Makapuku Forum

Makapuku Forum

1a68134fe29a4887cc3f125b8905a9e7.jpg
 
Barca waendelee kuzionea timu km ArsayNO kuwanyanganya wachezaji
Man Utd pesa ya kulipa mishahara mizuri ipo kilichopungua siku hizi ni kushiriki UCL league tu(sasa tumerudi na tutajirekebisha) km ni makombe hata enzi za SAF kuna kipindi tulikuwa tunaambulia Community Shield pekee

Herrera keshasema haondoki sasa sijui mbwembwe za nini
.......
Ukipenda chongo utaliita kengeza. ManSix. Manure.
 
Siyo kwamba hakilipi
Kinanufaisha wafanyabiashara wakubwa na walanguzi wa mazao
Mfano wanaenda vijijini huko Kyela wanasomba cocoa au mpunga kwa bei chee kisha wanaenda kuviuzia viwanda kwa bei ya juu na hata kusafirisha nje ya nchi
Mkulima wa kijijini anabaki tu kuneemesha wafanyabiashara wakubwa
. ......
Ni kweli. Madalali ndiyo wananufaika zaidi. Kilimo, kwa maoni yangu, ndiyo mkakati mama utakaoikomboa nchi hii na kuitoa hapo ilipokwama. Hata Wachina walipoweza kuleta mabadiliko ya kilimo ndiyo milango mingine ikafunguka. Sisi tunataka kurukia viwanda. Sijui viwanda bila malighafi za kuaminika itakuwaje. Inatakiwa unaleta mapinduzi ya kilimo kwanza unakuwa na umma unaoshiba na kuzalisha malighafi unazozitaka kwa ajili ya viwanda vyako. Kwa hali hii unainua maisha ya wakulima kwa kuwapatia soko la kuaminika la mazao yao na wakati huo huo unalisha viwanda vyako. Sisi nadhani tunakwenda kinyume nyume....
 
Leo Katika Historia:

1937 - Kampuni ya magari ya Volkswagen ( VW )yaanzishwa.

Volkswagen ina maana ya Peoples' car ilianzishwa kwa msukumo kwa Kiongozi wa wakati huo wa Ujerumani, Adolf Hitler aliyeshinikiza yatengenezwe magari ya bei rahisi ili wananchi wake waweze kumiliki usafiri kila mmoja.
Ahsante mkuu, ila ni vizuri uwe unatuwekea na tarehe kabisa, mfano leo tarehe 28/1/2017 ili ieleweke hata baada ya tarehe ya leo kupita!
 
The little magic angel

Last edited by Shimba ya buyense

Sehemu ya Kwanza

Califonia Marekani

Katika nchi ya Marekani ndani ya jimbo la California majira ya saa nne unusu usiku pembezoni kidogo mwa mji wa San Francisco, jeshi la kiusalama la Navy Seals linapokea simu kutoka makao makuu ya jeshi hilo huko Virginia Beach. Simu hiyo ilipokelewa na Lauren McClaw akiwa kama kamanda wa jeshi la majini (navy).

"Hallo" aliipokea simu na kujibu
"Mkuu kuna habari zo zote umezipata?"aliongea kwa hofu na mashaka

"Hapana kwani kuna nini" kamanda aliuliza kwa shauku na udadisi.

"Tupo hapa Miami Beach kuna kiumbe kimedondoka toka juu na kimeleta maafa makubwa. Mpaka sasa watu wapatao mia moja ishirini na tatu wameshapoteza maisha" Mkuu aliongea kwa haraka haraka sana kana kwamba anakimbizwa.

"Whaaat?" McClaw alijibu kwa mshangao sana

"Hallo hallow hallo" kimyaa simu haikujibiwa tena.

Miami Beach

McClaw akiwa kama Chief Commander wa jeshi alipanga kikosi haraka haraka ili kulikabili lile alilolisikia. Alitumia dakika 3 tu kupanga kikosi ambacho ataambatana nacho

Umbali kutoka Virginia Beach mpaka Miami Beach ni kilometer 46 na helikopita za kivita ziliitwa na kuianza safari kuelekea eneo la tukio. Ilichukua nusu saa kufika eneo la Miami Beach. Wanajeshi walishuka upesi kuchukua nafasi tayari mashambulizi huku wakiongozwa na kamanda wao.

Eneo la tukio lilionekana kimya sana na moshi utokanao na kuunguzwa kwa vitu ulitanda kila mahali. Wanajeshi walikuwa katika umakini wa hali ya juu vidole kwenye trigger macho nyuzi tisini mbele wakisubiria agizo kutoka kwa mkuu wao.

Kwa kuwa moshi ulikuwa mwingi sana kiasi ambacho kuona mbele ilikuwa ni shughuli ngumu, McClaw aliwaamru wanajeshi wake watulie na wasikilize sauti zaidi. Haikuwa busara kutegemea macho pekee kwa maana haikuwa raisi kuona kilicho mbele japo tochi na night goggles zilikuwepo.

"Nimemwona" sauti ya mkazo ilisikika. Ilikuwa ni sauti ya mwanajeshi mmoja aitwaye Kelvin Ago wa jeshi hilo.
"Shhhs" McClaw alimjibu kwa ishara ya kwamba akae kimya asiongee.

Kwa kuwa Chief Commander alijua kuwa anapambana na kiumbe asichokijua, kiumbe ambacho kinaaminika kuwa kimedondoka kutoka juu, aliwaza labda kiumbe hicho kinaweza kuwa alien; na kinaweza kuwa kiumbe cha ajabu na hatari. Alitumia ujuzi wa kijeshi kwa kujaribu kuwaambia wanajeshi wake wazime tochi pia wakae kimya. Alitaka kujua kama hicho kiumbe kinaona na kinasikia. Na kinatumia njia na silaha gani katika kujilinda? Hayo ndiyo yalikuwa mawazo ya haraka haraka ya Chief Commander McClaw.

Je ni kiumbe gani hicho???
Mkinga, asante kwa kazi nzuri ila ukiendelea hivi nitaacha kazi kama wewe ulivyoacha kazi yako ya ulinzi. Kuna mambo kadhaa hukuzingatia.

Nilisema kuwa jina la hadithi lote ni lazima lianze na herufi kubwa yaani The Little Magic Angel. Sijui kwa nini umempuuza editor wako.

Pia proper names zote ni lazima zianze na herufi kubwa mf. Shimba ya Buyenze. Bado unafanya kosa hili. Halafu unakosea jina langu mimi mhariri wako. Kweli?

Kuwa siriazi bana kama mimi msaidizi wako nilivyo siriazi vinginevyo tutaparaganyika. Sehemu ya pili lini? Editor niko tayari!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom