Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ivi kweli tumeshindwa kuwa na DOF au glazers na ed lao moja kutuulia timu then wasepe....
Glazers hawawezi ruhusu DOF. Wakiajiri basi watahakikisha anakuwa puppet asiye na meno kama wale akina Neville au Rio na wapuuzi wengine wa the class of 92 ili tu kuwaridhisha mashabiki na investors wengine.

Hofu yao kubwa ni kuwa wakiwa DOF anayejielewa watashindwa kudhibiti spending hasa kwenye short run. DOF anayejitambua hawezi ruhusu timu iwe na Mata/Lingard kama RW tegemezi ilhali washindani wana Mahrez/Sterling/B.Silva kwenye eneo hilo.
 
Acha mahaba

Acha ushabiki maandazi

Backup yako ya CB ni tomory, juz kacheza Zuma na christsten mmeruhusu zaid ya goli 2 kwa hiyo beki,

Willian akijitahid kwa msimu anafikishaga goli 5 , na ndio matumain yenu yapo hapo, na Jana kafikisha miaka 31 au 32 kama sikosei.

Halafu unajifariji una timu nzuri,
Tumia akili magoli 5 ya Willian yamempa Europa na EPL 3rd runner ,magoli 25+ ya Auba na 17+ ya Lacazette yamewapa nini Arsenal ? Watu wengine mkashabikie mapishi .
 
Usiwe mwingi wa hofu mkuu. Ingawaje hakuna binadamu asiyekosea, tuamini maamuzi yaliyofikiwa na Menejimenti ya United kuhusu usajili ni sahihi na yalizingatia maslahi ya club. Ni wataalam kuliko ss na wanazo zana za ku-facilitate maamuzi wanayofanya kuliko sisi.
Yes ni wataalam kuliko sisi (ukimtoa Woodward) lakini vipi kuhusu malengo yao. Umejiuliza kwa nini United hawajamchukua Bruno ilhali ilikuwa dhahiri kuwa wanahitaji mchezaji wa aina yake? Sababu siyo kuwa hawajui bali kuwa hawajali kuhusu maendeleo ya uwanjani. Kocha anajua ila kwa kuwa kapewa kazi ya ndoto yake akiwa hastahili anabaki kuwa puppet wa management na wachezaji mastaa.
 
Mkuu soka limebadilika sasa. Sahau enzi za Fergie ambapo ushindani ulikuwa mdogo hivyo hao kinda wangepata play time ya kutosha. Unajua ni kwa nini City walimpoteza Sancho. Tazama sakata la dogo Odoi wa Chelsea.

Tatizo jingine United inaendeshwa kwa hisia na sio utaalamu. January iliyopita ilikuwa Gomez, Greenwood, Garner na Chong watafutiwe timu ndogo ambako watapata playtime ya kutosha kama ilivyokuwa kwa Tuanzebe.

That way baada ya misimu miwili unakuwa na Gomez anayeweza kuvaa jezi namba 10 na kupewa mikoba. JM alisema kuwa hao madogo hawawezi develop kwa kuingia uwanjani dk ya 85 au 88. Wanahitaji dk nyingi ambazo pale hawawezi pata. Unacheza na Wolves au Everton na unaongoza 1-0 ni dk ya 70 ila bado hujaua mchezo. Unawaingizaje hao kinda?

Enzi za Fergie ilikuwa rahisi. Nakumbuka ujio wa Ronaldo. Kuna mechi ya City tuko dk ya 72 (3-1) na tumekwisha ua mchezo. Dk 20 kila mchezo zilitosha kumkomaza kwa kipindi kifupi akaivaa vyema no 7.

Sasa alipoingia OGS kaja na mihemuko kuwa kuwapeleka hao kinda kwa mkopo ni kuwatenga na utamaduni wetu wa academy! Kila mmoja kacheza dk ngapi kwa nusu ya msimu iliyofuatia baada ya kufuta zile loan program?

Kwa kifupi United ina safari ndefu sana na hawa Glazers.

Mkuu huwezi kuwa na sera ya Galacticos halafu ukaweza ku apply na sera ya kutumia wachezaji kutoka academy wakang'ara

Mfano Chong atang'ara vipi ukimletea Pepe (japo mimi pia nilitamani aje), Greenwood atapata vipi playing time ukimletea Lukaku mwingine, Gomes atang'ara vipi ukimletea Griezeman

Diego Dalot mwenyewe tulikuwa hatutaki aletewe Wan Bissaka kwa sababu hizo hizo

Angalia Madrid kwa miaka 10 hii, kuna makinda hata 5 wametokea academy yao na sasa wanang'ara duniani? Labda unikumbushe.

Ndio maana nasema huwezi kuwa na vyote viwili kwa wakati mmoja, kusaini wachezaji wakubwa 5 au 6 kwa wakati mmoja na wakati huo huo kuendeleza vipaji kutoka academy.

Mimi binafsi sikumbuki ni lini mara ya mwisho SAF alisajili wachezaji 4 wakubwa kwa mkupuo. Akijitahidi sana ni wawili halafu anaongezea na potential mmoja au wawili kisha maisha yanaendelea.
 
mkuu kama ni hivyo basi hakuna faida ya klabu kufanya usajili wa wachezaji kama ishu ni kuhofia young players kutoka academy hawatopata game time ya kutosha, hata huyo maguire kwa mujibu wa hoja yako ujio wake utasababisha tuanzebe na vijana wengineo kutoka academy watumie muda mwingi kukaa benchi au kucheza mechi za under 23.

nilichokuwa nakihitaji mimi ni kuona kwanza tunaziba madhaifu yetu kwa kufanya usajili wa sehemu zote zenye ufa baadae ndio tuwape nafasi vijana ila alichokifanya OGS msimu huu ni kuwabebesha mzigo wa misumari vijana wadogo wasiokuwa na uzoefu wa mapambano kwa kuwategemea wawe wazibaji wakubwa wa nyufa zetu.

nitatoa mfano mwengine wa manchester city tumeona timu yao jinsi ilivyoimarika kila eneo kiasi ambacho hata ikitokezea david silva amewekwa benchi nafasi yake inazibwa vizuri na kijana phil Foden kutoka academy.

kwa nini phil foden anacheza vizuri?
jibu ni rahisi tu ni kwamba pindi akiwa uwanjani hujikuta amezungukwa na mafundi wa mpira kila pembe jambo ambalo humpunguzia presha ya kuwa tegemeo kwenye mechi husika.

lakini ukija kwetu sisi unapomuanzisha angel gomez au greenwood kwenye kikosi kinachoundwa na dead players mfano wa ashley young, fred,jones, perreira, matic na wengineo wanajikuta wanabeba mzigo mkubwa sana wa matumaini ya kuwa wabebaji wakubwa wa timu kimatokeo.

nikatoa mfano wa barcelona nyakati ambazo kwa muda tofauti wanawakuza kisoka sergio bosquets, messi, gerrard pique,pedro, sergio roberto, thiago alcantara, cristian tello, bojan krkik na wengineo hawakuwabebesha majukumu sana kwa sababu walikuwepo wachezaji watakaowafanya ile presha ya kuibeba timu isiwepo kwenye mabega yao.
yupo henry, etoo, gaucho, deco,guily, abidal, toure, puyol, marquiz,xavi, iniesta, david villa, zambrotta, dani alves,alba na wengineo kwa nini usiufarihie mpira wako?

kama ni young players kwa nini usiufurahie mpira wako kwenye timu inayozungukwa na kevin debruyne, gundogan,aguero, sane, sterling, silva double, concelo, mendy,otamendi, walker, aguero?

kama ni young player kwa nini usiufurahie mpira wako kwenye timu inayoundwa na roy keane, rooney, scholes, giggs, ferdinad, vidic, evra, nistelrooy na wengineo?
Very good view.
 
Acha mahaba

Acha ushabiki maandazi

Backup yako ya CB ni tomory, juz kacheza Zuma na christsten mmeruhusu zaid ya goli 2 kwa hiyo beki,

Willian akijitahid kwa msimu anafikishaga goli 5 , na ndio matumain yenu yapo hapo, na Jana kafikisha miaka 31 au 32 kama sikosei.

Halafu unajifariji una timu nzuri,
Utakuwa umechanganya ma-file mkuu. Pia chunga lugha unayotumia. Nimetumia lugha rahisi tu kufikisha maoni yangu. Nawezaje kuwa na mahaba na timu nisiyoishabikia. Narudia. Chelsea wana kikosi kizuri na wala hawawezi singizia ban endapo watashindwa kupata matokeo. Mafanikio yao yatategemeana na uwezo wa kocha.
 
Mm nakwambia sasa wana kikosi kibovu
 
Hii game ni ya kushinda mkuu..Hatuwezi tukafungwa OT game ya kwanza ya ligi na tukakubali tu matokeo kirahisi

Vijana wapambane watupe ushindi by any means

Afterall chelsea sio hatari kama tunavyowafikiria in my opinion
Record zinaonyesha man u hupata matokeo kwa mbinde sana akicheza na chelsea.

Hata Leo kuna uwezekano mkubwa wa sare
 
Wakuu Mimi msimu huu nimeanza kabisa mazoezi ya kujiandaa kisaikolojia kupokea chochote kitakachokuja upande wetu man u,mpango wa kuumia na kukondeana kisa man u kafungwa naupinga kwa nguvu zote msimu maana hata sielewi kinaenda kutokea nini.so tukifungwa sawa tukishinda poa tukitoa drop mukide maana huwa naumiaga Sana aisee man u akipigwa au akicheza hovyo hovyo.tatizo langu nimeanzaga kushabikia man u enzi zile za miaka ya tisini mwanzoni wakati tunajenga himaya yetu kiasi kwamba ilikuwa ni kichekesho eti tunaanza msimu tukifikiria top four,hizo zilikuwaga ndoto za wanaotawala epl kwa Sasa...ndio hivyo kibao Cha matangazo kimegeuka juu chini ni muda Sasa umefika kuukubali ukweli huo mchungu,though I still hope haitakuwa kwa miaka mingi Kama livafool walivyosota coz natarajia Kuna siku wakati bado naishi nitazishuhudia siku za furaha Kama wakati ule.sasa itabidi tuanze kwenda kuangalia mechi tukiwa na vidonge vya kutuliza maumivu kwa sababu kiukweli kabisa siwezi kuishi bila kuangalia mechi za man u!!!unaweza kuniona bwege lakini jamani eeeh kila binadamu ana ulevi wake ujue,wangu mie ni soka na timu mbili zinazonilazaga njaa zikikwama ni Simba na man u!!
I still hope for the best msimu huu,nitasimama pamoja na man u till the end.
 
Kwa sasa shabiki anayepata taabu ni yule aliyeishabikia timu iliyokuwa na "responsibility" ya ushindi. Kama ulivyosema, ni vema ku-lower expectations vinginevyo United kwa sasa ni miongoni mwa vile vitu vinaweza mpa mtumiaji maradhi kama vile ya moyo.
 
Ni timu pekee ambayo aijasajili epl. While timu zingine zimekuwa zikifanya upgrades.. chelsea imefanya offload. So huwez kusema wana kikos kipana wkt wamepunguza wachezaji.
Gemu hii ya leo naiona chelsea ik struggle kwenye ushambuliaji na defence.. lakin pia kwa man u iki struggle eneo la katikati na mbele.

Ila kujib hoja yako. Chelsea hawana kikosi kipana kwa sasa.

Back
Top Bottom