Muziki: Makosa Hayako Mbali, Ikaribie Sheria
Ni siku nyingine tena tunakutana hapa baada ya kuwa tumefanya michakato ya kujiingizia kipato. ubinadamu kamili ni kuwajibika kwako mwenyewe, family na taifa kwa ujumla.
Nasema kila wakati na sitochoka kusema kuwa uwepo wako hapa, yes, wewe Kapuku mwenzangu una maana kubwa sana kwenye jukwaa hili. Hii ni kwa sababu unaleta kitu cha ziada ambacho huwezi kukipata sehemu nyingine (well, huwa nakuwa hapa mara nyingi na lile Jukwaa la chini kabisa-kuliweka kwao chini kulinifanya nikatafiti, sikufanya makosa)
Kuliwekwa picha ya mtoto akichafua sakafu isiyokauka na wadau
torvic ,
Clkey ,
Sakayo na BH kutaja wachache walichangia na haja ya mtoto kuachwa ajifunze ikaibuka nami naongeza makosa ni kosa, hilo la kwanza. Si kwa mtoto wala mtu mzima isipokuwa mtoto ana haki ya kuyafanya maana asipoyafanya sasa kujifunza itakuwa ngumu. Anaruhusiwa kufanya makosa akijifunza kutembea, ataanguka na usipomwangalia ataamka na kutembea tena, ukimwangalia atajua kakosea na atalia umuhurumie. Tuwafundishe watoto kuwa mbali na makosa sababu sheria ikaribiwe kisawasawa. Sijamaliza.
Kingine, leo Wi-Fi hapa ninapodoea imekuwa na shida na inakuja kwa mbwembwe kama ripoti ya makinikia lakini nikitaka niupload itu inagoma yaani kama waziri anakataa kuwa ripoti ya makinikia ni ya rahisi na kwa kuwa wewe si rais sahau kujua kilichomo.
Muziki sasa, wakati mwingine ni furaha sana kumtazama mwanamuziki akighani bila kuwaona wapiga vyombo kama gitaa, tumba na kadha wa kadha vyombo. Ndicho tutakachoangalia leo
Anaitwa Rory Graham almaarufu Rag'n'Bone Man, na sasa hivi anatamba na wimbo wake Human. Ni mwingereza na sifa zake zinatambaa sasa kutokana na wimbo huu ambao unachezwa sana online. Hebu burudika na wimbo huu, natamani mashairi niliyokuwa naandika miaka ya A-level ningeyawekea umiliki maana hakyanani tena mengi yaliyoimbwa yamefanana