boss.
" Mmmh kwa muda huu niite Tariq.
" Kwanini wakati wewe Ni boss wangu?
" Basi Kama hutaki kuniita boss niite jina lolote unalojiskia kuniita . Mwanaheri akacheka kidogo
" Basi mume wa Naina.
" Mmmh sawa achaniongee shida iliyonifanya nikupigie simu .
" Nakusikiliza
" Naomba kesho majira ya saa kumi tukutane comfort.
" Sawa .
" Ok uwe na usiku mwema .
" Nawe pia . Baada ya kukata simu Tariq aliweka simu pembeni na kulala akiwa anaangalia juu.
" Aisee hii mbona shuhuri Sasa Yani nimeshindwa kabisa kuwa mbali nae kutokumuona siku mbili tu ni Kama mwezi , sijui kwanini ametokea kunivutia hivi nimetokea kumpenda Sana na sitaki kumpoteza mwanaheri wewe Ni wangu kwa garama yoyote nitahakikisha na yeye unanipenda
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI. 19

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Kesho yake mwanaheri alijiandaa na kuelekea comfort,alipokuwa njiani alikuwa anawasiliana na Tariq , Tariq alimwambia alifika aagize chochote yeye atachekewa kidogo . Mwanaheri alikuwa wakwanza kufika aliagizia kinywaji na chakula akaendelea kula .

Baada ya kakika 25 Tariq alifika na kwenda kukaa alipokaa mwanaheri
" Pole kwa kukuweka
" Wala usijali mwenyewe nakula zangu Wala sipo boadi kabisa .
" Nimefurahi kusikia hivyo . Muhudumu alifika na kumuhudumia Tariq , waliendelea kula huku wakiongea
" Kwanza nitangulize samahani kwa kile kilichotokea siku Ile Kati yako wewe na Naina , pia naomba unisamehe kwa kumuongelesha kwa ukali
" Kwakuwa umelitambua kosa lako nimekusamehe .
" Nashukuru. Pia nilikuwa naomba urudi kazini .
" Nitarudi Ila narudi kwaajili ya mama yangu na usingekuwa mama yangu Wala nisingerudi na hapa nisingekuja alafu nikwambie kitu kimoja kwa Sasa sitakuwa na uvumilivu juu ya huyo Naina akiniletea ujinga nampasua Sasa hivi sitaki kucheka na nyani kabisa . Tariq alitabasamu
" Sawa nimekuelewa miss Mambo Kama hayo sidhani Kama yatajitokeza kwasababu nimeshaongea na Naina na nimempiga marufuku asije pale kazini
" Hapo umefanya la maana Sana . Kimnya kilitawala huku wakiendelea kula Tariq akaamua kuvunja ukimnya kwa kuuliza
" Hivi kwanini huwa mnagombana na Naina ?
" Mmmh hujawahi kumuuliza sababu ya yeye kunichukua?
" Nimekuuliza Ila kwasasa nataka kujua kutoka kwako
" Kikubwa nilichokigundua kwa Naina Ni mtu ambae hajiaminipia anatawaliwa Sana na wivunahisi kila mwanamke ambae atakuwa na ukaribu na wewe anajenga nae uadui au ulishawahi kumsaliti?
" Hata siku moja sijawahi kumsaliti.
" Basi anawivu mbaya Mimi na yeye tulianza uadui tangu siku ya kwanza tunaonana.
" Da pole
" Pole yake yeye ambae anataka kuujua undani wangu siku nikiamua akiniona atatafuta kwakujificha maana nimempa heshima Sana Tena kwaajili yako .

Kwa muda waliyokaa Tariq aligundua mwanaheri ni mtu mwenye busara Sana, mvumilivu tofauti na Naina,akazidi kuvutiwa nae .

Kesho yake mwanaheri alirudi kazini wafanyakazi wenzake wakaanza kumcheka
" Mwanaheri wewe kiboko Yani umeondoka kwa mbwembwe watu tukajua kweli hurudi. Mmoja akadakia
" Kwahiyo na nyie miamuamini kabisa
" Nashangaa naachaje kuacha kazi nitaishije hapa mjini waliojua kweli pole yao ndio nimerudi hivyo. Mwanaheri akaenda ofisini kwa Tariq akaweka vitu vizuri wakati anataka kutoka Tariq aliingia .
" Habari za asubuhi
" Salama boss karibu
" Asante na wewe karibu tena kazini .
" Nimesha karibia . Tariq alisogea mezani akaangalia Kisha akamtania
" Leo hujamwaga maji mezani
Mwanaheri alicheka
" Hahaha Mambo hayo Sasa hivi hayapo nipo makini na kazi zangu.
" Ok naomba unihudumie kahawa.
" Sawa unaonaje nikiweka sukari ?
" Nitakuja kukunywesha mpaka iishe. Wote walicheka mwanaheri akatoka kwenda kumuandalia kahawa.
Kuanzia siku hiyo walikuwa karibu na Kuna wakati walienda lunch pamoja pia siku za weekend Tariq alikuwa anaenda kumtembelea mwanaheri ukaribu wao ulifanya Tariq na Naina wasiwe na mawasiliano mazuri, Naina kila alipotaka kuonana na Tariq , Tariq alimwambia Yuko bize na kumpiga kalenda kuwa wataonaba siku nyingine . Siku moja Tariq alimfuata mwanaheri akamwambia
" Leo naomba tukifika kazini tupitie sehemu .
" Umeanza unataka kunizurulisha
" Kwani hutaki kuongozana na mr handsome ?
" Hapana sitaki naogopa kupigwa na Naina
" Umeshaanza kuzingua
" Usijali boss Tariq tutaenda pamoja .
" Safi Mambo si hayo bwana .

Jioni waliondoka pamoja wakaenda kukaa ufukweni mwa bahari wakipunga upepo huku wakitelemshia na maji ya dafu mwanaheri alikuwa anakula ice cream, Tariq alikuwa anamuangalia Sana mwanaheri usoni akashindwa kujizuia akajikuta alinyoosha mkono wake na kuzilaza nywele za mwanaheri zilizokuwa zinapeperuka kwaajili ya upepo mwanaheri aligeuka akamuangalia wakawa wote wanaangaliana macho ya Tariq yalikuwa yanaanisha kitu mwanaheri akainamisha macho yake kwa aibu
" Mwanaheri naomba uniruhusu niwe wako nakupenda . Mwanaheri alishituka hakutegemea Kama Tariq angemtamkia maneno Kama yale.
" Boss hivi unanielewa hicho ulichokiongea?
" Ndio hili nililoliongea sio bahati mbaya limetoka moyoni
" Hiyo tabia ya kunipenda imeanza lini na huyo mwanamke wako akijua si ndio atanitunia majambazi waje kuniuwa .
" Hakuna kitakachokupata ukiwa na Mimi na usijali kuhusu Naina najua jinsi ya kumalizana nae.
" Utamalizana nae vipi wakati umemvalisha Pete
" Kumbuka niliyomvalisha Ni Pete tu na uchumba huwa unavunjika
" Jamani kumbe Naina alikuwa sawa kuwa na wivu.
" Usinifikirie vibaya Ni mapenzi yangu ya kweli ndio yamenisukuma nikufuate .
" Unajua nashindwa hata nikujibu Nini unanivuruga tu hapa .
" Siwezi kukulazimisha ukubali ombi langu kwa Sasa nenda kafikirie.
" Sawa Ila huu Ni mtihani wa chuo kikuu unampa mwanafunzi wa darasa la Saba .
" Nina Imani utafauru mpenzi .
" Hahahaha umeshaanza kuniita na mpenzi kweli wewe boss Ni kung'ang'anizi
 
MWANAHERI BINTI WA KIJAKAZI 20

MTUNZI SMILE SHINE

WHATSAPP:0688156169

Usiku kila mmoja alimuwaza mwenzake mwanaheri alikuwa anayafikiria maneno alivyoambiwa na Tariq na Tariq nae alikuwa anafikiria afanye Nini ili kumuaminisha mwanaheri kuwa anampenda . Baada ya siku chache wakajikuta wanaingia kwenye penzi zito lakini mwanaheri hakupenda watu walipokuwa kazini ilikuwa ni mfanyakazi na boss wake na walipofika kazini walikuwa wapenzi , Tariq alitaka kumuonyesha mwanaheri kuwa ananianjema na yeye alianza kubadilisha mazingira ya nyumbani kwao aliwahamisha kutoka uswahilini na kwenda kukaa sehemu yenye muonekano na nyumba nzuri pia alimuongezea pesa kwaajili ya kufungua biashara ,haya yote Tariq hakuyafanya waziwazi aliyafanya kupitia mwanaheri. Mama mwanaheri alishangaa kwa mwanae kufanya Mambo makubwa kwa muda mfupi lakini mwanaheri alimtoa hofu na kumwambia
" Mama unanijua mwanao sinaga Mambo ya kijinga haya yote nafanya kwa pesa yangu .
" Sawa sijakataa Ila naona Kama ghafla Sana
" Nilikuwa nahifadhi pesa pia Sasa hivi napata marupurupu na mshahara nimeongezewa .
" Hongera Sana mwanangu hivi ndivyo nilivyokuwa nataka .
"Sasa kuanzia kesho kutwa hakuna kwenda kazini ujiandae na kuuza duka.
" Kweli Mungu mkubwa hivi Ni kweli mwanaheri wangu ndio unafanya haya yote natoka kuwa kijakazi mpaka kuuza duka .
" Mama maombi yetu Mungu ameyasikia na kila anaemuomba huwa anampa na sisi tumepewa . Mama mwanaheri alifurahi na kumkumbatia mwanae

Baada ya siku chache mwanaheri alikamilisha kila kitu Cha dukani wakafungua duka kubwa la urembo mama yake ndio alikuwa analisimamia yeye aliendelea na kazi .

Siku moja Naina alienda kazini kwa Tariq
" Vipi mbona umekuja bila taarifa?
" Kuna kipi Cha ajabu ambacho sitakiwi kuiona au kukijua.
" Hakuna kitu ambacho hutakiwi kukijua Ila inaonekana una mashaka
" Mashaka ninayo Tena Sana tu kwasababu hueleweki siku hizi mapenzi yako kwangu yako wapi Tariq ?
" Naina huu no muda wa kazi hayo Mambo mengine tutaongea badae .
" Sasa hivi Ni saa sita na nusu naomba twende lunch pamoja tukaliongee hili swala .
" Sawa acha nimalizie hii kazi tutatoka . Mara mwanaheri aliingia akiwa na tabasamu alipomuona Naina tabasamu likapotea akageuza akataka kutoka Tariq akamuita
" Mwanaheri mbona unarudi?
" Malizana na mgeni wako . Naina akadakia
" Nani mgeni hapa?
" Sijaongea na wewe naongea na boss wangu upo dada .
" Tariki hivi huyu kichefuchefu wako utamuondoa lini hapa ? mwanaheri hakutaka kujibishana na Naina alitoka .
"Sijui kwanini Unamuendekeza huyu mtu ipo siku utakuta nimefanya kitu kibaya . Tariq alikasirika akasimama
" Naina inatosha sitaki Wala sipendi umuongelee vibaya mwanaheri. Naina alisimama
"Kwahiyo yeye Ni Bora kuliko Mimi?
" Yawezekana maana wewe hujui wapi kwakuongea ujinga wako kwa taarifa yako mwanaheri Ni mwanamke anaejielewa kuliko wewe .
" Unamtetea Ni mwanamke wako?
" Vyovyote utakavyohusi ni sawa siwezi kupingana na hisia zako . Naina alitoka kwa hasira akamfuata mwanaheri na kuanza kumfanyia fujo
" Leo nakukomesha Malaya mkubwa unajifanya umekuja kufanya kazi kumbe umekuja kujiuza. Matusi ya Naina yalimchosha mwanaheri akaamua kujibu hatimae walishikana na kuanza kupigana watu walikusanyika kuja kuamua lakini bado walirushiana maneno kwa zile kelele ikabidi Tariq atoke ofisini kwake alienda kuamua ugomvi Naina hakutaka kunyamaza ikabidi Tariq awe mkali
" Kwahiyo unanifokea unamtetea huyo kahaba wako?
" Ndio yeye Ni kahaba na Mimi ndio mwanaume pekee ninae mnunua unataka Nini Sasa.
" Tariq!
" Nini sI umetaka kuujua ukweli Sasa nakwambia na kutangaza kwa kila mtu kuwa mwanaheri ndio mwanamke ninae mpenda na ndio mwanamke pekee anaenijulia na yeye ndio mke nitakae funganae ndoa. Kila mtu alimuangalia mwanaheri, mwanaheri aliinama kwa aibu Tariq alimsogelea akamkumbatia na kumbusu kwenye paji la uso .Kama ujuavyo kwenye wengi hapakosi wapambe , wapambe walishangilia na kupiga makofi wengine walipiga miruzi Naina aliondoka huku akiwa analia , Tariq alimchukua mwanaheri wakaenda ofisini kwa Tariq.

Baada ya Hilo tukio kutokea kila mtu alijua mahusiano ya wawili hao ,Tariq aliwaeleza wazazi wake kuhusu kuvunjika kwa uchumba wake na Naina na kutaka kutangaza ndoa na mwanaheri wazazi wake hawakuwa na kipingamizi kwasababu yeye ndio muowaji na ndio atakaeishi na huyo mwanamke.

Mama mwanaheri alivyoambiwa hizo habari alishituka
" Mwanaheri mwanangu umevunja uhusiano wa watu.
" Wameachana wenyewe kwa mapenzi yao Mimi sihusiki alafu mama kila tunalolipanga sisi binadamu sio lazima litimie mipango minime tumuachie Mungu Tariq alikuwa ni haki yangu kwa Sasa japo ya mbele siyajui.
" Uliyosema Ni ukweli mtupu mwanangu .

Sameer alipopata taarifa za Tariq na mwanaheri kutaka kufunga ndoa akimtafuta Tariq
" Kaka naomba tusameheane na yote yaliyotokea sikujua Kama unampenda mwanaheri.
" Usijali damu yangu hata Mimi sikuwa nakuelewa Kama nampenda Ila ndio hivyo imeshakuwa anaenda kuwa wife .
" Daaaa kweli kisicho rizki hakiliki naomba uniombee msamaha kwa Shem.
" Usijali . Taratibu zote zilikamilika hatimae siku ya ndoa ikafika Tariq na mwanaheri wakafungua ndoa ya baraka na kwenda kuanza maisha mapya ya ndoa .

"""""""MWISHO"""""
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom