Je ni kweli kujitolea sio sababu ya kuajiriwa

Am For Real

Senior Member
Nov 21, 2023
165
453
Katika pita pita zangu YouTube nikakutana na hili bandiko.
Ni kweli kabisa watu wengi wanategemea wakifanya kazi sehemu Fulani basi wapate ajira siku moja hapo hapo.
Je hii inaweza kuapply Serikalini pia kwamba ukijitolea kazi serikalini unapata kipaumbele?

Je inakuwaje Kwa watu wenye Uzoefu ambao hawajaamua kujitolea wakiomba wanyimwe? Kwa kuwa Kuna mtu kajitolea?

Je ni haki kuwanyima ajira ambao hawajajitolea? Je ni haki kuwapa ajira ambao wamejitolea tu?

Hii ni tofauti na private sector ambako anayejitolea ana uwezekano mkubwa wa kuajiriwa.
 
Wakati unajitolea unakula mizizi ya miti?, Kujitolea ni uoga wa maisha!. Kama wanaona kujitolea ni rahisi mawaziri, wabunge, wakurugenzi na wakuu wa wilaya nao wajitolee miezi walau 3 wasichukue mishahara yao.
 
Jamaa yangu mmoja yeye alikua anajitolea hospital ya wilaya (ilikua hakuna katibu wa afya) so jamaa akawa anafanya kazi zote za katibu kwa miaka kama skosei miwili, wakamuahidi kuwa serikali ikitoa ajira tu wanamfanyia mchongo anabakishwa.

Siku ajira zikatoka, akapewa recomendation letter na RMO kabisa.

Majina yakatoka, jama hayumo akaletwa jamaa mwingine kabisa kwa position yake. Akaambiwa awe anamfundisha jamaa kazi.

Jamaa aliacha kazi mpaka leo ukitaka aanze kumwaga matusi mkumbushe hio ishu.

The point is, serikalini possibility ni ndogo sana. Ila private sector ni kubwa
 
Kwanza nini lengo la kujitolea. Lengo mama la kujitolea ni kupata uzoefu wa kazi. Sasa kama unajitolea ili upate kazi utakuja kuwa disapointed pale hiyo nafasi atakapopewa mtu mwingine. Kama kutakuwa na nafasi na ikaonekana unafaa basi kupitia uwepo wako utapata nafasi lakini hautakiwi kusononeka pale atakapo pewa nafasi mtu mwingine.

Wewe jitolee usijiaminishe kuajiriwa moja kwa moja.
 
Serikalini kama una connection nzito tena kwa taasisi zinazoajiri zenyewe jitolee ila tofauti na hapo bora huo muda uutumie kulima tu.
 
Ajira za siku hizi zinaenda kwa connection tu na kujuana. Hivyo wanaojitolea wote watambue fika wanajitesa tu na kupoteza muda.
 
Katika pita pita zangu YouTube nikakutana na hili bandiko.
Ni kweli kabisa watu wengi wanategemea wakifanya kazi sehemu Fulani basi wapate ajira siku moja hapo hapo.
Je hii inaweza kuapply Serikalini pia kwamba ukijitolea kazi serikalini unapata kipaumbele?

Je inakuwaje Kwa watu wenye Uzoefu ambao hawajaamua kujitolea wakiomba wanyimwe? Kwa kuwa Kuna mtu kajitolea?

Je ni haki kuwanyima ajira ambao hawajajitolea? Je ni haki kuwapa ajira ambao wamejitolea tu?

Hii ni tofauti na private sector ambako anayejitolea ana uwezekano mkubwa wa kuajiriwa.
Inaweza ikawa au isiwe hivyo.Mahitaji ya sehemu hiyo kulinganisha na sifa zako zimekaaje?Kama una fit kwa nini uachwe?Na kama haufai kwa nini ung'ang'anie kuhudumu?Mizani isome kwa haki.
 
Back
Top Bottom