Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Dkt. Nchimbi amesema amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha uamuzi wake wa kuachia nafasi hiyo.

Amesema uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa wakati alipomuahidi Rais Samia mwaka 2025 kuwa atamsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo na uaminifu wake wote, pia aliahidi kuwa angeachia nafasi hiyo siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine.

Amesema amefanya uamuzi huo pasipo shaka baada ya kubaini kuwa Rais anatarajia mabadiliko.

View attachment 3656524
Ilikuwa ni suala la mda tuu ,ufukuzwe au ustaafu Kwa hiari walau Kwa Heshima kidogo.

Sasa ni zamu yake kuamua kwenda upinzani au kukaa kimya.

Huwezi kwenda kinyume na chama chako na boss wako harafu wakuchekee.
 
Umeunganisha doti kiintelijensia sana! Kumbuka hata ile kauli yake ya nyuma kuhusu katiba mpya ilivyoleta mtikisiko. Lazima kuna trap ilitegwa na mshkaji akaingia mzima mzima mzima.

Ukiangalia kwa jicho la tatu, utagundua kabisa kuwa mchezo ulichezwa kimkakati sana. Hakuna kiongozi wa ngazi hiyo anayeachia ngazi kirahisi hivyo nchini kwetu bila kushikwa pabaya. Security threats au hata tishio la kuchafuliwa vibaya kisiasa lazima vilikuwepo mezani, naona kabisa aliamua kupiga hesabu za haraka akaona it's not worth the fight.
Zile speech zake za mabadiliko tena mbele ya camera zinaendana na kauli za Lissu za kukinukisha...ni kauli fulani ambazo unaona kama muhusika alifanya kusudi ili mchoro fulani ukatimizwe.
Nina shaka makamu ni mgombea 2030 (iwe kwa upinzani ama huko huko ccm)tukiwa hai.
 
Alisimama kumnadi kampeni za 2015 kutoka kumwita fisadi papa anayetakiwa kufungwa
Jee ufisadi wa Lowassa unakumbuka CHADEMA kwenye ile list of shame iliyotolewa na Dr. Slaa ulikuwa unahusiana na nini?

CHADEMA kusema Lowassa ashtakiwe walikuwa wanatega mtego ambao CCM hawakuingia... Kuna mengi huyajui.
 
Jee ufisadi wa Lowassa unakumbuka CHADEMA kwenye ile list of shame iliyotolewa na Dr. Slaa ulikuwa unahusiana na nini?

CHADEMA kusema Lowassa ashtakiwe walikuwa wanatega mtego ambao CCM hawakuingia... Kuna mengi huyajui.
Lissu na Dr Slaa walishaeleza hili jambo kwa uswazi na ufasaha, ni mkenge uliochorwa na Mwenyekiti wa zamani
 
CCM isidhani kwamba haitatikisika, kwamba imezoea mitikisiko na iko imara. Safari hii inakwenda kuparanganyika bila kupenda. Mambo ni mengi nje na ndani yake, kuna kesi ya Lissu na viambata vyake jumuiya za kimataifa, halafu tena Nchimbi? Muziki unazidi kuwa mnene miaka minne ni mingi sana badiliko lolote linaweza kutokea, ngoma inogile, hakuna marefu yasiyo na mwisho. Zama za CCM kusambaratika zimewadia, kuna mtu CCM inamfia mikononi mwake whether kwa kupenda au kutopenda
 
Muda wake utafika tu.

Kwanza kwa sasa legacy yake ishakufa na ni chafu.

Ataondoka kwa aibu
Huyu mama amewaangusha sana wanawake wenzie. hata zile kelele mara wanawake tunaweza mara sjui nini hazisikiki tena kwasasa, coz Boss ashayatindinganya mambo. Nilipatapo kumsikia mwanamama mmoja akisema Kutokana na jinsi anavyoongoza haamini tena kama wanawake wanaweza kuongoza madaraka makubwa kama Urais

BINAFSI NADHANI HATA HUKO MBELE YA SAFARI KAMA AKIJA KUTOKEA MWANAMAMA AKAGOMBEA URAIS, HATAMTUMIA HUYU BIBI KAMA MFANO AU ROLEMODEL WAKE.
 
Back
Top Bottom