Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Nchimbi naye mzushi fulani hivi.

Kama mtu anaamini katika principles zake, anaamini anapigania mambo fulani, na yuko tayari kuzilinda principles hizo at any cost, kwa nini ajiuzulu?

Na kama hayuko tayari kuzilinda principles hizo at any cost, kwa nini kaingia katika siasa za kitaifa Tanzania?
Toka ujana wake,nchimbi ni mtu asiyeaminika.Huyu jamaa toka anagombea uenyekiti wa vijana wa ccm mimi nilimuona na niliona harakati zake na niliwauliza jamaa wa siasa wakati ule,na wengi waliniambia mambo yake.Anyway ni binadamu mwenzangu namtakila kika la kheri na Mungu amlinde
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Dkt. Nchimbi amesema amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha uamuzi wake wa kuachia nafasi hiyo.

Amesema uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa wakati alipomuahidi Rais Samia mwaka 2025 kuwa atamsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo na uaminifu wake wote, pia aliahidi kuwa angeachia nafasi hiyo siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine.

Amesema amefanya uamuzi huo pasipo shaka baada ya kubaini kuwa Rais anatarajia mabadiliko.

View attachment 3656524
Je nni kimemponza ? Ni kutaka katiba mpya na kupinga utekaji ????

Tukio la Makamu wa Rais kujiuzulu akiwa na afya njema ni nadra sana Afrika, lakini kuna mifano michache ya kihistoria:
Jaramogi Oginga Odinga (Kenya, 1966): Alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Kenya na alijiuzulu kwa hiari kutokana na tofauti kubwa za kiitikadi na sera dhidi ya Rais Jomo Kenyatta, akieleza kuwa serikali ilikuwa imejitenga na misingi ya kisoshalisti.

Joseph Murumbi (Kenya, 1966): Alichukua nafasi ya Odinga lakini alijiuzulu miezi michache baadaye akitaja sababu za binafsi, ingawa ilifahamika kuwa ilitokana na mizozo ya ndani ya kisiasa.

Kgalema Motlanthe (Afrika Kusini, 2014): Alijiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais chini ya Rais Jacob Zuma kufuatia mabadiliko na muundo mpya wa uongozi wa ndani ya chama cha ANC.

Atiku Abubakar (Nigeria, 2006–2007): Alitofautiana waziwazi na Rais Olusegun Obasanjo na kujiunga na chama cha upinzani kabla ya muhula wao kuisha, jambo lililosababisha mpasuko mkubwa serikalini.

Katika Ngazi ya KimataifaSpiro

Agnew (Marekani, 1973): Alijiuzulu chini ya utawala wa Richard Nixon akiwa na afya njema ili kukabiliwa na mashtaka ya jinai ya ukwepaji kodi na kupokea rushwa.

John C. Calhoun (Marekani, 1832): Alijiuzulu chini ya Rais Andrew Jackson kutokana na tofauti za kisiasa na kiitikadi kuhusu haki za majimbo (Nullification Crisis) na ili akachukue nafasi ya useneta.

Carlos Álvarez (Argentina, 2000): Alijiuzulu kupinga kashfa ya rushwa ndani ya Baraza la Seneti na jinsi utawala wa Rais Fernando de la Rúa ulivyoshughulikia tuhuma hizo
 
Wewe ndiyo hujaelewa.

Mimi nauliza kwa nini Makamu ashurutishwe kujiuzulu.Wakati kama ulivyosema kilichoshinda ni chama, na Makamu wa Rais kashinda katika ticket moja na Rais.

Basically Makamu wa Rais ni Rais Mwenza.

Kama tunachagua vyama, sio watu, kwa nini Nchimbi anajiuzulu kwa sababu Samia anataka mabadiliko?

Samia ndiye chama?
Hapana. Yy ni mwenyekiti wa chama . Yy ni Rais wa JMT.
Zaidi, suala la Makamu wa Rais akishachaguliwa na watu, hapo hata akiondolewa kwenye chama hilo halimuondoi kwenye u Makamu wa Rais.

Sasa kwa nini Nchimbi kajiuzulu?

Sababu aliyotoa kwamba Samia anataka mabadiliko haina mashiko.

Nchimbi si Makamu wa Rais wa Samia, ni Makamu wa Rais wa Tanzania.
Uko sahihi. Nchimbi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Hapana. Yy ni mwenyekiti wa chama . Yy ni Rais wa JMT.

Uko sahihi. Nchimbi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sasa kama ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tena aliyechaguliwa kwenye tiketi moja na Samia, maana yake huwezi kutenganisha kura za Nchimbi na za Samia, kimsingi ni mbia wa urais wa Samia, kwa nini kakubali kujiuzulu kwa sababu tu Samia anataka mabadiliko?
 
Wakati anatoa ile kauli alikuwa ameshaamua kuachana na hii serikali. Hata Tulia nae aliamua kuachana kabisa na ukaribu kwa Samia akaondoa mpaka jina lake kwenye uspika na aligoma hata kuhudhuria uapisho wake ila akalazimishwa.
Siasa ni michezo michafu. Samia aliuupata urais kibahati tu. Wakati anaapishwa mara tu baada ya kifa JPM alisema adui yake namba moja watakuwa rangi kijani wenzake. Sio kwamba Samia kafanya nini, ila kuna ambao walitaka kubadili hata vifungu vya Katiba ili Samia asiwe Rais. Kundi hilo bado lipo ndani ya CCM.

Kama Nchimbi na Maria Sarungi ni marafiki, na Maria Sarungi ni rafiki na Polepole na Polepole ni rafiki na Warioba na warioba ni rafiki ya Kitima na Gwajima na hao wote wanamlilia Lissu, unaweza kuona ukubwa na udogo wa tatizo.
 
coincidence?👇👇
Sidhani wangetaka kumfuta nchimbi wangekuwa wameshamfuta way back, Msoga gang ndo masterminds Wana access na kila kitu

Huenda hiyo ni onyo kwa mafisadi wote wa mboga mboga wanaotaka Kuota mapembe baada kula kuwa wanawamudu.

Nchimbi anafuata maelekezo ya msoga gang kwa upole na nidhamu ya hali ya juu and soon atapangiwa nini kingine cha kufanya
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Dkt. Nchimbi amesema amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha uamuzi wake wa kuachia nafasi hiyo.

Amesema uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa wakati alipomuahidi Rais Samia mwaka 2025 kuwa atamsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo na uaminifu wake wote, pia aliahidi kuwa angeachia nafasi hiyo siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine.

Amesema amefanya uamuzi huo pasipo shaka baada ya kubaini kuwa Rais anatarajia mabadiliko.

View attachment 3656524
Screenshot_20260825_124659_WhatsAppBusiness.jpg

The cunning mastermind has done it again.
 
Sasa kama ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tena aliyechaguliwa kwenye tiketi moja na Samia, maana yake huwezi kutenganisha kura za Nchimbi na za Samia, kimsingi ni mbia wa urais wa Samia, kwa nini kakubali kujiuzulu kwa sababu tu Samia anataka mabadiliko?
Ni Gashagwa wetu, tofauti ni kwamba huyu wetu kajiuzulu mwenyewe baada ya kutiwa kishindo na CCM wenyewe. RIPOTI ya Jaji Chande nadhani haikumuacha salama. Hawa ndio waliomchomekea agenda ya Katiba kwenye ilani ya chama.
 
Siasa ni michezo michafu. Samia aliuupata urais kibahati tu. Wakati anaapishwa mara tu baada ya kifa JPM alisema adui yake namba moja watakuwa rangi kijani wenzake. Sio kwamba Samia kafanya nini, ila kuna ambao walitaka kubadili hata vifungu vya Katiba ili Samia asiwe Rais. Kundi hilo bado lipo ndani ya CCM.

Kama Nchimbi na Maria Sarungi ni marafiki, na Maria Sarungi ni rafiki na Polepole na Polepole ni rafiki na Warioba na warioba ni rafiki ya Kitima na Gwajima na hao wote wanamlilia Lissu, unaweza kuona ukubwa na udogo wa tatizo.
Tatizo mnaongea siasa za watu badala ya principles na policies.

Hao watu wote wanasimamia nini?

Principles zao ni zipi?
 
Sasa kama ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tena aliyechaguliwa kwenye tiketi moja na Samia, maana yake huwezi kutenganisha kura za Nchimbi na za Samia, kimsingi ni mbia wa urais wa Samia, kwa nini kakubali kujiuzulu kwa sababu tu Samia anataka mabadiliko?


Ata Rais anaweza kujihudhulu👈

na Makamu Rais
anachukua nchi
anaendelea mbele
Kwakuteuwa Makamu Rais
Kisha mambo yanaendelea ✍️
 
Back
Top Bottom