Mkuu I feel your pain, but I also try to understand the fact
Kwa upande wa beki ni ukweli usiopingika tumejiimarisha msimu huu, ni kweli tulitamani Shaw awe na compitition na back up pindi akiumia lakini huwezi kusajili timu nzima katika msimu mmoja.
Back four ya Wan Bissaka/Dalot, Tuanzebe/Lindelof, Maguire, na Shaw sio mbaya kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha. Ni timu ngapi zenye subs za beki kama Smalling, Bailly na Rojo aliye mzima bila majeraha? Ni chache sana.
Lingard. Kabla hatujamuhukumu, tunapaswa kujiuliza kwanini pale Three Lions lazima apate namba piga uwa. Hiyo ni ishara kuwa ana kitu flani. Lakini nikukumbushe kwa United hana uhakika wa namba.
Tatizo kwa usajili wa msimu huu ninaloliona ni kuongeza angalau mid fielders wawili, defensive 1 na creative 1. Pia tulipaswa ku replace magoli ya Lukaku kwani Rashford hana uwezo, ila Sanchez mzima anaweza kutufungia magoli kama false number 9 na Martial akiaminiwa (kama ilivyokuwa msimu wake wa kwanza United) anaweza kufunga magoli. Namuunga mkono Lukaku kuondoa, United fans hatukumuonesha upendo kabisa.
Kwa mtazamo wangu hata Lukaku angebaki bado asingetusaidia kwani kocha hampi nafasi. Hivyo ni bora tu alivyoondoka. Angebaki ni wale watoto wangeendelea kuanza, ameondoka bado ni hao watoto wataendelea kupata namba, kwa hiyo mbadala au bila mbadala ninaona ni yale yale
Kuna watu walitamani tuwaondoe wachezaji wote tusiowataka. Rojo, Jones, Lingard, Sanchez, Smalling, Young, Mata, Lukaku, Matic na wengine,wote waondoke. Je tungesafisha timu nzima?Je tungepata wanunuzi kwa bei tunayotaka? Kumbuka mashabiki huwa tunataka quick fix, je unajua wamiliki nao wanataka hela? Hata ungekuwa wewe ndio mmiliki ungewaondoa tu ili uwaondoe bila kujali hasara?
Je kwa soko la sasa hao wachezaji wote unawa replace vipi? Muda unao wa kuwa replace dirisha lenyewe ni fupi, tuchukulie una muda. Kwa soko la sasa una hela ya kuwa replace hao wachezaji?
Utasema hela ya kuwauza akina Lingard, sasa ukiwa desperate utawauza kwa hasara je hela ya kuwauza wote hao utapata hela ya kununua hata wachezaji wawili wenye kiwango ukitakacho? Na kumbuka hapa utatakiwa ununue wachezaji wa kujaza squad sio unaondoa 8 unaleta wawili au watatu.
Kuna maswali mengi kuliko majibu. Nakubaliana na wewe kuna shida kwenye hierarchy ya United, lakini kuna mambo tunayakuza sana.
Mfano, kuna baadhi yetu tunamlaumu OGS kwenye usajili, je ni kweli OGS hakumtaka BF au hakumtaka winger wa kulia. Tunapenda sana kulaumu.
Ed Woodward ni shida, hilo halina ubishi, Glazers ni shida, hilo halina ubishi, Board ni shida hilo halina ubishi. Wote hao wanaangaalia zaidi commercial aspect pale klabuni kuliko football aspect.
Angalau tukipata Sporting Director tunaweza kufanya vizuri zaidi kwenye madirisha ya usajili yajayo.