Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

mnataka kusema CCM haitatikisika, kwamba ni mlima Sayuni usiotikisika? kujiuzuli kwa Nchimbi kuna athari kubwa kwa CCM mjuba, Hii inaweza kupelekea hata Rais kulazimika naye kujiuzulu katika hali fulani ya kisiasa nchini. Msichukulie poa mkaona mbona Kenya naibu rais alilazimishwa kujiuzulu na rais wake akaendelea na siasa zake freshu mpaka sasa anadunda tu kana kwamba hakuna athari kwenye siasa zake za kenya kuelekea uchaguzi wao ujao. Hapa CCM imekanyaga miwaya sijui itajinasua vipi, mambo ni mengi
Nchimbi Hana hayo maajabu
 
Maswali ambayo najiuliza.

Ni trick ipi waliyotumia kum force Nchimbi mpaka kuachia ngazi?

Maana huko nyuma kumekuwa na tetesi za Nchimbi kulazimishwa kujiuzulu.

Je usalama wake ulitishiwa? Au pengine ameamua kukubali kwa lengo la kulinda familia yake kwasababu ni easy target?

Kwasababu hili swala ukilitafakari kuwa ni maamuzi ya hiari, hali make sense kabisa.
IMG-20260825-WA0023.jpg
 
Sidhani kama wananchi wa Tanzania wanashida sana na vyama. Wanachagua wanachagua mtu na sio vyama. Ni mjinga tu ndie ataamini kuwa kila aliye chadema ni msafi na kila aliye ccm ni mbaya. Na kwa taarifa yako bora hata ccm wanaozoefu kidogo wa mambo wanaweza kuingia hao wengine ndio kila kitu kikaharibika.
Naunga mkono hoja.
 
Unajichanganya, kilichoshinda ni chama, ukijiuzuru umakamu bado chama chako kina haki ya kupeleka jina lingine kwa spika ili bunge likuidhinishe kuwa makamu mpya.

In deep uchaguzi wa Tanzania tunachaguwa vyama siyo watu ndio maana ccm hawataki kusikia habari ya mgombea binafsi wanajuwa wazi ndio mwisho wa ccm.
Wewe ndiyo hujaelewa.

Mimi nauliza kwa nini Makamu ashurutishwe kujiuzulu.Wakati kama ulivyosema kilichoshinda ni chama, na Makamu wa Rais kashinda katika ticket moja na Rais.

Basically Makamu wa Rais ni Rais Mwenza.

Kama tunachagua vyama, sio watu, kwa nini Nchimbi anajiuzulu kwa sababu Samia anataka mabadiliko?

Samia ndiye chama?

Zaidi, suala la Makamu wa Rais akishachaguliwa na watu, hapo hata akiondolewa kwenye chama hilo halimuondoi kwenye u Makamu wa Rais.

Sasa kwa nini Nchimbi kajiuzulu?

Sababu aliyotoa kwamba Samia anataka mabadiliko haina mashiko.

Nchimbi si Makamu wa Rais wa Samia, ni Makamu wa Rais wa Tanzania.
 
mnataka kusema CCM haitatikisika, kwamba ni mlima Sayuni usiotikisika? kujiuzuli kwa Nchimbi kuna athari kubwa kwa CCM mjuba, Hii inaweza kupelekea hata Rais kulazimika naye kujiuzulu katika hali fulani ya kisiasa nchini. Msichukulie poa mkaona mbona Kenya naibu rais alilazimishwa kujiuzulu na rais wake akaendelea na siasa zake freshu mpaka sasa anadunda tu kana kwamba hakuna athari kwenye siasa zake za kenya kuelekea uchaguzi wao ujao. Hapa CCM imekanyaga miwaya sijui itajinasua vipi, mambo ni mengi

Samia ni Rais wa nchi
Amiri Jeshi Mkuu
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
Unataka kumtisha kwa lipi?
 
Anaweza kuwa kakataa kujiuzulu ila mfumo ukafanya yake.
Nchimbi naye mzushi fulani hivi.

Kama mtu anaamini katika principles zake, anaamini anapigania mambo fulani, na yuko tayari kuzilinda principles hizo at any cost, kwa nini ajiuzulu?

Na kama hayuko tayari kuzilinda principles hizo at any cost, kwa nini kaingia katika siasa za kitaifa Tanzania?
 
Naombeni ufafanuzi baada ya hili, utaratibu wa kumpata Makamu wa Rais mwingine upoje?

WanaCCM tufikirieni Watanganyika, msituumize kwa Maslahi binafsi mnapoenda kuchagua Makamu wa Rais mwingine.

Binafsi machungu ya October 2025 hayajaisha mpaka leo sasa msizidi kutuumiza.
Rais atateua mtanzania kutoka bara, kisha jina lake litapelekwa Bungeni, wabunge watapiga kura kuidhinisha uteuzi.
Ikiwa kura hazitatosha atateuliwa mwingine.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Dkt. Nchimbi amesema amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha uamuzi wake wa kuachia nafasi hiyo.

Amesema uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa wakati alipomuahidi Rais Samia mwaka 2025 kuwa atamsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo na uaminifu wake wote, pia aliahidi kuwa angeachia nafasi hiyo siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine.

Amesema amefanya uamuzi huo pasipo shaka baada ya kubaini kuwa Rais anatarajia mabadiliko.

View attachment 3656524


coincidence?👇👇
 

Attachments

  • IMG-20260825-WA0370.jpg
    IMG-20260825-WA0370.jpg
    95.7 KB · Views: 6
Back
Top Bottom