Mambo muhimu ya kuzingatia unapoitwa kwenye Usaili wa Kazi

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
32
37
Fahamu mambo ya kuzingatia wakati unapoitwa kwa ajili ya Interview:

1. Fanya Utafiti kuhusu Kampuni iliyokuita kwa kufahamu Huduma na Maono yake ili majibu yako yalingane na malengo ya Kampuni

2. Elewa vizuri Majukumu ya nafasi uliyoiomba yaani (Job discription) ili uwe tayari kujadili jinsi uzoefu na ujuzi wako unavyolingana na Mahitaji ya Nafasi husika.

3. Chagua Mavazi yanayofaa kulingana na Kampuni husika. Hakikisha Nguo zako ni safi na zinakuwasilisha vizuri.

4. Fika Mapema eneo la Usaili angalau dakika 10-15 mapema kabla ya muda uliopangwa. Hii itaonesha Uadilifu na kukupa muda wa kupumzika na kuweka sawa fikra zako.

5. Jitayarishe kujibu Maswali ya Kawaida ya Usaili ikiwemo "Tuambie kuhusu wewe, Uwezo na udhaifu wako ni upi na Kwanini tukuajiri?"

6. Ikiwa umewahi kufanya Kazi awali, jiandae vizuri kuzungumzia Mafanikio ya majukumu yako ya awali. Toa mifano thabiti ya Ujuzi wako.

7. Si lazima sana kubeba Nyaraka za Vyeti vyako lakini ni muhimu kuwa navyo wakati huo, hasa kama uliambatisha nakala zake kwenye Maombi ya Kazi.

Muhimu zaidi: Usiongee vitu visivyohusiana na Maswali au Kujieleza kupita kiasi. Maelezo yako yawe mafupi, yenye kueleweka na yenye maana.
 
Swali la kiwaki sana hili

Kwanini mniajiri? Nyie si ndo mnatafuta mtu/ mfanyakazi 😆😆
Hapo wanataka ueleze working experience yako tu, waeleze uzoefu ulionao katika kazi ulizowahi kufanya zinazohusiana kazi uliyoitwa,then conclude kwa kuwaambia mm nafaa kwasababu ya uzoefu ktk eneo husika, simple 😀
 
Usije kutaja shida zako ukadhani watakuonea huruma,,,,,

Like mm mjane, nna mzazi, nauguza n.k,,, usiweke shida mbele
Yeah maana utaonekana utakuwa mtu wa ruhusa sana😀😀(kidding).

Ila kikubwa kuanza kutaja shida zako inaonyesha udhaifu wako
 
Then,nawashauri pia kama unaenda kwenye usaili wowote tumia technologia pia....ukiingia you tube andika possible questions i.e Human resource Manager in an interview utapata lecturer nzuri nyingi sana namna ya kujibu maswali,hata Job description utafundishwa.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom