Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

finally nime maliza kusoma hii story binafsi nimejifunza vitu vingi nimepata picha ya maisha ya maofisini pia ni mejifunza kuto kujisahau kama big
 
Hongera kwa kupata kazi na pia uandishi mzuri wa wasifu. Mwajiri yoyote atavutiwa na hili
 
EPISODE 11: Nilijifunza kuacha kuwahurumia kabisa watu wenye ulemavu

Hii experience najua itawashangaza wengi au labda watu kutokunielewa kabisa. Kabla ya kujifunza kwamba sipaswi kabisa kuwahurumia watu wenye ulemavu namimi pia nilikuwa ni mmoja wa watu katika kundi ambalo nawaonea huruma sana watu wenye ulemavu.

Kikawaida nilikuwa nikiona au nikikutana na mtu mwenye ulemavu wowote kama vile wasioona, wanaotambaa, wenye magongo, viziwi au hata albino nilikuwa nawahurumia sana Nilikuwa nafikiria ni watu wenye shida sana na wanahitaji kuhurumiwa na kupewa misaada hivyo nilikuwa najitoa sana hasa hasa kwa wale ombaomba wa barabarani. Nakumbuka kuna omba omba alikuwa anatega kituo ambacho mimi ndio ilikuwa nashukia au napita kwenda na kurudi kwenye mihangaiko yangu, yule jamaa alikuwa anatembelea mikono (ni kama anatambaa vile) basi nilikuwa mara kwa mara namsapoti na kiasi kidogo cha pesa mpaka akanizoea yule mlemavu.

Yaani ilikuwa hawa omba omba wa wenye ulemavu mitaani hususani wanawake nilikuwa mara nyingi sana nawapa vijisenti kidogo maana nilikuwa nawahurumia sana. Hali hii iliendelea kunitawala sana na ilifikia hatua kama nikipata nafasi ya kuongea na mtu mwenye ulemavu basi ilikuwa ni yale maongezi ya kumpa moyo yaliyotawaliwa na majonzi. Yaani niliona hawa walemavu ni kama vile wanahitaji kufarijiwa kila mara na kama Mungu anawatumia kutukumbusha wengine ukuu wake.

Sasa bhana baada ya kuona kule serikalini hakuna tena dalili ya kurejeshwa job (maana niliachishwa kazi kabla sijaanza kuifanya hahaha) nikajikita kwenye kutafuta mchongo mwingine ili maisha yasije kunipiga mjini hapa. Huku na huku nifanikiwa kupata kazi kwenye shirika moja ambalo lenyewe lilikuwa linadili na maswala ya kuwainua watu wenye ulemavu na mambo mengine yanayohusiana na haki zao.

Pale niliajiriwa kama Program advocacy coordinator hivo ilikuwa ni managerial position ambacho kwenye idara yangu nilikuwa na staff kama wanne hivi ambao walikuwa wanareport kwangu direct, na pia nilikuwa naingia kwenye vikao vya menejimenti, hapa nilipanda ngazi katika career yangu. Sasa kwenye organization unadili moja kwa moja na watu wenye ulemavu ambapo wengi tulikuwa nao pale ofsini kama staff wenzangu nawengine walikuwa ni wanufaika wa program mbali mbali za pale ofsini.

Kama ilivyokawaida kazi zangu pia zilikuwa zinahusisha sana safari za mikoani katika kutimiza majukumu mbaalimbali ya program za pale ofisini. Basi ilikuwa katika zangu watu ambao na-engage naokwa asilimia kubwa walikuwa ni wenye ulemavu. Ilikuwa nikienda mikoani nakutana na walemavu, nikifanya seminars workshops basin i walemavu, nikialikwa kwenye mikutano basin i walemavu yaani ilikuwa ni walemavu walemavu kila kitu.

Sasa baada kufanya kazi na watu wenye ulemavu tena wa aina tofautitofauti kwa muda mrefu na mimi nikaaza kuwafahamu tabia zao kwa undani, lakini pia niliweza kujifunza mambo mengi sana yanayohusiana na watu wenye ulemavu. Niliweza kuzielewa hisia zao, mitazamo yao, mahitaji yao na mikakati mbali mbali ambao walikuwa nayo kibinafsi, kisera au kiprogamu yenye lengo la kutetea haki zao na kuwainua kujikwamua na hali ngumu za maisha.

Kwanza kabisa nikaja kugundua kumbe hawa jamaa ni binadamu kama binadamu wengine despite their disabilities. Kwamba mapungufu yao ya kimwili au kiakili hayawafanyi wasiwe na hisia, matamanio au mipango katika maisha yao ya kila kitu. Kikubwa sana katika hilo nikaja kuelewa kwamba watu wenye ulemavu hawataki kabisa kuonewa huruma. Yaani vile nilivyokuwa nikiwachukulia kama watu wenye kuonewa huruma na kuongea nao kwa lugha flani hivi ya kuwasikitia hicho wenyewe walikuwa hawaki kabisa.

Nakumbuka wakati naanza kufanya kazi pale ilikuwa kila kitu nafanya kwa kuwapendelea watu wenye ulemavu. Mathalani kwenye mikutano kwa kuwa mimi ndio nilikuwa organizer na facilitator mkuu basi nikatoa maagizo labda waaanze kwanza kula watu wenye ulemavu, au naweza agiza malipo waanza kulipwa wenye ulemavu, ukiniuliza sababu nakuwa sababu yenye mashiko isipokuwa ni kasumba tuu ya kuona kama wanahitaji zaidi sympathetic treatment. Nakumbuka wengi wao walikuwa hawapendi hizi privilege nilizokuwa nawapa. Nakumbuka kuna siku jamaa wawili wenye ulemavu waliniita chemba na kunichana live kwamba nakosea sana ninavyowapa upendelea wa wazi mambo mengine ambayo hayana athari moja kwa moja napaswa kuwachukulia kwa usawa na watu wengine ambao hawana ulemavu.

Nilishangaa sana inakuwaje mimi nawapa upendeleo halafu wao wanakataa? Basi ikabidi nianze kuwasoma sasa kwa ukaribu zaidi. Nikaja kugundua yafuatayo:

kwanza, Watu wenye ulemavu hawataki kuonewa huruma pasipo sababu za msingi. Kwamba wanataka kama hakuna umuhimu na sababu yoyote ya maana basi wewe wachukulie ni kama watu wengine tuu na sio kama kundi spesho. Mimi nimesafiri nao sana, nimeenda nao sana maeneo ya mitoko na kupitia hayo n imejua tabia zao nyingi sana. Wanapenda kubishana mpira, wanajichanganya kwenye starehe, wanapenda kuabudu na kufanya kazi. Hiyo ni mifano michache tuu niliyoianisha.

Nakumbuka kwenye moja ya safari zangu nilisafiri na jamaa mmoja ambaye yeye alikuwa hana miguu kabisa. Sasa kwenye hizi safari ujue mnakuwa na mda mwingi wa kufanya mambo mengi pamoja kwenye tripp kama vile kula nk. Sasa yule jamaa nikaja gundua ni mtu wa kupenda sana kutoka usiku kwenda kwenye viwanja vya starehe. Sasa siku moja nikasema ngoja nitoke na mshikaji nikampe kampani. Basi tumefanya mambo yetu pale mara jamaa akaopoa demu mmoja mkare sana. Yule manzi alikuwa pisi kwelikweli na jamaa aliondoka naye. Asubuhi nikawa namtania namtani kaka ile pisi hata mimi niliielewa jamaa akacheka sana akaniambia zile ndio pigo zake na anazo nyingi tuu na nikisema tushindane Taidume huwezi kuwin. Ila nilichokuja kugundua jamaa alikuwa ni muhongaji mzuri sana dadeki.

Pili, Watu wenye ulemavu wanakereka sana kuona wenye ulemavu wengine wanavyoomba omba mitaani kwani wanadai wanawadhalilisha. Pale ofsini kulikuwa na program ambazo zilikuwa zinawakutanisha walemavu wanaoomba omba mitaani ambazo zilikuwa zinakuwa na lengo la kuwekana sawa na kupeana mikakati ya kujiinua. Kwenye vile vikao nilikuwa naingia na wale omba omba walikuwa wanatoa shuhuda kwamba wanapata pesa nyingi sana. Akikupigia hesabu sometimes kiwango cha chini mtu anaondoka hata 50k kwa siku. Sasa wakawa wanapeana makavu wenyewe kwa wenyewe kwamba kama mtu umeomba omba kwa mwaka mmoja tu si unakuwa na pesa za kutosha na hata kuwa na uwezo wa kuanzisha biashara ya heshima tuu. Hapo nikaja gundua kwamba wale omba omba wa mitaani wengi wao ile wameishaifanya ni ajira na hawawezi kuacha.

Hii ikanifanya nikumbuke siku moja kipindi cha nyuma wakati nipo nafanya kazi kwenye lile shirika la kugawa ruzuku, nilipita pale Rombo green view shekilango kula ilikuwa ni kama saa saba hivi mchana. Basi wakati nasubiri msosi pale liliingia kundi la omba omba wasioona kama nane wakiwa na wale watoto wanaowaongoza. Basi mimi kwenye akili yangu nikawa nawaza pale leo tumevamiwa ila nikawa nimetenga buku wakipita mezani kwangu pale niwape. Gafla nikaona kuna meza ni kama zilikuwa reserved wakaenda wale ombaomba kukaa na vitoto vyao. Haikuchuka hata dakika 10 nikaona misosi ya maana ya inapekwa kwenye zile meza zao nikama wametoa oda na ndivyo ilivyokuwa. Maana nilipoletewa msosi wangu nilimuuliza yule muhudumu mbona wale ombaomba wameletewa chakula haraka je mnawasaidia kuwapa na misosi. Akanijibu kwamba wale ni wateja wao wakubwa na huwa wanakulaga pale lunch. Nikashangaa sana pale na bei za misosi rombo ya kipindi kile zilikuwa zimesimama. Kwa wale ombaomba sikutegemea kama wangemudu kula pale.

Tatu, Watu wenye ulemavu hawahitaji kuhurumiwa bali kutengenezewa mazingira mazuri yatakayowafanya waweza kujumuika pamoja na raia wengine katika shughuli mbalimbali. Nilikuja kugundua watu wenye ulemavu ni very potential. Wapo wenye vipaji na vipawa vikubwa katika field mbali mbali lakini wengi vipawa vyao wanashindwa kuvionesha na kuwanuifa kwa sababu tuu wengi wetu tumeishia tuu kwenye kuwaonea huruma badala ya kuwatengenezea mazingira wezeshi ili waweze kuonesha uwezo wao. Tena kwenye hili nina idea nzuri sana ya tv program yenye kuhusisha watu wenye ulemavu, ambayo nina uhakika itabamba sana. So kama kuna wadau wa hizo connection tuwasiliane nishee hiyo idea na kama wana uwezo wakaifanyie kazi, mimi sitaki hata kumi hapo – nipo siriasi.

Amini ama usiamini kwamba mazingira wezeshi (accessibility) plays a crucial role in empowering people with disabilities to showcase their talents and contribute to economic empowerment. By removing barriers and creating an inclusive environment, society can tap into the diverse skills and abilities of individuals with disabilities. Kwa kutowekeza katika mazingira wezshi tuapote viongozi wazuri, tunapoteza wafanyabiashara wakubwa, tunapoteza wasanii mahiri kabisa, tunapoteza wasomi wabobevu kisa tu wamezaliwa na ulemavu au kupata ulemavu katika hatua za ukuaji. Sio fair kabisa

Kwahiyo katika maana hiyo nikaachana kabisa na tabia ya kuwaonea huruma watu wenye ulemavu na badala nikajikita kushiriki kikamilifu kutengeneza mazingira ili kuwawezesha kwa nafasi nilizokuwa nazo. Mfano sasa hivi kuna wale watu wanaowatumia watoto wenye ulemavu kuomba omba mitaani. Asee siku hizi nakuwa mkali sana kwanini yule mtoto asikazaniwe kupelekwa shule instead ya kuzungushwa kwenye jua muda wa kusoma. Nimekuwa nikiwakkaripia wengi sana kuachana na tabia hizo na mara nyingi sitoi pesa ila naweza nikamnunulia chakula.

Nakumbuka hata yule mlemavu aliyekuwa anaomba omba pale kituo cha daladala mtaani kwangu kuna siku moja nikaongea nae na kumshauri kwavile lile eneo analokaa pale kituoni kumechangamka sana nikamwambia aanzish biashara yoyote. Akadai nimpe mtaji, nikamchana live kwamba nikimpa mtaji mimi au mtu mwingine hawezi kuwa na uchungu na biashar. Nikamwambia wewe anzisha biashara yoyote hata kuuza pipi mimi nitakuwa mmoja wa wateja wako na nitakuletea wateja. Ikawa kila nikipita namkomalia ishu ya biashara. Kuna kipindi nikawa nimesfairi kama wiki hivi. Nilivyorudi nikakuta ameanzisha biashara ya kuuza maji ya kandoro anauzia kwenye ndoo. Huwezi amini alipata wateja wengi sana hususani madereva na makonda wa daladala. Hapo usiniulize kama nilikuwa nanunua ama sinunui ila nakumbuka nilimfanyia mpango nikamuunganisha na jamaa yangu mmoja alikuwa anafanya kazi tigo wakampa mwamvuli na benchi. Nilihama ile mitaa lakini naamini aliiendeleza na kukuza biashara yake.

Kabla sijamaliza hii episode ngoja niwapeni shule ndogo. Tunatakiwa sana kuheshimu utu wa mtu mwenye ulemavu. Watu wengi sana wanawadhalilisha watu wenye ulemavu bila kujua kupitia au kutokana na majina tunayowaita mitaani kila siku. Ni kawaida sana kusikia mtu akimwita mtu mwenye ulemavu kipofu, kiwete, kilema, asiyesikia, zeruzeru nk. Ndugu zangu haya ni baadhi tuu ya majina yanayotweza utu wa mtu mwenye ulemavu.​
  • Usahihi upo hivi, kwanza unapotaka kutaja majina ya walemavu anzia na neno “mtu” au “watu”.​
  • Mfano,​
  • Mtu asiyeona badala ya kipofu. Ukiita kipofu wenyewe hawataki watakupiga na zile fimbo zao.​
  • Mtu mwenye ulemavu wa viungo/miguu badala ya kiwete. Ukiita kiwete wenyewe wanakuwa wakali kweli kweli.​
  • Mtu kiziwi badala ya asiyesikia. Ukiita asiyesikia wanasema wao sio watukutu maana mitoto mitukutu ndio huwa haisikii.​
  • Mtu mwenye ualbino badala ya zeruzeru.​
  • Mtu mwenye ulemavu badala ya kilema/vilema.​
Nadhani nimetoa shule kidogo hapo. See you next episode hakutakuwa na arosto jamani.​

Muendelezo soma Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa
Nukta.
 
Back
Top Bottom