Mambo niliyojifunza katika maisha yangu nikiwa nina miaka kati ya 20 mpaka 30

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
MAMBO NILIYOJIFUNZA KATIKA MAISHA YANGU NIKIWA NINA MIAKA KATI YA 20 MPAKA 30

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli

Nilianza kutafuta maarifa na hekima tangu nikiwa mdogo, mtoto wa miaka saba hivi. Katika umri huo wakati wengine wakicheza Kibabababa na kimamamama mimi nilikuwa katika kusoma vitabu mbalimbali na kusoma mazingira. Nilikuwa napenda kukaa mwenyewe. Kijana wa nyumbani, Nilikuwa nikiitwa Yakobo kutokana na sifa zangu za kupenda kushinda nyumbani.

Kukaa mwenyewe mara nyingi kulifanya Watu watambue kuwa mimi ni mkimya, mpole na nisiyependa mazoea na watu. Sikuwa na marafiki.

Katika umri wa miaka 10 mpaka 13 nilishakuwa nimejifunza habari za dini kadhaa kubwa ikiwepo dini ya uislamu kwani Baba yangu ni Muislam. Dini za kikristo nazo nilizipitia katika umri huo. Nilijifunza kuwa katika dini kuna mambo makuu manne. Imani, upendo, Haki na ukweli ambao ndio humpa mtu Maarifa na Hekima. Nilihitimu katika awamu yangu ya kwanza. Nikiwa nimejua kwa uchache Maisha ni kitu gani.

Nilikuwa ni wale watoto ambao huwaambii chakufanya kwa sababu najua nini natakiwa kufanya. Sipendi kuburuzwa yaani mtu anipandie akilini au aniambie jambo fulani la uongo au ambalo halipatani na akili yangu nami nikubali. Jambo hilo lilifanya nionekane nina jeuri, kiburi na wakati mwingine dharau. Lakini sikupenda majibizano zaidi ya vitendo. Kitu kama sikutaka nisingekifanya kwa kinyongo kwa kile kiitwacho heshima. Nilijua heshima na Unafiki havikai pamoja.

Ni umri huohuo ambao nilijifunza kuwa MIMI. Na sio kuwa vile Watu wanavyonifikiria au vile wanavyotaka niwe. Hiyo pia ilinifanya nionekane ninadharau lakini hiyo haikuwa na nafasi yoyote kwenye akili yangu.

Nikiwa na umri wa miaka 15 nilihitimisha kuwa binadamu ni kiumbe mwenye ubinafsi wa ajabu. Na hiyo ilizidisha tabia yangu ya kutokumuamini mtu yeyote hata angekuwa nani Mama yangu. Lakini nisingeweza kuishi kwa kujiamini pekee yangu ukizingatia bado nilikuwa mtoto. Hivyo nilichagua kumuamini Mungu ambaye sikuwahi kumuona lakini mara kadhaa alikuwa akisema nami kwa sauti yangu mwenyewe katika kichwa changu.

Niliingia kwenye mapenzi nikiwa ninamiaka 15. Nilikuwa mdogo. Lakini sikuingia kwa starehe bali kuna mambo nilitaka kujifunza huko. Nilifanikiwa kujifunza mambo mbalimbali ambayo mpaka hivi leo nachelea kusema ninajua nini cha kufanya linapokuja swala la mahusiano na mapenzi.

Tangu nikiwa mtoto nipambana kutimiza ahadi yangu kupitia ndoto ya kuwa Msomi. Kwa kufika chuo kikuu. Ahadi hiyo niliitimiza nikiwa ninamiaka 21. Hapo nikamaliza chuo. Lakini kabla sijamaliza chuo nikiwa kidato cha sita nilipanga mpango mwingine ambao niliupa jina la siri katika Dayari yangu ya kuandikia mipango na mikakati yangu kwa baadhi ya ishu zangu.

Mpango ule ulilenga kupata mwenza wa Maisha. Niliupa title " 7 Diamonds 7 Years" "Almasi 7 miaka 7" ambapo zilikuwa kwa mwanamke mmoja ambaye ningemuita Mke wangu. Niliweka vigezo saba ambavyo Mwanamke nitakayemuoa angekuwa navyo. Vigezo hivyo ndio nikavipa jina 7 Diamonds. Kisha nikaweka miaka saba kama muda wa kumtafuta Mwanamke huyo mwenye Almasi 7 maisha mwake. Mpango huo ungeanza mapema mara baada ya kuingia chuo kikuu mwaka wa kwanza.

Nilipoingia chuo kikuu nilijipa Majukumu makuu matatu:

1. Kuhakikisha napata Elimu
2. Kufanya kazi za mikono kwani sikulelewa kwenye mazingira ya kazi za mikono.
Mpango huu ulikuwa ni maandalizi ya mapema ya kukabiliana na maisha baada ya chuo kikuu.
3. Kuhakikisha nampata mwenye "Seven Diamonds"

Moja ya kanuni nilizojifunza tangu nikiwa chini ya miaka 20 ni kushughulikia jambo kabla muda haujafika. Nilikuwa na kanuni isemayo; Tafuta kitu ukiwa hauna shida nacho muda huo" Kanuni hiyo naitumia mpaka hivi leo. Inanisaidia kufanya jambo kwa utulivu na weledi. Sio rahisi kupata hasara wala kukosea. Kanuni hiyo ni ngumu kukufanya kulalamika au kulaumu. Hiyo ilinifanya nisiwe mtu wa kulalamika au kulaumu wengine.

Sasa nimemaliza chuo nikiwa nimefanikiwa katika yale majukumu yangu kwa asilimia kubwa tuu. Elimu 80%, Kazi za mikono na kujichanganya mtaani 75%, Kumpata mwananmke mwenye 7 Diamonds 90%. Yalikuwa mafanikio makubwa. Ilinichukua miaka mitatu kuthibitisha Mwanamke huyu kweli ndiye mwenye 7 Diamonds. Miaka minne iliyobakia ilikuwa kujua namna ya kutumia hizo Diamonds saba ambapo nilikuja kugundua kila Diamonds itanichukua mwaka mmoja hivyo nitahitajika miaka mingine saba ya kujifunza. Jumla ingeisha miaka kumi. Hata hivyo umri wangu ungekuwa bado unaniruhusu kwani bado ningekuwa sijafikisha miaka thelathini (30).

Hivyo kwenye ule mpango wa 7Diamonds 7Years" nikafanya amendments kidogo ukawa "7Diamonds 10 Years"

Kitu pekee ambacho Taikon niko nacho ni kutokukimbia UKWELI. Umri huo nilijifunza kuwa ndio umri ambao uongo unanguvu na kama utaushirikiana nao basi uongo utashinda ukweli wa maisha yako lakini hiyo haimaanishi kuwa maisha yako yatabadilika.

Uongo huanzia kwenye matamanio yako. Vile unavyohitaji Watu wakuone badala ya vile wewe ulivyo. Kumbuka nilikuambia awali kuwa mimi nilijifunza kuwa Mimi na sio vile Watu wanavyonifikiria au ninavyotaka wanifikirie.

UKWELI ni kitu pekee ambacho kitakufanya uwe HURU. Ujiamini na baadaye kuaminiwa. Ukweli utakuongoza kufanya mambo sahihi.. ukweli utalinda Future yako. Hakuna kitu sipendi kama kujidanganya. Sipendi uongo kwa sababu uongo huharibu Future. Kuukubali ukweli ndiko huitwa KUJITAMBUA. Kujua wewe ni nani na unataka nini kwenye maisha yako.

Umri wa miaka 20-30 ndio umri ambao utapaswa ujitambue ikiwa hukujitambua ukiwa kwenye miaka 10-20.

Ukweli utakufanya ujione upo mwenyewe kwenye huu ulimwengu kwani hautamwamini yeyote.na kujiona upo Mwenyewe itakufanya utafute kujitegemea"UHURU" Kujitegemea ndio maisha yako ya furaha.

Ni kawaida kwa umri huo kujidanganya, kutegemea wengine, msaada wa mali na mawazo lakini huko ni kujidanganya tuu. Hakuna ambaye yupo kwaajili ya kukusaidia usipokuwa wewe mwenyewe. Kusubiri msaada ni kujaribu kuyaangamiza maisha yako. Kuiharibu future yako.

Ukweli ndio jambo pekee litakalo kufanya uwe "Mbunifu na Mthubutu" usiwe mwoga. Hakuna mtu mkweli alafu akawa mwoga wa Maisha. Wanaoshindwa kujaribu kufanya vitu ni Watu waliotawaliwa na Uongo kwani huangalia wengine watamuonaje, watasemaje, wanajilinganisha na mwishowe huingia woga.

Uaminifu ni njia ya kuthibitisha ukweli wa mtu. Ni katika umri huohuo wengi hupoteza uaminifu wa wao wenyewe kisha kuyaamini Maisha. Hiyo hufanya kukataa tamaa na matumaini. Ni rahisi mtu asiye mkweli na mwaminifu kukata tamaa.

Ukiwa mkweli maisha yatakuwa kweli kwako siku zote. Hii sio nadharia bali ni kweli. Kwa sababu maisha ni kweli (halisi) na maisha ni maaminfu sana. Kile utakachokipanda ndicho utakachokivuna. Hayo ndio maisha. Maisha ni KWELI.

Ndoto na malengo yako huhitaji ukweli, haki, upendo na akili (maarifa na ujuzi) kisha huhitaji muda ambao utazitimiza. Miaka ya 20- 30 ni miaka ambayo unahitaji mambo yatokee kwa upesi na haraka sana. Huko ni kujidanganya na hiyo sio Haki kabisa.

Jambo ambalo huna uzoefu nalo sio haki litokee au kutimia kwa haraka. Utajifunzaje? Jambo linalotokea au kufanyika kwa haraka ni lile ambalo unauzoefu na ujuzi nalo.

Taikon kama Mastermind amechoka, ataendelea siku nyingine akijaliwa na Mungu wake.
Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Tangu nikiwa mtoto nipambana kutimiza ahadi yangu kupitia ndoto ya kuwa Msomi. Kwa kufika chuo kikuu. Ahadi hiyo niliitimiza nikiwa ninamiaka 21. Hapo nikamaliza chuo. Lakini kabla sijamaliza chuo nikiwa kidato cha sita nilipanga mpango mwingine ambao niliupa jina la siri katika Dayari yangu ya kuandikia mipango na mikakati yangu kwa baadhi ya ishu zangu. Mpango ule ulilenga kupata mwenza wa Maisha. Niliupa title " 7 Diamonds 7 Years" "Almasi 7 miaka 7" ambapo zilikuwa kwa mwanamke mmoja ambaye ningemuita Mke wangu. Niliweka vigezo saba ambavyo Mwanamke nitakayemuoa angekuwa navyo. Vigezo hivyo ndio nikavipa jina 7 Diamonds. Kisha nikaweka miaka saba kama muda wa kumtafuta Mwanamke huyo mwenye Almasi 7 maisha mwake. Mpango huo ungeanza mapema mara baada ya kuingia chuo kikuu mwaka wa kwanza.

Nilipoingia chuo kikuu nilijipa Majukumu makuu matatu ;
1. Kuhakikisha napata Elimu
2. Kufanya kazi za mikono kwani sikulelewa kwenye mazingira ya kazi za mikono.
Mpango huu ulikuwa ni maandalizi ya mapema ya kukabiliana na maisha baada ya chuo kikuu.
3. Kuhakikisha nampata mwenye "Seven Diamonds"

Moja ya kanuni nilizojifunza tangu nikiwa chini ya miaka 20 ni kushughulikia jambo kabla muda haujafika. Nilikuwa na kanuni isemayo; Tafuta kitu ukiwa hauna shida nacho muda huo"
Kanuni hiyo naitumia mpaka hivi leo. Inanisaidia kufanya jambo kwa utulivu na weledi. Sio rahisi kupata hasara wala kukosea.
Kanuni hiyo ni ngumu kukufanya kulalamika au kulaumu. Hiyo ilinifanya nisiwe mtu wa kulalamika au kulaumu wengine.

Sasa nimemaliza chuo nikiwa nimefanikiwa katika yale majukumu yangu kwa asilimia kubwa tuu. Elimu 80%, Kazi za mikono na kujichanganya mtaani 75%, Kumpata mwananmke mwenye 7 Diamonds 90%. Yalikuwa mafanikio makubwa. Ilinichukua miaka mitatu kuthibitisha Mwanamke huyu kweli ndiye mwenye 7 Diamonds. Miaka minne iliyobakia ilikuwa kujua namna ya kutumia hizo Diamonds saba ambapo nilikuja kugundua kila Diamonds itanichukua mwaka mmoja hivyo nitahitajika miaka mingine saba ya kujifunza. Jumla ingeisha miaka kumi. Hata hivyo umri wangu ungekuwa bado unaniruhusu kwani bado ningekuwa sijafikisha miaka thelathini (30).
Hivyo kwenye ule mpango wa 7Diamonds 7Years" nikafanya amendments kidogo ukawa "7Diamonds 10 Years"

Kitu pekee ambacho Taikon niko nacho ni kutokukimbia UKWELI. Umri huo nilijifunza kuwa ndio umri ambao uongo unanguvu na kama utaushirikiana nao basi uongo utashinda ukweli wa maisha yako lakini hiyo haimaanishi kuwa maisha yako yatabadilika.
Uongo huanzia kwenye matamanio yako. Vile unavyohitaji Watu wakuone badala ya vile wewe ulivyo. Kumbuka nilikuambia awali kuwa mimi nilijifunza kuwa Mimi na sio vile Watu wanavyonifikiria au ninavyotaka wanifikirie.

UKWELI ni kitu pekee ambacho kitakufanya uwe HURU. Ujiamini na baadaye kuaminiwa. Ukweli utakuongoza kufanya mambo sahihi.. ukweli utalinda Future yako.
Hakuna kitu sipendi kama kujidanganya. Sipendi uongo kwa sababu uongo huharibu Future.
Kuukubali ukweli ndiko huitwa KUJITAMBUA. Kujua wewe ni nani na unataka nini kwenye maisha yako.

Umri wa miaka 20-30 ndio umri ambao utapaswa ujitambue ikiwa hukujitambua ukiwa kwenye miaka 10-20.

Ukweli utakufanya ujione upo mwenyewe kwenye huu ulimwengu kwani hautamwamini yeyote.na kujiona upo Mwenyewe itakufanya utafute kujitegemea"UHURU" Kujitegemea ndio maisha yako ya furaha.

Ni kawaida kwa umri huo kujidanganya, kutegemea wengine, msaada wa mali na mawazo lakini huko ni kujidanganya tuu. Hakuna ambaye yupo kwaajili ya kukusaidia usipokuwa wewe mwenyewe. Kusubiri msaada ni kujaribu kuyaangamiza maisha yako. Kuiharibu future yako.
Ukweli ndio jambo pekee litakalo kufanya uwe "Mbunifu na Mthubutu" usiwe mwoga. Hakuna mtu mkweli alafu akawa mwoga wa Maisha.
Wanaoshindwa kujaribu kufanya vitu ni Watu waliotawaliwa na Uongo kwani huangalia wengine watamuonaje, watasemaje, wanajilinganisha na mwishowe huingia woga.

Uaminifu ni njia ya kuthibitisha ukweli wa mtu. Ni katika umri huohuo wengi hupoteza uaminifu wa wao wenyewe kisha kuyaamini Maisha. Hiyo hufanya kukataa tamaa na matumaini.
Ni rahisi mtu asiye mkweli na mwaminifu kukata tamaa.

Ukiwa mkweli maisha yatakuwa kweli kwako siku zote. Hii sio nadharia bali ni kweli. Kwa sababu maisha ni kweli (halisi) na maisha ni maaminfu sana. Kile utakachokipanda ndicho utakachokivuna. Hayo ndio maisha. Maisha ni KWELI.

Ndoto na malengo yako huhitaji ukweli, haki, upendo na akili(maarifa na ujuzi) kisha huhitaji muda ambao utazitimiza. Miaka ya 20- 30 ni miaka ambayo unahitaji mambo yatokee kwa upesi na haraka sana. Huko ni kujidanganya na hiyo sio Haki kabisa.
Jambo ambalo huna uzoefu nalo sio haki litokee au kutimia kwa haraka. Utajifunzaje? Jambo linalotokea au kufanyika kwa haraka ni lile ambalo unauzoefu na ujuzi nalo.

Taikon kama Mastermind amechoka, ataendelea siku nyingine akijaliwa na Mungu wake.
Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Jamii forum imefika wakati sasa muweke kitufe cha zawadi ya pesa kwa watu wenye maandiko yanayokosha na wanaojituma kama hawa.
Ulimwengu wa sasa mitandao ni ajira tosha.

Msipo fanya hizi mwakani mwezi 5 nitashawishi kampuni kubwa ya media hapa tanzania waanzishe jf yao na nitahakikisha wanaweka vitufe vya kipekee na kuiunganisha na IA then mtajua hamjui.

Ulizeni ipp media wanjuta kinachowata sasa. Zingatieni sana maoni ya watu na tekinolojia.
 
Watafanyia kazi ushauri wako hasa kwenye dunia ya ushindani
 
Hongera andiko zuri sana hili kuhani wa Tibeli ila Funga naye ndoa basi na muoe binti Kimoso na si umchezee tu😀😃😄😁😆😅😂

"Naomba umuoe huyo Binti maana mnaendana"

"Umenifurahisha hapo kwenye hilo ombi lako. Mungu ndiye ajuaye"

Pale mpango na malengo yetu vitakapokutana na kusudi la Mungu yote yatafanyika.

Hakuna msamiati kumchezea kwa Watu huru walioamua kwa akili zao.

Mungu ndiye ajuaye
 
MAMBO NILIYOJIFUNZA KATIKA MAISHA YANGU NIKIWA NINA MIAKA KATI YA 20 MPAKA 30

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli

Nilianza kutafuta maarifa na hekima tangu nikiwa mdogo, mtoto wa miaka saba hivi. Katika umri huo wakati wengine wakicheza Kibabababa na kimamamama mimi nilikuwa katika kusoma vitabu mbalimbali na kusoma mazingira. Nilikuwa napenda kukaa mwenyewe. Kijana wa nyumbani, Nilikuwa nikiitwa Yakobo kutokana na sifa zangu za kupenda kushinda nyumbani.

Kukaa mwenyewe mara nyingi kulifanya Watu watambue kuwa mimi ni mkimya, mpole na nisiyependa mazoea na watu. Sikuwa na marafiki.

Katika umri wa miaka 10 mpaka 13 nilishakuwa nimejifunza habari za dini kadhaa kubwa ikiwepo dini ya uislamu kwani Baba yangu ni Muislam. Dini za kikristo nazo nilizipitia katika umri huo. Nilijifunza kuwa katika dini kuna mambo makuu manne. Imani, upendo, Haki na ukweli ambao ndio humpa mtu Maarifa na Hekima. Nilihitimu katika awamu yangu ya kwanza. Nikiwa nimejua kwa uchache Maisha ni kitu gani.

Nilikuwa ni wale watoto ambao huwaambii chakufanya kwa sababu najua nini natakiwa kufanya. Sipendi kuburuzwa yaani mtu anipandie akilini au aniambie jambo fulani la uongo au ambalo halipatani na akili yangu nami nikubali. Jambo hilo lilifanya nionekane nina jeuri, kiburi na wakati mwingine dharau. Lakini sikupenda majibizano zaidi ya vitendo. Kitu kama sikutaka nisingekifanya kwa kinyongo kwa kile kiitwacho heshima. Nilijua heshima na Unafiki havikai pamoja.

Ni umri huohuo ambao nilijifunza kuwa MIMI. Na sio kuwa vile Watu wanavyonifikiria au vile wanavyotaka niwe. Hiyo pia ilinifanya nionekane ninadharau lakini hiyo haikuwa na nafasi yoyote kwenye akili yangu.

Nikiwa na umri wa miaka 15 nilihitimisha kuwa binadamu ni kiumbe mwenye ubinafsi wa ajabu. Na hiyo ilizidisha tabia yangu ya kutokumuamini mtu yeyote hata angekuwa nani Mama yangu. Lakini nisingeweza kuishi kwa kujiamini pekee yangu ukizingatia bado nilikuwa mtoto. Hivyo nilichagua kumuamini Mungu ambaye sikuwahi kumuona lakini mara kadhaa alikuwa akisema nami kwa sauti yangu mwenyewe katika kichwa changu.

Niliingia kwenye mapenzi nikiwa ninamiaka 15. Nilikuwa mdogo. Lakini sikuingia kwa starehe bali kuna mambo nilitaka kujifunza huko. Nilifanikiwa kujifunza mambo mbalimbali ambayo mpaka hivi leo nachelea kusema ninajua nini cha kufanya linapokuja swala la mahusiano na mapenzi.

Tangu nikiwa mtoto nipambana kutimiza ahadi yangu kupitia ndoto ya kuwa Msomi. Kwa kufika chuo kikuu. Ahadi hiyo niliitimiza nikiwa ninamiaka 21. Hapo nikamaliza chuo. Lakini kabla sijamaliza chuo nikiwa kidato cha sita nilipanga mpango mwingine ambao niliupa jina la siri katika Dayari yangu ya kuandikia mipango na mikakati yangu kwa baadhi ya ishu zangu.

Mpango ule ulilenga kupata mwenza wa Maisha. Niliupa title " 7 Diamonds 7 Years" "Almasi 7 miaka 7" ambapo zilikuwa kwa mwanamke mmoja ambaye ningemuita Mke wangu. Niliweka vigezo saba ambavyo Mwanamke nitakayemuoa angekuwa navyo. Vigezo hivyo ndio nikavipa jina 7 Diamonds. Kisha nikaweka miaka saba kama muda wa kumtafuta Mwanamke huyo mwenye Almasi 7 maisha mwake. Mpango huo ungeanza mapema mara baada ya kuingia chuo kikuu mwaka wa kwanza.

Nilipoingia chuo kikuu nilijipa Majukumu makuu matatu:

1. Kuhakikisha napata Elimu
2. Kufanya kazi za mikono kwani sikulelewa kwenye mazingira ya kazi za mikono.
Mpango huu ulikuwa ni maandalizi ya mapema ya kukabiliana na maisha baada ya chuo kikuu.
3. Kuhakikisha nampata mwenye "Seven Diamonds"

Moja ya kanuni nilizojifunza tangu nikiwa chini ya miaka 20 ni kushughulikia jambo kabla muda haujafika. Nilikuwa na kanuni isemayo; Tafuta kitu ukiwa hauna shida nacho muda huo" Kanuni hiyo naitumia mpaka hivi leo. Inanisaidia kufanya jambo kwa utulivu na weledi. Sio rahisi kupata hasara wala kukosea. Kanuni hiyo ni ngumu kukufanya kulalamika au kulaumu. Hiyo ilinifanya nisiwe mtu wa kulalamika au kulaumu wengine.

Sasa nimemaliza chuo nikiwa nimefanikiwa katika yale majukumu yangu kwa asilimia kubwa tuu. Elimu 80%, Kazi za mikono na kujichanganya mtaani 75%, Kumpata mwananmke mwenye 7 Diamonds 90%. Yalikuwa mafanikio makubwa. Ilinichukua miaka mitatu kuthibitisha Mwanamke huyu kweli ndiye mwenye 7 Diamonds. Miaka minne iliyobakia ilikuwa kujua namna ya kutumia hizo Diamonds saba ambapo nilikuja kugundua kila Diamonds itanichukua mwaka mmoja hivyo nitahitajika miaka mingine saba ya kujifunza. Jumla ingeisha miaka kumi. Hata hivyo umri wangu ungekuwa bado unaniruhusu kwani bado ningekuwa sijafikisha miaka thelathini (30).

Hivyo kwenye ule mpango wa 7Diamonds 7Years" nikafanya amendments kidogo ukawa "7Diamonds 10 Years"

Kitu pekee ambacho Taikon niko nacho ni kutokukimbia UKWELI. Umri huo nilijifunza kuwa ndio umri ambao uongo unanguvu na kama utaushirikiana nao basi uongo utashinda ukweli wa maisha yako lakini hiyo haimaanishi kuwa maisha yako yatabadilika.

Uongo huanzia kwenye matamanio yako. Vile unavyohitaji Watu wakuone badala ya vile wewe ulivyo. Kumbuka nilikuambia awali kuwa mimi nilijifunza kuwa Mimi na sio vile Watu wanavyonifikiria au ninavyotaka wanifikirie.

UKWELI ni kitu pekee ambacho kitakufanya uwe HURU. Ujiamini na baadaye kuaminiwa. Ukweli utakuongoza kufanya mambo sahihi.. ukweli utalinda Future yako. Hakuna kitu sipendi kama kujidanganya. Sipendi uongo kwa sababu uongo huharibu Future. Kuukubali ukweli ndiko huitwa KUJITAMBUA. Kujua wewe ni nani na unataka nini kwenye maisha yako.

Umri wa miaka 20-30 ndio umri ambao utapaswa ujitambue ikiwa hukujitambua ukiwa kwenye miaka 10-20.

Ukweli utakufanya ujione upo mwenyewe kwenye huu ulimwengu kwani hautamwamini yeyote.na kujiona upo Mwenyewe itakufanya utafute kujitegemea"UHURU" Kujitegemea ndio maisha yako ya furaha.

Ni kawaida kwa umri huo kujidanganya, kutegemea wengine, msaada wa mali na mawazo lakini huko ni kujidanganya tuu. Hakuna ambaye yupo kwaajili ya kukusaidia usipokuwa wewe mwenyewe. Kusubiri msaada ni kujaribu kuyaangamiza maisha yako. Kuiharibu future yako.

Ukweli ndio jambo pekee litakalo kufanya uwe "Mbunifu na Mthubutu" usiwe mwoga. Hakuna mtu mkweli alafu akawa mwoga wa Maisha. Wanaoshindwa kujaribu kufanya vitu ni Watu waliotawaliwa na Uongo kwani huangalia wengine watamuonaje, watasemaje, wanajilinganisha na mwishowe huingia woga.

Uaminifu ni njia ya kuthibitisha ukweli wa mtu. Ni katika umri huohuo wengi hupoteza uaminifu wa wao wenyewe kisha kuyaamini Maisha. Hiyo hufanya kukataa tamaa na matumaini. Ni rahisi mtu asiye mkweli na mwaminifu kukata tamaa.

Ukiwa mkweli maisha yatakuwa kweli kwako siku zote. Hii sio nadharia bali ni kweli. Kwa sababu maisha ni kweli (halisi) na maisha ni maaminfu sana. Kile utakachokipanda ndicho utakachokivuna. Hayo ndio maisha. Maisha ni KWELI.

Ndoto na malengo yako huhitaji ukweli, haki, upendo na akili (maarifa na ujuzi) kisha huhitaji muda ambao utazitimiza. Miaka ya 20- 30 ni miaka ambayo unahitaji mambo yatokee kwa upesi na haraka sana. Huko ni kujidanganya na hiyo sio Haki kabisa.

Jambo ambalo huna uzoefu nalo sio haki litokee au kutimia kwa haraka. Utajifunzaje? Jambo linalotokea au kufanyika kwa haraka ni lile ambalo unauzoefu na ujuzi nalo.

Taikon kama Mastermind amechoka, ataendelea siku nyingine akijaliwa na Mungu wake.
Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Kwaiyo mkuu kwenye maisha yako hujawahi kukosea? Kujutia? au kuzembea ?
 
Niliwahi Mkuu na sio mara moja.

Makosa yangu mengi yalitokana na msimamo na kupenda kuwa mkamilifu. Pia kupenda Haki.
Hapo nilijifunza jambo jingine muhimu kwenye Maisha, yakuwa sio kila vita upigane na sio kila ukinyimwa Haki yako uparangane kuitetea.

Nikajua kuwa kuna wakati lazima uwianishe kati ya usiku na mchana. Haki na dhulma, ukweli na uongo.
Ninajifunza kuwa hata uongo kuna wakati unamatumizi.
Nikajua kuwa Uongo unafaa kwa waongo.
Na giza lafaa kwa wanaopenda kukaa gizani.

Nilijifunza kuwa sitakiwi kumbadilisha mtu zaidi ya kujibadilisha mimi mwenyewe. Ni makosa makubwa kumbadilisha mtu. Ni kutwanga maji kwenye kinu.
Mtu atabadilika mwenyewe au kupitia víle akuonavyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom