Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Yani mashabiki wako bize wanalialia tuu kama vitoto vya ndege,
Nani amewaambia tunataka kufika ilipo Liverpool?

Lengo ni kufanya vizuri na kushinda mataji, wimbi la mashabiki wa timu pinzani kuja kulinganisha timu zao na timu yetu limechukua akili za wenzetu kiasi kwamba na sisi tuko bize tunalinganisha timu yetu na Liverpool, Barcelona, madrid, man city

Tunasahau kama kuna sterling wa man city hawezi kuwepo na wa man u, kwamba wacheze mchezo unaofanana, kila mtu atumie raslimali alizo nazo, mwisho wa siku tukumbuke panga na shoka vyote vina ncha kali na vinaweza kukata mwanzi ni suala la utumiaji tuu.

Kwani goli akifunga greenwood mwenye miaka 17 na akifunga sterling si bado ni goli?
Mimi nimependa hapo panga na shoka vyote vina ncha Kali na vinaweza kukata mwanzi.
 
Let's hope for the best..
hivi tatizo la Manchester United ni wachezaji wabovu au hakuna spirit fighting inakosekana wachezaji wapo so relax kwa sana. Mie naona kama watabadilika na kuja na spirit ya wakati Ole20 anaichukua team tunaweza kuwa miongoni mwa team zinazowania U champion lakini wachezaji wakicheza kwa kuwa wapo tu katika team ata aje nani ndio itakuwa hivyo hivyo
 
Unadiriki kuitaja Chelsea kama giant msimu huu

Kwanza nianze kwa kusema nashukuru kama umejua hizi game saba za mwanzo hakuna atakae pona wakiwemo chelsea,

Pili nikukumbushe tuu baada ya mechi saba hatutabadilisha kikosi, moto ni ule ule

Tukutane kesho Ollachuga Oc
Kwenye izo gemu saba iyo ya Chelsea iondoe, kipigo kipo pale pale mkuu.

Man united 1-3 Chelsea
 
Unastahili kunywa bia zangu soon
mkuu kama ni hivyo basi hakuna faida ya klabu kufanya usajili wa wachezaji kama ishu ni kuhofia young players kutoka academy hawatopata game time ya kutosha, hata huyo maguire kwa mujibu wa hoja yako ujio wake utasababisha tuanzebe na vijana wengineo kutoka academy watumie muda mwingi kukaa benchi au kucheza mechi za under 23.

nilichokuwa nakihitaji mimi ni kuona kwanza tunaziba madhaifu yetu kwa kufanya usajili wa sehemu zote zenye ufa baadae ndio tuwape nafasi vijana ila alichokifanya OGS msimu huu ni kuwabebesha mzigo wa misumari vijana wadogo wasiokuwa na uzoefu wa mapambano kwa kuwategemea wawe wazibaji wakubwa wa nyufa zetu.

nitatoa mfano mwengine wa manchester city tumeona timu yao jinsi ilivyoimarika kila eneo kiasi ambacho hata ikitokezea david silva amewekwa benchi nafasi yake inazibwa vizuri na kijana phil Foden kutoka academy.

kwa nini phil foden anacheza vizuri?
jibu ni rahisi tu ni kwamba pindi akiwa uwanjani hujikuta amezungukwa na mafundi wa mpira kila pembe jambo ambalo humpunguzia presha ya kuwa tegemeo kwenye mechi husika.

lakini ukija kwetu sisi unapomuanzisha angel gomez au greenwood kwenye kikosi kinachoundwa na dead players mfano wa ashley young, fred,jones, perreira, matic na wengineo wanajikuta wanabeba mzigo mkubwa sana wa matumaini ya kuwa wabebaji wakubwa wa timu kimatokeo.

nikatoa mfano wa barcelona nyakati ambazo kwa muda tofauti wanawakuza kisoka sergio bosquets, messi, gerrard pique,pedro, sergio roberto, thiago alcantara, cristian tello, bojan krkik na wengineo hawakuwabebesha majukumu sana kwa sababu walikuwepo wachezaji watakaowafanya ile presha ya kuibeba timu isiwepo kwenye mabega yao.
yupo henry, etoo, gaucho, deco,guily, abidal, toure, puyol, marquiz,xavi, iniesta, david villa, zambrotta, dani alves,alba na wengineo kwa nini usiufarihie mpira wako?

kama ni young players kwa nini usiufurahie mpira wako kwenye timu inayozungukwa na kevin debruyne, gundogan,aguero, sane, sterling, silva double, concelo, mendy,otamendi, walker, aguero?

kama ni young player kwa nini usiufurahie mpira wako kwenye timu inayoundwa na roy keane, rooney, scholes, giggs, ferdinad, vidic, evra, nistelrooy na wengineo?
 
Kwa lingard labda. Maana ni wa hovyo sana..
Ndio maana hata kikos cha kwanza hana number.

Ila martial sidhani. Kipind amekuja alikuwa akicheza kama striker.. na alikuwa effective akiwa CF.. kiwango kilishuka aliporudihwa winga ya kushoto.

Martial bado ana kitu na umri unaruhusu. Ambao siwaamini ni lingard na rushford. Hawa hamna kitu
Lukaku ni faita sana sasa hao watoto mchele mchele lingad na Masho watamfukuzisha Ole kazi mapema..
 
Aman iwe nanyi wapendwa

Man u ndo inaenda kuwa pombe ya ngoman musimu

Kila mtu atakuwa anajichotea tu

Saiz wamejificha kwenye mgongo wa Chelsea


LONDON BOY
Ukikaa kimya na kusubiri itakuwa heri kwako, mengine haya utakuja kuaibika siku moja ukose pa kushika. Mpira uache uitwe kwa jina lake maana haukosi maajabu kila siku.
 
Naona washabiki wa Manchester united tumegeuka kuwa watabiri
Maneno kama,
*kwa kikosi chetu hatuendi popote
*kocha hatafika january
*hatutashinda kombe kwa kumtengemea rashford
*tutafungwa hadi na watford
*tutamkumbuka mourinho
*tutaishia kugombania top four
Yamesikika sana.


Kwangu hali ni tofauti, ninaamini katika teamwork na nimejipanga kuwashuhudia vijana wetu wakisakata kabumbu kwa moyo wao wote, ninaipenda timu yangu
GGMU
Tuko pamoja mkuu, niliwahi kushabikia Man U iliyokuwa ikimtegemea Striker Chadwick sembuse hii ya Rashford na Martial?
 
Back
Top Bottom