Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Guys kuna raha kua Mwanamke na raha ya Mwanamke kuhudumiwa,
acheni sasa niwaambie mimi ni yule mwanamke hata nikipata mshahara sasa hivi, bado nitapiga simu kwa kaka zangu (wananipenda sana lastborn wao) wanitumie hela ya chips au icecream,
Siwezi kwenda lunch na kuna wanaume halafu mimi nilipe bill hata kama ni yangu, hapana nitatulia tuliii wanaume walipie,😐

Kuna siku ilikua lunch na co-workers sasa bill ilivyofika mdada mmoja naona anafungua wallet weeh acha nimpige kofi la bega, akashtuka nikamwambia "tulia ufurahie uanamke wako" akacheka akaweka wallet chini,🙃

Tukija nyumbani ndio kabisaaaa siwezi kubeba majukumu ya kununua chakula na kulipa bills, nope! labda kununua vitu vidogo vidogo kama chumvi na viberiti au snacks zangu, lol

Haya mambo ya 50/50 yaishie kwenye mabiashara hukooo ila kwenye mahusiano hapana jamani kila mtu asimamie majukumu yake yanayomuhusu, mimi jukumu langu ni kuleta utulivu, nuru na amani nyumbani,
Mtauliza sasa wewe mshahara wako unaufanyia nini sawa nitajibu, nanunua vitu vidogo vidogo kama mapambo ya ndani, kufix issues ndogo ndogo zitakazojitokeza na kuspend kwenye mambo yangu,🥰 wanawake tuna vitu vingi jamani na pesa kwetu haijawahi kutosha,😂

Ewe mwanamke unayejiita mwanamke wa shoka, unayevuja jasho na damu ili kuhudumia familia kwanza nakupongeza sana ila kama ukipata nafasi ya kufanyiwa jiachie ufanyiwe, Mwanamke ni pambo la dunia, kaumbiwa kutunzwa, kudekezwa, kupendwa, kubembelezwa, mwanamke anatakiwa awe laini laini sio wanaume wapo wewe mwanamke unabeba ngazi unaparamia ukuta kuweka umeme au unapanda kwenye stuli kufunga kamba za nguo jamani mtakuja kutenguka nyonga mshindwe kutoa raha kwa my zenu,🙄

Binafsi hizo 50/50 zenu pelekeni hukoooooooo mimi ni old school naelewa uanamke wangu unathamani kiasi gani.
Tchaooooo
K

Kimsingi hiyo kitu HAIWEZEKANI. Sababu yangu ni moja tu; Utofauti wa mwanaume na mwanamke KIBAIOLOJIA ndio unaoondoa uwezekano wa kuwa sawa. Labda tuanze upya wote tuwe wanawake au wanaume.
 
Ungemchunguza vizuri pesa zake anapeleka wapi, labda alikuwa anafanya ujenzi wa nyumba yenu ya kuishi au anajipanga kununua gari msiteseke kwenye dalaladala na boda.
Wanaume mnajifanyaga mko positive sana mambo yakiwa upande wenu ila sio kwa sisi mnatuita majina ya kipuuzi tu!
 
Mke ni "Mindset", ukikosa mwanamke anaekuhurumia na kukusaidia, basi unakuwa na bahati mbaya sana kwenye life. 😊
Hakuna kanuni ya kuishi watu wawili, ila kuna namna ya kuishi watu wawili. Mindset za wanawake hazifanani; Mindset za wanaume pia hazifanani.
Wanawake wana vitu vinashabihiana, ila hawapo sawa.
Wapo watu wametengeneza utajiri, kupitia hao hao wanawake, wapo watu wamekuwa masikini wa kutupwa kupitia hao hao wanawake. Yupo mwanamke anataka kuwezeshwa akupunguzie majukumu, yupo mwingine anawaza kukuibia. 😊
Well said brother! Hapo umenena vyema! Basi kuanzia leo waelimishe vijana kuwa wanawake hawafanani, wapunguze zile mada za mwanamke this mwanamke that😁
 
J
Sijajua boyfriend wako ni wa hadhi gani, kama ni tajiri au mwenye access ya pesa za walipa kodi wavuja jasho inaweza kuwa sawa wewe kudoea pesa zake ila kama ni mpambanaji anayejitafuta sio sawa kumpa mzigo wa wazazi wako wa kukulea.
Umesahau kwamba Jf Kila mtu ana standard Kila mtu tajiri Kila mtu anakula KFC Kila mtu ana nyumba Kali na ana gari Kali

Kwa ground waweza kukuta hata huyo mwanaume tu wa kumjulia Hali asubuhi mchana na usiku Hana 🤣🤣😄
 
Alikua ana madeni ikiwemo kazini.
Akanihadithia chanzo cha madeni ni mshahara wake hautoshi sababu analipa mkopo aliouchukua huko nyuma 35M

Nikamuuliza uliufanyia nini akaniambia aligawanya nusu kwa nusu na ex gf wake
Hela yake yeye akamlipia ada mdogo wake nyingine akanunua gari.

Binafsi niliona hanifahi! Kama anakopa pesa kwa ajili ya kumfurahisha mwanamke na kununua gari
Ungekuwa wewe ni huyo ex girlfriend wake halafu akupe 10m ungeuliza imetoka wapi?
Au sasa hivi upewe 17m ya biashara na mtu wako utaikataa kama amekopa?
 
Nikisemaga kumsomesha mtoto wa kike ni upotevu wa rasilimali naitwa misogynist. Kupewa elimu maana yake unajengewa uwezo wa kuyatafsiri mazingira na kuja na majibu ya changamoto zinazokuzunguka. Sasa mtoto wa kike apewe elimu halafu baada ya kuhitimu changamoto zake na mahitaji yake kifedha abebeshwe mwanaume. Kuna maana gani ya mtoto wa kike kupewa elimu from the first place
Nilikuwa nasubiri your comment 😄😄
 
Sikumuacha kisa bahili nilimuacha sababu ya tabia zake ambazo hazikunivutia ikiwemo mtu wa madeni na kuniomba nijaze mtungi wa gas kwa pocket money yangu mzazi alonitumia halafu huko chuo ningetumia nini?
Hakuwa mtu mzuri bora ulitoka mita, ndiyo wale wa kusema tumalizie nyumba yangu kwanza alafu tumalizie yako.
 
Hata gari yako mafuta yanamuhusu aisee. Hao wa hivyo labda wale mataita wenye kibunda. Ambapo 1.5m haoni km ni pesa ya kumstua ubongo.

Life is very tricky! Kibunda waga kinakata, kuna ups and downs kwenye life, watu wengi wanakimbiwa na wanawake ikitokea wakaanguka!
Hivyo ni muhimu sana, kucheki mtu utakae kuwa nae kwenye "ups and downs".😊
Pesa huisha bosi; na jinsia kinzani haiamini katika kuisha kwa pesa! 😊
 
Back
Top Bottom