Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Nikisemaga kumsomesha mtoto wa kike ni upotevu wa rasilimali naitwa misogynist. Kupewa elimu maana yake unajengewa uwezo wa kuyatafsiri mazingira na kuja na majibu ya changamoto zinazokuzunguka. Sasa mtoto wa kike apewe elimu halafu baada ya kuhitimu changamoto zake na mahitaji yake kifedha abebeshwe mwanaume. Kuna maana gani ya mtoto wa kike kupewa elimu from the first place
 
Vizuri mkuu! Shida ya hawa wenzetu, cha kwao chao, cha mwanaume chao. 😊
Hahaha wapo bwashee , tatizo mnakomaa na hawa wa mjini , nenda huko kibondo, Busagara kigoma , tafuta mtoto wa kiha , mpe mtaji wa laki tatu tu afungue genge , wewe pambana kivyako , ukipate kipesa mtupie afuge kuku, baada ya miaka mi 5 tu, anakufanya unakua na uhuru wa kipato
 
Guys kuna raha kua Mwanamke na raha ya Mwanamke kuhudumiwa,
acheni sasa niwaambie mimi ni yule mwanamke hata nikipata mshahara sasa hivi, bado nitapiga simu kwa kaka zangu (wananipenda sana lastborn wao) wanitumie hela ya chips au icecream,
Siwezi kwenda lunch na kuna wanaume halafu mimi nilipe bill hata kama ni yangu, hapana nitatulia tuliii wanaume walipie,😐

Kuna siku ilikua lunch na co-workers sasa bill ilivyofika mdada mmoja naona anafungua wallet weeh acha nimpige kofi la bega, akashtuka nikamwambia "tulia ufurahie uanamke wako" akacheka akaweka wallet chini,🙃

Tukija nyumbani ndio kabisaaaa siwezi kubeba majukumu ya kununua chakula na kulipa bills, nope! labda kununua vitu vidogo vidogo kama chumvi na viberiti au snacks zangu, lol

Haya mambo ya 50/50 yaishie kwenye mabiashara hukooo ila kwenye mahusiano hapana jamani kila mtu asimamie majukumu yake yanayomuhusu, mimi jukumu langu ni kuleta utulivu, nuru na amani nyumbani,
Mtauliza sasa wewe mshahara wako unaufanyia nini sawa nitajibu, nanunua vitu vidogo vidogo kama mapambo ya ndani, kufix issues ndogo ndogo zitakazojitokeza na kuspend kwenye mambo yangu,🥰 wanawake tuna vitu vingi jamani na pesa kwetu haijawahi kutosha,😂

Ewe mwanamke unayejiita mwanamke wa shoka, unayevuja jasho na damu ili kuhudumia familia kwanza nakupongeza sana ila kama ukipata nafasi ya kufanyiwa jiachie ufanyiwe, Mwanamke ni pambo la dunia, kaumbiwa kutunzwa, kudekezwa, kupendwa, kubembelezwa, mwanamke anatakiwa awe laini laini sio wanaume wapo wewe mwanamke unabeba ngazi unaparamia ukuta kuweka umeme au unapanda kwenye stuli kufunga kamba za nguo jamani mtakuja kutenguka nyonga mshindwe kutoa raha kwa my zenu,🙄

Binafsi hizo 50/50 zenu pelekeni hukoooooooo mimi ni old school naelewa uanamke wangu unathamani kiasi gani.
Tchaooooo
wife material
 
491815633_1203620358430058_1646739210781561765_n.jpg
 
Sijajua boyfriend wako ni wa hadhi gani, kama ni tajiri au mwenye access ya pesa za walipa kodi wavuja jasho inaweza kuwa sawa wewe kudoea pesa zake ila kama ni mpambanaji anayejitafuta sio sawa kumpa mzigo wa wazazi wako wa kukulea.
Wewe ndo unaileta kwenye bf na gf, mada na mimi tumejikita kwenye 50/50 ya watu wanaoishi pamoja au malengo ya pamoja.

Kwanza ni ajabu mwanaume kutaka 50/50 hata kama uliyenaye ana kipato kukuzidi kidume jitutumue uhudumie kila kitu ndani na mkeo umpe pocket money.
 
Unasema mambo ya 50/50 huyataki,why unafanya kazi? Si ungetulia tu nyumbani ulelewe,udekezwe,ufanye kazi za nyumbani,uzae,ulee watoto?
Labda kazi anayofanya ni ya kwenda kupiga umbea au kubangaiza tu unakuta kwa mwezi labda kipato net hakizidi hata laki tano, vinginevyo haiwezekani mtu awe anaenda kwenye kazi ya maana kila siku inayompa kipato cha maana halafu aanze kuomba pesa ya kusuka, kununua pedi, VICOBA vyake n.k
 
Wewe ndo unaileta kwenye bf na gf, mada na mimi tumejikita kwenye 50/50 ya watu wanaoishi pamoja au malengo ya pamoja.

Kwanza ni ajabu mwanaume kutaka 50/50 hata kama uliyenaye ana kipato kukuzidi kidume jitutumue uhudumie kila kitu ndani na mkeo umpe pocket money.
Yaani unamzidi mwanaume kipato na bado akupe pocket money na anunue vitu vyote vya ndani?

Na wewe pesa zako muda huo unazifanyia kitu gani?
 
Wewe ndo unaileta kwenye bf na gf, mada na mimi tumejikita kwenye 50/50 ya watu wanaoishi pamoja au malengo ya pamoja.

Kwanza ni ajabu mwanaume kutaka 50/50 hata kama uliyenaye ana kipato kukuzidi kidume jitutumue uhudumie kila kitu ndani na mkeo umpe pocket money.
Mahusiano yako ya aina tatu
1.Boyfriend & Girlfriend
2.Mume&Mke (kwa ndoa rasmi au bila ndoa)
3. Mahusiano ya ngono tu (michepuko au casual sex tu)

Kama mnazungumzia mahusiano ya mume na mke huwa hakuna ligi za 50/50, mambo yanafanyika kwa makubaliano tu kulingana na ukubwa wa kipato, uhalisia na majukumu ya kifamilia. Kwanza hata hiyo 50/50 ni lugha ya Waswahili wenye akili ndogo tu walioshindwa kutafsiri au kuelewa dhana ya usawa wa kijinsia iliyokuwa ikipigiwa chapuo na feminists.
 
Back
Top Bottom