Rais Samia unagombanishwa kwa wananchi kuzuia kuuza mazao nje ya Nchi. Unatutakia Watanzania umaskini wa lazima

ndoto2020

JF-Expert Member
Feb 25, 2017
203
315
Heshima yako Rais wangu Samia. Mimi ni mmoja wa Watanzania wasiokupinga wala kukubali sana nipo 50/50 kwa sababu nakuona kama Rais mwema, msikivu, mwenye hekima, una diplomasia nzuri sana ya kimataifa.

Kwenye uwekezaji wa Royal Tour nia njema nilikupa 100% utekelezaji unahitaji maboresho kidogo sio shida, kwenye kutenga budget ya kilimo ulitukuna sana watanzania tulio wengi na wadau wa kilimo, kwenye sekta ya umeme na nishati kurudisha miradi ya LNG Lindi ahsante sana, kwenye utulivu wa kisiasa na watu kupunguza woga safi sana.

Lakini nakuona kama Rais usiye na maamuzi yako, unayumba sana kwenye misimamo kama amiri jeshi mkuu na raia number moja. Mifano michache halafu nakuomba uwe na msimamo sahihi knye soko huria la mazao.

1. Issue ya wamachinga uliwafukuza mitaani ukasema wakapangwe lakini utekelezaji wake mpaka kesho watendaji wako wamekudharau na umewatia umaskini zaidi wamachinga kuliko awamu ya tano na hawa watu ni hawana option B ya maisha.

2. Kutowachukulia wabadhirifu hatua, ni ajabu na dhambi kubwa sana Rais kulalamika hadharani, wewe ni amiri jeshi mkuu ukitoa kauli kama hatua haijachukuliwa na wanaotakiwa kuchukua ina maana wewe ni dhaifu.

Kuwaita nonsense na kutishia kuwa watajua rangi yako si sahihi, sahihi ni kutangaza hadharani ili kufikisha ujumbe kwa wengine kuwa flani flani flani wamesimamishwa kazi na TAKUKURU na mahakama ndani ya miezi 3 nataka matokeo ya hukumu PERIOD.

3. Kutamka hadharani mawaziri wale urefu wa kamba zao, pale mheshimiwa Rais ulifungulia dirisha la confidence ya wizi.

4. Ulipomjibu waziri wako wa kilimo enzi hizo Prof. Mkenda mbele ya TV kuhusu kukataza vibali vya sukari pale kila mtu alitafsiri Rais umewekwa mfukoni na wafanyabiashara wa sukari na kweli mpaka leo zile juhudi za kufufua viwanda vya sukari imeisha, wakati ni eneo ambalo Tanzania tungeweza kufanya wonders dunia nzima, Thailand wana viwanda vya sukari 115 sisi mpaka leo 4 ukiweka cha Bakhera na Mbigiri Morogoro ndo sita shame on us.

Kama Rais Usiyumbe msimamo ubaki pale pale bora sukari iwe kilo efu 5 mpaka tujitosheleze wawekezaji waone fursa na waje kwa wingi kuwekeza na toa incentive kwa wawekezaji wa ndani wenye uwezo.

5. Machozi yamenitoka umelegea tena kwenye kodi ya mafuta ya kupikia kutoka nje, sasa lini tutajitegemea, lini bei ya alizeti na michikichi itavutia watu wakimbilie kwenye kilimo kama tayari bei itakuwa chini?

Tafadhali kama raia mwenye heshima kwa mamlaka naomba tafakari tena hili jambo, Serikali imeshawekeza kwenye ruzuku ya mbegu za alizeti, scheme za umwagiliaji, watu wameshachukua matrekta ya mikopo ghafla unashusha kodi ya mafuta kutoka nje from 35% to 25% labda kama ujashirikishwa au waziri wa fedha awe kashikishwa mpunga mrefu.

MSINGI WA MALALAMIKO YANGU
Toka umetoa kauli mwanza kuwa tusiuze mazao nje wakuu wa mikoa wametekeleza agizo lako kama inavyotakiwa kwamba Rais akisema ni agizo, lakini naomba nikushauri kuwa futa ile kauli. Tena rudia kwa kutangaza kwa sauti kubwa kuwa jamani uzeni mazao yenu kokote kule na sisistiza sana na sana na sana.

Ni kweli kawaida kabisa watu wa chini wanauza mazao halafu wanalia baadae njaa, hiyo ni kawaida sana na isikutishe, hakuna chakula cha msaada kamwe. TFRA inunue haraka iweke akiba, wafanyabiashara wanunue kwa bei juu wakauze wapate faida wote kulima na mfanyabiasha November bei ya mazao unga na mchele utapanda maradufu hiyo ndo fursa na kichocheo muhimu sana tena ndo nzuri kabisa yule mfanyabiashara ataamua kuwekeza knye kilimo ili mwaka kesho awe na mazao yake na atanunua na watu wa kati wengi watawekeza kwenye kilimo maana kinalipa (KWA NINI HAKUNA KAMPENI YA KUFUNGUA MABAA NA ZINAFUNGULIWA KILA SIKU?ZINALIPA).

Ifike mahali kilimo kilipe sawasawa kwa sababu ya tija, miundombinu wezeshi na rafiki ambayo umeanza kama ya umwagiliaji na kusafisha mapori kupata ardhi ya kulima.

Kilimo tukikifanyia haki kina watu wengi sana na mazao mengi sana kwa ujumla wake kitapunguza umaskini sana sana hata haya madeni tunakopa kama taifa wakulima watakuwa na disposable income kubwa ya kuwa taxable.

Rais Samia naomba utuvushe kwa kicheko 2025 tusiumie moyo, watanzania ni walalamishi sana na wabishi ila kwenye sera sahihi.

Usiyumbishwe na mitandao, mtu akiona mchele au unga ghali ale bundle. Wakulima tumewatesa sana wakauze kokote kwa bei yeyote ya soko, kuwapangia pangia kila wakivuna ndo chanzo cha umaskini wote huu wakati hatuwapangii wakalime.
 
Samia shikilia hapo hapo mbwa Hawa walikuwa wanakutukana kucha kutwa wakati umeruhusu mazao kwenda Nje na bei kuwa Juu..

Mbona Mwendazake hamkuchukia na bei za mazao zilikuwa za kutupa? Anawalinda Wanyonge,Wanyonge si ndio wenye nyie au? 😁😁

Mumewe akimpenda inatosha wewe ongeza juhudi za kumchukia.

Dalali wa Wakenya fuata utaratibu
 
Wewe jamaa ushawahi kunitukana humu baada ya mimi kupinga kuuzwa kwa mazao nje ya nchi,ukawa upande wa bashe na kudai tunaokataa mazao yasiuzwe nje ya nchi tukalime mazao yetu,leo serikali imepiga marufuku kuuza mazao nje ya nchi umepiga u turn ya nguvu upo na serikali tena!
 
Heshima yako rais wangu SSH, Mimi ni mmoja wa Watanzania wasiokupinga wala kukubali sana nipo 50% 50% kwa sababu nakuona kama rais mwema , msikivu, mwenye hekima, una diplomasia nzuri sana ya kimataifa , Knye uwekezaji wa Royal tour nia njema nilikupa 100% utekelezaji unahitaji maboresho kidogo sio shida, knye kutenga budget ya kilimo ulitukuna sana watanzania tulio wengi na wadau wa kilimo, knye secta ya umeme na nishati kurudisha miradi ya LNG LINDI ahsante sana, knye utulivu wa kisiasa na watu kupunguza woga safi sana, lakin nakuona kama Rais usiye na maamuzi yako, unayumba sana knye misimamo kama amiri jeshi mkuu na raia number moja.
Mifano michache halafu nakuomba uwe na msimamo sahihi knye soko huria la mazao.

Nimependa hii statement

"Mimi ni mmoja wa Watanzania wasiokupinga wala kukubali sana nipo 50% 50%"

Inatia moyo kusikia bado kuna wa Tanzania sincere
 
Heshima yako rais wangu SSH, Mimi ni mmoja wa Watanzania wasiokupinga wala kukubali sana nipo 50% 50% kwa sababu nakuona kama rais mwema , msikivu, mwenye hekima, una diplomasia nzuri sana ya kimataifa , Knye uwekezaji wa Royal tour nia njema nilikupa 100% utekelezaji unahitaji maboresho kidogo sio shida, knye kutenga budget ya kilimo ulitukuna sana watanzania tulio wengi na wadau wa kilimo, knye secta ya umeme na nishati kurudisha miradi ya LNG LINDI ahsante sana, knye utulivu wa kisiasa na watu kupunguza woga safi sana, lakin nakuona kama Rais usiye na maamuzi yako, unayumba sana knye misimamo kama amiri jeshi mkuu na raia number moja.
Mifano michache halafu nakuomba uwe na msimamo sahihi knye soko huria la mazao.

1. Issue ya wamachinga uliwafukuza mitaani ukasema wakapangwe lakini utekelezaji wake mpaka kesho watendaji wako wamekudharau na umewatia umaskini zaidi wamachinga kuliko awamu ya tano na hawa watu ni hawana option B ya maisha.
2. Kutowachukulia wabadhirifu hatua, ni ajabu na dhambi kubwa sana Rais kulalamika hadharani wewe ni amiri jeshi mkuu ukitoa kauli kama hatua haijachukuliwa na wanaotakiwa kuchukua ina maana wewe ni dhaifu ( kuwaita nosense na kutishia kuwa watajua rangi yako si sahihi , sahihi ni kutangaza hadharani ili kufikisha ujumbe kwa wengine kuwa flani flani flani wamesimamishwa kazi na takukuru na mahakama ndani ya miezi 3 nataka matokeo ya hukumu PERIOD.
3. Kutamka hadharani mawaziri wale urefu wa kamba zao, pale mheshimiwa Rais ulifungulia dirisha la confidence ya wizi.
4. Ulipomjibu waziri wako wa kilimo enzi hizo Prof Mkenda mbele ya TV kuhusu kukataza vibali vya sukari pale kila mtu alitafsiri rais umewekwa mfukoni na wafanyabiashara wa sukari na kweli mpaka leo zile juhudi za kufufua viwanda vya sukari imeisha, wakati ni eneo ambalo Tanzania tungeweza kufanya wonders dunia nzima, Thailand wana viwanda vya sukari 115 sisi mpaka leo 4 ukiweka cha bakhera na mbigiri Morogoro ndo sita shame on us. Kama Rais USIYUMBE MSIMAMO UBAKI PALE PALE BORA SUKARI IWE KILO EFU 5 MPAKA TUJITOSHELEZE wawekezaji waone fursa na waje kwa wingi kuwekeza na toa incentive kwa wawekezaji wa ndani wenye uwezo .
5. Machozi yamenitoka umelegea tena knye kodi ya mafuta ya kupikia kutoka nje RAIS SSH UNATUKWAZA SANA, sasa lini tutajitegemea lini bei ya alizeti na michikichi itavutia watu wakimbilie knye kilimo kama tayari bei itakuwa chini?
Tafadhali kama raia mwenye heshima kwa mamlaka naomba tafakari tena hili jambo , serikali imeshawekeza knye ruzuku ya mbegu za alizeti, scheme za umwagiliaji, watu wameshachukua matrecta ya mikopo ghafla unashusha kodi ya mafuta kutoka nje from 35% to 25 % labda kama ujashirikishwa au waziri wa fedha awe kashikishwa mpunga mrefu.

MSINGI WA MALALAMIKO YANGU.

Toka umetoa kauli mwanza kuwa tusiuze mazao nje wakuu wa mikoa wametekeleza agizo lako kama inavyotakiwa kwamba Rais akisema ni agizo, lakini naomba nikushauri kuwa futa ile kauli , TENA RUDIA KWA KUTANGAZA KWA SAUTI KUBWA KUWA JAMANI UZENI MAZAO YENU KOKOTE KULE NA SISISTIZA SANA NA SANA NA SANA .

nNi kweli kawaida kabisa watu wa chini wanauza mazao halafu wanalia baadae njaa, hiyo ni kawaida sana na isikutishe HAKUNA CHAKULA CHA MSAADA KAMWE , TFRA inunue haraka iweke akiba, wafanyabiashara wanunue kwa bei juu wakauze wapate faida wote kulima na mfanyabiasha November bei ya mazao unga na mchele utapanda maradufu hiyo ndo fursa na kichocheo muhimu sana tena ndo nzuri kabisa yule mfanyabiashara ataamua kuwekeza knye kilimo ili mwaka kesho awe na mazao yake na atanunua na watu wa kati wengi watawekeza knye kilimo maana kinalipa ( KWA NINI HAKUNA KAMPENI YA KUFUNGUA MABAA NA ZINAFUNGULIWA KILA SIKU ? ZINALIPA) ifike mahali kilimo kilipe sawawsaw kwa sababu ya tija , miundo mbinu wezeshi na rafiki ambayo umeanza kama ya umwagiliaji na kusafisha mapori kupata ardhi ya kulima. Kilimo tukikifanyia haki kina watu wengi sana na mazao mengi sana kwa ujumla wake kitapunguza umaskini sana sana hata haya madeni tunakopa kama taifa wakulima watakuwa na disposable income kubwa ya kuwa taxable

RAIS SSH naomba utuvushe kwa kicheko 2025 tusiumie moyo , watanzania ni walalamishi sana na wabishi ila knye sera sahihi USIYUMBISHWE NA MITANDAO MTU AKIONA MCHELE AU UNGA GHALI ALE BUNDLE WAKULIMA TUMEWATESA SANA WAKAUZE KOKOTE KWA BEI YEYOTE YA SOKO KUWAPANGIA PANGIA KILA WAKIVUNA NDO CHANZO CHA UMASKINI WOTE HUU WAKATI HATUWAPANGII WAKALIME
Wananchi wanafki sana. Hivi unajua mkiuza chakula nje Cha ndani kisipotosha mtaenda kukinunua Tena? Mnajua mtauziwa kias gan?
Na mauza nje, chakula Cha ndani kikapanda bei unajua kama hakitashuka na mpaka mbegu zitapanda?
 
Naunga hojaaa. Namuomba samia store ruhusa ya mkulima auze apendapoo. Kumzuia mkulima na kumfungia mpaka nikumtia umasikinii. Hivyo basi ili kilimo kiwe na tija na faida Kwa mkulima, tunaomba afungue mipakaa.
 
Wananchi wanafki sana. Hivi unajua mkiuza chakula nje Cha ndani kisipotosha mtaenda kukinunua Tena? Mnajua mtauziwa kias gan?
Na mauza nje, chakula Cha ndani kikapanda bei unajua kama hakitashuka na mpaka mbegu zitapanda?
Kupanda Kwa bei ya chakula ndio FURAHA ya mkulima. Mkulima atasomesha na atajenga nyumbaa
 
We jamaa akili huna kweli. Bei ya mazao haipandi kipindi mazao yapo Kwa mkulima. Mkulima kashauza wakati bei inaongezeka shamba tayari Kuna njaa, vyakula vinatoka mjini vinaenda kijijini. Dah! Kumbe ndo mana unaongea Kwa mihemko tu. We akili yako bei ya chakula ikipanda mkulima ananufaika nayo vipi?
 
Kupanda Kwa bei ya chakula ndio FURAHA ya mkulima. Mkulima atasomesha na atajenga nyumbaa
We kilaza kweli. Kwa taarifa tu hakuna mkulima anaenufaika na Madalali wa kibongo wanaokuja shamba kumlalia kwenye bei. Foreigners ndio wanalipa hela nzuri na mzigo pia wanaufata mashambani.

Kwa kutambua hilo nao madalali wanabeba mzigo wanaenda kuuza nje huko huko. Matokeo yake chakula kinaadimika nchini na mabei yanapanda bila kujali uchumi wetu ni dhaifu kuliko wa Kenya tunakowauzia. Sisi tunaumia bila sababu.
 
Kwani akiuza humu ndani hapati faida.
Hapanaaa kabisa mkulima atapata hasara kubwaa saaana. Ngoja nikuambie kituuu, kabula hajafunga mipakaa mazao kama mahindii debe Moja tumeuza Hadi elfu 18000 baaada ya kufunga mipakaa mpaka Sasa debe Moja inaelekea elfu tanooo. Mimi ni kindakindaki wa mama SAMIA, ila Kwa hili la kutufungia mipakaa sisi wakulima, hapa tutamchukia saana. Labda niwajulishee tuuu kwamba, baaada ya mazao kupanda bei, yamefanya vijana wengi saana kupenda kilimo maana kunafaida saana. Mama SAMIA nakuomba sikia kilio Cha wakulima, wewe ni raisi wanguu msikivu saana. Tusaidie wakulima. Kulima ni matesoo saaanaaa. Tuhurumie
 
Back
Top Bottom