Maana hata sky sports au BBC au whatever sio kila taarifa zao zina ukwelii zingne zinakuwaga tetesi tu
 
Uchambuzi mzuri.Lakini swali ni je,kipi kilichomuondoa Real Madrid na pia Bayern Munich? (Kote huko hakujiuzulu ila mbinu zake zilioneka kufikia ukomo?)

dah maswali magumu kama haya yatanifanya niikimbie hii thread rafiki yangu.
kama nilivyoandika maoni yangu kwenye comment zangu za nyuma ni kwamba mpira wa siku hizi umevamiwa na wanyanganyi na matajiri wanaojifanya wanapenda soka lakini kumbe ni wachache wanaofahamu mchezo wa soka.
cha ajabu hawa matajiri kwa kiasi kikubwa hawataki kusikia msamiati wa kukosa hivyo basi kila mwaka wanataka kusikia neno kufanikiwa ndio maana tunashuhudia makocha wengi wanashindwa kudumu kwenye timu angalau kwa miaka 4.

kwa uoni wangu finyu kwa sababu sijakamilika inapotokezea kocha amefanya vibaya kwa msimu mmoja lakini ndani ya msimu huo akaonyesha maendeleo japo kwa 60% basi anastahili kupewa nafasi nyengine msimu unaofuata. Mbinu hii ndio ilisababisha sir alex ferguson adumu kwa muda mrefu kwenye klabu licha ya kwamba kuna vipindi tofauti alifikisha miaka 3 bila ya kupata ubingwa wa ligi kuu na pia kuishia kutolewa robo fainal kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kwa kipindi kirefu, jaribu kurejea msimu wa 2003, 2004, 2005. Bahati mbaya sana utamaduni huu wa kuwavumilia makocha walioleta maendeleo kwenye klabu kwa 60% ndani ya msimu mmoja umeshaondoka na hautakiwi tena na tajiri yoyote, hautakiwi tena na legends yoyote na pia hautakiwi tena na shabiki na mdau yoyote yule.kadri siku zinavyosogea Inakuwa ni vigumu kumvumilia kocha ajenge timu kwa miaka 3 wakati huku jirani yako anajenga timu kwa mwaka mmoja.

labda tuanzie tena kwa jose felix mourinho na hapa niwe mkweli mimi ni miongoni mwa watu ambao nilijawa na imani kubwa sana na jose mourinho ya kwamba atatufikisha kwenye nchi ya ahadi na kilichonifanya niamini zaidi ni yale maendeleo yake ya msimu wa kwanza aliyoyaleta kwenye klabu licha ya kwamba tuliishia nafasi ya 6 lakini alitupa makombe mawili muhimu na bila ya kusahau timu ilionyesha ukomavu wa hali ya juu husuani roundi ya pili ya ligi kuu ukilinganisha na kipindi cha makocha waliopita. Hivyo basi nikajenga imani ya kwamba msimu wake wa pili ataikamilisha 40% iliyobakia kama alivyofanya jirani yake josep guardiola, nikumbushe tu klabu ilimpa mahitaji yake ya wachezaji aliowataka kwenye maeneo yaliyohitaji mabadiliko kama vile nafasi ya kiungo wa ulinzi, mshambuliaji, mlinzi wa kati. Kosa kubwa walilolifanya klabu ni kutokumpatia huduma ya ivan perisic kwenye dirisha la usajili lakini kwenye dirisha dogo ed woodward alifuta makosa yake baada ya kumsajili alex sanchez, kwa maoni yangu msimu uliopita jose mourinho alifikisha 80% ya ujengaji wa timu.
msimu huu wa pili kilichoniumiza ni kuona baada ya henrik mkhitaryan perforamance yake kupwaya hususan kuanzia mwezi wa 10 jose mourinho hakutumia nguvu kubwa sana kwa ajili ya kumjengea kujiamini mkhitaryan.

ed woodward pengine hakucheza mpira lakini na yeye ana uelewa wa mpira hivyo basi alipo ona klabu imefikia level nzuri sana uwanjani hakuona umuhimu mkubwa wa kutumia tena zaidi ya pound millioni 100 kwa ajili ya biashara ya wachezaji na ndio maana aliamua kumuongeza mlinzi diogo dalot na fred kwenye kiungo. Huyu fred hakuja kuziba pengo la michael carrick kama wengi wetu tunavyojiaminisha kwa sababu msimu uliopita michael carrick hakuleta athari yoyote ndani ya uwanja. Kinachoumiza msimu huu baada ya kuziba ile 20% iliobakia matokeo yake tumepunguza tena 40%, ina maana mpaka dakika hii jose mourinho katurudisha tena zama za david moyes kwa hoja dhaifu eti hajapewa fungu la kutosha la usajili.

Tukirudi kwenye ishu ya carlo ancelotti siamini kama kufukuzwa kwake bayern munich, real madrid na chelsea kuna uhusiano wowote na kuishiwa mbinu za ufundishaji ila ni uvumilivu mdogo waliokuwa nao mabosi wake.
  1. msimu wake wa kwanza na chelsea (2009-2010) aliwapa ubingwa kwa tofauti ya pointi 1 dhidi ya manchester united na alitolewa kwenye hatua ya 16 bora na klabu ya inter milan ya jose mourinho baada ya kufungwa 3-1 aggregate.Inter milan hii ya mourinho ndiyo ilimfunga barcelona ya guardiola magoli 3-2 na kubeba ubingwa mbele ya bayern munich ya luis van gaal hivyo basi bila ya shaka chelsea walitolewa na timu bora.kwenye ligi chesea walivunja rekodi ya tottenham hotspurs ya kufunga magoli mengi (103), vile vile chelsea walibeba ubingwa wa FA baada ya kuwafunga portsmouth. msimu wa 2010–11 chelsea walimaliza ligi wakiwa nafasi ya pili nyuma ya manchester united na pia walitolewa robo final ya ligi ya mabingwa dhidi ya manchester united. pia kuna mabadiliko mengi yaliochochea chelsea kuwa na msimu usioridhisha ukilinganisha na msimu uliopita kwa mfano kuondoka kwa ricardo carvalho ambaye alikuwa ni nguzo ya ulinzi, michael ballack, belletti na pia kuondoka kwa mwalimu Ray Wilkins na nafasi yake kuzibwa na michael emenalo, ujio wa fernando torres nao ulizidisha presha kwa mwalimu kutoka kwa tajiri ambaye asingelikubali kuona fernando torres aliyemnunua kwa pound millioni 50 anakaa benchi na kwa ushahidi wa hilo rejea mgogoro wa mourinho na abramovich kuhusiana na usajili wa andrey shevchenko. Japokuwa walifanya biashara ya usajili kwa wachezaji kama nemanja matic, david luiz, yossi benayoun na ramirez kivyovyote walihitaji muda ili waweze kuendana na mazingira mapya lakini tajiri hakutaka kusikia chochote licha ya kwamba carlo alifikia malengo japo kwa 60%, ndio ubaya wa matajiri wa mpira ukiwaonjesha utamu wa ushindi wanasahau matokeo mengine ya mpira.
  2. msimu wake wa kwanza na real madrid(2013-2014) aliwaongeza wachezaji kama vile isco alcaron, gareth bale na illaramendi na pia tulishuhudia kuondoka kwa gonzalo higuain. Madrid walibeba ubingwa wa copa dela rey, champions league ambapo kwa mara ya mwisho kwa madrid kubeba ubingwa huo ilikuwa ni mwaka 2002 chini ya vicente del bosque. Msimu wake wa pili alishinda club world cup, uefa super cup pia walitolewa nusu final na juventus, haukuwa msimu mzuri sana na hili lilichangiwa zaidi kwa kuondoka key players kama angel dimaria, morata na xabi alonso. Tajiri anapoamua kuwaondoa key player kwa ajili ya kutaka wachezaji anaowataka yeye wapewe nafasi kivyovyote patazaliwa tatizo na ndicho kilichoikuta real madrid baada ya kuondoka kwa watu hao wawili, palihitajika muda wa kutosha ili new comer kama toni kroos, gareth bale waendane na falsafa ya mwalimu ila ndio hivyo tajiri ukisahaanza kumuonjuesha raha ya ushindi husahau madhila ya kufungwa. perez alizungumza maneno yafuatayo siku ya kutangaza maamuzi ya kumuondoa ancelotti (Ancelotti had won the hearts of both the board and fans, and would always have a place in the club's history because he was the coach that led them to the Décima. "However at this club the demands are huge and we need a new impulse in order to win trophies and be at our best)
  3. kwa ufupi msimu wake wa pili bayern munich alifukuzwa baada ya kupoteza nguvu ya ushawishi kwa wachezaji muhimu kama robben, ribery, muller kwa kisingizio cha kuwa na falsafa mbovu za ufundishaji. licha ya kuwa timu haikuanza vizuri lakini hapakuwa na sababu ya msingi sana kumfukuza mwezi oktoba japokuwa alifungwa magoli 3 na PSG hii ya mbappe,neymar na cavani, Suali la kujiuliza je tokea aondoke carlo ancelotti hao kina robben, ribery, muller, boateng viwango vyao vimeongezeka?
Kama sir alex ferguson amewahi kukaa miaka 3 bila ubingwa kwa nini iwe ajabu kwa carlo ancelotti kukaa mwaka mmoja tu bila ya ubingwa?
1538740471177.png
 
Home hakuingiliki sa hivi...


From Hero to Nothing...

At the end kwa kua mioyo yetu ipo hapa tuendelee kuipenda timu yetu tu..
Kama in mabadiliko Utd inahitaji mabadiliko makubwa sana...

Hata manager anatakiwa abadilike.. CV doesn't matter kwa wakati huu..
Kitendo cha kumnunua Mkhi, Bailly, Pogba, Alexis na kushindwa kuwa-manage bado anafaa kweli???

Katika ulimwengu huu Wa soka LA kutaka mafanikio kila timu inafanya inachoweza kuleta mafanikio..

Mashabiki hatuna cha kujifariji kama Utd itabak kua Simba Wa kuchora uwanjani ili hali Forbers wanaongoza..

Madrid toka 2011 wamepta kina Jose, Carlo, Rafa na Zidane

Barca wamepta kina Pep, Tito, Martino, Lucho

Munchen wamepta kna LvG, Jupp, Pep, Carlo, Jupp tena

Kwa nini? Kwa sababu wanahitaji mafanikio..
Mbali ya waliostaafu au kumalza mkataba kama Pep, Lucho, na Jupp wengi hawakufikia malengo ndo maana wakaondoka au kuondolewa
Except Tito(RIP) na Zidane alijiondoa.

Why not Utd wakati tunahitaj mafanikio?

Kama ni kusajili sidhani kama Utd hawawezi kuleta hao anaowahtaji.. Swali ni Je ataweza kuwatumia?? Mani kamleta Mkhi, Pogba, Lukaku. Alex's and co??

Spurs hawana usajili Wa kutisha ila bado wanasimama na kina Barca, sisi je?

Kwa mini Ed alimleta Pogba, Matic and co. Then akamshindwa Toby?? kna swali hapa?

Kocha unamtaka nani kujenga timu?
Jerome Boateng... Really??

Sometime CV isn't enough..
Katika hili Jose ana wapnzan wachache..

To me Legends wapo sahihi,, na kama sikosei ni wachambuzi wale.. Mbna hata Sourness sio Mancunian ila kaongea?..

Si kosa mwanadamu kusema ukweli..
Macho ya wengi yalitazama mechi ya Juzi..
Utd is finished.. He hali ibaki hivi au mabadiliko? Ndio kitendawili.. Tunawaachia wenye mamlaka..

I'm nothing hata kiatu chake sina nafasi ya kukiosha ila kwa kua nina Uhuru wa kuchangia,, JM is finished.. hasa katika Man Management..
Mo Salah ypo Slow kwa sasa ila Jurgen Simwon katka media akiwaponda..

Nani akupiganie wakati kila siku unamsimanga?

Rio
Schools
Neville and co.
Wanataka mafanikio ya Utd ndio Furaha yao.. Otherwise wangekua wanafurahi now kama kina Jamie Carragher.

GGMU
Umeongea facts hadi nasubiria nione Pro Mourinho Wa kwanza kukupinga.
 
Hahahah this is madness.. Leo hii tunalaumu legends kina Rio, Scholes n Co kisa kumkosoa Mourinho? Like Mourinho is too perfect kukosolewa or what?? Eti mtu unafikia kusema 'u-jobless' unawasumbua.?! Hahah

Hata kama tunataka kutoa support kwa Mourinho, hiyo sawa ila mwisho wa siku yeye anachangia asilimia kubwa katika hii situation iliyopo Utd.

Wakati Scholes anamkosoa Pogba huku Mourinho anamtetea tuliona sawa, ila sasa hivi akimkosoa Mourinho eti ni 'jobless' guy anapiga tarumbeta.
Kuna watu hata ukae uwafikirie vipi huwezi pata jibu humu.
 
Waje kufanya nini?

Utetezi ni mmoja tu, Mou hakupewa wachezaji anaowataka.
Tatizo la morinho anapenda kuendesha wachezaji kama anavotaka yeye kitu ambacho ni kigumu. Ndo maana anagombana nao, na mfumo wake wa ku defence hata kwa vutimu vidogo
 
Back
Top Bottom