Msaada wa mawazo yenu nipo katika harakati za kupambania maisha yangu

aBuwash

Senior Member
Dec 26, 2023
107
201
Hello wana JF,

Mimi ni kijana wa miaka 21 naish kijijin kwa sas Mimi bhan katika maisha yangu Kuna ndoto kubwa Sana nawza ambayo natamani sana kuitimiza Ila nashindwa kwa sababu kwa sasa nipo kijijin na huku kijijin wazazi Wangu wamenipa duka nirithi la nguo.

Hili duka cha kwanz siipendi hii biahsra pili mazingira niliyopo hayanipi vision yeyote ya kimaisha pia watu wanaonizunguka huku kijijni ni watu negative Sana kitu amabcho wanweza nifanya.

Mimi kuwaza vitu vinyu Sana na sio vitu vipya kiufup nahitaji kutoka huku kijijin na kuja Dar kuanzisha biashara nyingine ambayo Nina vision nayo na naamin ni sahihi kwang Ila sas shida jinsi ya kutoka hapa na kuliacha duka kiufupi wazazi wangu na watu kwa ujumla hawatanielewa.

Je nikaja Dar na nikafeli itakuwaje nyumbani huku sura yangu nitaiweka wapi naomba ushauri nifanyaje? Wana jf
 
Ni ushauri tu sio lazima, futa majina yako uliyoyataja kwenye bandiko lako.

Mjini sio kugumu na sio kurahisi umejipangaje kukabiliana na maisha ya mjini?

Usikurupuke tu kisa unajua mjini kumechangamka kuna fursa, zipo ila upo tayari kwa yote maana naona ushaanza kuwaza kuhusu kufeli.
 
Kuna dogo mmoja ngosha(23 yrs) nae alipewa vya kupewa na mzee wake akaamua kuuza ili aende dar kufanya biashara ya malengo yake.

Alikuwa na 7.5m mzee wake akamshauri amtafute ndugu yake anaeishi dar ili ampokee afikie kwake kwa siku za mwanzoni hadi atapopata nyumba ya kupanga, akafanya hivyo.

Cha ajabu siku anatoka kwao hakufikia kwa ndugu akaamua kwenda lodge, akiwa huko akasogezewa lishangazi limpe raha za dunia, dogo akanogewa akasahau kilichomleta mjini ni nini. Anakuja kushtuka hela imekata na hakuna alichofanya.

Umakini unahitajika sana
 
Hello wana jf Mimi ni kijana wa miaka 21 naitwa Abdul naish mtwara kwa sas Mimi bhan katika maisha yangu Kuna ndoto kubwa Sana nawza ambayo...
Pambania unachokiamini na kukupenda kufeli kupo na ukifeli anza upya na usiwaze watu watakuonaje ukifeli. Na je vipi watakuonaje endapo ukitusua?
 
Back
Top Bottom