Makapuku Forum

Makapuku Forum

12e8d15f4cb9c2df12cee9238880219c.jpg
 
Ni kweli. Madalali ndiyo wananufaika zaidi. Kilimo, kwa maoni yangu, ndiyo mkakati mama utakaoikomboa nchi hii na kuitoa hapo ilipokwama. Hata Wachina walipoweza kuleta mabadiliko ya kilimo ndiyo milango mingine ikafunguka. Sisi tunataka kurukia viwanda. Sijui viwanda bila malighafi za kuaminika itakuwaje. Inatakiwa unaleta mapinduzi ya kilimo kwanza unakuwa na umma unaoshiba na kuzalisha malighafi unazozitaka kwa ajili ya viwanda vyako. Kwa hali hii unainua maisha ya wakulima kwa kuwapatia soko la kuaminika la mazao yao na wakati huo huo unalisha viwanda vyako. Sisi nadhani tunakwenda kinyume nyume....
Ndiyo maana viwanda vyenyewe vipo kwenye makaratasi na mifomoni tu
Ukiwa na mbuzi wanne wanaoporomosha kinyesi rundo tayari una kiwanda cha mbolea by Mwijage

.....
 
Siyo kwamba hakilipi
Kinanufaisha wafanyabiashara wakubwa na walanguzi wa mazao
Mfano wanaenda vijijini huko Kyela wanasomba cocoa au mpunga kwa bei chee kisha wanaenda kuviuzia viwanda kwa bei ya juu na hata kusafirisha nje ya nchi
Mkulima wa kijijini anabaki tu kuneemesha wafanyabiashara wakubwa
. ......
Hii kweli mkuu maana mkulima anapata maumivu mfanya biashara ananemeka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom