Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Chelsea siyo hatari lakini je wewe ni hatari kwake?
Hii game ni ya kushinda mkuu..Hatuwezi tukafungwa OT game ya kwanza ya ligi na tukakubali tu matokeo kirahisi

Vijana wapambane watupe ushindi by any means

Afterall chelsea sio hatari kama tunavyowafikiria in my opinion
 
Ole akifukuzwa United atakuja kocha mpya mwenye falsafa nyingine kabisa.

Hapo itabidi auze wachezaji wa Ole wa Pressing style atataka wachezaji wapya watakaofit kwenye style yake ya uchezaji.

Moyes alikuja na wachezaji wake.

LVG akaja na wake na mfumo wake.

Alivyokuja Mou akaja na aina yake na akataka alete wachezaji wake ndo wakashindwana na boss Ed akatimuliwa akaja Ole na akaanza kuuza wachezaji wa Mou akianza na Lukaku kisa hawafiti kwenye style yake ya uchezaji.

Kutokuwa na Technical Director ni tatizo kubwa sana pale United.
Ukweli mchungu ambao mashabiki wengi wa United hawapendi kuusikia.
 
Ningekuwa niko kwenye nafasi ya ED.

Ninapomfukuza kocha, kocha anaefuata lazima awe anatumia falsafa kama ya kocha aliyepita.

In short, unaajiri kocha anaendana na falsafa ya timu. Ndio maana si rahisi barca kumuajiri Mou kama kocha.

Van gaal aliwahi kusema ,wakati anajadiliana na uongozi wa Man u, kuhusu kupewa kibarua. Football matters hazikupewa kipaumbele.
Hili ni tatizo kubwa,
Tatizo kwa sasa ni ngumu sana kutambua falsafa ya United. Nionavyo timu inaenda tu kwa maarifa binafsi ya kocha husika. Muhimu kwa wamiliki ni kuwa kinachoendelea uwanjani hakina athari yoyote kwenye maendeleo ya biashara.
 
Kwani academy ya United imeanzishwa Fergie alipoondoka?

Haya embu niambie kuna senior players wangapi wanaowika Ulaya pale Man City tangu timu iundwe (achilia mbali, tangu 2013 Fergie alipoondoka, maana hicho si ndio kipimo chako)

Vipi kuhusu Barcelona wapo wangapi wanaowika tangu 2013?

Nirudi kwenye swali lako, kwa uchache hao ndio wanaowika Ulaya tangu SAF aondoke United kutoka United Academy

Rashford Three Lions

Scot Tominay Scotland

Tuanzebe Three Lions

Henderson Goalkeeper - Shefield Wednesday - Three Lions

Pereira - kaitwa Selecao mara moja
Januzaj anaitwa pia several times
 
Sasa Chelsea kwa tuna kikosi bora sana japo tuko underrated kwa sababu ya ban na kuondoka kwa msaliti Luiz na legendary Hazard kumefanya mujiamin Chelsea itakuwa ya kupigwa pigwa tu kama Arsenal au ninyi manure. Sisi tuna vijana wenye kiu ya kupambana na kufunga magoli mengi. Hatuna vijana mabisho kama Masho au Rashid wao wakifikisha goli kumi kwenye ligi imeisha iyooo wana relax wanasubiri msimu uishe. Nina uahakika Tammy anamaliza juu ya Auba wa arsenal kwa idadi ya magoli...

Man united 1-3 Chelsea..
Chelsea ina kikosi kizuri sana. Mafanikio yake yatategemeana na uwezo wa Lampard.
 
Sipingani na wewe mkuu shida inakuja unaachaje wachezaj wazur wakat huna replacement mfano lukaku na harrrera?

Tunajenga timu watu muhimu tunaacha wasepe binafsi naona hapo kidogo pana upungufu
Lukaku hata angebaki still angeendelea kuwa back up ya Rashford so kimpira hili ni tusi ila kiuhalisia hakuna kinachoshindikana

Romario to Ronaldinho..............Scolali
Ronaldinho to Messi...................Pep
Nestlerooy to Ronaldo/Rooney........SAF
Lukaku to Rashford up next.........Solksjær
 
Chelsea ina kikosi kizuri sana. Mafanikio yake yatategemeana na uwezo wa Lampard.
Acha mahaba

Acha ushabiki maandazi

Backup yako ya CB ni tomory, juz kacheza Zuma na christsten mmeruhusu zaid ya goli 2 kwa hiyo beki,

Willian akijitahid kwa msimu anafikishaga goli 5 , na ndio matumain yenu yapo hapo, na Jana kafikisha miaka 31 au 32 kama sikosei.

Halafu unajifariji una timu nzuri,
 
Hii manure inakufa taratibu kama Ac Milan..
United ni zile brand ziko AAA rated. Yaani zimejengwa kwenye msingi imara kiasi kwamba hata ikiwa zitapata misukosuko (kutofanya vizuri uwanjani) mingi kiasi gani haziwezi kuanguka kwa miaka mingi sana ijayo.

United inaweza enda misimu 10-20 bila kombe na bado ikaingiza pesa kuliko wanaoshinda! Ikishuka daraja usishangae umaarufu wa premiership ukapaa na ikaanza kutazamwa kuliko epl!

Sasa hapo ndipo wamiliki Glazers na kibaraka wao Ed wanapocheza. Hawataki kuumiza akili kufanya rebuild & restructuring ili timu ipate mafanikio uwanjani. Ya nini uwekeze sana ilhali pesa zitakuja hata usipowekeza?

Hivyo unaweza ona kuna mgogoro wa kimalengo baina ya mashabiki na wamiliki & management. Shabiki anataka matokeo ilhali mmiliki anataka vitabu vikae sawa.

Washindi hapo ni wamiliki ambao wamefanikiwa "kuwahadaa" mashabiki na kuwaaminisha kuwa forward line ya akina Martial-Rashy-Greenwood-Gomez-Lingard-Mata-James-Sanchez inaweza shindania ubingwa na ile ya City, Liverpool au Totenham!

Kwamba midfield ya United ya akina Andreas inaweza shindana na ile ya City na Liverpool!

Ngoja tusubiri tuone.
 
Wasiwasi wangu ni kwamba hata mid ya Chelsea itatupoteza sana leo.
 
Back
Top Bottom