Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ila Fernandes aisee amedrop sana..sijui wenzangu mnamuonaje..
Mkuu, bila kupata DM kwenye hii timu kila mchezaji tutaanza kumuona hamna kitu.

Hebu tujiulize ni kwanini Maguire alikuwa mzuri hapo Leicester na leo tunamuona mzembe?

Muda sio mrefu hata Martinez tutaanza kuona tumepigwa,timu haina mtu wa kuichezesha. Tominay akipata mpira anafanya kazi ya kurudisha nyuma kwa kipa,akitaka kwenda mbele ndio kituko zaidi hajui hata pa kuupeleka mpira.

Mimi nadhani tukipata DM ataongoza pale kati vizuri,pale kati pamekosa kiongozi hawa akina Macfred wanacheza kama wamekatwa vichwa lazima akina Maguire waendelee kuonekana vituko. Japo Maguire amekuwa mzembe mzembe bado siamini kama ni beki mbaya sana kama tunavyomsema.

Tatizo lingine lipo kwa DDG, uwezo wake wa kucheza na wachezaji ni mdogo sana,ni muoga na hajiamini kila akirudishiwa mpira anabutua. Sasa sijajua labda ni hawaamini wachezaji wake au ni yeye hajiamini.
 
Huwa humuoni kama mchezaji, sasa unamuona kama nani? Alafu Maguire ni bonge la beki, tatizo liko kwa kocha. Timueni kwanza huyo kocha anawachelewesha sana
Tupambane mizigo yote iondoke. Rashford, Maguire, Fred, Mctomy, Martial and last but not least Phil Jones japo huwa simuoni kama ni mchezaji.
 
sikuangalia mechi, lakini kwa mujibu wa statistics, hasa kwenye ball possession basi naona timu iko poa ukilinganisha na mwaka jana.

Matokeo ya jana cocha yuko responsible kwa kuwapanga Shaw na Sancho ambao hawakuwa fit for the match almost during the whole of last week.

He even made it worse kwa kumuingiza Ronaldo.
Ungeangalia Mechi ungelia machoziii...
 
Mkuu, bila kupata DM kwenye hii timu kila mchezaji tutaanza kumuona hamna kitu.

Hebu tujiulize ni kwanini Maguire alikuwa mzuri hapo Leicester na leo tunamuona mzembe?

Muda sio mrefu hata Martinez tutaanza kuona tumepigwa,timu haina mtu wa kuichezesha. Tominay akipata mpira anafanya kazi ya kurudisha nyuma kwa kipa,akitaka kwenda mbele ndio kituko zaidi hajui hata pa kuupeleka mpira.

Mimi nadhani tukipata DM ataongoza pale kati vizuri,pale kati pamekosa kiongozi hawa akina Macfred wanacheza kama wamekatwa vichwa lazima akina Maguire waendelee kuonekana vituko. Japo Maguire amekuwa mzembe mzembe bado siamini kama ni beki mbaya sana kama tunavyomsema.

Tatizo lingine lipo kwa DDG, uwezo wake wa kucheza na wachezaji ni mdogo sana,ni muoga na hajiamini kila akirudishiwa mpira anabutua. Sasa sijajua labda ni hawaamini wachezaji wake au ni yeye hajiamini.
Mtu anaposema eti Maguire alikuwa mzuri Leicester huwa simuelewi kabisa, kwamba anajisahaulisha Leicester ni timu ndogo au?
 
Acha tu mzee, Huyu Maguire sijui ilikuaje tukamnunua kwa bei mara mbili ya Gharama tulizojengea UDSM new library.

Jamaa hajui kujipostion hata haangalii mazingira ajue anaenda wapi yeye jicho kwa mpira movement nyuma yake halijui.

Kilichokera zaidi eti Captain

Hata huko Leicester alikua mtu wa maboko tu.

Alafu watu wanasema tumvumilie Ten Haag, anajiharibia sana ilitakiwa Rashford, Maguire, Martial, na takataka zote zilizotukwamisha msimu uliopita zinapunguzwa benchi.

Kwanini asiamini madogo Like Gernacho badala ya Rashford ambae kashajiona amepatia maisha baada ya kupewa MBE.

Kiungo aamini mmoja kati ya Garner au Charlie Savage au Zidane Iqbal, Garner.

Kutoa warning kua hapa hakuna tena ujuaji bali Form and delivery.

Mshambuliaji hata sijui why hatusajili.
Ronaldo na drama zote nae anahitaji challenge ya namba vinginevyo tutapandwa kichwani hadi tukome.

Unakuta eti Martial mshambuliaji wa kumpa challenge Ronaldo?

Sokoni hakuna mtu aggressive na goli wa kijipostion vizuri.

Ronaldo anayaweza hayo tatizo drama kelele hadi kuharibu morale mara kuondoka mara vipi?

Brand over team no man

Leten forward wa kudelvery ambae hajaonja ubishoo. Ili wawe wanabadilishana namba na faza Ronaldo.

Kingine Ten Haag afanye kazi aache kusikiliza mafala. Wakimsumbua awaambie "HAPANGIWI" In Magufuli Voice na kingine ili awe na nguvu inatakiwa anao wapanga awe ndio amewaibua sio waliofukuzisha makocha.
 
Licha ya kufanya changes kwenye top management club bado ina shida,ilikuwa big mistake kumpa kazi Ralf Rangnick then baadae akafukuzwa,moja ya sababu kubwa kumpa kazi ilikuwa aje kuwa mshauri na i believe kipindi alichokaa tayari kuna matatizo mengine aliyagundua na alishaanda ushauri kwenye some decision.
 
Natural Ralf hawezi Kumshauri ETH, tabu ya hii club ni kwamba kila siku tunaajiri mifumo mipya, kama tulitaka ushauri wa Ralf, ETH hakupaswa kuja, ilibidi Aje mtu mwengine mwenye Philosophy za Kijerumani.
 
Now ETH ana-struggle kwenye some issue but RR alisha-observe mengi i hope angemsaidia,kuna matatizo ETH atayajua baada ya msimu kuisha ndio maana ameanza kutaka kufanya panic buy baada ya kufungwa juzi.
ETH anaweza fukuzwa au jiuzulu within 2 years then tukaanza upya
 
Eth kuondoka sio issue, ila kuwa na Consistency ya makocha ndio tunakosea.

Wachezaji wa RR wasingefit kwa ETH, kama unakumbuka speech zake alisema tunamiss Physical and Agressive players, mfumo wa Gegenpress unataka watu wa design hii, ndio maana Klop anaweza Manage na watu kama Wijnaldum, Henderson, Mane etc.

ETH yeye ni mould ya kina Pep na LVG, mtu wake wa kwanza aliemtaka ni FDJ si physical player, Then kaja Malacia, Martinez na Eriksen, wote hawa si Physical players angalau kidogo Martinez ni Agressive. ETH yeye ni technical zaidi anataka wachezaji ambao wapo comfortable na mpira.

So Kivyovyote vile hawa wachezaji wasingekuja chini ya RR sababu ya philosophy tofauti Zingegongana.

Cha muhimu ni kutengeneza Culture, sisi kama timu tunataka tuwe wapi? Kama tunaamua ku invest kwenye mfumo wa ETH basi hata kama ETH ataondoka aje mtu wa mifumo hii hii, hii itasaidia kupunguza rebuild na hata Academy yetu tutajua wachezaji tunawaandaa vipi.

Timu zote kubwa kama Barcelona, Madrid, Bayern, Man city, Liverpool etc wana Culture na philosophy zao.
 
Ungeangalia Mechi ungelia machoziii...

Tulianza vzr bhn. Dynamics za mchezo huwa zinabadilika kulingana na scoreboard kwa wakati fulani. Kama Bruno angefunga ile nafasi pengine tungekuwa tunazungumza mambo mengine.
Hali ilianza kuwa mbaya baada ya kufungwa. Second half kulikuwa na drastic improvement baada ya Eriksen kushuka chini.
 
mpira ulibadilika zile dakika alizoingia ronaldo tu huku kwingine ujingaaa hakuna kituuu..
 
Now ETH ana-struggle kwenye some issue but RR alisha-observe mengi i hope angemsaidia,kuna matatizo ETH atayajua baada ya msimu kuisha ndio maana ameanza kutaka kufanya panic buy baada ya kufungwa juzi.
ETH anaweza fukuzwa au jiuzulu within 2 years then tukaanza upya

Afukuzwe ETH halafu aje nani?? Bado kuna watu wanaamini shida ya Man U ni kocha??
Work rate, mentality, technical ability, aggressiveness, physicality etc.. ya wachezaji wengi (60%) ni poor(in Steve Nyerere's voice).
Ralf Rangnick alikuwa sahihi aliposema tunahitaji overhaul/open heart surgery.
Nadhani siku atakayofukuzwa ETH mashabiki wanaweza ku turn against the board.

Msimu wa mwisho wa Ferguson alikuwa na wachezaji wa kawaida ila work rate yao ilikuwa kubwa. Hawa wachezaji wa sasa tumejaza majina ila uwanjani mdebwedo.
 
Eth kuondoka sio issue, ila kuwa na Consistency ya makocha ndio tunakosea.

Wachezaji wa RR wasingefit kwa ETH, kama unakumbuka speech zake alisema tunamiss Physical and Agressive players, mfumo wa Gegenpress unataka watu wa design hii, ndio maana Klop anaweza Manage na watu kama Wijnaldum, Henderson, Mane etc.

ETH yeye ni mould ya kina Pep na LVG, mtu wake wa kwanza aliemtaka ni FDJ si physical player, Then kaja Malacia, Martinez na Eriksen, wote hawa si Physical players angalau kidogo Martinez ni Agressive. ETH yeye ni technical zaidi anataka wachezaji ambao wapo comfortable na mpira.

So Kivyovyote vile hawa wachezaji wasingekuja chini ya RR sababu ya philosophy tofauti Zingegongana.

Cha muhimu ni kutengeneza Culture, sisi kama timu tunataka tuwe wapi? Kama tunaamua ku invest kwenye mfumo wa ETH basi hata kama ETH ataondoka aje mtu wa mifumo hii hii, hii itasaidia kupunguza rebuild na hata Academy yetu tutajua wachezaji tunawaandaa vipi.

Timu zote kubwa kama Barcelona, Madrid, Bayern, Man city, Liverpool etc wana Culture na philosophy zao.
Pep EPL imembadilisha alivyokuja amemtumia Fernandinho ambaye ni physical na alivyoona amechoka akam-replace na Rodri ambaye ni physical pia ni ngumu kupata success kwenye EPL kwenye hii era kama huna DM mzuri na hii ndio weakness yetu kubwa kwa sasa.Fabinho,Rodri,Kante,Hodjberg,Rice,Ndidi,Neves ni wachezaji ambao wanaleta balance kwenye timu zao DM ilipaswa kuwa priority ya United hata kama wangempata FDJ ,I think ETH atakuja kugundua hili January au mwisho wa msimu while ni tatizo ambalo linajulikana wazi.There must be balance kati ya results & rebuild ,kama matokeo hayatakuwa mazuri Glazers wanaweza mfukuza kazi mapema .I believe wachezaji bora wapo na sio tu wale aliowafundisha tu au waliocheza Holland tu,hizi habari za kutaka kuwasajili Rabiot na Arnautovic zinaonyesha hakuna kilichobadilika
 
Kama unaona tetesi za sasa sokoni tunatafuta DM, tumekuwa linked na DM kadhaa, Rabiot, yule wa Real Betis etc. Mpaka sasa hatujui ETH anataka nini. Kuna uwezekano amemkosa FDJ hivyo ameamua kwenda na DM wa kawaida na box to box (kama tetesi za sms ni za kweli)

Na Fernandinho na Rodri wote ni Baller mkuu. Ni Dm ila sio zile design za Destroyer wapo average kwenye ukabaji ila wapo vizuri zaidi kwenye kupiga pasi na kuretain possesion angalia stats za rodri hapa

Pia kante sio DM, Dm wa chelsea ni Jorginho,same situation kama ya FDJ ambaye ni Playmaker ila anakaa nyuma na mbele yake anacheza Midfield kazi.

Kwa sisi Dm wetu ni lazima ajue kuchezea mpira, kina Mcfred hawana uwezo wa kutoa mipira haraka kutoka kwa beki kwenda kwa viungo washambuliaji, mtu kama FDJ anatufaa sana kuliko Ndidi.

Kina leicester wanaweza cheza na watu kama Ndidi sababu ya wachezaji kama Tielemans na Madison ambao wanacover weakness yake ya Ushambuliaji sisi hatuna Tielemans wetu.

Angalia mechi ya Brighton Eriksen alivyoshuka mpira ulivyobadilika.
 
Chief stats zao haziwezi kuwa juu kwenye kukaba sababu most of the time wao ndio wanamiliki mpira na there is nothing to destroy when you have most of the ball na inategemea unawalinganisha,Kante hata kama sio DM but ni mchezaji muhimu kuliko Jorginho na ndio anamfanya Jorginho awe free.Assesment yangu sio kwa game ya juzi i will be back tukicheza hizi big match kama 2
 
Tunarudi pale pale kuku na yai nani katangulia, hawakabi sana sababu wana possesion, wana possesion sana midfield zao zinajua kukaa na huo mpira, ingekua wana Ndidi ama kante unafikiri wangekaa na mpira hivyo?

Concept ni hivyo hivyo kwa ETH, anacheza Possesion based football anahitaji Midfield ambazo zipo comfortable na mpira, ndio maana nikakupa mfano wa Brighton Eriksen alivyorudi nyuma, you could see tunatengeneza nini, Fdj ni much better kuliko Eriksen kwa hio role.
 
Back
Top Bottom