msimu uliopita marcus rashford na antony martial kwa pamoja wamefunga magoli 20 kwenye ligi kuu ya uingereza kama nitakuwa nipo sahihi.
ili tusolve tatizo la ushambuliaji mabwana hao wawili watalazimika kutufungia magoli takribani 40 kwenye mechi 38.
je uwezo huo wanao?
naomba tuzungumze mambo ya soka tukiweka mbele uhalisia na si matumaini ya uongo ya kumpa ahueni mgonjwa mahututi aliyebakisha nusu saa kabla hajakata roho.
nilisema na nitaendelea kusema timu yetu tulipaswa kwanza tuongeze mshambuliaji mwengine atakeyetufanya tuwe na safu kali ya ushambuliaji kama waliokuwanayo liverpool au man city, tulichokifanya sisi ni kumuondolea mgonjwa kifaa kilicho chakaa cha kumsaidia kupumua bila ya kuwa na mipango ya kutafuta kifaa chengine.
sielewi kwa nini timu tajiri kama manchester united wanazidiwa na klabu ya arsenal kwenye harakati za usajili wa mchezaji hodari kama pepe, jamani huyu pepe alipaswa aje manchester united ili aongeze nguvu safu ya ushambuliaji na si arsenal. nyakati za SAF nimewahi kushuhudia timu yetu ikiwa na washambuliaji wanne mahiri kwa miongo miwili tofuti, sielewi kwa nini nyakati hizi imekuwa ngumu.
andy cole + dwight yorke + sheringham + solskjaer
nistelrooy + rooney + saha
rooney + tevez + berbatov + ronaldo
rvp + rooney + hernandez
leo hii tunaianza ligi tukiwa na mshambuliaji asiyekuwa na uhakika wa kufunga magoli 20 kwa msimu halafu kuna wadau wanajipa matumani ya uongo eti tutafanya vizuri.
kuna wadau wameshukuru kuondoka kwa lukaku huku wengine wakimdhihaki kwa sababu ya mwili wake kuwa na uzito mkubwa akiwemo gary neville, lukaku huyu mzito mwenye kg 300 ana uhakika wa kukupa magoli 20 kwa msimu haijalishi timu ipo kwenye kiwango kibovu kama ilivyokuwa msimu uliopita.
kupitia kurasa hii mutakuja kumuomba radhi romelu lukaku kwa aibu na fedheha itakayowakumba.
mume wetu wa soka wolverhampton anatusalimia