Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,327
24,209
Nimeshangazwa na kauli hii ya Mh Rais, kuita msimamo wa mteule wake Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje, kuwa NONSENSE, tena hadharani.

Nimesikitishwa na kauli hiyo kwa sababu mbili.

Moja, public reprimand kwa kiongozi mwandamizi, sidhani kama ni utawala bora.

Na hii naanza kuhisi ile power is getting to the head, and power corrupts.

Pili, nimesikiliza arguments za Mkenda, though pompous, kuna relevance pale.

Argument ni kuagiza sukari kama kuna shortage, si kwa matakwa ya wafanyabiashara.

Sasa wale wawekezaji wanaovipanua viwanda ili ku boost uzalishaji wa sukari, wale ni nonsense?

All in all, Mkenda anapaswa kujiuzulu ku-save face.
 
Hivi bado kuna uhaba wa sukari mpaka leo? Sijasikia zile kelele muda mrefu.

Rais wetu naona kama amekubali kutumiwa na Museveni nae akatumika, kama Museveni ana sukari nyingi kwake haina soko ameona aje kulitafuta huku na sisi badala ya kujiuliza kama tunaihitaji naona tumekimbilia kukubali ombi tu ili kukuza urafiki na majirani.

Suala la kuita msimamo wa waziri wake Nonsense tena public nalo nalipinga, kama alikerwa na huo msimamo ana kila nafasi ya kuonana na waziri wake na kumweleza aliyonayo, sio kumsubiri Museveni aje ndio anamnanga mbele za watu, hizi ni tabia typical za kike - umbea.
 
Bro ni vizuri pia ujue kuwa Uganda nao wamesucrifice sana kwa kuleta bomba Tanzania, hilo bomba kiuhalisia lilitakiwa lipite Kenya but wao wakalileta kwetu na pia kuna benefits kubwa tunazipata kwa waganda kutumia bandari za Tanzania badala ya za Kenya hivyo na sisi ni lazima tuoneshe mkono wa shukrani
 
Hivi bado kuna uhaba wa sukari mpaka leo? sijasikia zile kelele muda mrefu.

Rais wetu naona kama amekubali kutumiwa na Museveni nae akatumika, kama Museveni ana sukari nyingi kwake haina soko ameona aje kulitafuta huku na sisi badala ya kujiuliza kama tunaihitaji naona tumekikbilia kukubali ombi tu ili kukuza urafiki na majirani.

Suala la kuita msimamo wa waziri wake public Nonsense nalo nalipinga, kama alikerwa na huo msimamo ana kila nafadi na kuonana na waziri wake na kumweleza aliyonayo, sio kumsubiri Museveni aje ndio anamnange mbele za watu, hizi ni tabia typical za kike - umbea.
Mkuu!

Magufuli hakuzuia sukari toka nje kwa sababu ya roho mbaya hapana.

Alisema kabisa tuna mashambe mengi tuzalishe sukari yetu hapa hapa nchini na kufaidisha viwanda vyetu vya ndani.

Yule mzee aliambulia matusi toka wapumbavu badala ya kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji ili kuinua vipato na kuongeza ajira.!

Kila siku huwa nasema hapa kwamba kumpigania mpumbavu malipo yake ni upumbavu!

Ona sasa tunaenda kuwa dampo la sukari toka uganda!

Nmeona uzi hapa jana mtu anashauri Samia aruhusu cement toka Kenya, na usishangae na yeye akafanya hivyo.
 
Back
Top Bottom