Simulizi ya kweli: Binti aliyepewa mimba na Nabii

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,463
21,945
Utangulizi

Binti aliyepewa mimba na Nabii ni story ya kweli kabisa, mhanga kaniomba nisambaze ili mabinti wengine wajifunze, karibuni nyote.

Anaanza kwa kusimulia.

PART 1

Nimelelewa kwenye familia ya kitajiri, Baba yangu na Mama yangu ni watu wenye uwezo tu. Sikuwa na maisha ya shida hata kidogo.

Namshukuru Mungu nimesoma vizuri na nimepata kazi nzuri tu ninafanya. Wazazi wangu hawakuwa watu wa kusali sali walikuwa watu wa starehe sana Baba ni mlevi na Mama ndio usiseme. Yani wao ni pombe pombe na wao.

Kuna kipindi Baba yangu aliumwa sana alipata tatizo la moyo. Wakati huo alikuwa hawezi hata kutembea na ana hema hema ovyo muda wote, akaja Mama mmoja rafiki yake Mama akamwambia Mama wampeleke Baba kwa Nabii mmoja hapa Dar yuko maeneo fulani huduma yake ni kubwa sana atamuombea atapona.

Kweli Baba na Mama kunasiku walijipanga wakaenda, kufika huko waliombewa sana na wakaambiwa wawe wanahudhuria maombi mara kwa mara hivyo kwa wiki wanaenda mara tatu. Walinishawishi na Mimi kwenda nikasema sina muda nikipata muda tutatenda.

Baada ya muda Baba alipata unafuu sana kwa maombi na dawa alizokuwa anatumia, akaanza tembea bila shida kabisa hivyo kama familia wakaamua kwenda kumshukuru Mungu na kutoa sadaka ya shukrani. Ikabidi nyumba nzima, Baba, Mama, Kaka zangu, na Mimi na ndugu wengine twende hapo kanisani kumsindikiza Baba kutoa sadaka ya shukrani.

Basi tukafika pale kwa Nabii kwenye Ibada, Baba alitoa sadaka ya shukrani na akaamua kutengeneza lile kanisa kwani lilikuwa halijajengwa vizuri, Baba akasema atajenga hilo kanisa na kununua vyombo na viti vya kanisa. Ilikuwa sadaka kubwa sana watu walishangilia tukapewa mikono na kuombewa na Nabii tukatoka.

Baba akajenga lile kanisa vizuri sana na kununua vitu vya kanisa alivyosema. Tena nakumbuka alimtuma kaka yangu mkubwa na mkewe waende china kununua vifaa vya kanisa na wakavileta. Kiukweli Baba na Mama walimpenda sana Nabii yani huwaambii kitu kuhusu Nabii. Ukitaka kugombana nao mseme Nabii.

Kuna siku Mama alipigiwa simu na Nabii akamuuliza Binti yako ana umri gani akamwambia miaka 26, akauliza ana mchumba akasema hana na wala hajui mwanaume akasema naona adui anamtafuta mwambie aje kuniona jumamosi asubuhi siku ambayo siendi kazini. Mama akanisihi sana na kuniomba jumamosi nisikose kwa Nabii anataka kukuombea. Nikasema sawa. Jumamosi nikajiandaa nikaenda kwa Nabii

PART 2

Kiukweli kabisa Mimi binafsi maswala ya maombi sikuwa napenda sababu sikuona tatizo kwangu, hivyo kusali ilikuwa sio sana kivilee. Sasa niliposikia Nabii ananiita nikawa natamani kujua kuna nini.

Huyu Nabii sio mkubwa kivile ana umri wa miaka 33 au 34 hivi. Ana mke lakini mkewe hayuko karibu nae kabisa hata hapo kanisani ukimuona huwezi jua kuwa ni mkewe. Na baadae ndio nikaja kujua Nabii ana nyumba yake ya maombi ambayo anaishi mwenyewe na mkewe na watoto wanaishi sehemu nyingine.

Mke wake ukimuona yuko so down, hana raha na wala hapendezi kama Nabii kifupi wako tofauti sana. Nabii yuko smart, gari zuri simu kali yani kakamilika lakini mkewe hapana kwakweli.

Basi nikafika kanisani wakasema Baba yuko ofisini wakasema subiri wakamwambie. Basi baadae nikaingia ile naingia tu Nabii akaamka kwenye kiti kaja mlangoni kunikumbatia waooow, akanipiga na mabusu mengi jamani uwiii nikashangaa utafikiri ni mtu anaenifahamu muda. Akasema nilikuwa na hamu sana ya kukuona nikashangaa.

Akaanza kuniuliza mbona huji kanisani yani nilipokuona siku ya kwanza moyo wangu ulikupenda, nikawa nazidi kushangaa tu.

Sasa nikawa nimekaa nasubiri maombi au kitu gani hakuna ni story tu jamani, ilikuwa hivi ikaenda hivi. Mara ananiuliza una mchumba, nikamwambia sina na wala sijawahi lala na mwanaume akasewa waooow umenifurahisha. Tukaongea sana akaniambia nataka unisindikize mahali tukapate chakula halafu nikupeleke nyumbani. Nikashangaa sielewi elewi.

Nikatoka nje akaonana na watu akawaombea alipomaliza akaniambia twende nikaingia kwenye gari lake tukaenda Hotel moja maeneo ya mbezi tukapata Lunch, tukamaliza akasema naomba nikikupigia simu pokea, na nikikuhitaji muda wowote uje plz kwa gharama yoyote. Akanipa pesa kama laki tatu akasema ni vocha na usafiri anytime nikikuita uje na usimwambie mtu kitu chochote.

Basi nikarudi nyumbani, Mama akafurahi kuniona akasema imekuwaje nikamwambia safi tu, umeombewa ndio kasema niende tena. Mama akasema safi na kesho twende wote ibadani. Kiukweli sikuelewa, nikaona Mama kumpigia Nabii kumshukuru kwa maombi na akamuahidi kuwa atahakikisha sikosi ibada.

Jumapili nikaenda Ibadani kimya Nabii anahubiri namuangalia tu. Kesho yake jumatatu akaanza kunipigia simu akasema naomba ukitoka kazini tuonane, nikashangaa ila nikasema sawa. Natoka kazini akanifwata, nilipoingia kwenye gari mabusu jamani uwiii, alinibusu kanikumbatia akasema nakupenda sana wewe ndio mwanamke wa maisha yangu, nikawa naendelea kushangaa, tukaenda sehemu tukakaa tukala, baada ya hapo akanirudisha nyumbani. Ikawa ndio mchezo wetu tuna chat tunatoka outing, tunakiss ni kawaida kabisa.

Mawasiliano yetu yakapamba moto, kunasiku Mama aliona simu yangu inaita ilikuwa usiku akaniletea alikuwa Nabii anapiga Mama akastuka ila akaniuliza mbona nabii anakupigia sahizi nikamwambia aliniambia niombe sasa anahakikisha kama ninaomba. Mama akasema sawa akaniacha. Nikawa nachat nae tunatoka outing kila mara na jumapili naenda kanisani na wazazi wangu. Jumapili hatuongei wala hatusalimiani na Nabii kimya kimya.

Sasa kuna siku akaniambia huwa ninafanya maombi ya utakaso kwa wanawake na mabinti akasema uje basi kwenye hayo maombi nikasema sawa. Hayo maombi anayafanya kwenye apartment yake so wanawake wanaenda wanatakaswa. Ukitakaswa unatolewa nuksi zote na mikosi. Kama hujaolewa utaolewa, hupati watoto utapata. Nilifika nikakuta mabinti na wanawake wengi kwakweli na akiingia mtu anakaa muda baadae anatoka anakuwa kachokachoka hivi, sikuwa naelewa ila ndio hivyo. Ikafika zamu yangu akaniambia panda juu ya meza vua nguo zako nikavua akaanza nipaka mafuta sehemu za siri, ananitekenya tekenya aisee nikawa napata kama usingizi halafu akaniacha. Akasema next uje nikutakase vizuri mpenzi.

Nilitoka pale na mawazo sana, nikasema nataka nikatakaswe tena. Yani ile hali ilihamsha hisia za kimapenzi nikawa namuwaza yeye tu.

Kuna siku akanipigia simu usiku kama saa nne akasema njoo tuonane nikatoka mbio, Mama akashangaa sahizi wapi nikamwambia nakuja maramoja. Nilienda kwa Nabii akanitakasa tena siku hiyo tukafanya mapenzi, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kulala na mwanaume, hivyo Nabii akawa my first man.

Nikawa nampenda sana, ananipa hela tunatoka tunaenjoy akawa boyfriend wangu. Kuna siku kaka yangu akaniambia nimekuona mahali na Nabii nikikuona tena nitakupiga, kaka akanikunja blouse akanipiga vibao nikapiga kelele Mama akaja akauliza nini, akamwambia huyu nimemkuta mahali na Nabii wanashikana shikama, Mama wacha amfokee kaka yangu yani Nabii awe na Grace never, hii ni dhambi utubu. Mama usiku kucha akawa anaomba rehema juu ya kaka yangu Mama hakulala anatubu juu ya kaka yangu.

PART 3

Sijui nilifungwa na nini, sikuwahi kuwaza kusuhu wale wanawake wanaokuja kutakaswa kama na wao analala nao, nilikuwa najiona ni Mimi tu ndio nalala na Nabii na nilimpenda sana sana. Sikumfikiria mkewe, maana aliniambia mkewe sio chaguo lake kabisa alimuoa bahati mbaya.

Mapenzi yetu yalinoga, akaniambia naomba uhame nyumbani nikupangie nyumba ukae, kweli nikitoka nyumbani nikasema nijitegemee, Mama akasema hapana mpaka nikamuulize Nabii kama ni sawa wewe kuhama nyumbani, maana Mama hafanyi kitu bila kumuuliza Nabii, alimuamini sana. Mama akaenda kwa Nabii akamuuliza kama naweza kupanga Nabii akasema ndio naona amani tu akapange. Mama akarudi akasema sawa Nabii kasema ukapange hapo uko huru.

Nikatafutiwa apartments mikocheni nikawa nakaa, jamani Nabii akawa anakuja kulala pale, kifupi alinihamisha nyumbani ili animiliki maana alikuwa anakaa pale, siku zingine anatoka kwangu anaenda ibadani. Nikawa mkewe. Nilitokea kumpenda sana jamani uwiii.

Kumbuka wazazi wangu wanasali hapo kwa Nabii na Mama yangu kwakuwa yuko sharp alipewa uzee wa kanisa. Kwahiyo Mama alikuwa anatumika kwenye ile madhabahu na kujitoa sana bila kujua kama Nabii anatembea na binti yake wa pekee na anaishi nae.

Nilikuwa naishi maisha yangu huku boyfriend wangu akiwa Nabii, nikitoka bila ruhusa anakasirika, kuna siku nilienda kazini nikachelewa nilitoka outing na marafiki zangu, narudi nyumbani namkuta kakasirika, anasema nimwambie ukweli sikuwa na wanaume, yani usiku wote nambembeleza akaniambia naomba usiniumize, nakupenda sana usijaribu kutembea na mwanaume yoyote nitakufanya kitu mbaya wewe na huyo mwanaume, na akasema ameweka walinzi wanifwatilie popote nitakapokuwa anapewa taarifa. Nikajua ni wivu tu.

Sasa kuna siku rafiki yangu alinipigia simu akaniambia Grace nimepata Boyfriend anahela huyo kaniomba niende na ndugu yangu mmoja amfahamu ndio akanipeleka Mimi akamwambia ni cousin wake. Kweli tulipata dinner ya nguvu na nauli laki moja nilipewa. Sasa Bwana kunasiku Nabii wangu aliniambia kuna rafiki yake kamualika afanye seminar kanisani kwake nikasema sawa.

Mama pia akanipigia nakuomba uje kanisani kuna seminar, kuna Nabii anafanya seminar, basi nilivyotoka kazini huyoo mpaka kanisani ile naingia tu namkuta Mtumishi anahubiri kupiga jicho ni yule Boyfriend wa rafiki yangu tuliyekuwa nae juzi dinner, ikabidi nitoke nje asinione. Nikampigia rafiki yangu nikamwambia kumbe jamaa yako ni Mtumishi akasema sijui, nikamwambia yupo hapa kanisani kwetu anahubiri, alicheka akasema mbona katoka kwangu hapa tumelala wote, tulicheka nikakata simu nikaondoka.

Siku zilienda baada ya muda nikawa siko vizuri kiafya, nikila natapika sana, sipendi harufu mwili unahoma kali sana. Hali ilikuwa mbaya ikabidi nirudi nyumbani. Nyumbani wakanipeleka hospital kupima wakagundua nina ujauzito weeeh ikawa balaa. Baba yangu alilia sana akasema mwanangu imekuwaje, Mama akasema nitawaambia nini kanisani mimi mzee wa kanisa binti yangu anamimba kweli. Na Mimi nilistuka sana jamani, sikutaka kuzaa kabla ya ndoa.

Nikamwambia Mama naomba usimwambie Nabii akasema namwambiaje hii aibu. Mama akamwita mama Mdogo aje kuongea na Mimi, nikaulizwa nani mwenye mimba nikanyamaza nikawa nalia tu. Walinihoji sana wakitaka kujua kuhusu mwenye mimba naangua kilio siwezi sema.

Mama mdogo akasema ngoja kuna Mchungaji namfahamu anafanyaga counseling ngoja nimwite aje aongee nae. Ndio wakamwita Pastor Anni Kaleb sasa aje.

PART 4

Sikuwa tayari wazazi wangu wajue kama Nabii ndio amenipa mimba maana ni mtu waliyemuamini sana, na pia sikutaka kaka zangu wajue maana wangeniua, lakini pia sikutaka Nabii ajue kama nina mimba yake maana nilipanga kuitoa kwani ni mume wa mtu. Nilitoka kwenye ile apartment wiki mbili Nabii akaanza nitafuta, anaomba nirudi nikamwambia ninaumwa lakini pia Baba kanizuia nisitoke nyumbani. Alikuwa ananitafuta sana, kuna siku alinivizia natoka kazini ile anafika tu Mama na kaka zangu walikuwa wananisubiri pia nikamwambia Mama yupo hapa alitoka mbio kama mwizi.

Kwasababu nilikuwa weak na ile hali ya ujauzito familia yangu ikaamua kuwa karibu na Mimi. Hivyo napelekwa kazini na wananifwata waliogopa nisije kujidhuru.

Mama mdogo alimleta Pastor Anni Kaleb kwetu, akaja akaongea na Baba na Mama na akawaambia msijali nitaongea nae na kila kitu kitakaa sawa. Pastor alikuja akaingia chumbani kwangu, kumuona tu akawahi kunikumbatia akaanza kuimba wimbo sitausahau "NI WEWE TU BWANA NI WEWE TU" aliimba aliimba kwa hisia sana huku kanikumbatia baadae akaanza kunena kwa lugha, alinena alinena nikaanza kulia nililia jamani uwiii baada nikajipata niko chini Mama aliniambia nilikuwa namapepo makali, majini mahaba mengi tu, ilibidi watu waje kumsaidia Pastor kunishika nilikuwa nanguvu balaa. Na mapepo yalikuwa yanasema huyu ni mke wetu, tumechukua nyota yake tunaitumia hawezi olewa tena wala kifanikiwa ilikuwa balaa.

Pastor Anni alipomaliza kuniombea akasema leo ngoja nimuache nitakuja siku nyingine, akamuombea na Mama yangu akaanguka chini kiufupi tulifunguliwa. Pastor Anni aliniongoza sala ya toba akasema mpokee Yesu leo nikakubali akaondoka. Baada ya kama wiki nikawa nimetengemaa hali yangu ilikuwa imeimarika nilianza kula nikamuomba Pastor Anni tuonane akaniambia niende kijichi kanisani kwake nikaenda.
Nilikaa nae kwa masaa matatu akaniambia niamini tu niambie ukweli wotee. Nikampa story yote Pastor, jinsi ilivyokuwa mpaka Mama yangu ananilazimisha kwenda kwa Nabii mpaka aliponipangia na kuanza kuishi nae Pastor Anni alistuka sana, akaniuliiza Nabii gani nikafungua Facebook nikamuonyesha picha yake, akasema uwiii huyu tena.

Pastor Anni Akaniambia hembu subiri kidogo, akampigia binti mmoja simu huyo Binti baada ya muda akaja. Huyo binti surayake sio ngeni tulikuwa tunasali wote pale kwa Nabii na nilikuwa namuona kwenye ibada ya kutakaswa kwa Nabii .

Pastor Anni akasema sijui kwanini nyinyi wote mmekuja kwangu, najua ni mpango wa Mungu sasa naomba niwaeleze ukweli ili mjijue na mjue hii vita sio ndogo. Akasema nyinyi wote mna mimba ya mtu mmoja, yani wote mmelala na Nabii na amewapa mimba wote. Uwiii tulijikuta tunalia tukamkumbatia Pastor Anni, akasema naomba mkubali hilo kwanza na mjue ili tujue tunapambanaje. Alianza kuimba wimbo wa kuabudu kama kawaida yake, akaanza kuomba aliomba alilia sana sana akasema Mungu rehema watoto wako, Mungu rehemu Kanisa lako. Akasema tuwafiche wapi watoto wetu, alilia Pastor Anni kuliko hata sisi wenye matatizo.

Akasema nawaomba kesho tuonane tukae kikao tujue tunaanzia wapi maana wote sisi wazazi wetu ni wazee wakanisa pale kanisani kwa Nabii. Na wanamuamini sana sana. Akasema inabidi tuwaokoe wazazi wenu na wajue ukweli ili tuwe huru.

PART 5 MWISHOOO

Kwakweli nilikuwa kama naota, kwajinsi yule Nabii alivyokuwa kwangu sikuwaza kama angekuwa na wanawake wengine, niliumia sana ufahamu ukanirudia nikajikuta najutia bikra yangu, imetolewa na mpuuzi moja, nikaumia zaidi juu ya Wazazi wangu jinsi walivyompenda na kumuamini Mtumishi, nikajilaumu sana kwanini sikumueleza Mama yangu ukweli wa kile nilichokuwa nakutana nacho wakati naenda kwa Nabii yamkini tusingefika huku.

Niliumia sana moyo, nikatamani kujiua sikuwa tayari Mama yangu asikie haya. Nikampigia yule Dada mwingine mwenye mimba ya Nabii nikamwambia tusiende kwa Pastor Anni tuachane nae sisi tuonane. Basi tukaonana tukasema hatuendi kwa Pastor na Wazazi wetu wasijue twende tukatoe mimba tutulie. Zote zilikuwa mimba changa kuna Dada tukamtafuta akatupa dawa tumeze za kusafisha, akasema ukinywa hii unableed tu kawaida mimba inatoka taratibu. Basi nikameza sikuona chochote nikarudi nyumbani.

Jamani usiku tumbo lilinikata niliumwa nikaamza kubleed kidogo kidogo nikamfwata kaka yangu nikamwambia nipeleke hospital nakufa, kaka akasema sawa nikamwambia asimuamshe Mama kaka akasema sawa akanipeleka hospital, tumbo linawaka moto napiga kelele nilikuwa naona nakufa. Kumbe kaka alivyonishusha akampigia mama kidogo Mama huyo hospital, nikaanza kupiga kelelee Mama nisamehe, Mama nakufa. Nikamwambia Mama nakufa lakini siwezi kufa bila kusema hii siri, nikamwambia Mama mpigie Pastor Anni aje nakufa nataka kutubu. Mama akatoka akampigia Pastor aje, baada ya kama saa nzima Pastor Anni alikuja. Kanikuta nalia tumbo linanikata Doctor kaja nikamwambia Doctor naomba Pastor akija uwepo nikiri maana najua nakufa, Doctor akawa haelewi wakiniuliza kitu sisemi nalia.

Kwenye chumba alikuwepo Mama, Pastor Anni, Doctor na Mama mdogo nikamwambia Pastor Anni nisamehe sikurudi kwako Pastor anashangaa nini, ndio nikasema ukweli wotee wa Mimi kutembea na Nabii, jinsi ilivyokuwa nikawa naishi nae, mpaka kupata mimba na kunywa dawa za kuitoa. Namaliza kuongea Mama yangu akaanguka akazimia, wakamtoa wakampeleka chumba kingine, nikaomba kaka yangu aingie nikamuomba msamaha maana aliwahi kunikuta na Nabii ila nilikataa na sikumsikiliza. Baada ya hapo Doctor akaita manesi faster wakaanza kunihudumia, kweli mimba iliharibika nikasafishwa, ila nilipata maumivu makali sana sana siwezi kueleze jamani.

Mama yangu pressure ilipanda akawa amelazwa hapo, Baba kuja kanikuta natoka kisafishwa ananiangalia hanimalizi. Pastor akaniambia tulia tuombe rehema kwa Mungu, Mungu atusamehe kwa yote, ombea na wazazi wako Mungu awasaidie kulipokea. Pastor Anni akaniambia kwasasa umeshaliharibu kubali matokeo, ukisemwa ukitukanwa kubali ila within time yatakwisha.

Kaka yangu akatoka akaenda kwenye ila Apartment akabeba vitu vyangu vyote akakodi gari akavileta nyumbani, alikuta nguo za Nabii viatu alichukia sana.

Baadae tuliruhusiwa tukarudi nyumbani, kwakweli hakuna mtu alinisemesha, walinichukia sana sana ila Pastor aliniambia nitulie yataisha. Nikampigia yule Binti na yenye alipata kisanga kama changu mimba ilitoka lakini chamoto alikiona. Baadae Pastor akaita kikao wazazi wangu na wayule binti mwingine wote tulikuwa tunasali pamoja kwa Nabii, Pastor akazungumza ukweli na akatuomba tupige magoti tuwaombe msamaha wazazi wetu laiti kama tungekuwa wazi kwao yasingetukuta haya. Tuliomba msamaha wazazi wakatuombea ilikuwa ngumu sana na ya maumivu makali sana.

Kiukweli hili swala limekuwa ni changamoto, na nimeomba Pastor Anni aweze kushare kwa page yake ili mabinti wengine waone na wajifunze. Ukiona unasali kanisa na Mtumishi anakutongoza acha waambie wazazi na muhame hilo kanisa. Mimi maisha yangu yameharibika kwa namna fulani na furaha ya familia yangu nimeitia doa hasa mama yangu .

MWISHOOOOO

Special appreciation kwa Mchungaji Anni Kaleb kwa kazi kubwa uliyofanya hadi binti huyu kuvuka na kuweza kutoa ushuhuda huu mzito ili wengi wapone!

Mimi nimeshare hii kutoka mtandaoni ili iwafungue macho mabinti na wanawake wote ambao ndio wahanga wakuu wa watumishi wa Mungu wa kizazi chetu!

Na ijulikane si kila mtumishi wa Mungu ni muharibifu, wewe unayepitia haya usimkatie tamaa Yesu au kujidhuru, unaweza kushinda pia!

Ninaelewa kuna watumishi wengine ni wa Mungu kweli lakini wanateswa na tamaa ya mwili na roho za giza japo hawajui wakafunguliwe wapi au watokeje kwenye maisha haya ya uchafu, hivyo wanaendelea kuhudumu huku wakiwa wahanga sirini!

Kama ni mtumishi wa Mungu na unapitia uchafu huu, na ungetamani kufunguliwa na kumtumikia Mungu katika ROHO NA KWELI, kwa neema ya Mungu naweza kukusaidia, HAIPENDEZI UFIE DHAMBINI NA UPOTEZE WENGI PAMOJA NA UOVU WAKO HUU.

LAKINI

Wako watumishi ambao si issue kama ya hapo juu, bali wao wanajua ni mawakala wa kuzimu wanakusanya nyota za wanawake hasa mabinti wadogo ili kuwa na mvuto, ushawishi, na nguvu za kuendeshea huduma zao za upotevu zinazoua nafsi nyingi na kuunganisha watu na kuzimu!

Kivyovyote, kama binti umepitia haya, umekutana na mtumishi wa hivi, akakutumia na unahitaji msaada wa kuvuka hapo na kurudi kwa Bwana Yesu akupendaye mno, kama una amani share na mimi inbox WhatsApp na nitakusaidia au kukupa mtu wa kukusaidia ili uvuke!

By Pastor Ann Kaleb
 
tutajie huyo nabii.

ila wanawake mmekuwa wajinga sana.... mnadanganywaga kipumbavu, mnakazwa kirahisi sana... wewe kama ni mkristo ni mahali gani yesu aliwatakasa watu kwa kuwaambia wavue nguo? ni maombi gani yanayokusanya wanawake tu tena usiku?
muwe mnatumia akili, mmekuwa masikule ya viongozi wa dini.ni sawa na wale waliokuwa wanakazwa na yule bwana ake ebitoke, yan nimeshangaa ni wanawake wengi ajabu wamefanyiwa ule ujinga, wengine wasomi, wengine wake za watu .
wanawake wa tz mnatia kinyaa ndo maana kampeni ya KATAA NDOA ina mashiko
 
Aiseee
Shetani yupo makanisani sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom