Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Bwashee , utapewa mtaji uzalishe ili uone kama pesa ni rahisi, yani hauwezi kufuga hata kuku ookote mayai ukayauze bwashee ?
Kazi kufanya ni lazima sababu nina watu na mimi wananipiga vizinga ila hela yangu naitaka na yako naitaka pia.

Ukikwama tutatumia zangu ila ukiinuka tena lazima nikupige vizinga nirudishe hela zangu.
 
Guys kuna raha kua Mwanamke na raha ya Mwanamke kuhudumiwa,
acheni sasa niwaambie mimi ni yule mwanamke hata nikipata mshahara sasa hivi, bado nitapiga simu kwa kaka zangu (wananipenda sana lastborn wao) wanitumie hela ya chips au icecream,
Siwezi kwenda lunch na kuna wanaume halafu mimi nilipe bill hata kama ni yangu, hapana nitatulia tuliii wanaume walipie,😐

Kuna siku ilikua lunch na co-workers sasa bill ilivyofika mdada mmoja naona anafungua wallet weeh acha nimpige kofi la bega, akashtuka nikamwambia "tulia ufurahie uanamke wako" akacheka akaweka wallet chini,🙃

Tukija nyumbani ndio kabisaaaa siwezi kubeba majukumu ya kununua chakula na kulipa bills, nope! labda kununua vitu vidogo vidogo kama chumvi na viberiti au snacks zangu, lol

Haya mambo ya 50/50 yaishie kwenye mabiashara hukooo ila kwenye mahusiano hapana jamani kila mtu asimamie majukumu yake yanayomuhusu, mimi jukumu langu ni kuleta utulivu, nuru na amani nyumbani,
Mtauliza sasa wewe mshahara wako unaufanyia nini sawa nitajibu, nanunua vitu vidogo vidogo kama mapambo ya ndani, kufix issues ndogo ndogo zitakazojitokeza na kuspend kwenye mambo yangu,🥰 wanawake tuna vitu vingi jamani na pesa kwetu haijawahi kutosha,😂

Ewe mwanamke unayejiita mwanamke wa shoka, unayevuja jasho na damu ili kuhudumia familia kwanza nakupongeza sana ila kama ukipata nafasi ya kufanyiwa jiachie ufanyiwe, Mwanamke ni pambo la dunia, kaumbiwa kutunzwa, kudekezwa, kupendwa, kubembelezwa, mwanamke anatakiwa awe laini laini sio wanaume wapo wewe mwanamke unabeba ngazi unaparamia ukuta kuweka umeme au unapanda kwenye stuli kufunga kamba za nguo jamani mtakuja kutenguka nyonga mshindwe kutoa raha kwa my zenu,🙄

Binafsi hizo 50/50 zenu pelekeni hukoooooooo mimi ni old school naelewa uanamke wangu unathamani kiasi gani.
Tchaooooo
Unalipiwa lunch na co-workers wako wa kiume kisa wewe ni mwanamke?! Hapo lazima kuna kitu utakuwa unawapa au wanategemea kutoka kwako, haiwezi kuwa hivi hivi tu au labda ni simps.
 
Utawapata wanaotaka kuhudumiwa na wazazi wao na sio wewe.

Uzuri mimi wangu anajua napenda pesa na atapita kusoma tu huu uzi.
Sijajua boyfriend wako ni wa hadhi gani, kama ni tajiri au mwenye access ya pesa za walipa kodi wavuja jasho inaweza kuwa sawa wewe kudoea pesa zake ila kama ni mpambanaji anayejitafuta sio sawa kumpa mzigo wa wazazi wako wa kukulea.
 
Back
Top Bottom